• Tidak ada hasil yang ditemukan

SEMINA KWA AJILI YA WAZEE WA KANISA

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "SEMINA KWA AJILI YA WAZEE WA KANISA"

Copied!
15
0
0

Teks penuh

(1)

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO

NORTH

EAST

TANZANIA

CONFERENCE

SEMINA KWA AJILI YA WAZEE WA KANISA

MTAA WA MUHEZA

Pr. Almodad Amos

E-mail:

Phone no:

(2)

2 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Asante kwa kuhudumu ukiwa kama Mzee wa kanisa mahalia popote ulipo. Kanisa lako limekupatia majukumu yatakayohitaji maombi muda, juhudi, uvumilivu na wakati mwingine hekima ya Sulemazi. Ikiwa unahisi kuwa na hofu hiyo ni hali ya kawaida kabisa.anguka magotini na umgeukie Mungu. Yeye anatawala na atakutumia ikiwa ataruhusiwa kufanya hivyo.

Kabla hujaanza kuhudumu, nivizuri kuyajua majukumu yako na mamlaka ya kiblia inayojenga hitaji la Mzee wa kanisa katika kanisa. Huu mwongozo umetengenezwa ili ukufahamishe kazi na majukumu yam zee wa kanisa. Kwa nyongeza, utakuwa na wakati mzuri wa kuyatazama makujumu yako ktk jamii utakayoiongoza na utaona ni jinsi gani unaweza kutimiza mahitaji ya wanafamilia wa kanisa unaloliongoza

Kazi a uzee wa kanisa na ichukuliwe katika hali ya kawaida. Biblia inatupatia maelekezo mahususi juu ya majukumu na kujiweka wakfu juu ya kazi ya uzee wakanisa, na kile ambacho Mungu anatarajia kwa wale wanaowekwa kusimamia nafasi hii. Hii si aina ya kazi ambayo inakutaka tu uonekane kila sabato asubuhi kuwaita watu kuleta sadaka, au umtambulishe muhutubu, inahitaji ujitoe kikamilifu katika muda wako binafsi. Kazi hii inamuhitaji mtu aliyeamua kwelikweli, makubaliano baina yako na wale unaowaongoza pamoja na usri mkubwa katika baadhi ya mambo makubwa yatakayolihusisha kanisa na waumini wake.

Unapoendelea kujifunza mwongozo huu, unaweza kujenga hitaji la kutaka kujua Zaidi na zaidi. Utaweza kupata ufafanuzi Zaidi katika Mwongozo wa kanisa la Waadventista Wasabato (Kanuni ya kanisa) na Kitabu cha wazee wa kanisa la Waaventista Wasabato. Hivi vinapatikana katika maduka ya vitabu ya ABC. Kama Mzee wa kanisa lazima ujifunze na kuelewa utume wa kanisa lako, kazi zako na muundo wa uongozi pamoja na ngazi zake katika kanisa la Waadventista Wasabato.

(3)

Biblia Inasema nini juu ya wazee wa kanisa?

Katika agano la kale, neno Mzee linamaana Zaidi ya mtu aliye na umri mkubwa sana; inaweza pia kuwa mtuambaye amefikia kiwango flani cha utu uzima, uzoefu na hekima. Kwa ujumla, neno Mzee linasimama kwa jili ya mtu ambaye ni kichwa cha familia au ukoo.

Mungu alipouumba ulimwengu, aliweka pia namna flani za uongozi katika jamii ya watu wake. Katika nyakati za Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Mungu alitumia mfumo wa wazee kama msingi wa usimamizi wa ibada katika familia. Alitoa maelekezo ambayo yako wazi kabisa juu ya utoaji wa kafara na kile zilichowakilisha.

Kadri vizazi vilivyoendelea kusogea, Mungu aliwaita watu wake kutoka katika nchi ya utumwa na kwenda nchi ya ahadi. Katika kipindi hiki, Wana wa Israeli waliitwa kushuhudia upendo wa Mungu na ahadi zake za kweli.

Hata hivyo Mungu alikua amemchagua Musa kuwa kiongozi wa kundi na kuwatoa Misri, hata hivyo ilionekana kwamba ugawaji wa majukumu ktk kazi ni jambo ambalo linaongeza ubora wa kazi. Jethro, Baba mkwe wa Musa, alionyesha hekima na uzoefu alipomwambia Musa, “maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. Utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.” (Kutoka 18: 17, 21-23).

Kisha Bwana akamwambia Musa, “Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe.Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako.” (Hesabu 11:16, 17).

Katika agano jipya, neno lililosimama kwa nafasi hii lilikua Mzee, askofu na mwangalizi. “Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.” (Matendo 14:23 NIV). Baada ya haya aliwaacha waingie shambani kwa ajili ya kazi

Kwa kweli, baada tu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, Mungu aliwaita tena watu wake kwa mara nyingine, safari hii wayahudi na wayunani, kuwa jamii moja ya waumini. Wakati huu pia alitoa maelekezo juu ya nafasi na majukumu ya viongozi.

(4)

4 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Wazee katika Historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato

Kanisa la Waadventista Wasabato liliiweka nafasi ya oungozi wa wazee mapema katika historia yake. Jamii ya kwanza ya waumini walichagua mashemasi tu, lakini hili lilibadilika mwaka 1861. Baada ya kujifunza kwa umakini, viongozi wa kanisa walitamka kwamba, muundo wa wazee wa kanisa na mashemasi ulikua ni muundo wa kibiblia.

katika Muundo wa kanisa la Waadventista Wasabato, ikiwa kanisa halijapewa mchungaji wa kanisa au mtaa na Konferensi, Mzee wa kanisa atatimiza mahitaji ya kichungaji katika kanisa mahalia, ikiwa ni pamoja na kutembelea, kuhubiri, uinjilisti pamoja na maswala ya kiutawala.

Kunapokua na hitaji la kuamua kufanya kazi flani makini, Mungu huchagua

wanaume na wanawake kuifanya kazi yake, na ndipo itaonekana hasara ikiwa

talanta zao hazitaunganishwa.

(Evangelism, Uk 469)

SIFA ZA MZEE WA KANISA

Ili kibaraza kidogo kimchague mtu katika nafasi ya uzee wa kania, kuna vigezo muhimu sana vya

kuangali. Vigezo hivi ni pamoja na:

1. Ajitoe kikamilifu kwa Mungu na kwa kuwatumikia wengine.

2. Kuwa na uhusiano unaokua baina yake na Yesu. Hali yako ya kiroho si jambo linalojitokeza kila asubuhi ya sabato tu unapotaka kwenda kanisani.

3. Pamoja na kuwa tayari kuutumia muda wako; unatakiwa kuweka uwiano katika mambo ya kanisa, familia na ajira yako binafsi. Utatakiwa kuwa na muda wa masaa 2 – 4 katikati ya juma ukikamilisha majukumu yako ya uzee wa kanisa.

4. Hutakiwi kuongea kinyume na kanisa, na kinyume Imani za msingi, kinyume na viongozi wako na kinyume na taratibu za kanisa. Uongozi wako wa mambo ya kiroho ujengeke juu ya Yesu Kristo na katika Biblia.

5. Hakikisha kuwa tabia za wanafamilia zinaaksi uhusiano wako na Kristo

(5)

7. Ukijua kuwa Mungu aliwaumba na anawapenda wanadamu wote wasa. Kama watu tunaomuaksi hatuna la kufanya isipokua kuwapenda watu wote kwa usawa.

8. Kurudisha zaka kwa uaminifu na

kuiungamkono kazi ya utume kwa michango mbalimbali, kwa banisa mahalia na kimataifa pia.

9. Kiri dhambi na makosa yako. Kuwa kiongozi muwazi na mfano kwa kanisa lako.

10. Kuwasuluhisha waumini penye migogoro na hata uongozi pia. Unaliweza hili ikiwa tu utajenga mahusiano na waumini pamoja na kuwaombea. majukumu yote ya kanisa na hata utendaji wa shughuli za kikanisa. Wazee husaidia katika kutoa njizi za kanisa na katika utekelezaji wa utume wa kanisa katika jamii.

Kushiriki ktk vikao ni moja tu kati ya majukumu yam zee wa kanisa. Wazee wote ni sharti wahudhurie vikao vya baraza la kanisa, na halimashauri za kanisa zima. Kwa nyongeza, wanaweza kuombwa kuhudumu katika baadhi ya kamati zinazowekwa na kanisa mahalia.

Sifa za Mzee wa kanisa

1.

Uhusuano binafsi na unaokia baina yako na

kristo.

2.

Anachaguliwa na kuwekwa madarakani na

kanisa mahalia.

3.

Anaheshimika sana na analiunga kanisa mkono

pamoja na mafundisho yake makuu.

4.

Anazosifa za uongozi na utawala

5.

Awe tayari kutuia muda na talanta

6.

Awe na unyenyekevu wa mtumwa, ajue kuwa

watu wote ni sawa.

Kazi za Mzee wa kanisa

Wazee wataitwa kuhudumu katika shughuli

mbalimbali za kanisa. Hii ni pamoja na:

o

Uongozi na utawala wa kanisa mahalia

na pia kutumia karama za roho.

o

Kuliongoza kanisa katika uinjilisti

o

Kushiriki katika vikao vya kanisa

o

Kudumisha ushirikiano wa mchungaji

na Mzee wakanisa

o

Kuandaa washiriki ili wawe

viongozi wazuri baadae

(6)

6 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Katika kamati hizi, Mzee anakua na fursa ya kuwasaidia washiriki kuboresha huduma za kiinjilisti kwa jamii. Kama Mzee, ni lazima uwe na uelewa wa uongozi wa kanisa. Tambua majukumu ya viongozi wenzako kama karani wa kanisa, muhazini, shemasi, huduma binafsi, shule ya sabato, nk.

Nidhamu Ya Kanisa

Kwa kuwa tunaishi katika ulimwengu wa dhambi, inatulazimu kuwa na taratibu za kinidhamu kanisani. Elewa kwamba nidhamu ni jambo la muhimu sana ili kudumisha uadilifu wa waumini na kulifanya kanisa kuwa bora. Kama Mzee ni lazima utambue hatua mbalimbali za kinidhamu, ikiwemo kumpa mtu karipio na kumfuta mtu ushirika. Kumbuka kuwa utahusika sana na mambo ya watu binafsi, nay a siri ambayo yanatakiwa kubaki katika usiri wake. Utatakiwa kuhusika na wazee wengine katika maombi pale utakapo kabiliana na maamuzi magumu ya kuishughulikia dhambi kwa mujibu wa biblia na katika hali ya upendo mwingi. Kumbuka kwamba: kushindwa kumwadhibu mtu inaweza kumpeleka mbali na Mungu wake kuliko kama ungelimwadhibu mtu huyo.

Kuweka Mikakati

Kanisa linapokua na njozi ya mpango mkakati wa muda mrefu kwa jamii, inawasaidia kuweza kuanzisha huduma mbalimbali na shughuli za kiinjilisti zitakazowaleta watu kwa Yesu. Wazee husaidia kupangilia hii mikakati.

Mpango mkakati kwa mwaka uzingatie mambo yafuatayo kwa umakini mkubwa:

1.

Uinjilisti

– Kanisa lako litafanya nini kueleza juu ya kisa cha ukombozi mwaka huu? Je,

mtakua na majuma kadhaa ya mikutano ya injili? Je, washiriki watafundisha masomo ya Biblia? Je, shabaha yako ni watu wa kundi flani au umri flani? Utawezaje kufanikiwa kuifikia jamii yako kiinjilisti?

2.

Malezi

– unapopangilia uinjilisti, usisahau kwamba unatakiwa kuwa na malezi kwa washiriki

na waumini wapya katika familia ya kanisa lako. Utafiti unaonyesha kwamba washiriki wapya ni lazima wapate marafiki sita katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya ubatizo, vinginevyo watarudi tena nyuma.. kumbuka kulitangaza hili kila mara mtu anapobatizwa au anapopokelewa katika ushirika. Uwe na mkakati mapema kabisa wa kuwalea na kuwatunza washiriki wapya kabla hawajajitokeza. Tafakari yafuatayo: je kanisa lako linahitaji kamati ya malezi ya waumini? Je, utawapaia (washiriki wapya) walezi? Utahakikishaje kwamba mzunguko wa marafiki wao kanisani unakua? Pamoja na kuwalea waumini wapya, kanisa lako ni kwavipi litawafikia washiriki wa muda mrefu kanisani? Je, unampango wa kuwatembelea waliorudi nyuma, wasiojiweza, wagonjwa na wasiohudhuria kanisani? Je, utafanya nini kukidhi mahitaji ya watu walio katika jamii yako, kwa mfano wazazi wasioishi na wenzi wao, wasio na kwao, watoto wa mitaani? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wapya waliohamia katika kanisa lako kupata ushirika au kuhamisha ushirika wa walioondoka muda mrefu?

3.

Vijana

– hii ni sehemu muhimu sana ya kuandaa na kutayarisha kanisa la kesho. Fanya kazi

(7)

kuwaacha wapangilie mambo mazuri katika nafasi za uongozi wao, katika huduma zao ili wakuze ujuzi wa taaluma ya uongozi.

4.

Wanafunzi wa vyuoni

– hakikisha unawatambua wanafunzi vya vyuoni na unawajali. Ikiwa

unawanafunzi

ambao wanakwenda katka vyuo vya mbali na nyumbani, je, kama kanisa

mnawatumia ujumbe kwamba

kuonyesha umuhimu wao?

Mnaweza kuwa na utaratibu wa kuhakikisha wanapata miongozo ya kujifunzia Biblia, na matoleo mengine kutoka kanisani. Uwaalike kushiriki uzoefu wao chuoni wanaporejea (Watoe huduma). Tafuta namna ya kuwashirikisha katika shugnuli za kanisa, wanaporejea nyumbani

Je, kuna wanafunzi wanaosoma vyuo vya serikali karibu na wewe? Ikiwa ni hivyo, je, unakidhi mahitaji yao? Wako mbali na nyumbani, na wangependa kushiriki chakula cha nyumbani, je mnawajali angalau hata kwa hilo?

Makundi ya kulea (

Wanaosahaulika

):

• Washirki wapya waliobatizwa

• Wazazi walioachana na wenzi wao

• Wasio na watoto

• Watu walio katika wakati mgumu

• Wastaafu

• Wafungwa

• Wasiohudhuria

• Wahitimu

• wanafamilia wapya

• Wanafunzi wa vyuoni

(8)

8 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Wanafunzi Waadventista katika vyuo hasa vya serikali, wanakumbana na changamoto za kufanya kazi Ijumaa jioni na siku ya sabato. Na mara nyingi mabweni yao na mazingira yao si mazuri sana kwa utunzaji wa sabato. Je, kuna namna ambayo kanisa lako laweza kuleta tofauti kwa ajili ya hali hii?

Jaribu kulitumia kundi hili katika shughuli za uinjilisti. Wanafunzi wa vyuoni wanapenda sana kuulizwa na kushirkishwa kimawazo. Wasikilize na wapatie

Nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo. Wanajua kile kinachoendelea na wanaweza kushiriki katika kuwafikia wengine.

5.

Vijana Wakubwa

– hili kundi mara nyingi hupuuziwa na halitumiwi. Kwa ujumla hawa wanaumri wa watu waliomaliza vyuo; wanatafuta kazi ya kufanya, na wanajaribu kutulia katika jamii na katika kanisa pia. Wanapenda wapewe majukumu na nafasi za uongozi kanisani lakini hawajui waanzie wapi. Kama kanisa likiwatia moyo na kuwatambua itasidia kuonyesha umuhimu wao katika kanisa. Watalifanya kanisa lako likue na liwe moto moto.

6.

Vifaa vya kanisa

– Ni vizuri kulichunguza jengo la kanisa kila mwaka. Kila kinachohitajika kurekebishwa na kirekebishwe: Kapeti, rangi, maliwato, vyoo, n.k. Je, kuna mambo makubwa yanayohitaji kujadiliwa? Ikiwa ndivyo bajeti yake itakua je?

7.

Kalenda kuu ya kanisa

– hii inalisaidia kanisa kuona matukio makuu ya mwaka. Itasaidia pia, maidara kujipanga kuunga mkono shughuli mbalimbali za kanisani na kijamii pia.

8.

Misisitizo mikuu

– Jaambo gani hasa umgependa ulisisitize katika kwaka – uwakili, michango ya ujenzi, au mikutano ya injili? Nani ataongoza kamati hizi? Je, matukio haya yameingizwa kwenye kalenda kuu ya mwaka? Kumbuka matukio makuu mawili hayawezi kugongana kwa siku moja hiyo hiyo. Hii inaweza kufanya mambo yasifanikiwe au yafanyike kwa viwango dhaifu sana.

Kuongoza Huduma za Kiibada

bada ni jambo muhimu sana katika maisha ya kanisa lolote. Ili ibada imtukuze Mungu, lazima kufikiri vizuri na kupangilia jambo hio kwa ustadi mkubwa. Hii haina maana kwamba Mzee wa kanisa apangilie kila kitu mwenyewe, lakini anapaswa kuwasaidia wale ambao wanahusika katika kupangilia huduma za ibada.

(9)

Kutembelea

Moja kati ya majukumu ya Mzee wa kanisa kibiblia, ni kujenga mahusiano na watu wa kanisani na jamii kwa ujumla. Hili si jambo linaloweza kufikiwa kwa mtu kuongea na washiriki kila siku ya sabato kwenye shule ya sabato au kusalimiana nje tu ya jingo la kanisa.

Utembeleaji ni jambo linaloonekana kufifia. Wazee wanaweza kuwa mfano kwa kuweka mfano wa kutembelea watu. Shirikiana na mchungaji na viongozi wengine kuweka

Ikiwa kuna watu ambao wamehitaji kujifunza Biblia, je, kanisa linawatembelea watu hawa? Wanaweza kupoa na kupotea ikiwa kanisa halitajali kabisa.

Tumia mida huu kujenga urafiki na kutambua mahitaji yao ya kiroho. Unapowatembelea watie moyo, na uwaunge mkono. Usiruhusu muda wote utumike kwa kujadili jambo flani ambalo ahaliko sawa kanisani, kumjadili mchungaji au kiongozi flani. Fanya jambo hili kuwa jema na fupi.

Ikiwa inadhani kuna haja ya kumtembelea mtu kwa muda mrefu, weka mpango ili ajiandae na umjulishe mapema kabisa.

Mambo ya kuzingatia kwa mahubiri

Ukiwa mzee wa kanisa, tarajia kwamba mara kadhaa

utaombwa kutoa huduma ya mahubiri sana. Ikiwa

unadhani unahitaji msaada juu ya hili, muone

mchungaji wako na ikiwezekana akupatie kozi ndogo

ya jinsi ya kuandaa mahubiri. Tumia muda wako wa

maandalizi katika maombi, ukimwomba Mungu

akusaidie kuupata ujumbe. Hii sio ajenda yako, ni

ajenda ya Mungu kutaka kukutumia ili uwalete

wengine kwa Yesu.

Lipitie hubiri lako kabla ya sabato asubuhi. Jinsi

unavyotumia muda wa kutosha kufanya marudio,

ndivyo utakavyojiona umekua tayari. Hii itakusaidia

kulitoa somo lako kwa kujiamini na kwa usahihi Zaidi.

(10)

10 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Kwa sababu ya ratiba ngumu za siku hizi, wakati mwingine ni vizuri kutumia hata

simu zetu. Jambo hili lisitumike kuwa mbadala wa matembezi ya nyumbani,

inaruhusiwa kulifanya hili mara kadhaa ukiwa nyumbani. Hapa kuna mambo

machache unayoweza kufanya kwa kupitia simu:

1.

Piga simu

.

Kijatambulishe vizuri na mjulishe kwamba wwe ni Mzee wa kanisa.

Waambie kwamba wazee wanawapigia washiriki wote simu ili kuwajulia hali na

maendeleo yao kiroho.

2.

Onyesha urafiki

.

Onyesha kuwajali na kuzijali familia zao.

3.

Zungumza mambo mazuri

.

Zungumziamambo mazuri

yanayotokea kanisani na waulize jinsi Mungu anavyowabariki

4.

Mambo Binafsi

.

Ikiwa mazungumzo yataelekea kwa mshiriki

kumlaumu mshiriki mwingine, mshauri kwanza aende

akamuone mshiriki huyo, kwa mujibu wa Mathayo 18:15-17.

5.

Kushughulika na maombi (Matakwa ya mtu

)

.

Ikiwa mtu ataomba jambo flani

lifanyike, mwambie kuwa utalifuatilia na kurejesah majibu kwake haraka

iwezekanavyo. Hakikisha unawarejeshea majibu haraka iwezekanavyo.

6.

Kumbuka kuwa msiri mara zote

.

Ikiwa mshiriki amekueleza jambo lake la siri,

usisahau kwamba umefungwa na kukuamini kwake kutokumweleza mtu

mwingine yeyote juu ya jambo hilo. Ikiwa unadhani kwamba ni jambo linalohitaji

utaratibu wa sharia za kikanisa, wasiliana na mchungaji wako ili akueleze jambo la

kufanya

7.

Hakikisha unapatikana

.

Wafahamishe kwamba unaweza kuwatembelea muda

wowote ule nyumbani. Wapatie namba yako ya simu.

(11)

Kuwaandaa Washiriki Kuwa Viongozi

Kuwaanda waashiriki kuwa viongozi wa baadae ni moja kati ya

majukumu ya Mzee. Hii inahusika na kuwaimarisha kiroho,

kuwaleta watu kwa Yesu na kuwafundisha kuzitumia karama zao

za roho kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbai kanisani.

Wasaidie washiki kuzitambua karama zao za roho na wasaidie

kujua wapi na jinsi gani karama zao zinaweza kutumika ktk huduma. Msaidie kila mshirki kujifunza

Zaidi juu ya hizi karama za roho na uwatie moyo kufahamu namna bora ya kuzitumia katika utumishi

wao. Wapatie nafasi ya kutumika kama viongozi katika nafasi mbalimbali ili kanisa itambue kuwa

lnaweza kuwa na viongozi wanaohitajika kabisa.

Inashauriwa kwamba viongozi wa kike wawafunze viongozi wa kike huku wale wa kiume wakifunzwa

na viongozi wa kiume. Nafasi ya Mzeee wa kanisa iheshimikena yasiwepo matendo yoyote yale

yanayoonyesha matumizi mabaya ya nafasi hiyo au ulegevu wa namna yoyote katika kazi hii.

Kunawakati utahitajika kutoa ushauri kwa mshirki wa kanisa mwenye jinsia tofauti. Kudumisha uadilifu wako wakati wa kutoa ushauri ni jambo la muhimu sana. Viongozi hawapangi kabisa kuanguka katika mitego ya yule mwovu lakini mara nyingi inatokea kuliko tunavyodhani.

Tabia ya uasherati ni dhambi ambayo inaweza kukuharibu wewe, familia yako na kanisa lako pia. Tumia mwongozo huu ili kujepusha na hatari, na uwe mwangalifu kuchunguza mahali tatitzo lipoelekea. Usiruhusu aina yoyote ile ya tetesi kuvuma kanisani mwako na katika jamii yako.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kutoa ushauri:

1. Usijiweke mwenyewe katika hali ambayo watu hawatakuelewa vizuri. Ikiwezekana wanaume wapate

ushauri kutoka kwa wazee wa kanisa na wanawke wapate ushauri kutoka kwa mashemasi wa kike.

2. Usimshauri mtu mkiwa wawili peke yenu. Uwe na mtu flani karibu (Huyu anaweza kuwa ni kiongozi wako

mkubwa wa kanisa au mwenzi wako – mjulishe mtu aliye karibu na wewe kuwa mazungumzo hayo ni ya siri

ya hali ya juu sana.) au muwe katika mazingira ambayo ni wazi na watu wanawaona waziwazi.

3. Ushauri wenu huu uwakutanishe mara moja au mara mbili, isizidi muda wa saa moja. Ikiwa muda huu

hautawatosha mwelekeze aende kwa mchungaji wake au kwa mtaalamu wa ushauri.

4. Hakikisa mahusiano yako na Mungu wako yanakua kila siku. Huwezi kuisikia saiti ya Mungu ikiwa hutaki

kuzungumza naye.

5. Angalia viashiria vifuatavyo, ikiwa vinajitokeza, simamisha mazungumzo yenu na muelekeze kwa mtu

mwingine. Uko hatarini na unamuweka mtu hatarini ikiwa utajibu maswali yafuatayo kwa kuonyesha ukubali wako:

o Natzamia tutaendelea na mazungumzo haya? Usijali lakini jinsi nilivyovaa.

o Narekebisha ratiba yangu, angalau nipate muda wa kuonana na wewe tu. Sawa?

Hata awe ni mojakati ya viongozi wa kansia kuwa makini naye sana, jihoji:

(12)

12 Pr. Almodad Amos

Semina Fupi kwa Mzee wa kanisa

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

mchana?

Je, nimeanza kumpenda na kuvutiwa na huyu mtu?

Je, nimeanza kumficha huyu mwenzi wangu baadhi ya mambo ninayofanya pamoja au

ninayoshauriana na huyo mtu?

Je, nadhani siwezi kupoteza uaminifu wangu kwake?

Uasherati ni dhambi. Kama kiongozi unaomvuto kwa awtu na watu wanakutazama jinsi unavyoenenda matendo yako yataathiri watu flani katika umilele wao. Kuchagua kuwa msafi wa tabia inaaksi usafi wa tabia ya Mungu wako.

Mahusiano ya Mzee na Mchungaji

Kama Mzee, utafanya kazi yako karibu sana na mchungaji. Wakati mchungaji ni mwanadamu, kumbuka ametumwa na Mungu. Mchungaji hakuja kanisani kwako kwa mapenzi yake mwenyewe, lakini kwa kuchaguli na kutiwa mafuta na Mungu kupitia mpango uliowekwa na Konferensi. Mzee anawajibika kuiunga mkono ofisi ya mchungaji (Hesabu 12:1-10; Ebr 13:7, 17).

Muombee mchungaji na familia yake kila siku, na wajulishe kuwa unawaombea. Hili litakua jambo la kutia moyo sana. Huwezi kujua mzigo walionao ambao hawawezi kumwambia mtu mwingine. Tambua kwamba mchungaji anajua mambo mengi ya siri yanayoendelea katika

1. Iombee familia yake kila siku.

2. Uwe na urafiki na mchungaji wako kwa Zaidi

ya shughuli za kikanisa.

3. Muunge mkono hadharani. Kasha jadilini

tofauti zenu faraghani.

4. Hakikisha mchungaji wako anapumzika.

Hakuna mtu anayeweza kufanya vizuri ikiwa hana muda wa mapumziko.

5. Tambua karama za mchungaji wako na jazia

yale ambayo ni mapungufu yake.

6. Kumbuka hakuna anayeweza kufanya kila kitu.

(13)

Weka na jenga mahusiano ambayo ni Zaidi ya salamu za jumamosi asubuhi

tu. Tambua mambo ambayo mchungaji wako anayapenda. Tafuta namna

mnavyoweza kuzifanya familia zenu ziunganike katika mambo ya kijamii.

Mnapokutana katika mambo ya kijamii, achaneni na mambo ya shughuli za

kanisa, vinginevyo itawazuia kufahamina kwa kuwa mnamambo mengine ya

kikanisa yatakayowafanya msifahamiane.

Usimpinge na kumdhalilisha mchungaji wako hadharani. Ikiwa kunatofauti,

nenda naye faragha na uzungumze kile ambacho ni maoni yako. Kukosoana

hadharani kwa viongozi, kunaleta mpasuko kwa washiriki na huleta hisia

mbaya. Ikiwa waumini watakuletea tetesi juu ya mchungaji, usikubali kabisa.

Ikiwa wanamambo ya kukosoa juu ya mambo ambayo si ya-kikanuni waeleze

kwamba unamuunga mkono mchungaji. Wakumbushe kuwa ikiwa

wanadhani mchungaji amekosea kuna kanuni ya kibiblia ya Mathayo 18 ya

kutatuta tatizo lao. Waulize kama wameifuata kanuni hii na kama sivyo, basi

watie moyo kuifuata

Hakikisha mchungaji wako anamuda na familia yake. Ni jambo rahisi sana

kwa mchungaji kuiacha familia yake kwa sababu ya kazi za ufalme.

Elewa kwamba mchungaji naye ni mwanadamu na hawezi kufanya kila kitu

mwenyewe. Ndiyo maana viongozi wengine huchaguliwa ili wasaidie katika

kazi za kanisa. Muunge mkono na uwe tayari kufanya naye kazi.

Hitimisho

(14)

Maelekezo mafupi kwa wale wanaoanza kazi ya uzee wa kanisa

Maelezo ya Huduma ya Mzee wa Kanisa katika Kanisa Mahalia

Utangulizi

Mungu analitaka kanisa kuwa jamii ya watu wenye kusudi moja, ushirika, kukua wakati wote katika Imani na kumjua Yesu Kristo Mwana wa Mungu. Paulo analielezea kanisa kama “. . . mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote” (Waefeso 1:22).

Mungu anatuita katika mwili wake kwa kusudi la kuimarisha uhusiano kwa ajili ya kazi ya wokovu pamoja naye, na katika jamii kila mmoja kushughulikia wokovu wa mwenzake. Roho Mtakatifu huthibitisha fikra zetu, hutuongoza katika toba na kutusimamisha katika kanisa.

Ishara ya ubatizo wa maji inaashiria kuingia kwetu katika mwili wa Kristo na pia huashiria uzoefu wa ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa huyu mshiriki mpya. “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” (Yohana 3:5). Roho Mtakatifu ndiye ambaye ni siri ya uhai wa kanisa. Unapokuja kwa Kristo ni kwa sababu umeandaliwa na Roho Mtakatifu, whoambaye amekuongoza ktk toba ili uwe tayari kwa utumishi (huduma).

Kanisa linapouhudumia ulimwengu ni namna ya kuonyesha upendo wa Kristo kwa Ulimwengu huu. Ni kanisa linalotakiwa kuyafikia mahitaji ya jamii na kutumiwa na Roho Mtakatifu kama wakala wa wokovu. Kwa hiyo, kanisa ni kiungo kitumishi. Humtumikia Kristo kwa Kumsifu, na kumtumikia kwa kumuhudumia muumini, na pia huutumikia ulimwengu kwa unyenyekevu.

“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo” (Waefeso 2:10).

(15)

Kazi za Mzee wa Kanisa

Utumishi ambao mtu anaitwa kuufanya pale anapochaguliwa kuwa Mzee wa kanisa, unaweza kuelezwa kwa namna ifuatayo:

1. Kutembelea. Malezi yanalifanya kanisa likue, hasa washiriki wanapotiana moyo mmoja kwa mwingine. Katika jamii kama hiyo inayojali, hata Mzee wa kanisa anapewa huduma hiyo. Mzee wakanisa anaweza kuwa mtu wa muhimu sana katika kanisa kama hilo. Mzee awatembelee watu majumbani mwao, awatie moyo watu wengine kufanya hivyo, na awasasidie pia hata wale ambao si washiriki kujifunza kushiriki katika huduma hiyo. (Angaalia makundi ambayo hayana familia nayo pia uayatembelee mahali yalipo).

2. Utume wa kanisa. Ni jambo la muhimu sana kwa Mzee wa kanisa kujikita katika utume wa kanisa na uinjilisti. Washiriki wanataka kujua kama Mzee wao wa kanisa anautambua utume wa kanisa na kuona akishiriki kikamilifu kabisa. Inasemekana kwamba kanisa linakua kwa waumini kuiga mfano badala ya kufundishwa tu. Ikiwa Mzee wa kanisa atatenga muda wake kwa ajili ya shughuli ya uinjiliasti, watu wengine watarithi tabia hiyo na watajiweka wakfu na makini kwa ajili ya utume wa kanisa. Mzee anatakiwa aweke muda kwa ajili ya kazi ya uinjilisti. Mzee wa kanisa anakazi ya kusimamia kazi ya kutimiza utume wa kanisa

3. Kuongoza Ibada. Jinsi Mzee anavyoongoza ibada za kila juma ni jambo ambalo linaweza kuleta mabadiliko makubwa sana katika kanisa la Mungu. Uongozi bora katika ibada unaweza kulifanya kanisa lililopoa, au ibada isiyokua na uhai kuwa ibada yenye maana na iliyo na uhai katika kumtukuza Mungu. Ujuzi wa kuongoza ibada, kusoma mafungu, maombi ya hadhara, kupangilia matiririko wa ibada na jinsi ya kufanya mahubiri, ni mambo ambayo Mzee anatakiwa kujifunza.

4. Mwalimu wa mambo ya kiroho. Maisha ya kiroho ya mzee wa kanisa marazote yanatakiwa kuwaongoza washiriki wa kanisa kuutafuta uzoefu wa kina kabisa katika maisha isha yao binafsi ya kiroho. I Timotheo, sura ya 3, anaelezea maisha ya kiroho ya Mzee wa kania kwa namna ifuatayo:

“. . . mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu,

mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu

wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha. . .” Mzee atengeneze maisha yake ya kiroho,

kwa kuwa na muda wa faragha wa ibada na mambo binafsi ya kiroho, (jambo hili ni muhimu kwa kila mkristo anayehitaji kukua kiroho). Mzee ni sharti aaksi tunda la roho kwa kila mtu atakayehusiana na naye: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, ukarimu, uaminifu, upole na kuwa na kiasi.

Referensi

Dokumen terkait

Aidha, lengo la utafiti huu kama lilivyobainishwa katika sura ya kwanza ilikuwa ni kuchunguza dhima ya vipengele vya kimtindo katika tamthiliya za kihistoria kwa

Kama anavyoeleza Leech (1969) kazi ya fasihi haiwezi kueleweka vizuri bila kuwa na maarifa ya lugha ambayo ndiyo njia ya kujieleza. Kwa hiyo, ili kuielewa kazi ya fasihi ni

Kulingana na tafiti ya N.Mohamed(2013)katika uatafiti wake nimeshaubainisha kwenye mwanzoni mwa sura hii umetumia nadharia kidhi ya mawasiliano, pia kazi ya Ali

Nitoe rai kwa wadau wote kushirikiana na kulitumia Baraza katika kuratibu, kutetea na kuwafikia WAVIU pale walipo katika mwitikio wa kitaifa wa shughuli za UKIMWI

Inakadiriwa kuwa katika mkoa wa Shinyanga kiwango cha “ujinga” kinafikia 35%, Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ujinga na kutokuwa na elimu ya stadi za maisha katika jamii

Ni dhahiri kwamba tafsida ni moja ya kipengele kiacho patikana katika tamathali za semi, hivyo ipo haja ya kuona kazi ambazo zilifanywa kupitia wataalamu na watafiti tofauti kama

i) Mafunzo ya siku 5 ya kuendeleza elimu rika katika maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo Mbeya Mjini/Vijijini yaliyoenda sambamba na mkutano wa uhamasishaji kwa wamiliki

Idara ya Huduma za Wanawake ipo kwa ajili ya kuunga mkono, kutia moyo, na kutoa changamoto kwa wanawake Waadventista wa Sabato katika mwenendo wao wa kila siku kama wanafunzi wa