• Tidak ada hasil yang ditemukan

MBINU ZA UTAFITI

3.5 Mbinu za Kukusanyia Data

Utafiti huu ulitumia data za msingi ambazo zilipatikana kwa kutumia njia mbalimbali. Mbinu au njia za kukusanyia data ni mbinu ambazo mtafiti huzitumia ili kupata data za utafiti (Kothari 2004). Utafiti huu ulitumia mbinu za aina tatu ambazo ni mbinu ya dodoso, mbinu ya usaili na mbinu ya uchunguzi makini. Mtafiti amefikia

uamuzi wa kutumia mbinu za aina hiyo ili kupata uthabiti wa matokeo ya utafiti anaokusudia kuufanya. Mbinu alizotumia katika utafiti huu

ni:-3.5.1 Dodoso

Kwa mujibu wa Kothari (keshatajwa) dodoso ni mbinu ya kukusanyia data ambapo mtafiti huandika maswali na kisha kuyapeleka kwa watoa taarifa ili wayajibu na baadaye kumrudishia mtafiti yakiwa tayari yameshajibiwa.

Adam na Kamuzora (2008), wanaeleza kuwa dodoso ni mbinu ya kukusanya data ambapo inahusisha maswali yaliyoandaliwa kuhusu mada fulani na kumtaka mtafitiwa kujibu kwa maandishi. Maswali haya yanaweza kuwa yanahitaji majibu mafupi au marefu kutegemena na taarifa inayohitajika pia na mtu anayepewa dodoso.

Walliman (2011) anaelezea kuwa maswali ya dodoso yako ya aina mbili. Aina ya kwanza ni ile inayohusisha maswali funge ambayo hutoa fursa kwa watafitiwa kuchagua jibu miongoni mwa majibu kadhaa yaliyopendekezwa. Aina hii ya dodoso ni rahisi kujibu na inasaidia kupata majibu mahususi na huepusha upendeleo. Aina ya pili ya maswali ya dodoso ni ile inayohusisha maswali yasiyo funge ambayo hayatoi fursa kwa watafitiwa kuwa huru kueleza wanachokijua juu ya dhana fulani kutegemeana na kile kilichoulizwa. Aina hii haitoi uhuru kwa watafitiwa kueleza mawazo yao kwa ubainifu na uwazi na pia husaidia kupata taarifa nyingi zaidi.

Mbinu ya dodoso iliyotumika katika utafiti huu ilihusisha aina ya maswali funge . Mtafiti alitumia aina hii ya maswali ya dodoso katika utafiti wake kwa kuwapatia watafitiwa maswali ya aina hii kwa kuamini kuwa maswali ya aina hii ndio

yatakayopelekea majibu ya uhakika na umakini na kwa upande wa watafitiwa watakuwa huru na itawawezesha kuelezea kwa uhakika na ukweli bila ya woga wowote, mtafiti ameitumia mbinu ya dodoso kutokana na sababu ya kuona mbinu hii itaepusha usumbufu mkubwa kwa watafitiwa kutokana ndio maswali yanayoendana na watafitiwa kulingana na kiwango chao cha umri, hii ni kwa sababu dodoso ina umadhubuti na upungufu wake. Mtafiti ameona kwamba iwapo mbinu hii ilitumika ipasavyo itakuwa ni mbinu nzuri na ameitumia mtafiti kukusanya data za uhakika na kuweza kukamilisha utafiti kwa haraka sana. Vile vile ameona mbinu hii itamsaidia katika kukusanya data zake kwa muda mfupi ambazo zitampelekea kukamilisha utafiti wake kwa muda aliojiwekea. Pia itapeelekea kuwatafiti watafitiwa aliowateua sawa sawa bila ya upendeleo wowote. Hata hivyo itampelekea mtafiti kupata taarifa nyingi kwa muda mfupi sana.

3.5.2 Uchunguzi Makini

Uchunguzi makini ni mbinu ya kukusanya data inayohusiana na kurikodi tabia za watu, vitu na matukio katika mpangilio maalumu kisayansi (Kothari 2004). Mbinu hii inachunguza vitu vyote vinavyotuzungumka. Uchunguzi makini ni wa aina mbili; uchunguzi makini unaodhibitiwa, huu hupatikana kwa kupitia vitu vilivyowekwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na uchunguzi makini usio na udhibiti, uchunguzi huu hupatikana katika sehemu za maumbile halisi na haupatikani kwa kutumia dhana za uchunguzaji bali hupatikana katika mazingira halisi yaani ya kimaumbile (Kothari 2004). Mtafiti alitumia mbinu hii ili kupata data za uhakika zilizoaminika na

kupunguza dosari kutokana njia ya uchunguzi makini ni njia ambayo mtafiti wa utafiti huu alitampatia data za awali na uhakika endapo atatumia uchunguzi makini wa udhibibiti na endapo hatatumia uchunguzi makini usio na udhibiti mtafiti hatopata data za awali za uhakika na umakini na dosari zitatokea kwa kukosa udhibiti wa wazungumzaji wa asili wa lahaja ya Kipemba . Kama anavyosema Walliman (keshatajwa) kuwa data za awali ni data zinazoaminika kwa sababu zimepatikana au kurekodiwa moja kwa moja kutoka kwenye tukio. Mtafiti katika utafiti huu alitumia uchunguzi makini wa kuweza kudhiti matukio kwa kwenda katika eneo la utafiti na akatafiti kwa kupitia watafitiwa halisi aliowateua ili kuweza kupata data za uhakika na kuepusha dosari kutokea.

3.5.3 Mbinu ya Usaili

Mbinu hii inahusisha mkusanyiko wa masuali kwa wasailiwa na kujibiwa ana kwa ana tu kwa wakati huo huo na mtafiti anarikodi katika daftari la kumbukumbu au katika tepu ya kurikodia. Kwa mujibu wa Kothari (2004) mbinu hii inamsaidia mtafiti kuweka bayana istilahi ambazo hazieleweki kwa watu walioulizwa pia mbinu hii humuwezesha mtafiti kupata taarifa za ziada na za kina. Kothari anaendelea kueleza kuwa mbinu hii inamruhusu mtafiti kuuliza masuali ya ziada na pia kumuwezesha kuwa karibu na watoa taarifa.

Walliman (keshatajwa) amegawa mbinu ya usaili katika aina tatu ambazo ni usaili wa ana kwa ana, usaili wa kikundi na usaili wa kutumia simu (mtandao). Ingawa mbinu hii inaweza kufanywa kwa njia zote hizo, katika utafiti huu, mtafiti aliitumia

mbinu hii kwa kuwasaili watafitiwa wake wa data za lahaja ya Kipemba kwa kutumia maswali wazi ambayo hayakufungwa hata kidogo akayagawa kwa watafitiwa wake na akawafanyia usaili wa ana kwa ana kwa lengo la kupata data za uhakika.

Aidha, mtafiti alitumia mbinu hii kwa sababu kadhaa, kwanza, ni kwa ajili ya kupata uthabiti wa majibu ya watafitiwa. Pili, ni rahisi kwa mtafiti kudhibiti sampuli yake kwa wepesi na kwa usahihi zaidi. Hii imewezekana kwa sababu mtafiti alipata fursa na wahojiwa ana kwa ana na kuwauliza maswali na kurikodi majibu yao papo kwa papo wakati mahojiano yao yanaendelea. Pia maswali ambayo yalikosa majibu aliweza kuyatafutia ufumbuzi papo kwa papo. Tatu, ilikuwa ni rahisi kwa mtafiti kukusanya taarifa nyingi na kwa kina zaidi, kwasababu watafitiwa waliweza kuuliza maswali na mtafiti alikuwa na uhuru wa kuuliza maswali ya ziada fursa ambayo isingepatikana katika mbinu nyingine za kukusanyia data kama vile usaili na nyinginezo.

Dokumen terkait