• Tidak ada hasil yang ditemukan

2 Tim 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao,

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "2 Tim 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao,"

Copied!
5
0
0

Teks penuh

(1)

JE

,

NINAWEZA KUIAMINI BIBLIA

?

(M

AHUBIRI YA

H

ADHARA

N

GARA

M

TONI

A

RUSHA

|

2017)

Na Almodad Amos

Tunakwenda kuanza mfululizo wa mafundhisho ya Neno la Mungu kama tutakavyoyasoma katika vitabu vitakatifu. Na unajua kwamba kusoma Neno la Mungu ni faida kwako na kwangu pia kwani:

- Neno la Mungu ni pumzi ya Mungu, Lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza katika maisha haya, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema

- Ni Mungu ailyesema kwamba: | Isa 40:8 Neno litasimama milele | Math 24:35 – lakini maNeno yangu hayatapita kamwe | Yoh 17:17 – Neno la Mungu ni kweli na hutakasa | Zab 119:105 – Nuru na mwangaza katika maisha ya mwanadamu

Lakini kabla hatujazama na kuanza kuyachunguza yote hayo, kuna swali makini sana ambalo limekuwa likiwasumbua wanadamu wenye nia njema na hamu ya kutaka kumtafuta Mungu wa kweli na kuifuata kweli yote. Swali hilo linasema Je, Naweza kuiamini Biblia? Maswali mengine yanayoambatana na swali hilo ni kama vile:

- Je, naweza kuwa na uhakika kuwa kile inachokisema Biblia ni kitu cha uhakika?

- Je, upo ushahidi gani unaoweza kudhihirisha kuwa yale yaliyoandikwa ndani ya Biblia yametoka kwa Mungu na ni kweli tupu?

- Nawezaje kupata uhakika unaothibitisha kuwa Biblia si kitabu kilichoandikwa na watu tu kwa ujanja wao na utashi wao?

Wapendwa maswali haya si madogo hata kidogo. Ni maswali makini sana yanayohitaji majibu makini pia. Somo la leo litakwenda kujibu swali hili kubwa na litakuwa ni msingi wa masomo mengine yatakayofuata kwani yote yatakuwa yamejengwa ndani ya Biblia na kabla hatujaendelea ni vema ukajiridhisha kwa fafanuzi makini za uchunguzi wa kile Mungu alichotufunulia kwamba Biblia ni Neno la Mungu tena Neno ni Neno lililotoka kwa Mungu na kamwe halikuchakachuliwa hata kidogo.

Tunaishi ndani ya jamii ambayo taratibu inaendelea kupoteza mweleko wake. Tabia ya Kikristo (Tabia ya Mungu), maadili mema, matazamo wa ki-dini, na mawazo mazuri ya Mungu vinaendelea kufutwa taratibu na sehemu yake inaendelea kuchukuliwa na kuharibiwa na hali ya wanadamu kukataa kuwepo kwa viwango vya tabia na uadilifu alivyoviweka Mungu, na kama hali hii itaendelea katika jamii zetu, tukubali au tukatae kutakuwa na hali ya kuvurugika kwa tabia na amani katika jamii zetu. Zaidi ya hapo, utafiti umebaini kwamba katika miaka ishirini iliyopita kumekuwa na poromoko la uelewa wa kile Biblia inachofundisha.1

Kwa hiyo nini kinaendelea hapa? Sikiliza, Katika hali hii ya kutokuyafuata maandiko unaweza ukawa shahidi wa maovu ambayo yamaendela kuongezeka kila kunapokucha, na kutokana na watu kupuuza usomaji wa Neno la Mungu, leo hii pamekuwa na madanganyo mengi yaliyojivika vazi la dini mbalimbali. Kwa sababu gani? Kwa sababu Ibilisi anajua vizuri kabisa kwamba siku utakapo yatambua yale yakupasayo kwa mujibu wa Neno la Mungu, utakua umejinasua kutoka katika makucha yake na mtego wake mbaya wa dhambi.

Kwa hiyo anachofanya ni nini?

1. Ni kukujengea mashaka kwamba Biblia si Neno la Mungu hata kidogo.

2. Akiona unaanza kuamini-amini, atakujengrea mashaka kwamba sehemu ya Biblia ni Neno la Mungu lakini sehemu nyingine si Neno la Mungu kwani imetiwa mikono na wanadamu. Lakini sehemu hizo ambazo mashaka yako yanajengwa, ukizichunguza kwa makini sana utagundua jumbe za pekee sana ambazo kwa kweli zinaijenga Imani yako kwa Mungu na kukuimarisha kitabia na kimwenendo ili uwe mtu aliyekamilika na kufaa kusimama mbele za Mungu.

Sasa moja kwamoja tuanze kujibu swali la Msingi kwamba Je, Biblia tutakayoitumia katika mikutano hii ni Neno la Mungu kweli au ni kitabu tu kama vitabu vingine?

1Walter A. Elwell and Douglas Buckwalter, vol. 5, Topical Analysis of the Bible: With the New International Version, Includes

(2)

Swali ni kwamba tumejuaje kwamba Biblia ni Neno la Mungu?

1. Ujumbe Mmoja Uliozungumzwa na Watu 40 tofauti tofauti kwa miaka zaidi ya 1,500

Ukiyachunguza maandiko kwa umakini sana bila upendeleo, unaweza kugundua kwamba, Neno la Mungu lililowaongoza mitume wa kwanza kabisa, lilianza kuandikwa wakati wa Mtume Musa. Baada ya hapo, toka kizazi hata kizazi, manabii wengine waliendelea kuandika kwa kadri Mungu alivyowaongoza. Baadaye, kile alichokuja kuhubiri Yesu na kile walichohubiri mitume na kukiandika… vyote vilidhihirisha kutokutofautiana katika maana nzima ya ujumbe ulioandikwa.2 Waandishi wake walikua watu tofauti sana

wapatao 40. Kulikua na wakulima , wavuvi kama Petro, wafalme kama Daudi, matajiri kama Sulemani, maskini kama Yeremia, wafugaji nabii Amos, kulikuwa na wasomi kama Luka na Paulo. Lakini pamoja na tofauti za kiutamaduni na kikabila, pamoja na tofauti zao za kimazingira [waandishi walitokea mabara 3 tofauti tofauti na wengine hawakufahamiana], pamoja na kwamba waliishi katika vipindi tofauti-tofauti vilivyotofautiana kwa miaka mingi sana; wakiandika kwa takribani miaka 1,600 kuanzia 1500 K.K mpaka 100 B.K bado kile walichoandika kilikuwa na ujumbe mmoja usiopingana wala kuhitilafiana. Ipo sifa moja

makini sana katika Biblia…

Ukweli usiopingika ni kwamba, palihitajika mwasisi mmoja, mwenye kulisimamia zoezi la uandishi uliochukua muda mrefu kiasi hiki1, ili kuifanya Biblia kuwa na ujumbe mmoja na kusomeka jinsi inavyosomeka. Vinginevyo nenda kaangalie vitabu vya elimu dunia ambapo waandishi wenye taaluma moja na wanaoishi ktk kizazi kimoja wanashindwa kupatana wao kwa wao, katika uandishi wao. Biblia inaujumbe mmoja kwa sababu Mungu mmoja ndiye aliyewaongoza waandishi hawa mbalimbali kuandika kitu chenye ujumbe mmoja wa Ukombozi wa maisha ya mwanadamu.

2. Ugunduzi wa Kisayansi (Akiolojia)

Baadhi ya wanazuoni waliwahi kudai kwamba, isingaliwezekana kwa Musa kuandika vitabu vitano vya kwanza vya Musa kwa sababu wakati unanodaiwa kwamba Musa aliandika, suala la kujua kuandika na kusoma lilikuwa bado halijafahamika. Lakini sasa Akiolojia3

iligundua hapo baadae katika utafiti wa Historia ya zamani kwamba walikuwepo watu wa kipindi cha Musa walioitwa wa-Hamurabi na mabaki ya baadhi ya maadhishi yao yanasemekana kuandikwa miaka 1700 K.K; yalipatikana na hivyo suala la uandishi wa vitabu Vitano vya sheria lisingalikuwa changamoto kwa Musa aliyeandika kitabu cha Mwanzo miaka 200 baadaye (mwaka 1500 K.K)

Kama umepata bahati na fursa ya kuisma Biblia, utakuwa wakati Flani umekuatana na watu wanaoitwa Wahiti, ambao Biblia imewarejea mara 40. Watu wanaotafuta kuikosoa na kuipinga Biblia walidai kwamba hapakuwahi kuwa na taifa hilo wala jamii ya watu

hawa katika Historia ya Dunia. Mwaka 1906 Hugh Winckler aliugundua mji Mkuu wa Wahiti ulioitwa Boghaz-Koi na pia akavumbua maelfu ya maandishi waliyoandika Wahiti,5 nataka tu kukwambia kukuhakikishia kwamba Imani tuliyonayo katika maandiko haya haikujengwa juu ya visa mkasa au hadithi za kubuni. Ni matukio halisi kabisa ambayo moja kwa moja yanahusiana na maisha yako mwanadamu uliyepata neema ya kusikiliza Neno la Mungu katika wasaa huu.

Ndiyo maana Yohana anazungumza katika

2Don F. Neufeld and Julia Neuffer, Seventh-day Adventist Bible Student's Source Book, Commentary Reference Series

(Washington, D.C.: Review and Herald Publishing Association, 1962).

3

Inc Merriam-Webster, Merriam-Webster's Collegiate Dictionary., Includes Index., Eleventh ed. (Springfield, Mass.: Merriam-Webster, Inc., 2003).

5 Ibid., p. 85.

2 Tim 3:16Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

1 Kor 14:32Na roho za manabii huwatii manabii.

(3)

3. Unabii wa Biblia

Huenda kama kuna vitu ambavyo ingalikuwa muhimu sana kuvifahamu kuihusu Biblia ni jambo Unabii maana huu ni ushahidi wa wazi kabisa na usio na kipingamizi. Ngoja tuone kidogo Neno hili linavyotumika katika Biblia. Yule aliyekuwa muwasilishaji wa Neno la Mungu aliitwa Nabii.

a.

ה ֶאֹר

ebr [ roeh]Mwonaji: Hii ilishughulika na jinsi nabii alivyopokea kile alichopaswa kuwasilisha kwa watu wa Mungu. Ni jina lilimaanisha kwamba kile alicholeta haukuwa ubunifu wake bali alikipokea kuoka kwa Mungu

b. προφητεία

grk

[ profeteia] kuusema ujumbe wa Mungu; kuwasilisha tamko lenye uvuvio wa Mungu.

Hili jina lilifafanua kazi ambayo alikuwa nayo yeye abebaye ujumbe wa Neno la Mungu na kuufikisha kwa watu wa Mungu. Ni jina lililomaanisha kwamba kile alichotamka na kusema nabii Sharti kiwe kimetoka kwa Mungu.

Neno unabii katika lugha ya kiyunani (ambayo ilitumika pia ktk uandishi wa Biblia) linamaana ya mtu anayezungumza kwa niaba ya mwingine. Ndiyo maana Haruni anaitwa nabii wa Musa katika kitabu cha

Kwa hiyo unabii kwa maana hiyo haujafungwa na kipengele kimoja cha kuhusika tu na mambo ya utabiri wa baadae; inaweza ikawa ni kutangaza Neno la Mungu lilizongumzia wakati uliopita, linalozungumzia wakati uliopo na pia linalozungumzia wakati ambao bado haujatimilika. Kwa hivyo basi Biblia yote ni unabii (kila aya, sura na kitabu; maana manabii walileta kile Mungu alichowataka kuleta, walinena kwa niaba yake Mungu).

Lakini basi mara nyingi tunapozungumza habari za unabii, tunazungumzia habari za utabiri wa mambo ya huo mbeleni ambayo bado hayajatokea. Ukweli wa mambo ni kwamba, unabii nija kati ya vitu vinavyothibitisha kwa wazi kabisa kwamba Biblia ni Neno la Mungu. Na aliyeongoza uandishi wa Biblia ni Mungu ambaye peke yake anajua kila kitu: anajua mambo ya sirini kama anavyoyajua yale ya wazi, anayajua ya gizani kama anavyoyajua yanayofanyika nuruni, anayajua yale yatakayokuwako katika miaka maelfu huko mbele kama anavyoyajua yale ya jana na leo. Na hivyo anapoutia unabii katika Biblia, anakusudi tu la kumsaidia mwanadamu kuelewa kwamba Biblia imetoka kwa Mungu, kwani hakuna mwingine tena mbinguni au duniani au majini chini ya dunia, awezaye kutoa habari za hapo baadaye ambazo hazijakuwako

bado, isipokuwa Mungu ajuaye mambo yoye peke yake amemfunulia habari hizo.

Na sasa kwa nini Mungu anatia unabii ndani ya Biblia? Kwa nini asingalitoa tu maelekezo moja kwa moja?

Leo hii watu wamekuwa wakienda kwa waganga, wamekwenda kwa wachawi, wamekwenda kwa hao wapigao ramli na wasihiri na washihiri au kwa mababu na dnugu waliokufa huko zamaini, eti, ili kupata habari za maisha yao ya hapo baadaye. Lakini ni kwa sababu aidha wamesahau au hawajui au wamepuuzia sehemu 1,239 zenye utabiri ambao unahusu maisha yetu ya leo katika sehemu ya Biblia inayoitwa Agano la Kale. Aidha pia wamesahau au hawajui au wamepuuzia sehemu 578 zenye utabiri kuhusu maisha yetu sisi wanadamu katika Agano jipya. Jumla kuna sehemu 1,817 ambazo Biblia imetoa unabii kuhusu maisha yetu.

wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.

Kutoka 7:1 Bwana akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako.

Isaya 41:23 Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu; naam, tendeni mema au tendeni mabaya, ili tujipime, tukaone pamoja.

(4)

Mungu alitupatia ushauri wa bure kabisa kuhusu hasa kwa wale ambao wanataka kupata habari flani zinazohusu maisha haya:

Wapendwa Mungu amenituma kuja katika viwanja hivi ili tu niwatangazie kwamba Mungu amechora mpango wa hatima ya maisha kila mmoja wetu anayesikiliza maNeno haya, na hivyo usitumie gharama sana kutafuta tafuta nini kitakachotokea hapo baadae. Na katika hili ametupatia mwongozo na ametupatia ishara itakayotofautisha miongozo mingine usuyokuwa ya kuaminikana ishara hii ni si kitu kingine ni unabii.

- Unaweza ukawa gizani na umepoteza tumaini, ukawa ktk hali flani ambayo huoni kama kuna nuru ya faraja mahali popote na kila unayemgeukia unaona kama hana msaada kwako. Kabla hujaenda kwa

mganga na wachawi na hao wanaonong’ona kama ndege igeukie Biblia maana Mungu anaompango kwa kila mwanadamu ndani ya Neno lake, Biblia. Kama pasingelikuwa na mpango na maisha yeyu au kama angalikuwa hajali, asingetupatia utabiri wa matukio ya siku za usoni katika Biblia; hili Neno la Mungu lipo kwa ajili ya kukutia nguvu na kuyaongoza maisha yako.

- Ngoja tufafanue hii aya kwa undani kidogo. Anamaana gani anaposema shauri lake litasimama? Na kwamba atatenda mapenzi yake yote? Mahali flani nimesikia watu wakidai kwamba Biblia ni kweli ilikuwa Neno la Mungu hapo kwanza, lakini eti hapo baadae ilitiwa mikono (yaani iliingizwa mawazo ya kibadamu na hivyo basi Mwenyezi Mungu akateremsha kitabu kingine kupitia mtume mwingine). Nataka niwaeleze waziwazi kabisa kwamba Mungu hafanyi vitu vya bahati na-sibu.

Ikiwa Mungu angelizungumza kitu na ashndwe kukilinda mpaka hapo kitakapotimia, basi asingekuwa Mungu wa kutegemewa. Kusema kwamba lile alilosema limechafuliwa na kuchakachuliwa, ni kudhalilisha uwezo wa Neno la Mungu. Kama kungekuwa na mamlaka au uwezekano mwingine ambao ungeweza kupambana na Neno la Mungu mpaka Mungu afikie mahali pa kubadilisha alichosema kwanza na kuleta kingine basi asingalikuwa mwenye nguvu, lakini sasa alikwisha kusema tokea hapo awali kwamba Neno lake halitapita kamwe

Watu wameipiga vita, mitandao imejaribu kuichafua Biblia, baadhi ya wanasayansi wamejaribu kuipinga, Ibilisi amewaua wengi waliosimama kuutetea unabii wake, wahubiri wengi waliohuiri kweli zake wamepalekwa magerezani, chuki nyingi za wanadamu na Ibilisi zimedhihirika juu ya Biblia lakini bado imeendelea kusimama na itaendelea kusimama milele na milele

Math 24:35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maNeno yangu hayatapita kamwe.

John 10:35 …… maandiko hayawezi kutanguka

Mtu anaweza leo hii akasema anakupenda na kesho akageuka kuwa mtu mwingine

Mtu anaweza kuapa kwa maNeno yake mwenyewe na kesho akashindwa kuishi kama alivyoapa Mtu anaweza kutoa ahadi kwa hiyari yake mwenyewe kesho akashindwa kuitimiza

Upendo wa kibinadamu huja na kutoweka Mali na pesa huja na kutoweka

Teknolojia huja na kupitwa na wakati

Elimu dunia huwa na maana lakini mtu huzeeka na kushindwa kuitumia tena Lakini Neno la Mungu pekee litasimama milele na kamwe halitapita

Pepo zitavuma, tufani na ije, mawimbi na yavume sana, lakini Neno la Mungu, Biblia takatifu itasimama milele na milele. Neno la Mungu wapendwa, halitapita kwa sababu Mungu anayetaka wanadamu wafaidike nalo, atalilinda dhidi ya upinzani wote na hila zote za Ibilisi. Kwa nini? Kwa sababu hili lina umuhimu mkubwa sana

Isaya 8:19,20 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na Neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.

Isaya 46:9,10 maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

(5)

o Is 40:8 Neno lake litasimama milele

o Matt 24:35 Neno lake halitapita kamwe

o 2 Pet 1:21 Neno hili halikuja kwa mapenzi ya wanadamu

o Prov 30:5,6 Neno hili Limehakikishwa... na ameonya yeyote asije akalibadilisha

o John 6:63 Neno hili linao uzima ndani yake

o John 17:17 Neno lake ni kweli nalo hutakasa

o Heb 4:12 Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho

Na kwa makusudi hayo wapendwa, Mungu hatoacha Neno lake lipotee wala hatokuwa na kigeugeu cha kuleta Neno jingine eti kwa sababu kuna nguvu inapambana na Neno lake.

WITO

Mawazo ya Wanadamu walio wengi wa sasa na jinsi mtazamo wao juu ya mamlaka ya neno la Mungu maishani mwao

- Wanamashaka na kila kitu, mpaka neno la Mungu: Mwisho kila mtu anasema nitaishi ninavyoona au ninavyota na mtu asiniiingilie mambo yangu.

- Hakuna ukweli kweli-kweli: ukweli ulionao wewe si lazima niwe nao mimi. Kila mtu anaimani yake mwenyewe, tusifatiliane.

- Mtazamo Binafsi; Kile ambacho naona ni sahihi ni sahihi usiniingilie maisha yangu. Wewe ishi maisha yako na mimi niishi maisha yangu.

- Unawezakuitafsiri Biblia jinsi unavyotaka au unavyojisikia. - Hakuna (Meta-narrative)

Katika mikutano hii wapedwa ni vema tukafanya uamuzi jioni ya leo kutembea kwa Neno la Mungu na Neno lake pekee. Hatuwezi kutumaini maneno ya wachungaji, hatuwezi kutumaini maneno ya padri, hatutaweza kutumainia maneno ya mwinjilisti, wala kamwe hatutatumainia Neno la shehe au kiongozi yeyote yule wa kidini. Hatutatumainia maamuzi yaliofanywa na kundi flani la wanadamu waliojiita wenyewe mamlaka ya kanisa yenye uwezo wa kufanya maboresho ya Neno la Mungu. Kwa mtindo huo hatuwezi kuufikia ukweli. Wanaweza kuwa na maNeno ya kuvutia sana yenye hekima ya kibinadamu na amaarifa ya ulimwengu huu. Wanaweza kuwa na msamiati na lugha iliyopangiliwa vizuri na mvuto kwa jamii lakini pamoja na hayo hawataweza kuwa na busara ya kutosha kumuongoza mwanadamu kwa maNeno yao na maamuzi yao ambayo hayatokani na Neno la Mungu.4 Katika mikutano hii, kila Neno, kila fundisho, kila wimbo, kila onyo, kila karipio, kila maelekezo na kila sehemu itakapoonekana tumekosoa jambo flani, ni kwa sababu tutakuwa tumesoma katika Neno la Mungu ili kuwaandaa watu wa oldonyosambu kwa ajili ya uzima wa milele. Mungu awabariki na karibu tena katika siku ya kesho ili tuendelee kupata baraka za mikutano hii.

Referensi

Dokumen terkait

Kwa mujibu wa Nadharia ya Fasihi Linganishi, mtafiti amebaini kuwa katika riwaya ya Utengano, wanawake walikuwa ni tegemezi zaidi kwa wanaume tofauti na riwaya ya Kamwe si mbali

Katika tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani, utafiti huu ulichunguza na kubaini jinsi wasanii wa tamthiliya hizi teule walivyotumia vipengele vya

Taasisi ya Elimu Tanzania (1996) inaeleza kuwa, Sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya matamshi ya maneno, maumbo ya maneno, miundo ya tungo na maana

a) Kuhusu lengo la kwanza la utafiti lililotaka kubainisha tofauti baina ya fonimu za Kipemba na Kitumbatu utafiti huu umebaini kuwa, kuna muachano wa kifonimu, kwa

Kwa kuwa maadili hujikita katika uhusiano wa mtu na mtu, mtu na jamii yake, au mtu na mazingira yake, na kwa kuwa uhusiano huo humfanya mtu kuishi vema na jamii yake, mtafiti

Mang’ombe (ng’ombe weng) Hili ni jina analopewa mtoto wa kiume na wazazi wake kama kiashirio cha kuwa mtoto huyo ametoka katika familia. ambayo ni wafugaji wakubwa wa

Katika jamii ya wajita, majina ya asili hutolewa yakiwa na lengo la historia na matukio mbalimbali yaliyotokea kwa mtu mmoja mmoja au jamii, kwa mfano jina Nyabhita

yao toka siku hata siku... Watembelee mara kwa mara washiriki wapya majumbani mwao. Waalike katika familia ya kanisa lao na jitolee kujibu maswali yoyote yale