Katika nchi mpya, ambamo haki inakaa, Mungu atatoa makazi ya milele kwa waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa ajili ya uzima wa milele, upendo, furaha, na kujifunza mbele zake. Kwani hapo, Mungu mwenyewe atakaa na watu wake, na mateso na kifo vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limekwisha, na dhambi haitakuwapo tena. Vitu vyote, vilivyo hai na visivyo hai vitakiri kwamba Mungu ni pendo; naye atatawala milele. Amina. (2 Pet. 3:13; Isa. 35; 65:17-25; Mat. 5:5; Ufu. 21:1-7; 22:1-5; 11:15.)
Maelezo haya yana ufafanuzi kuhusu kanisa linavyoweza kufanya katika suala fulani mahususi. Kanisa linaweza kutumia njia zingine za kushughulikia mambo hayo. Njia hizo badala hazina budi kukubaliana na kanuni zinazokubalika za muundo na uendeshaji wa Kanisa.
Maelezo ya SURA YA 8
1. Sherehe ya Ndoa (tazama uk. 74)—Katika baadhi ya nchi au majimbo, mchungaji hana budi kuteuliwa rasmi na kusajiliwa ili aweze kuendesha huduma ya ndoa. Katika nchi nyingi mchungaji anaweza kuendesha huduma ya ndoa kanisani lakini mkataba huo husainiwa kisheria na msajili wa wilaya, ambaye kwa kawaida hukaa katika chumba cha kujiandalia na kusikiliza aina ya tamko la ndoa lililoidhinishwa. Na katika nchi zingine mchungaji hawezi kabisa kuendesha sherehe ya ndoa kwa kuwa inatambuliwa kuwa ni jukumu la serikali na inachukuliwa kuwa ni mkataba wa kisheria. Katika hali kama hiyo, washiriki kwa kawaida huwa wanarudi nyumbani au kwenye nyumba ya ibada ambapo mchungaji huendesha huduma maalum kuomba baraka za Bwana kwa wanandoa husika. (tazama uk. 146-154.)
2. Kufundisha na Kuandaa Wazee (tazama uk. 75)—Licha ya mchungaji kuwa na wajibu wa kwanza wa kufundisha wazee, konferensi zinahimizwa kupanga mikutano ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwafundisha. Ili kuboresha uhusiano wa timu ya mchungaji na wazee, inawapasa wachungaji kuhudhuria mikutano hiyo ya mafunzo. Viongozi wa makundi wanaofanya kazi mahali pa wazee hawana budi kualikwa pia.
3. Utunzaji na Ukarabati wa Mali za Kanisa (tazama uk. 78, 79)—Mashemasi wa kiume na wa kike hawana budi
kuhakikisha kuwa jengo la kanisa linasafishwa na kukarabatiwa wakati wote na kwamba maeneo ya nje yanasafishwa na kuwa
ya kuvutia wakati wote. Hii ni pamoja na kuhakikisha kazi ya ulinzi inafanywa. Katika makanisa makubwa ambapo ni lazima kuajiri mlinzi, inawapasa mashemasi kupendekeza kwa baraza
la kanisa mtu anayefaa na baraza litapiga kura ya kumwajiri, au baraza linaweza kuidhinisha mashemasi kuajiri mlinzi. Ni lazima idhini ya baraza itolewe kwa ajili ya pesa zote za ukarabati mkubwa. Bili zote za matengenezo, na gharama za kudumu, kama vile za maji, umeme na fueli hupelekwa kwa mhazini kwa ajili ya malipo.
4. Karani Hutunza Kumbukumbu (tazama uk. 79)— Kumbukumbu za vikao vya baraza hazina budi kuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za kanisa, au katika mfumo mwingine wa kumbukumbu unaofaa uliokubaliwa na kanisa, zikieleza wakati na tarehe ya mkutano, idadi ya waliohudhuria na taarifa ya uamuzi wote uliofanyika. Karani hana budi pia kuandika orodha ya kamati zilizoteuliwa katika kikao, kumpatia mwenyekiti orodha ya wajumbe wa kila kamati pamoja na hadidu za rejea na muhtasari wa kazi ambayo kamati imeombwa kufanya. Kitabu cha kumbukumbu za kanisa kinaweza kupatikana katika Duka la Vitabu vya Kiadventista au katika nyumba ya uchapishaji katika baadhi ya nchi.
Kitabu cha kumbukumbu za kanisa kina mahali pa kuandika washiriki, pamoja na sehemu ya kuonesha jinsi na wakati washiriki wanavyopokelewa na kuondolewa. Kumbukumbu hizo hazina budi kufuata wendo, na inapasa kuonesha ushahidi wa kila ingizo katika sehemu inayoandikwa uamuzi unaohusu washiriki. Kumbukumbu za washiriki hazina budi kutunzwa kwa usahihi na kuboreshwa kila wakati ili kuonesha hali rasmi ya washiriki.
5. Kuwasiliana na Washiriki (tazama uk. 80)—Inampasa karani kuwasiliana mara kwa mara na washiriki wasioonekana kanisani na inampasa kuwapatia habari za maendeleo ya kanisa, kuwatia moyo, na kutoa taarifa ya shughuli zao za Kikristo kila robo.
6. Pesa za Oda Binafsi za Vitabu (tazama uk. 82)—Mahali ambapo hakuna Duka mahalia la Vitabu vya Kiadventista, washiriki wanaweza kuweka pesa za oda binafsi za maandiko mbalimbali, vitabu, makabrasha, magazeti, na pesa za kuagizia
majarida yatolewayo kwa kipindi maalum katika bahasha pamoja na fomu ya oda iliyojazwa ipasavyo na kuzikabidhi kwa katibu wa huduma binafsi. Mhazini atawasilisha oda hizo pamoja na pesa kwenye Duka la Vitabu vya Kiadventista au nyumba ya uchapishaji, kulingana na mfumo uliokubaliwa na konferensi. Mwishoni mwa kila robo, katibu wa huduma binafsi atatoa taarifa kwa kanisa katika mkutano wake mkuu wa kila robo kuhusu akaunti ya kanisa katika Duka la Vitabu vya Kiadventista na/au nyumba ya uchapishaji na atampatia nakala mhazini. (tazama uk. 97, 98.)
7. Kulinda Watoto—Inalipasa kanisa kuwa mahali salama pa kuleta watoto wetu. Kila anayehusika na watoto wadogo hana budi kukidhi vigezo vya Kanisa na vya kisheria. Ili kuwalinda watoto wetu, makanisa yanahimizwa kuweka sera zitakazotoa hali ya usalama na ulinzi unaofaa kwa watoto. Sera hizo hazina budi kuwa pamoja na:
a. Kanuni ya Watu Wazima Wawili—Hakisha kuna watu wazima wawili katika madarasa au shughuli za watoto.
b. Mlango Wazi—Zuia mawasiliano ya faragha au ya mtu na mtu na himiza kanuni ya mlango wazi katika hali zote. Mahali ambapo kuwa na mlango wazi haiwezekani, weka mtu mzima mwingine mlangoni.
c. Kuhakiki Wanaojitolea—Hakikisha wanaojitolea wote wanajaza fomu ya taarifa ya mtu anayejitolea, chunguza historia zao na inapotakiwa na sheria, chunguza taarifa zao polisi.
d. Sera ya Miezi Sita—Weka kipindi cha kusubiri cha miezi sita kwa watu waliiotoka kubatizwa au kuhamia ambao wameonesha kuwa wanataka kuhudumia watoto.
e. Mafunzo—Toa mafunzo mara kwa mara kwa walimu na waliojitolea kuwasaidia kuwaelewa na kuwalinda watoto na jinsi ya kuwalea katika imani.
Viongozi wa kanisa mahalia hawana budi kushauriana na konferensi ili kuwa na uhakika juu ya taratibu na matakwa ya konferensi, pamoja na matakwa mahalia ya kisheria kwa watu wanaohudumia watoto. Miongozo ya
ziada inapatikana kutoka Adventist Risk Management kwenye www.adventistrisk.org.
8. Miongozo ya Huduma za Watoto (tazama uk. 86)—The Children’s Ministries Handbook: A Step-by-Step Guide for Children’s Leaders Around the World (2005); The Children’s Ministries Coordinator: A Step-by-Step Guide for Organizing Children’s Ministries in the Local Church (2005); and Pastor’s and Elder’s Handbook for Children’s Ministries (2005). Silver Spring, Md.: Huduma za Watoto, Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa huduma za watoto wa konferensi yako mahalia na www.gcchildmin.org.
9. Miongozo ya Huduma za Familia (tazama uk. 91)—Caring for Families Today: A Guide for Family Ministries (2009). Silver Spring, Md.: Huduma za Familia, Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa huduma za familia wa konferensi yako mahalia na www.adventistfamilyministries.org.
10. Miongozo ya Huduma za Afya (tazama uk. 92)—
CELEBRATIONS (muhtasari wa programu 12 za masomo muhimu ya huduma za afya, pamoja na maelezo na PowerPoint),
CHARTERS (mfululizo wa mihadhara yenye PowerPoint kwa ajili ya masomo kwa hadhira za walei), Misingi ya Huduma za Afya (Mihadhara 84 juu ya afya ya msingi kwa ajili ya viongozi wa huduma za afya), Breath Free (mtaala wa kuacha kuvuta), Youth Alive (programu ya kujenga uwezo wa kurudi katika hali ya kawaida kwa vijana wetu), Vegetarian Cuisine Instructor’s Course (Mwongozo namna ya kufanya), Birthing Companions (kusaidia wanawake vijana wajawazito katika ujauzito wao), Regeneration (programu ya hatua 12 za kutoka katika utegemezi), na My Vegetarian Food Pyramid (mabango makubwa au madogo).
93)—Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa mambo ya jamii na uhuru wa kidini wa konferensi yako mahalia au tembelea www.irla.org.
12. Miongozo ya Huduma za Uchapishaji (tazama uk. 94)—
Literature MinistryTraining Manual (vitabu namba 1-3 pamoja na masomo ya PowerPoint); The Publishing Ministry
(kijitabu); Student Literature Evangelism Manual; Miracles of Grace (kitabu chenye shuhuda 365 za wainjilisti wa vitabu ulimwenguni); The Literature Evengelist (Jarida la kila robo la idara ya Huduma za Uchapishaji ya Konferensi Kuu. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa huduma za uchapishaji wa konferensi yako mahalia au mkurugenzi wa union yako. Unaweza pia kwenda kwenye www.publishing. gc.adventist.org.
13. Miongozo ya Shule ya Sabato na Huduma Binafsi (tazama uk.
97, 99)—Miongozo ya kusoma Biblia ya Shule ya Sabato kwa ajili ya umri mbalimbali (CQ, Cornerstone Connections, Real- Time Faith, Vijana Wadogo, Msingi, Chekechea, and Awali); Mwongozo wa Shule ya Sabato; Keys for Sabbath School and Personal Ministries Leaders (mfululizo wa vitini); Reaching and Winning (mfululizo wa vijitabu kwa ajili ya huduma binafsi kwa watu wa mifumo mbalimbali ya imani); Adventist Community Services Handbook: The sharing) (barua ya taarifa). Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa shule ya Sabato au wa huduma binafsi wa konferensi yako mahalia. Unaweza pia kwenda kwenye www.sabbathschoolpersonalministries.org au kwenye GraceLink.net, JuniorPowerPoints.org, RealTimeFaith. net, CornerstoneConnections.net, CQBibleStudy.org, au SabbathSchoolU.org.
14. Miongozo ya Huduma za Uwakili (tazama uk. 99)—Steps to Discipleship (2009). Silver Spring, Md.: Huduma za Uwakili, Konferensi Kuu ya Waadventista wa Sabato. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mkurugenzi wa idara ya huduma za uwakili wa konferensi, union au divisheni yako mahalia au tembelea
15. Miongozo ya Huduma za Wanawake (tazama uk. 100)— Uthibibitisho wa viongozi ngazi ya 1-4; miongozo ya Siku ya Maombi, Siku Maalum ya Wanawake, na Siku ya Kupinga Udhalilishaji; Mwongozo wa Huduma za Wanawake kwa Wachungaji na Wazee. Kwa maelezo zaidi wasiliana na mkurugenzi wa huduma za wanawake wa konferensi yako mahalia na tembelea www.adventistwomensministries.org.
16. Mpango wa Uundaji wa Chama cha Vijana wa Kiadventista
(tazama uk. 102)—Maelezo ya kina kuhusu mpango wa uundaji wa Chama cha Vijana wa Kiadventista yanapatikana kwa mkurugenzi wa huduma za vijana wa konferensi. Kila kanisa halina budi kuchunguza taswira ya vijana na familia zake, miongozo, watendakazi, vitendea kazi na uhusiano na shule, likianzisha huduma bora ya vijana kulingana na vigezo hivyo. Katika maeneo mengine linaweza kutumika neno lingine badala ya “chama,” kama vile “ushirika” au “harakati” lakini jina “Vijana wa Kiadventista” halina budi kutumika kila wakati ili kukibainisha chama.
17. Miongozo ya Huduma za Vijana (tazama uk. 105)—Tembelea tovuti yetu kwa ajili ya masomo zaidi na maelezo zaidi katika
www.gcyouthministries.org au andika barua pepe kwenda
Maelezo ya SURA YA 9
1. Orodha Kielelezo ya Viongozi wa Kanisa (tazama uk. 108). Kamati ya mapendekezo itachagua washiriki watakaotumika kama
maofisa katika nafasi mbalimbali. Kanisa dogo linaweza kuwa na orodha ndogo ya maofisa. Kanisa kubwa linaweza kuwa na orodha ndefu ya maofisa. Orodha hii inaweza kufikiriwa:
Mzee/wazee
Shemasi/mashemasi wa kiume Shemasi/Mashemasi wa kike Karani
Mhazini na msaidizi/wasaidizi Mratibu wa waliovutiwa Baraza la kanisa
Bodi ya shule ya kanisa
Kiongozi wa Chama cha Vijana Wadogo wa Kiadventista na msaidizi/wasaidizi
Kiongozi wa Chama cha Vijana wa Kiadventista Mdhamini wa Chama cha Vijana wa Kiadventista
Katibu-mhazini wa Chama cha Vijana wa Kiadventista na msaidizi/wasaidizi
Mkurugenzi wa muziki wa Chama cha Vijana wa Kiadventista
Mpiga piano au ogani wa Chama cha Vijana wa Kiadventista Mkurugenzi wa Klabu ya Wavumbuzi
Mkurugenzi wa Klabu ya Mabalozi Mratibu wa shule ya Biblia
Mkurugenzi wa huduma za watoto
Mwimbishaji wa kanisa au kiongozi wa nyimbo au mratibu wa muziki
Mpiga ogani au piano wa kanisa
Katibu wa mawasiliano au kamati ya mawasiliano Mkurugenzi wa Huduma za Jamii
Kiongozi wa Chama cha Dorkas Katibu-mhazini wa Chama cha Dorkas Katibu wa elimu
Kiongozi/viongozi wa huduma za familia Kiongozi wa huduma za afya
Mratibu wa huduma kwa walemavu
Mkurugenzi wa Klabu ya Watafuta Njia na naibu mkurugenzi Kiongozi wa huduma binafsi
Mkurugenzi wa huduma za maombi Mkurugenzi wa huduma za uchapishaji Kiongozi wa uhuru wa kidini
Mrakibu/warakibu wa shule ya Sabato na msaidizi/wasaidizi Katibu wa shule ya Sabato na msaidizi/wasaidizi
Viongozi wa vitengo vya shule ya Sabato, pamoja na viongozi wa utandaaji kwa watu wazima
Katibu wa uwekezaji wa shule ya Sabato Kiongozi wa huduma za uwakili
Mkurugenzi wa Shule ya Biblia Wakati wa Likizo Kiongozi wa huduma za wanawake
Watenda kazi wa ziada wanaoonekana kuwa wa lazima
Maofisa wa Chama cha Kaya na Shule (kiongozi na katibu-
mhazini).
Kama kanisa moja peke yake linasimamia shule, kamati ya mapendekezo ya kanisa hupendekeza kwa baraza ambalo nalo hufanya uteuzi. Kama makanisa zaidi ya moja yanasimamia shule moja, bodi ya shule itaendesha mchakato huo. (Tazama uk. 88, 89.)
Maelezo ya SURA YA 10
1) Shule ya Sabato (tazama uk. 117)—Muda wa kawaida wa Shule ya Sabato ni saa moja na dakika kumi. Hata hivyo jambo hilo haliizuii konferensi kuamua kutumia muda mrefu au mfupi zaidi, ingawa ni muhimu kuwa na muda wa kutosha kuhamasisha mara kwa mara shughuli za umisionari na majukumu ya kanisa la ulimwengu, pamoja na sadaka ya utume na angalau dakika thelathini za kusoma Biblia.
2) Mfumo wa Ibada (tazama uk. 117, 118)—Mifumo ya ibada hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine na utamaduni mmoja hadi mwingine. Mifumo ifuatayo inapendekezwa:
Mfumo Mrefu wa Ibada
Muziki wa Utangulizi Matangazo
Kuingia wahudumu Wimbo wa sifa Ombi
Kusoma fungu la Maandiko Wimbo wa sifa
Ombi
Wimbo wa sifa au muziki maalum Sadaka