Tunapendekeza utafiti ufanywe katika kuchunguza kama kuibuka kwa mashairi ya kisasa yalichangiwa na siasa ama maendeleo ya taaluma katika ngazi ya Chuo Kikuu ama la!
Tunapendekeza pia utafiti ufanyike kuhusu kuchunguza mabadiliko yanayotokea katika mashairi ya kimapokeo ili kuweza kuona kama yanasaidia kuupeleka mbele ushairi wa kimapokeo au hakuna maendeleo yoyote.
MAREJELEO
Abeid, A., (1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: EALB. Babbie, E., (1999). The Basics of Social Research. Belmont: Wadsworth Publishing
Company.
Bathes, R., (1994). The Semiotic Challenge. Berkely: University of Califonia Press. Chandler, D., (1992). Semiotics: The Basics, London: Routledge Press.
Chuwa, M., (2011). “Uchunguzi wa Vipengele vya Fani Katika Mashairi ya Mathias Mnyampala”. Tasinifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Cohen, L. na Wenzke (2000). Research Methods in Education (5th end) London: Rouledge Press.
Creswell, J.W., (2009). Research Design: Qualitative, Quantitatie, and Mixed
Methods Approaches. Los Angeles: SAGE Publication.
Frolova, N., (2003). “Euphrase Kezilahabi: The Renewal of Kiswahili Poetry”. In
Kiswahili, Vol. 66 Dar es salaam. IKR.
Furlong, P. na Wenzake, (2000). Research Methods and Statistrics: An Integrated
Approach. New York: Harcourt College Publishers.
Haji, G.H., (1994). Kimbunga. Dar es Salaam: TUKI.
John, L., (2004). Critical Reading: A Guide. In http://www. Brocku. Ca/English/jlge/criticalreadig. Html. Accesssed, 30th, October 2006.
Juma, S.R., (2012). “Ufundishaji na Ujifunzaji wa Ushairi wa Kiswahili Katika Shule za Sekondari Jijini Dar es Salaam”. Tasinifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kandoro, S., (1978), Ushahidi wa Mashairi ya Kiswahili na Lugha Yake. Dar es Salaam: Longman Ltd.
Keys, B. na Wenzake (1989). “Four Faces of Fully Function Middle Manger;
California Management Review; Vol. XXIV. No, 4 pp. 59-67.
Kezilahabi, E., (1974). Kichomi, Nairobi: Heinemann Educational books.
Kezilahabi, E., (1977). “Mashari ya Saadan”, Mulika, Namba 14. Dr es Salaam: TUKI. Kur. 32-40.
Kezilahabi, E., (1983). “Uchambuzi katika ushari wa Kiswahili”. Katika Makala ya
Semina ya Kimataifa ya Waandsihi wa Kiswahili, Kur. 145-165. Dar es
Salaam: TUKI.
Kezilahabi, E., (1988). Karibu Ndani Dar es Salam: DUP. Kezilahabi, E., (2008). Dhifa, Nairobi: Vide-Muwa.
Kothari, C.R., (1992). Reserch Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: Wiley Eastern Limited.
Kothari, C.R., (2008). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New Age International Publishing Ltd.
Massamba, D.P.B., (1983), “Suala la Ushairi wa Kiswahili”. Katika Makala ya Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili-Fasihi namba 3. Dar es Salaam: TUKI.
Mayoka, J., (1984). Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Nairobi: EALB. Mlacha, A.K.S. na Madumulla, J.S., (1991). Riwaya ya Kiswahili. Dar es Salaam:
DUP.
Msokile, M., (1992). Uhakiki: Karibu Ndani. Dar es Salaam: DUP.
Mulokozi, M.M., (1975). “Revolution and Reaction in Swahili Poetry”. In Kiswahili,
Vol. 45/2. Dar es Salaam: IKR, Kur. 46-65.
Mulokozi, M.M., (1996). Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Mulokozi, M.M. na K.K. Kahigi, (1979). Kunga za Ushari na Diwani Yetu, Dar es Salaam: TPH.
Mulokozi, M.M. na T.S.Y. Sengo (1995). History of Kiswahili Poetry [AD 1000-2000]. Dar es Salaam: TUKI.
Newman, W.L., (2006). Social Reserch. Sixth Edition, Boston: Pearson.
Njogu, K. na Rocha, C., (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi, JKF.
Nyangwine, N. na Masebo, J., (2002). Uhakiki Katika Fasihi. Dar es Salaam: Nyambari Nyangwine Publishers
Omary, M., (2011), “Siasa katika Ushairi wa Kezilahabi: Uchunguzi wa Karibu
Ndani (1988) na Dhifa (2008), Tanisifu ya M.A Kiswahili Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Robson, C., (2007). How to do a Reserch Project: A guide for under graduate
students, Carton Victoria: Blackwell Publishing.
Said, K., (2010). “Matumizi ya Lugha Katika Nyimbo za Harusi za Kabila la Wazigua. Utafiti mdogo wa Kukamilisha Masharti ya Shahada ya Awali”, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Seleman, K. na Mtimbo, A., (2004), “Uhakiki wa Diwani ya Kimbunga”. Utafiti Mdogo wa Kukamilisha Masharti ya Shahada ya Kwanza, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Sengo, T.S.Y., (1994). “Utangulizi Katika Kimbunga”. Dar es Salaam: TUKI Senkoro, F.E.M.K., (2011). Fasihi. Dar es Salaam: KAUTTU.
Topan, F., (1974). “Utangulizi katika Kichomi”, Nairobi: Heiremann.
Wamitila, K.W., (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake, Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Wamitila, K.W., (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi, Nairobi: Vide-Muwa.
Yin, R.K., (1994). Case Study Research: Design ad Methods, (2nd eds. Thousands Oaks Calif: SAGE publishers.
Waliorejelewa Kupitia Mazungumzo
Mulokozi, M.M., (2009). Mazungumzo Katika Mihadhara ya Umahiri Katika Fasihi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mulokozi, M.M., (2011), Mazungumzo Katika Mihadhara ya Umahiri Katika Fasihi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sengo, T.S.Y., (2012), Mazungumzo Katika Semina za Umahiri, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Senkoro, F.E.M.K., (2010), Mazungumzo Katika Mihadhara ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
VIAMBATISHI
Kiambatishi Namba 1: Mashairi ya Haji Gora Haji yaliyotumika
Uchumi ukwamuliwe, ukwamuke kwa haraka Ukwamuke hima uwe, ukae tunakotaka
Kabisa huko usiwe, kunako janga kutoka Isiwe kuwekaweka, ukwamuliwe uchumi
Tumefanya sote kazi, pori hilo kulifyeka Na kuchimbua ardhi, shamba likakamilika Mbona hamtuulizi, kuvuna kunapofika
Kuzichukuwa nafaka, mkazila peke yenu (Madanganyo,uk. 06).
Tumefanya sote kazi, pori hilo kulifyeka Na kuchimbua ardhi, shamba likakamilika, Mbona hamtuulizi, kuvuna kunapofika
Kuzichukua nafaka, mkazila peke yenu (Madanganyo, uk.06).
Wenye vyao watubana, twaumia masikini La kufanyiza hatuna, hali zetu taabani Kwa sasa kilo ya dona, bei mia ishirini
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana (Wenye vyao Watubana, uk.10).
Washindana matajiri, kwa bei siyo utani, Ni pigo kwa mafakiri, tulio hali ya chini
Wezeni kutafakari, wanyonge tu madhilani
Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana, (Wenye vyao Watubana, uk.10).
Utalii tuukuze, uzidi kuimarika Uimarike uweze, nafasi hiyo kushika Ushike na uingize, madata kuminika Iwe kwa kila dakika, wauinue uchumi
Ukulima ni msingi, kwa dhati tukiushika Utapolima kwa wingi, nafaka bila kuchoka Na matunda kila rangi, yatakayonunulika Kwa madala si shilingi, na kuchangia uchumi
Uvuvi ule wa leo, ambao uliofika Kuendelezwa na huo, pia inahitajika Unao wake upeo, kwa uchumi kunyanyuka
Na juhudi zatakika, kwa kuokoa uchumi (Uokolewe, 05).
Ukimwi vielelezo, vyake vinaendeleza Mtu hasa ni wa mwanzo, yule anajituliza Hupata maambukizo wengine kuwanukiza Hiyo njia, moja wapo, inasambaza Ukimwi.
Damu nayo huchangia, pasi na kuichunguza Yenye vidudu vibaya, mwingine kumwuongeza
Kuona wasaidiya kumbe wamuangamiza
Na hilo ni mojawapo, lisambazalo Ukimwi (Vielezeo, uk.3).
Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika Kimeing’oa mibuyu, minazi kunusurika Nyoyo zilifadhaika
Nyumba kubwa za ghorofa, siku hiyo zimeruka Zikenenda kwa masafa, kufikia kwa kufika Vibanda vyao malofa, vyote vikasalimika Nyoyo zikafadhaika (Kimbunga, uk.01).
Punda kakosa thamani, sababu vitimbi vyake Milele akawa duni, wala asiheshimike Kwa wake umuhimu, kavunjiwa hadhi yake Ndiyo tabia ya punda, kurusharusha mateke Kuchunga akikushinda, mwachie aende zake.
Punda hakumbuki wema, hata kwa mchunga wake Humpa mwinga mtama, na maji anufaike
Katu haiwi salama, shukurani zake mateke Ndiyo tabia ya punda, kurusha rusha mateke
Paka nakuasa wizi, wacha kuiba samaki, Imekuwa yako kazi, majikoni huondoki Haufai uchokozi, si kizuri kitu hiki
Paka nakuasa wizi, vitoweo usiibe (Paka, uk.22).
Mkia baada kumpa, mambo yakawa mabaya Nguo zake kazitupa, unyani kumrudiya Kaanza kuchupa chupa, mitini akarukiya Akafanana na wenzake, akiwa nyani katimu
Wenzake wakamcheka, wote na kumzomeya Akakosa la kushika, kwa haya kujioneya Majuto yakamfika, akabakia kuliya
Akarudia porini, iliko yake kaumu (Kibwangai).
Kuna hadithi ya kale, kwa babu nimepokeya Kwa manyani zama zile, mkasa ulotokeya Nilikuwa mwanakale, hiyo miaka zingatiya Leo nawadokezeya, kwa nilivyoyafahamu.
Nyani baada kugunduwa, watu wanawaviziya Sababu yake kwa kuwa, hila yao mimea Na ndipo wakaamua, mwenzao kumtumiya
Rushwa kajenga kambi, na kuondoka hataki Afanya kila vitimbi, mkaidi hashikiki Tumzushieni wimbi, isiwe kutuhiliki
Kiambatisho Namba 2: Mashairi ya Kezilahabi yaliyotumika
Nitaandika wimbo juu ya mbawa za inzi Utoe muziki arukapo wa usikie walio wengi Ushairi wa jalalani utaimbwa
Juu ya vidonda vya wakulima Na usaha ulio jasho lao
Nitaandika juu ya mbawa za wadudu wote warukao.
Juu ya mistari ya pundamilia na masikio makubwa ya tembo,
Juu ya kuta vyooni, maofisini, madarasani Juu ya paa za nyumba na kuta za Ikulu! Na juu ya khanga na tisheti
Nitaandika wimbo huu.
Mti mkongwe umelalila upande Wa nyumba zetu hafifu
Upepo mkali uvumapo hatulali Kila kukicha twatazama mizizi yake Na mkao wake, na kuta hafifu za nyumba Lazima ukatwe kuanzia matawi hadi shina Mafuriko ya mwaka huu yaashiria
Tutabaki kuwasimulia wajukuu Mwaka ule wa mafuriko
Miti mingi mikongwe iliaanguka (Mafuriko, uk.4).
Ni chakula cha mchana, Walanchi wameshafika, Wazungu, Wahindi, Waarabu Washateka sehemu zao Chakula ki mezani Nidhifa
Mawaziri wenye kula Wabunge wapewa magari Waandishi waliosajiliwa Watangazaji wenye yale yale Wakereketwa wasokereka Kimya wamekaa (Dhifa, uk. 27).
Na hiki kibanda gani, ghafla mbele yangu Ni kibanda cha Msonge, mlango wake mmoja Mlango wenye uwazi, na ndani moto wawaka, Hodi hodi wenyewe, ni mimi kichwamaji Natafuta zangu njuga, na lile vazi la Kindu
Ingawa sina ubuyu, naja kukesha nanyi (Karibu Ndani, uk.34).
Akiyumbayumba
Na sarawili zee mawinguni
Akitoka magharibu kwenda mashariki Kisha akaanguka baharini kwa kishindo Binadamu tukasubiri. Tukasubiri
Halafu baharini ndege katoka Karuka juu mawinguni Wengine wakasema: Ndiye! Wengine: Siye!
Tukasubiri (Matumaini, uk. 06).
Jibwa likitoka jikoni Ulimi lajilamba Piga limekwiba piga Jibwa likishika hatamu
Haliwezi kuacha utamu, (Jibwa, uk.15).
Azimio sasa ni mabaki ya chakula Kwenye sharubu za bepari
Kalamu inayovuja
Katika mfuko wa mwanafunzi Vumbi zito
Baada ya ng’ombe kupita Kilichosalia sasa
Ni punje za ulezi
Zilizosambazwa jangwani
Sikiliza Monika
Sisi tumezoea vituko vya wakubwa Huyu mumeo anatoka kijiji jirani Tulimwona akilambwa na mbwa Alipomaliza kujisaidia
Na alikimbia siku ya tohara
Sasa naye avuta kidevu shingo upande Kama beberu, tayari kupigana
Wewe Monika
Twende ufukweni kuogelea Tuone hiyo cheni ya dhahabu.
Wewe Monika
Ulitoka kwetu bila ushanga kiunoni Kama kumbikumbi asi mbawa Ulipofika mjini ukaolewa na waziri Sasa wataka tusimame barabarani Kukupungia matawi mabichi Upitapo wainua kipua juu
Chogo limechongoka kama senene Aendaye kwenye harusi ya mende Na kutusanifu kwa mawani meusi Kama nyani achezaye sarakasi