• Tidak ada hasil yang ditemukan

SURA YA TATU MBINU ZA UTAFITI

3.2 Eneo la Utafiti

ya mbinu hizi, yalitokana na malengo ya utafiti huu kwa kuzingatia nadharia inayoongoza utafiti huu. Utafiti huu ulitumia mkabala wa utafiti usio wa kitakwimu. Hivyo matumizi ya mbinu hizi tatu za uteuzi wa sampuli yana umuhimu mkubwa ili kufikia lengo ya utafiti huu.

3.2 Eneo la Utafiti

Utafiti huu ulifanyikia katika maeneo ya jiji la Dare-es-salaam (Chuo Kikuu Huria) na Pemba (Zanzibar). Uteuzi wa maeneo haya ya utafiti ulitokana na sababu zifuatazo; kwanza kwa upande wa Dar es salaam ni eneo ambalo kuna maktaba za kutosha, upatikanaji wa vitabu, wataalamu wa fasihi ya Kiswahili ambao pia wanatarajiwa wataweza kumpatia mtafiti data za kutosha mtunzi wa kazi hizi kwa sababu ya kumbukumbu zao nyingi zimehifadhiwa katika sehemu hizo. Pia kwa kutumia Pemba kama eneo la utafiti, tuliamini kuwa itakuwa rahisi kuwapata wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria wanaosoma fasihi ya Kiswahili. Dar es salaam ni eneo ambalo kuna Maktaba kuu ya Chuo Kikuu Huria na Chuo Kikuu Cha Dae-es –salaam. Kwa maana hiyo, ilikuwa rahisi kupata vielelezo vinavyomuhusu Shaaban Robert, kwa kusoma taarifa zake zinazohitajika katika utafiti huu. Vile vile ilikuwa rahisi kuwapata watu ambao waliwahi kusoma kazi zake, kwa kuandika makala au kuzifanyia utafiti. Kwa hiyo tulitegemea kupata data za kutosha. Kwa upande wa Pemba ilikuwa rahisi kupata data za mwandishi wa kitabu cha Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, kwasababu vitabu hivi viliwahi kutumiwa mashuleni na bado vinatumika na pia watu wa kawaida wanendelea kuvisoma. Hivyo, Dar es salaam na Pemba ndio maeneo tuliyoyaona kuwa ni muhimu na kufaa kukamilisha utafiti huu.

37 3.3 Uteuzi wa Sampuli

Katika uteuzi wa sampuli utafiti ulitumia sampuli tatu: uteuzi wa madhumuni maalumu, uteuzi wa nasibu/mbinu bahatishi na mbinu ya uteuzi rahisi, zimejadiliwa kama ifuatavyo :

3.3.1 Kundi Lengwa

Kulingana na (Kothari, 2004; Bryman, 2004; Komba na Tromp, 2006) kundi lengwa ni jumla ya watu wote ambao huhusishwa katika utafiti. Cooper (1989) na Vans (1990), wanaeleza kuwa kundi lengwa ni wanachama wote, mtu mmoja, kikundi au elementi ambazo mtafiti amekusudia kuzihusisha katika utafiti wake. Walengwa waliohusishwa katika utafiti huu ni walimu na wanafunzi wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili Chuo Kikuu Huria hususani Idara ya Fasihi Taaluma za Kiswahili Pemba, wanafunzi wa Sekondari ya Uweleni kidato cha tano (5) na kidato cha sita (6) ambako tuliweza kuwapata wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili. Kwa upande wa walimu, mtafiti aliwateua kulingana na madhumuni maalumu. Hapa mtafiti alizingatia ufahamu na taarifa alizopata kuwa nani ni mwalimu wa fasihi ya Kiswahili hususan riwaya kwa Kiswahili na nani ni mwalimu anayefundisha fasihi kwa jumla.

Kundi lengwa la utafiti huu liliteuliwa kulingana na sifa na umuhimu wa kundi hilo katika utafiti huu; kwanza kwa mwanafunzi lazima awe anasoma au kulifahamu vyema somo la fasihi ya Kiswahili na umuhimu wa kila kundi katika utafiti huu. Kwa mfano, wanafunzi wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili katika Chuo Kikuu Huria waliteuliwa kwa kigezo kuwa ni wanafunzi wanaosoma fasihi, wana maarifa ya nadharia za uchambuzi wa kazi za fasihi na pia wana ujuzi na maarifa katika matumizi ya nadharia

38

na mbinu za uhakiki wa kazi za fasihi. Vile vile kigezo cha kuwa wanafunzi hawa wanasoma riwaya kwa Kiswahili kilifanya kundi hili kuwa ni rasilimali ya kutosha katika utoaji wa data za utafiti huu.

Sifa nyingine ya wanafunzi wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili wa fasihi Chuo Kikuu Huria ni kwamba walipatikana kwa urahisi. Lakini pia ilikuwa rahisi kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria kwa sababu wanasoma darasani na kuna eneo mahsusi la kuweza kuwapata na kuwatambua kuwa hawa ni wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili. Hivyo basi, sababu hizi ndizo zilizomfanya mtafiti kuchagua wanafunzi wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili wa Chuo Kikuu Huria, kuwa wahojiwa wake katika utafiti huu.

Walimu na wahadhiri wa fasihi wa muda mrefu ni kundi muhimu katika utafiti huu kwa sababu wao ndio wanaofundisha kozi ya fasihi, wana ujuzi na maarifa ya kutosha katika nadharia na vitendo kuhusu fasihi ya Kiswahili na uhakiki wa kazi za fasihi kwa jumla. Hivyo kwa kutumia kundi hili tuliweza kupata data za kutosha kuhusu Shaaban Robert kutokana na vitabu vyake teule katika utafiti huu.

Kwa upande mwingine, walimu wa fasihi wa muda mrefu ni kundi muhimu katika utafiti huu kwa sababu wao ndio wanaofundisha kozi ya fasihi, wana ujuzi na maarifa katika nadharia na vitendo kuhusu fasihi ya Kiswahili na uhakiki wa kazi za fasihi kwa jumla. Vile vile uliwahusisha wazee na vijana wanaoishi nje ya eneo la Mkoani – Pemba, wazee ambao ni kawaida kutamba hadithi kwa vijana na pia vijana ambao hutolewa hadithi za kale, ambao huwa na uzoefu wa kutoa hadithi na wanosimuliwa kuweza kuhifadhi hadithi hizo na kusimulia wenzao, hadithi kama zile za safari,

39

vichekesho, ujanja na pia za watu mashujaa waliokuwepo Ukanda wa Pwani Afrika Mashariki. Zikiwemo zile ambazo baadae ziliandikwa kama riwaya, mfano Adili na

Nduguze, hadithi ya Mkama Ndume, Mwana wa Mwana, Mwinyi Mkuu, Siti Binti Saad

n.k. Hivyo kwa kutumia kundi hili tuliweza kupata data za kutosha kuhusu vitabu vya

Adili na Nduguze pamoja na wasifu wa Siti binti Saad kwani hadithi zao sio ngeni kwa

wasimulizi wa hadithi na wasikiliza hadithi za utamaduni wa watu wa Afrika Mashariki.

3.3.2 Uteuzi wa Madhumuni Maalumu

Uteuzi, kwa kigezo cha madhumuni maalumu, ni uteuzi wa kuzingatia sababu mahsusi. Kombo na Tromp (2006) wanasema, ni uteuzi ambao mtafiti, kwa makusudi, hulenga kuteua kundi la watu ambao anafikiri kuwa ni rasilimali inayotegemewa katika utafiti wake. Kwa hiyo, mbinu hii ni bora na ya muhimu katika utafiti kwa sababu, baadhi ya watu, katika kundi lengwa, walionekana kuwa na uwezo na ni rasilimali kubwa zaidi katika kutoa data za utafiti huu kuliko wengine. Kwa mfano, suala la kiwango cha ufahamu wa fasihi, nadharia na uhakiki kati ya wanafunzi wanaosoma fasihi na wale wasiosoma fasihi, kati ya walimu wanaofundisha fasihi, hususani riwaya. Katika uteuzi wenye madhumuni maalumu uteuzi hufanywa kwa kuzingatia vigezo ambavyo vinahusu na maswali ya utafiti, kuliko kigezo cha uteuzi nasibu au wa kubahatisha. Hivyo, Katika mbinu hii, wahojiwa waliteuliwa kwa madhumuni maalumu kutokana na nafasi zao kwa kujuwa kuwa wao ndio rasilimali ya jamii juu ya data ya utafiti.

Sababu nyingine iliyomfanya mtafiti kutumia mbinu hii ni kwamba; mtafiti alikuwa na taarifa juu ya kuwapo kwa makundi yenye ujuzi, maarifa na uzoefu katika fasihi kwa Kiswahili na riwaya kwa Kiswahili, makundi hayo ndiyo yaliyokuwa rasilimali ya data

40

ya utafiti huu. Hivyo basi, mbinu hii ilitumika kufanya uteuzi kutoka kwa walengwa wa utafiti huu.

Kwa upande mwingine, wanafunzi wanaosoma riwaya kwa Kiswahili waliteuliwa kwa kigezo kuwa wanaelewa nadharia za uchambuzi wa riwaya ya Kiswahili. Wanafunzi walioteuliwa ni wale wenye maarifa ya riwaya kwa Kiswahili, historia na mabadiliko yake na hivyo, wana uwezo wa stadi za uchambuzi wa vipengele vya fasihi simulizi katika kitabu cha Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Kigezo hiki pia kilitumika kwa walimu wa fasihi waliobobea katika riwaya kwa kuzingatia uzoefu na maarifa na ujuzi juu ya nadharia za uchambuzi na uhakiki wa riwaya.

Kwa jumla, mbinu ya uteuzi kwa madhumuni maalumu, ilimsaidia mtafiti kupata kundi la watu wenye uzoefu, stadi na maarifa katika nadharia na uhakiki wa fasihi na riwaya kwa Kiswahili, na hatimaye, kupata data ambazo ni mhimili wa utafiti huu. Vile vile, data zilizopatikana katika makundi hayo, zilimsaidia mtafiti kupata na kufanya majumuisho mahususi aliyoyakusudiwa kulingana na madhumuni ya utafiti.

3.3.3 Uteuzi nasibu/Mbinu bahatishi

Mbinu nyingine ambayo ilitumika katika uteuzi ni mbinu ya uteuzi nasibu. Kombo na Tromp (2006) wanaielezea mbinu hii kuwa, ni mbinu ambayo hutumia watu ambao ni hadhira iliyomilikiwa, yaani watu ambao mtafiti alikutana nao bila kutarajia. Katika mbinu hii, wahojiwa huwa ni wale watu ambao walipita na kuonesha kupendezwa na utafiti unaofanywa. Mbinu hii ilitumika kuwateua wahojiwa ambao ni watoa hadithi na wapenda kusoma vitabu vya fasihi hususan vitabu vya Shaaban Robert. Kwa kuwa siyo rahisi, kuwafahamu watu hao, mbinu hii ilimsaidia mtafiti kuwashirikisha pale tu mtafiti

41

alipokutana nao na alipata taarifa kuhusu kitabu cha Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti

Binti Saad. Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kupata data na taarifa za kutosha kuhusu

hadithi ambazo Shaaban Robert kaziandika na kuwa riwaya.

3.3.4 Mbinu ya Uteuzi Rahisi

Mbinu hii ilitumika katika kupata uteuzi wa utafiti huu. Kwa kutumia mbinu hii ya uteuzi rahisi, Mtafiti alichukua orodha ya majina ya wanafunzi wa sekondari, na alitumia nafasi kila baada ya mwanafunzi wa nne, aliteua jina la mwanafunzi ambaye alishiriki katika kutoa data za utafiti. Hivyo, kwa ujumla utafiti huu ulikuwa na jumla ya wahojiwa 64 na mchanganuo wake ni kama inavyojionyesha katika jedwali lifuatalo namba 2:

Jedwali namba 2 - Idadi ya Washiriki wa Utafiti

Namba Aina Jinsia Jumla

Ke Me

1. Wanafunzi wa umahiri wa Chuo Kikuu wanaosoma

riwaya kwa Kiswahili

09 09 18

2. Wanafunzi wa sekondari (Uweleni) 15 15 30

3. Wlimu chuo Kikuu Huria 00 02 02

4. Walimu wa fasihi Sekondari Uweleni 04 04 10

5. Waliowahi kusoma kazi za Shaaban Robert 03 03 06

6. Wazee wasimulizi hadithi 01 01 02

7. Vijana wasikiliza hadithi 01 01 02

JUMLA 70

Chanzo kutoka data za Utafiti

Dokumen terkait