• Tidak ada hasil yang ditemukan

SEMINA WATENDAKAZI (MAOFISA) WA KANISA

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "SEMINA WATENDAKAZI (MAOFISA) WA KANISA"

Copied!
64
0
0

Teks penuh

(1)

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO - KONFERENSI YA MASHARIKI MWA TANZANIA

SEMINA YA WATENDA KAZI (MAOFISA) WA KANISA-2013

Miongoni mwa sifa za Uadilifu na za Kidini za Maofisa wa

Kanisa ni:

 Walio na uwezo

 Wenye kumcha Mungu

 Watu wa kweli / si wenye ndimi mbili

 Wenye kuchukia mapato ya udhalimu

 Wenye kujawa Roho wa Mungu

 Wenye kujali na kutunza familia zao / mahusiano mema katika familia

 Wenye kushuhudiwa mema na watu walio nje

 Watu wasiolaumika

 Wenye kiasi na busara/hekima

 Wenye kujali/kufuata utaratibu

 Si watu wa kujadiliana(:: si watu wa kubishana)

 Wasiwe wepesi wa hasira

 Wasiwe watu wa kujipendekeza nafsi zao

 Walio kielelezo kwa maneno mema na matendo mema, usafi, imani, na upendo.

{Kut.18:21; Mdo.6:3; 1Tim.3:1-13; 4:12-16; Tito 1:5-11; 2:1, 7, 8}

MZEE WA KANISA

(::: Mwangalizi wa Kanisa)

Ni daraja lenye madaraka makubwa.

Mzee wa Kanisa Apaswa awe:

1. Aliyejitoa kikamilifu kwa Kristo. “Huwezi kuwa na mvuto utakaowabadilisha wengine mpaka moyo wako mwenyewe

umenyenyekezwa na kusafishwa na kulainishwa na neema ya Kristo” (Evangelism, 458).

2. Kielelezo kwa washiriki: Wazee wa kanisa hawana budi kuwa kile wanachotaka wengine kuwa, kuamini kile wanachotarajia washiriki wao kukiamini, na kumpenda Kristo kama wanavyowataka kupenda.

Wazee wanachaguliwa na kuwekewa mikono katika kanisa si kwa ajili ya kufanya kazi ya kanisa tu, bali kudhihirisha tabia ya Kristo.

 Kuwa kielelezo sahihi kwa hakika kutajumuisha yafuatayo: a. Unga mkono mafundisho ya kanisa (Tito 2:1)

b. Dumisha mahusiano imara ya familia (1Tim.3:4, 5). Kama mzee wa kanisa, wewe ni sehemu ya familia mbili; familia yako mwenyewe na familia ya kanisa.

c. Uwe msafi kingono (Ebr.13:4). Epuka kuvunja miiko ya ngono kwa:

(2)

2) Kuelewa udhaifu wako

3) Kuwa na tahadhari unapomshauri mtu wa jinsia tofauti 4) Kuwa imara kiroho

5) Mit.6:32, 33; Thes.4:3-7 iwe kinga yako.

d. Epuka ubaguzi wa aina yo yote (Gal.3:28).

e. Uwe mrudishaji zaka na mtoaji sadaka kielelezo. Ukiwa kielelezo katika hili, unaweza kufanya vingi kuwatia moyo washiriki wa kanisa kuwa mawakili waaminifu.3

3. Kiongozi wa washiriki: Rum.12:8. “Karama ya uongozi ni uwezo wa kutoa mwelekeo na mwongozo kwa watu wa Mungu ili watende kazi pamoja

kutimiza kile Mungu wanachotaka watimize”(MwM,49).Wapende washiriki wako. Kama ukiwapenda wale

unaowaongoza,wengi pia watakupenda. Na kama wanakupenda watafuata uongozi wako.

Unganisha washiriki wako. Kuwasaidia washiriki kuvuta pamoja kwa umoja ni moja ya sehemu muhimu sana za uongozi wa mzee. Soma Zab.133:1.

Shauriana na washiriki wako. Lisaidie kanisa lako kupanga

malengo yake lenyewe. Panga na wale unaowaongoza na si kwa ajili yao tu.

4. Mwezeshaji wa washiriki: Kama mzee, unapaswa uwe mratibu na mwezeshaji ukitumia mvuto wako kumsaidia kila mshiriki wa kanisa lako kukuza uwezo kamili wa karama zao binafsi za kiroho kwa ajili ya ujenzi wa kanisa. >wasaidie washiriki kuzijua karama zao za kiroho, kisha wape mafunzo.

Baadhi ya Majukumu ya Mzee wa Kanisa

:

1. Kulilisha kanisa kupitia mafundisho na mahubiri kanisani na nyumbani mwa washiriki (Mdo.20:28; 1Pet.5:2; Yn.21:15-17).

2. Kulilinda kanisa kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kanisani.

3. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote, kupitia idara zote na vyama vyote kanisani.

4. Kuhimiza uwakili katika nyanja zote::: mwili, wakati,talanta, mali, mvuto,

5. Kusimamia ibada za kanisa. kuhakikisha kuwa ibada za kanisa

(Jumatano, Ijumaa, Sabato); zinaendesha inavyostahili, na wahudumu wanaostahili.

6. Kuwaandaa wanaotajiwa kubatizwa. Wale wanaohitaji kujiunga na kanisa wanapaswa kujua kanuni zinazoongoza kanisa hilo; wanapaswa kujua maana ya kutoa maisha yao kwa Kristo.

7. Kuwashikiria washiriki wapya. Yapo mambo manne uwezayo kufanya:

(3)

b. Wafundishe .

 Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20).

 Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo.

 Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.

 Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato

c. Watembelee .

 Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho.

 Waalike nyumbani mwako. d. Wahusishe .

 Washirikishe katika shughuli/programu za kanisa; mfano: huduma za Shule ya Sabato, vijana, uimbaji, kujifunza Biblia, kushuhudia, n.k.

 Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.

8. Kuwarudisha washiriki waliopotea. Ziko sababu zinazofanya washiriki kupoa kiroho/kurudi nyuma/kupotea; taz. MwM, 136. Ili kuwarejesha; kwanza

watambue, kisha watembelee. Hapa ni mashauri saba kuongoza safari yako: i. Uliza maswali kwa busara.

ii. Sikiliza kwa makini tena kwa maombi majibu wanayoyatoa. iii. Usilalie upande wo wote katika maongezi yako.

iv. Heshimu usiri.

v. Waombee.

vi. Waalike warejee kanisani. vii. Uwapende.

9. Kuwatembelea washiriki nyumbani. Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

4) Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. …. 5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.

– ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao; – mwombee kila mmoja kwa jina lake; - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7) Andika. - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa

(4)

mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

10.Kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja. Kiongozi anayejali hushauri na kufariji. Mwongozo wa kushauri:

i. Jifunze kusikiliza kwa makini.

ii. Jali ufumbuzi. Usitumie muda mwingi kujadili tatizo, bali jadili zaidi ufumbuzi wa tatizo.

iii. Wasaidie wachague mpango. iv. Omba pamoja nao.

v. Fahamu wakati unapokupasa kutoa rufaa. 11.Kuwaunga mkono viongozi wenzake.

 Mzee, ni mshauri wa idara zote kanisani.

 Mzee, anapaswa kufahamu mpango wa kila idara.

 Mzee, apaswa kubuni mbinu za kusaidia idara na vyama kanisani….

12.Kusimamia vikao vya kanisa (Baraza la Kanisa / Mashauri ya Kanisa), kwa kushauriana na Mchungaji wa Kanisa / Mtaa (Knn, 2005, 8-23, 25). 13.Kupokea barua na maelekezo toka ngazi za juu za kanisa na

kufikisha ujumbe panapohusika.

14.Kutunza siri za washiriki na za vikao vya kanisa.

15.Kupanga/kuratibu huduma maalumu:

 Ubatizo (MwM, 205-209).

 Meza ya Bwana (MwM, 217-223) {Sabato ya 12 ya kila robo. Knn, 2005, 8-15}.

 Kubariki watoto (MwM, 209-214).

 Uzinduzi wa kiwanja (MwM, 223-226).

 Kutenga kundi kuwa kanisa.

 Kuweka wakfu kanisa/jengo (MwM, 214-217).

 Mazishi (MwM, 229-232).

 Maombi kwa wagonjwa (MwM, 239-242).

 Kuweka wakfu nyumba (MwM, 226-229).

16.Kupanga ratiba ya wahubiri (kwa kushauriana na Mchungaji) na kuisimamia.

 “Mamlaka na Majukumu yao ni mapana mno, lakini hayana budi kutendwa chini ya mwongozo wa mchungaji na

mashauriano na baraza la kanisa” (MwM, 43).

Mamlaka na kazi ya mzee aliyewekewa mikono yanakomea katika kanisa lile tu alikochaguliwa (Knn, 2005, 7-12; Church Manual, 2010, uk.73).

(5)

 Chaweza kukutana mara mbili au moja kwa juma….

 Wajumbe ni maofisa wasimamizi (i.e.:wazee wote, mashemasi wakuu, karani wa kanisa, mhazini, mratibu wa usikivu)….

 Miongoni mwa mambo muhimu ya kuangalia:

 Tathmini ya ibada – lishe, matumizi ya muda, ….

 Kuona kwamba kalenda ya matukio inazingatiwa na viongozi wa kila idara na vyama kanisani.

 Kuona maeneo ya kushauri utendaji wa idara au chama kanisani.  Kuona kama mkakati wa malezi ya washiriki kwa mafundisho/

mahubiri na kutembelea unaenda vyema. Tathmini ifanywe mara moja kila juma.

 Kuangalia hali ya fedha ya kanisa kulingana na mahitaji ya kanisa. Kushauri idara ya uwakili na maendeleo kubuni njia za kuongeza warudisha zaka na watoaji kwa mpango kanisani.

 Kupitia/kuandaa agenda za kwenda baraza la kanisa/mashauri ya kanisa. Agenda isiyopitia katika kikao hicho, ikitajwa/ikiletwa, ipangwe kujadiliwa kikao kinachofuata. Agenda toka idara huwasilishwa kwa wazee na maelezo.

 Kutayarisha ratiba ya wahubiri wa kila robo na kuisimamia.  Kufanya tathmini ya maendeleo ya miradi ya kanisa - uinjilisti,

majengo, ….

 Kupitia barua toka ngazi za juu za kanisa na kuzifanyia kazi….

Vitabu muhimu kwa mzee wa kanisa

:

i. Biblia – uwe na ratiba ya kuisoma kwa ajili ya kukua kiroho. ii. Kanuni za Kanisa – kila sura iwe bayana kwa mzee wa kanisa. iii. Mwongozo wa Mzee – kisomwe kila sura na kueleweka.

iv. Vitabu vya Roho ya Unabii….- kwa kadri ya nafasi/uwezo. v. Mwongozo wa kujifunza Biblia (lesson) wa kila robo.

vi. Kitabu cha Mafundisho ya Biblia – kwa ajili ya darasa la Ubatizo na la Furaha.

vii. Pastor’s and Elder’s Handbook for Youth Ministry.

Majukumu ya Mzee wa Zamu wa Kan

isa:

1. Kuratibu, kuelekeza huduma zote za ibada na shughuli zote za kidini katika juma.

2. Kusimamia waongoza ibada wote, majukumu yao na programu zao (wa S/ Sabato na ibada kuu).

3. Kupokea, kupanga na kutoa matangazo.

4. Kutathmini huduma zote za ibada na shughuli za kidini na kutoa taarifa katika mkutano wa mchungaji na wazee unaokutana kila katikati ya juma.

5. Kupata msaada kutoka kwa wazee na maofisa wengine wa kanisa kila inapohitajika ili kupata uendeshaji wa shughuli za kichungaji uwe laini. 6. Kuratibu shughuli za idara za kanisa.

(6)

8. Kupokea na kushughulikia maswala ya waumini wa kanisa na ya wageni. 9. Kuwa mbunifu katika kuratibu/kuelekeza huduma za kanisa, hivyo kuwasaidia

waongoza ibada za kanisa.

10.Kuhamasisha na kuhimiza matumizi mema ya muda katika huduma na shughuli za kanisa kwa nadharia na matendo.

11.Kupangilia utembeleaji wake wa washiriki katika eneo lake alilopangiwa - akiwa na shemasi au mzee mwingine au mchungaji, au peke yake ikibidi.

12.Kupokea na kushughulikia majukumu mengine yo yote kama atakavyoelekezwa na mchungaji.

13.Kuitisha na kuwa mwenyekiti wa kikao cha mchungaji na wazee, mchungaji asipokuwepo.

14.Kuhudhuria darasa la walimu wa Shule ya Sabato.

15.Kushauriana na wazee wenzake kuona kama kuna agenda ya baraza na kuliitisha ikibidi.

16.Kuhakikisha kuwa kama kuna jukumu lo lote lililoagizwa na baraza la kanisa kutekelezwa, limefanyika.

17.Kuandika maoni, mapendekezo, mafanikio juu ya matukio yaliyojili, na mambo ya kutekeleza katika kitabu cha wazee kwa kumbukumbu na kumsadia mahali pa kuanzia mzee wa zamu baada yake.

18.Kuhakikisha kuwa matoleo yote yalikabidhiwa kwa mhazini kwa utaratibu usio na mashaka.

19.Kuthibitisha ufungaji wa taarifa za wiki/mwezi/robo umefanyika, na zile zinazotumwa konferensi zimetumwa vema na kwa wakati.

20.Kukumbusha kanisa matukio yaliyopo yanayotakiwa kufanyiwa kazi kwa pamoja.

---

NJIA 16 ZA KUONGEZA UTOAJI

{Toka Kitabu cha ‘Uwakili na Mtindo wa Maisha TUM’, uk.66-67}

(Mwongozo kwa Wachungaji na Wazee wa kanisa)

1. Anzisha Kamati ya Uwakili/Fedha ya Mwaka Mzima. Ukuaji wa uwakili ni zaidi ya tukio moja la mwaka. Uwakili ni tendo endelevu linalihitaji mikakati ya kutosha kanisani. Kufundisha kwa vitendo na kuwalisha washiriki mambo ya kiroho ndiyo njia pekee iletayo ufanisi.

2. Weka malengo makubwa zaidi. Uwezo wa utoaji wa makanisa mengi ni zaidi kuliko unavyoonekana. Malengo makubwa ndiyo yaletayo matokeo makubwa kuliko yaliyotazamiwa.

(7)

washiriki wote na kuwatia moyo, matokeo yake yatakuwa kama yale ya kanisa la mitume.

4. Toa zaidi kwa utume. Maofisa wa kanisa(wajumbe wa baraza la kanisa) wawe kielelezo katika utoaji kwa mpango….

5. Badilisha mtindo wa kumtembelea kila mshiriki. Badala ya kuanza

kufuatilia wasioitikia, wafuatilie kwanza unaowatarajia zaidi kuitika. Tumia 85% ya muda wako mahali unapotegemea 85% ya fedha.

6. Jizatiti. Kuwa mchungaji/mzee wa kanisa unayewezesha wakurugenzi wa uwakili ; usiwafanyie kazi yao. Usizuie juhudi yao. Usikubali kuwa mwenyekiti wa kamati yo yote ya uwakili.

7. Wapange watoaji wako wazuri. Katika upaliliaji na ukuaji wa uwakili tumia watoaji wako wazuri wakusaidie kuliambukiza kanisa lote kuwa na tabia ya kudumu katika utoaji.

8. Fundisha umuhimu wa utoaji. Fundisha, hubiri utoaji kwa mpango. Usikingie kifua utoaji wa ahadi ati kwa sababu kanisa linahitaji kupanga mipango yake. Washiriki wanahitaji kufanyia uamuzi juu ya uhusiano wao na Mungu.

9. Watie moyo washiriki juu ya kutoa kwa mpango. Kutoa zaka na sadaka ni sehemu muhimu ya ibada. Mungu alipanga utoaji wa mpango kwa faida ya mwanadamu ili aokolewe na doa la uchoyo.

10.Watambue na uwaheshimu watoaji waaminifu. Kwa ruhusa ya watoaji wafahamishe wengine mibaraka wanayoipata kama vyombo vyake.

11.Eleza jinsi ya kutoa. Kwa familia nyingi, tutoe kiasi gani ni jambo gumu. Jitayarishe kutoa maelekezo na vigezo vitakavyosaidia familia fulani na siyo maelekezo ya jumla.

12.Fanya maongezi ya faragha. Ushauri juu y utoaji wa kikristo wapaswa kuwa wa faragha sana na ufanyike nyumbani. Ruhusu jambo hili liwe kati ya mshiriki na mshiriki. Ni vyema wachungaji wasijiingize hapa, mshiriki amsaidie mshiriki. Fikiria mchungaji mwenye washiriki elfu tatu katika mtaa!

13.Tia moyo utoaji wa ushuhuda binafsi. Njia yenye nguvu na iliyo bora ni ile ya kutoa ushuhuda kwa wale wenye uzoefu wa injili na matokeo ya utoaji mwema.

14.Waachie wahiriki wajivunie (utoaji). Kadri utoaji unavyopanda kuelekea magoli yake, tangaza habari hizi njema. Endelea kutangaza kadri matoleo yamiminikavyo. Tangaza mafanikio sio ushindwaji.

15.Waelimishe na mapatie malengo washiriki wapya mara baada ya kubatizwa. Waonyeshe kuwa, kuwa mshiriki wa familia ya Mungu na kutoa ahadi ya ubatizo ni sawa na pande mbili za sarafu moja. Kwamba,

kufungamanisha fedha zake na ushirika wa kanisa, hufanya ushirika wake kuwa halisi, bila mashaka.

16.Fedha za mipango mikubwa zichangishwe tofauti na zingine. “Kama fedha za ujenzi zingelitafutwa kwanza, tena kwa bidii kubwa, kanisa

likaonekana halina madeni – Je mambo yangelikuwa vizuri iliyoje?” CS, uk.259, 260.

(8)

VITABU VYA REJEA

:

o Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005. o Mwongozo wa Mzee.

o Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM.

KARANI WA KANISA

- wadhifa muhimu.

A.

Baadhi ya Majukumu ya Karani wa Kanisa

:

1.

Huhudumu kama katibu wa baraza la kanisa.

2.

Huhudumu kama katibu wa mikutano yote ya Mashauri ya Kanisa.

3.

Hutunza orodha sahihi ya washiriki wa

kanisa:-

Kila jina la mshiriki liwe na kumbukumbu za mapokeo –tarehe ya baraza na jinsi alivyoingia: ikiwa ni kwa ubatizo, kuhamia (barua) au kupokelewa kwa mikono.

Kila jina lililoondolewa liwe na kumbukumbu za maondoleo –ikiwa ni kwa barua(kuhama), kuasi, kifo, au kutojulikana aliko.

4.

Hutunza orodha sahihi ya mahudhurio ya Meza ya

Bwana:-

Orodha ya mahudhurio ya Meza ya Bwana ni sawa na ile ya washiriki wa kanisa (mapokeo).

Majina ya wasio washiriki wa kanisa mahalia hawaorodheshwi katika orodha ya washiriki wa kanisa, wala ya mahudhurio ya Meza ya Bwana.

5.

Huandika majina ya wabatizwa katika kitabu cha washiriki mara baada ya ubatizo wao. Kila jina linaloongezwa kwa orodha ya washiriki, liongezwe pia kwa mahudhurio ya Meza ya Bwana.

6.

Kutayarisha na kukabidhi vyeti vya ubatizo, ushirika, kubariki watoto, kwa wahusika kwa wakati.

7.

Kutunza orodha ya mali za kanisa.

8.

Kuandaa taarifa kila robo; a) ya kwenda Konferensi, b) ya kuwasilisha

kanisani.

9.

Kutayarisha bajeti ya ofisi yake ya mwaka.

10.

Kutunza siri za washiriki.

11.

Kuzingatia uandishi wa barua za miito:

a)

Ndani ya mtaa;

b)

Nje ya mtaa, ndani ya Konferensi;

(9)

Karani wa kanisa huandika barua kwa agizo la Baraza la Kanisa, Mkutano wa Mashauri ya Kanisa, au bodi ya wazee wa kanisa.

12.

Kuratibu zoezi la kuelimisha washiriki juu ya mshiriki na ushirika.

B.

Mipaka ya Karani wa Kanisa

:

Asitunze pembeni orodha ya washiriki waliorudi nyuma au wasiojukana walipo.

Asitoe barua kwa mshiriki ye yote aliye chini ya karipio.

Asiongeze jina bila idhini ya Kanisa.

Asiondoe jina bila idhini ya Kanisa, isipokuwa kwa kifo.

REJEA: KANUNI ZA KANISA, Toleo la 17, 2005.

SHEMASI

(m.y. mtumishi wa kanisa) {Mdo.6:3-6; 1Tim.3:8-13; Rum.16:1,2}

 Wawe kielelezo katika tabia na mwenendo wa Kikristo (wacha Mungu).  Shemasi wa kiume sharti awekewe mikono kabla ya kushika kazi yake.  Shemasi mkuu (me & ke) ni wajumbe wa baraza la kanisa.

A. Baadhi ya Majukumu ya Shemasi: 1. Kusaidia katika Ibada na Mikutano,

 Kukaribisha wageni na washiriki wanapoingia kanisani.

 Kuhakikisha kuwa waabudu wamekaa katika mpango mpango stahili.

 Kuhakikisha kuwa kuna utulivu mahali pa ibada.

 Zamu ipangwe vizuri na kufuatiliwa na shemasi mkuu. 2. Kutembelea washiriki nyumbani mwao {malezi}

 Kufanikisha zoezi hili muhimu sana katika malezi ya washiriki, ni vyema kila shemasi awe na nyumba anazohudumia.

 Mpango mzuri na utaratibu wa kuwatembelea washiriki uwepo;

 Utembeleaji wa washiriki nyumbani mwao ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

(10)

5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi. – ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao; – mwombee kila mmoja kwa jina lake; - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7) Andika. - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa

nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo. - Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao. - Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo

mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

 Taarifa ya kutembelea hutumwa Konferensi kupitia katibu wa uwakili.

3. Kutunza mali za kanisa,

 Kuwe na orodha ya mali za kanisa na kutunzwa mahali stahili.

 Kufanya ukarabati inapobidi.

4. Kuangalia usafi wa jengo la kanisa, vifaa vya kanisa, na uwanja wake. 5. Kuwatunza wagonjwa na maskini (mfuko wa wenye shida uwepo).

6. Kukusanya zaka na sadaka siku ya ibada, kuzihesabu na kuzirekodi, kisha kumkabidhi mhazini, naye kuwapatia stakabadhi kwa kiasi alichokabidhiwa. 7. Kutunza siri za washiriki.

8. Kusaidia katika huduma za kanisa:

 Ubatizo {ufafanuzi wa kuandaa mahali pa ubatizo na kupokea wabatizwa toka majini}.

 Kutawadhana miguu {ufafanuzi wa namna ya kuhudumia wakati wa jukumu hili}.

 Meza ya Bwana {ufafanuzi wa namna ya kuandaa mkate na divai na namna ya kuhudumu}.

9. Kuendesha huduma ya mazishi (shemasi wa kiume) 10.Kuhudhuria katika bodi ya mashemasi.

11.Kuandaa bajeti ya mashemasi ya mwaka.

12.Wawe mstari wa mbele kuhudhuria ibada za kanisa.

B. Baadhi ya mipaka ya shemasi:

 Haruhusiwi kuendesha huduma zo zote zile za kanisa zitendwazo na mchungaji aliyewekewa mikono.

 Haruhusiwi kusimamia mkutano wa kupokea na kuhamisha washiriki.

(11)

MHAZINI WA KANISA

– Kazi Takatifu.

 Mhazini anaweza kwa sehemu kubwa kuchangia moyo wa uaminifu katika kurudisha zaka na kukuza roho ya ukarimu miongoni mwa washiriki.

Baadhi ya Majukumu ya Mhazini wa Kanisa

:-1. Mwangalizi/Mtunzaji wa fedha zote na kanisa:-a) Fedha za amana – ziendazo Konferensi. b) Fedha za kanisa mahalia.

c) Fedha za mashirika saidizi ya kanisa mahalia (fedha za idara na vyama kanisani)

2. Kutuma fedha za amana (Trust Funds) kulingana na ratiba ya Konferensi.

 Kanisa haliwezi kukopa, kutumia, au kuzuia fedha za amana kwa madhumuni yo yote yale.

3. Kusimamia matumizi ya fedha za kanisa mahalia na za mashirika saidizi kanisani.

 Fedha za kanisa mahalia hutumika kwa agizo la baraza la kanisa au mashauri ya kanisa.

 Fedha za idara na vyama (mashirika saidizi) hutolewa kwa idhini ya mabaraza ya idara/vyama husika.

 Awe mwangalifu kuona kuwa anapewa stakabadhi kwa malipo yote yaliyofanywa.

 Taarifa ya marejesho ni muhimu kabla kiongozi wa idara/ofisa hajaomba fedha zingine.

4. Kutoa risti kwa kila pesa anayopokea. 5. Kulinda kusudi la pesa

 Mhazini wa Kanisa au Baraza la Kanisa hawana mamlaka ya kuchepusha fedha zo zote kutoka kwa lengo ambalo kwalo zimetolewa.

6. Kutayarisha na kutuma taarifa Konferensi kila mwezi.

7. Kutayarisha na kutoa taarifa kwa Baraza la Kanisa na Mkutano wa Mashauri ya Kanisa kila robo.

8. Kujaza Jicho la Kanisa kila mwezi.

9. Kuhesabu na kuandika idadi ya wanaorudisha zaka na wanaotoa kwa mpango (washiriki na wasio washiriki).

10.Kuelimisha washiriki uzuri wa kutoa zaka na sadaka kwa njia ya bahasha tena kwa mpango.

11.Kuelimisha washiriki wanaorudisha zaka na kutoa sadaka zao kwa njia ya

hawala au hundi ya posta, mlipwaji awe ni kanisa, badala ya mtu binafsi ye yote yule. Kisha awasilishe pay in slip kwa mhazini ili amkatie risti.

12.Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi. 13.Kutayarisha bajeti ya ofisi yake kwa mwaka.

14.Kuzingatia utaratibu mzuri wa kutuma fedha

Konferensi:- Pamoja na kuandika vizuri jina na A/C ya Konferensi kwenye pay in slip;

(12)

 Kuhakikisha muhuri na sahihi ya ‘teller’ wa benki viko sawa. 15.Kutunza siri za washiriki.

REJEA:

Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

MRATIBU WA USIKIVU

Ni muhimu kwamba wengi walio na shauku iliyokuzwa kupitia juhudi za utume wa kanisa wahudumiwe mara moja. Kufikia hapo, mratibu wa usikivu ambaye anaweza awe mzee wa kanisa achaguliwe wakati wa uchaguzi wa maofisa wa kanisa. Mtu huyu ni mjumbe wa baraza la kanisa na wa Kamati ya Huduma za Uinjilisti wa Washiriki, naye hutenda kazi moja kwa moja na mchungaji na

mwenyekiti wa kamati hiyo. Majukumu yanayohusika na wadhifa ni pamoja na :-1. Kutunza orodha sahihi ya wale wote wenye shauku, iliyopokelewa na kanisa

kutokana na kila chanzo kama vile Huduma za Jamii (Chama cha Dorkas), Sadaka ya Mavuno, mikutano ya uinjilisti wa hadhara, masomo ya Biblia, uinjilisti wa walei, mawasililiano yatokanayo na kushuhudia, kugawa

magazeti, uinjilisti wa Shule ya Sabato, uinjilisti wa vitabu, uinjilisti wa afya na kiasi, radio-televisheni, na vitabu vinavyotolewa na kanisa kwa ajili ya utume.

2. Kumsaidia mchungaji na mwenyekiti wa Huduma za Uinjilisti wa Washiriki katika kuandikisha na kuorodhesha majina ya washiriki wenye sifa kwa ajili ya huduma ya ufuatiliaji.

3. Kutoa taarifa kwa baraza la kanisa kila mwezi juu ya idadi ya wasikivu waliopokelewa na idadi ya wale waliofuatiliwa. Pale ambapo mtu

aliyefuatiliwa anapokuwa amefundishwa vya kutosha, basi akabidhiwe kwa mchungaji.

REJEA

:

Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005; Sura 7-31, 32.

KIONGOZI / MKUU WA KUNDI

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi (Mkuu) wa Kundi

:

1. Kiongozi wa kiroho kundini (akimsaidia Mzee wa Kanisa) i. Anapaswa kuwapenda wale anaowaongoza

Mwenye huruma

Awe na tamaa ya kuwasaidia wakue kiroho Kuwapenda licha ya kasoro zao

ii. Tafuta ushauri wa washiriki kundini na kwa Mzee wa Kanisa

2. Kuwaunga mkono watendakazi wenzake kundini

Buni mbinu za kusaidia kila mtendakazi afaulu

(13)

3. Kulilisha kundi, mzee wa Kanisa asipokuwepo

Awe na uwezo wa kuendesha ibada za Kanisa, kuhubiri na kufundisha

Kusimamia huduma ya maombi kundini

Kutoa mafundisho na semina kulenga mahitaji ya wanakundi

4. Kuunga mkono / kutetea kanuni za Kanisa na Mafundisho ya Kanisa

5. Kushirikiana na Kanisa na Konferensi

 Kutekeleza mipango toka Kanisa mahalia na Konferensi  Kuwaheshimu viongozi hao na kuwaunga mkono

 Kuwashauri

6. Kulilinda kundi kwa kutoruhusu mafundisho potovu kuingizwa kundini

7. Kuhimiza uinjilisti katika nyanja zote.

8. Kuhimiza uwakili katika njanja zote, mkuu wa kundi ukiwa kielelezo (Lk. 12:42)

 Matoleo: Zaka na Sadaka i.e. utoaji kwa mpango

 Matumizi ya muda, ikiwemo utunzaji wa Sabato na kazi siku sita.  Matumizi ya talanta/karama

 Kutunza mwili kama hekalu  Mvuto

9. Kuwashirikisha vijana wadogo na watoto katika huduma za Kanisa na uinjilisti

10.Kuwashikiria washiriki wapya. Yapo mambo manne uwezayo kufanya:

a. Wafanye rafiki. Chagua watu miongoni mwa waumini wazoefu ambao watakabidhiwa jukumu la kuwa walezi wa kiroho wa waumini hawa wapya. (wajibu wa walezi-MwM, 143)

b. Wafundishe.

 Endelea kufundisha baada ya ubatizo (Mt.28:20).

 Wasidie kugundua karama za Roho walizo nazo.

 Waelimishe jinsi ya kutumia karama hizo kwa busara kuwabariki wengine.

 Wasaidie wadumishe mazoea ya kupenda madarasa ya Shule ya Sabato

c. Watembelee.

 Waumini wapya wanapaswa kutembelewa mara kwa mara ili kutiwa moyo katika ukuaji wao kiroho.

 Waalike nyumbani mwako. d. Wahusishe.

(14)

 Waelekeze namna ya kuongoa roho, wakianza na familia zao na marafiki.

11. Kusimamia kikao cha kundi

12. Kuhudhuria Baraza la Kanisa kila mwezi

13. Kuhimiza uwasilishaji wa taarifa zitokazo kundini kwenda Kanisa mahalia – Mhazini, Katibu wa Uwakili, Huduma za Washiriki, Shule ya Sabato na wengineo.

14. Kusimamia na kutetea kalenda ya matukio ya mwaka na mpango wa Kanisa.

15. Kutembelea waashiriki nyumbani;

Utembeleaji wa washiriki ni muhimu sana kwa malezi na ukuaji wao wa kiroho. Utaratibu wa kutembelea uzingatiwe:

1) Andaa. Andaa moyo wako, ukimwomba Mungu akusaidie kusema na kufanya kile ambacho kitaleta Baraka kwa kila kaya/familia.

2) Fanya urafiki. Unapofika kwenye nyumba husika, anza kuzungumzia mambo ya kawaida ya kijamii yanayojenga.

3) Soma. Baada ya dakika kadhaa, elekeza maongezi yako katika mambo ya kiroho. ….

4) Uliza. Uliza kama lipo jambo fulani au mtu fulani la/wa kuombea. …. 5) Maombi. Waalike watoto na wengine walioko nje wajiunge nanyi.

– ombea maswala waliyokueleza kuwa ndiyo mahitaji yao; – mwombee kila mmoja kwa jina lake; - ombea pia asiye muumini anayeishi katika kaya/familia.

6) Ondoka. Ondoka haraka wakati bado utukufu wa ombi unaendelea kutawala akili za uliowaombea. Katika tamaduni nyingi, nusu saa ni muda wa kutosha katika kutembelea.

7) Andika. - Mara uwapo mbali na nyumba hiyo, yaandike majina ya watu wa

nyumba hiyo, iwapo hukuwa nayo. - Andika mahitaji ya familia hiyo na mapendekezo yao. - Utakapowatembelea familia hiyo, na kutaja kwa ufasaha mambo

mliyogusia kwenye ziara yako ya awali katika familia hiyo, huishawishi familia hiyo kuamini kuwa kwa hakika unawapenda na kuwajali.

16. Kuliandaa kundi kuwa kanisa.

IDARA KANISANI (ASASI SAIDIZI KANISANI)

A. KWA NINI IDARA KANISANI?

Sababu za Kuwepo Idara Kanisani

:

(15)

3. Kutoa ushauri kwa uongozi wa kanisa

4. Kushirikiana idara moja na nyingine kutenda kazi za kanisa 5. Kuinua viwango vya kiroho kanisani

Viwango vya Kiroho Vipasavyo Kuinuliwa na Idara Kupitia Utendaji:

1. Uaminifu katika kurudisha zaka na sadaka 2. Ununuzi wa miongozo ya kujifunza Biblia 3. Usomaji wa miongozo hiyo

4. Mahudhurio katika ibada za kanisa na mikutano ya kiroho 5. Usomaji wa Biblia kwa mpango

6. Usomaji wa vitabu vya Roho ya Unabii 7. Ushuhudiaji.

B.

NJIA ZA KUENDESHA IDARA KANISANI

:

1) Tambua ukubwa wa idara unayoisimamia na changamoto zilizopo.

2) Mwombe Mungu akuongoze na akuwezeshe kutekeleza jukumu alilokupa.

3) Uliza mashauri toka kwa watu wengine – mf. Mchungaji, mzee wa kanisa, ….

4) Uwe na mipango/malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu.

5) Wahusishe wana idara katika mipango/malengo hadi waone kwamba ni yao wala siyo yako tu.

6) Peleka mipango na mapendekezo kwenye baraza la kanisa.

7) Wape wenzako madaraka, yaani, washirikishe wenzako katika kutekeleza majukumu.

8) Weka watu wanaofaa katika nafasi wanazostahili.

9) Wafundishe (unaowaongoza) katika lugha yao na kasi yao.

10)Kagua kazi ulizowapa, himiza ufanisi wa kazi; daima watie moyo.

11)Chukua taarifa ya kazi kwa wakati, peleka katika ngazi zinazohusika.

12)Shirikiana na maofisa wenzako.

13)Toa shukrani kwa kazi njema.

14)Kamwe usifanye matumizi ya fedha za idara bila kuidhinishwa na idara husika kupitia vikao vyake.

 Kiongozi, uwe kielelezo katika usemi, mwenendo, usafi, uwakili wa muda, uaminifu na uadilifu katika nyanja zote.

<><><> Tuma taarifa iendayo Konferensi kwa wakati, kulingana na utaratibu uliopewa

IDARA YA HUDUMA ZA WASHIRIKI

Idara ya Huduma za Washiriki hutoa nyenzo na kuwafunza washiriki wa

(16)

kuandikisha kila mshiriki katika utendaji wa dhati wa huduma ya Mungu ya uongoaji roho.

A.

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Hduma za Washiriki:

1. Kuongoza katika kufunza na kuliongoza kanisa katika huduma ya utendaji wa utume.

2. Mwenyekiti wa Baraza la Huduma za Washiriki

3. Kuwasilisha kwa Kanisa, katika hduma ya Sabato ya kila mwezi na mikutano ya mashauri ya kanisa, taarifa kuhusu shughuli kamili za utume wa Kanisa.

B. Baadhi ya majukumu ya Katibu wa Huduma za Uinjilisti:

1. Kufanya kazi kama Katibu wa Baraza la Huduma za Uinjilisti.

2. Kutoa taarifa kwa Kanisa juu ya shughuli za Huduma za Uinjilisti wakati wa huduma ya Sabato ya kila mwezi wa Huduma za Uinjilisti na katika mkutano mashauri ya Kanisa.

3. Kuhusika katika manunuzi yote yanayofanywa na Kanisa katika Duka la Vitabu la Waadventista.

4. Kulifahamisha Kanisa kuhusu nyenzo zinazopatikana kwa ajili ya matumizi yake.

5. Kupanga sadaka za mara kwa mara ili kuwezesha Huduma za Uinjilisti kupata vifaa kwa ajili ya washiriki kufanyia kazi ya utume pale ambapo vifaa hivyo havipatikani kupitia bajeti ya Kanisa. Sadaka ya huduma za Uinjilisti kwa ajili ya kusudi hili inaweza kutolewa katika Sabato ya kwanza ya mwezi.

6. Kuandaa na kuwasilisha kwa wakati taarifa iendayo konferensi kila robo, hali kadhalika ile iendayo mashauri ya Kanisa.

C.

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha

Wanaume Waadventista (AMO):

1. Kuratibu na kusimamia usajili wa wanachama 2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma 3. Kuongoza wanachama kutekeleza

uafuatayo:- Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magazeti, hospitalini, vituo vya kulea watoto yatima, n.k.

 Kuhudumia Nyumba za wenye shida, wazee wasiojiweza, wakongwe, (kuratibu ukaarabati au ujenzi wa Nyumba)

 Huduma kwa wagonjwa walio majumbani

 Huduma ya uinjilisti magerezani

 Kutoa ushauri

 Kuratibu na kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima pale inapohitajika.

D.

Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa Chama cha

AMO:

(17)

3. Kupokea michango ya wanacham na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama.

4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.

E.

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Chama cha Dorkas:

1. Kuratibu na kusimamia usaji wa wanachama 2. Kusimamia mikutano ya wanachama ya kila juma 3. Kuongoza wanachama kutekeleza

yafuatayo:- Kugawa misaada ya vitu (misaada ya kiutu) magerezani, hospitalini, vituo vya kulea watoto yatima, n.k.

 Kuhudumia Nyumba za wenye shida (maskini), wazee wasiojiweza, wakongwe (kwa maombi, mavazi, vyakula, n.k.

 Huduma kwa wagonjwa walio majumbani (kwa maombi, chakula, madawa, n.k.)

 Huduma ya uinjilisti magerezani

 Kutoa ushauri nasaha

 Kushirikiana na chama cha AMO katika utoaji wa elimu ya watu wazima pale inapohitajika.

F.

Baadhi ya majukumu ya Katibu-Mhazini wa chama cha

Dorkas:

1. Ni mwandishi na mtunza kumbukumbu ya vikao vya chama 2. Ni mtunzaji wa vifaa vya chama

3. Kupokea michango ya wanachama na kuwasilisha fedha kwa Mhazini wa Kanisa. Mhazini wa Kanisa ndiye benki ya chama

4. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kila mwezi.

G.

Baadhi ya majukumu ya Kiongozi wa Satelite:

1. Kuona kwa dishi na vifaa vingine vya Satelite vipo katika hali njema 2. Kupata vipindi vinavyorishwa kwa satellite vifaavyo Kanisa mfano Hope

Channel.

3. Kuwa na ratiba ya kuonyesha program za satellite zenye mafunzo / masomo yaffayo kwa Kanisa. Yaweza kurekodiwa na kuonyeshwa kwa washiriki kwa ratiba mwafaka, usingoje tu mikutano ya uinjili kwa njia ya satellite.

4. Pale ambapo Kanisa bado halina satellite, kiongozi huyu ahamasishe na kusimamia ununuzi wa vifaa na matumizi yake, akionyesha faida nono za kuwa na nyezo hii muhimu ya uinjilisti.

5. Kupanga na kusimamia bajeti ya satellite.

(18)

 Kupitia kwa Huduma kwa watu walemavu, Baraza la Huduma za

Washiriki la kanisa la palepale litoe uangalifu maalumu kwa washiriki na wengine walio walemavu. Likuze programu ya kushuhudia kwa

walemavu; likitoa mapendekezo kwa baraza la kanisa kuhusu hatua zitakazowezekana kuchukuliwa ili kufanya vifaa vya kanisa viweze kupatikana kwa urahisi kwa walemavu; kulisaidia kanisa kutatua matatizo ya usafiri kwa walemavu.

 Mratibu wa Huduma kwa watu walemavu hutumika kama kiungo kwa asasi zinazotoa huduma kwa watu walemavu kama vile Shirika la

Huduma za Kikristo kwa Wasioona na kukuza programu za shirika hilo kanisani.

REJEA:

Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005.

IDARA YA SHULE YA SABATO

Shule ya Sabato ndiyo mfumo kimsingi wa elimu ya kidini ya Kanisa la Waadventista Wasabato na una makusudi manne: kujifunza Maandiko Matakatifu, ushirika, kuifikia jamii (kushuhudia), na kukazia utume ulimwenguni.

A.

Kazi za Maofisa wa Shule ya Sabato

:-1. Kiongozi (Mrakibu) wa Shule ya Sabato

 Anatazamiwa kufuata maamuzi ya Baraza la Shule ya Sabato kuhusu utendaji wa idara.

Baadhi ya majumu yake:

i. Kusimamia viongozi wote wa Shule ya Sabato na kuwatia moyo kutekeleza majukumu yao kwa furaha na mafanikio.

ii. Kuitisha na kuwa mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Sabato.

iii. Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Kanisa katika idara ya Shule Sabato.

iv. Kusimamia mkutano wa Walimu wa Shule ya Sabato. v. Kuwakilisha Shule ya Sabato kwenye Baraza la Kanisa. vi. Kuona kwamba migawanyo yote inafanywa sawasawa.

(19)

viii. Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – uinjilisti kuhamasisha VBS, kufanya Matawi ya Shule ya Sabato, na uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato

ix. Kupanga na msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika kutafuta kurudisha washiriki waliorudi nyuma, kwa kuweka hai rekodi za Shule ya Sabato na kuwatia moyo viongozi na walimu kupanga program mathubuti za kutembelea

x. Kuwasiliana na Karani wa Shule ya Sabato juu ya ukamilifu wa rekodi na usahihi wa taarifa na utumiaji wa hizo taarifa haraka kila robo kwenda kwa Mkurugenzi wa Shule ya Sabato Konferensi kupitia kwa Mchungaji wa Mtaa.

xi. Kuhimiza malengo manne ya Shule ya Sabato

xii. Kusimamia mpangilio na uundishaji katika migawanyo kama

ifuatavyo:-a. Kupanga na kuratibu mikutano ya walimu wa Shule ya sabato

b. Kuwahi kila sabato asubuhi kuratibisha shughuli, kujibu maswali, kusaidia kutafuta wa badala pale ambapo waliopangwa kawakufika

c. Kutoa uongozi na kutia moyo viongozi wa migawanyo

d. Kuwa kiunganishi cha Kanisa na migawanyo mingine kwa kuhimiza matoleo ya Shule ya Sabato ya 13

e. Kuhimiza mahudhurio katika darasa la walimu.

2. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika

Baadhi ya majukumu yake:

i. Kutunza orodha ya washiriki wa Shule ya Sabato, anuani na namba zao za simu

ii. Kuhimiza utembeleaji wa washiriki wasiohudhuria vyema Shule ya Sabato

iii. Kusaidia kuhusishwa kwa wabatizwa wapya na wahamiaji katika programu za Shule ya Sabato

iv. Kuhudhuria baraza la Shule ya sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango kwa ajili ya kukuza ushirika.

v. Kuwa tayari asubuhi ya Shule ya Sabato ……

3. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Uinjilisti

Baadhi ya majukumu yake:

i. Kusimamia uinjilisti wa Shule ya sabato katika jumuiya

ii. Kupanga na viongozi wa migawanyo na walimu kwa ajili ya shughuli za uinjilisti kupitia madarasa ya Shule ya Sabato

iii. Kupanga kwa ajili ya siku za Wageni

iv. Kupanga pamoja na viongozi wa migawanyo kwa ajili ya siku za maamuzi

(20)

vi. Kupanga na viongozi wa migawanyo kufungua matawi ya Shule ya Sabato

vii. Kukuza ufuatiliaji kwa ajili ya wageni

viii. Kuhudhuria Baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli za mipango kwa ajili ya uinjilisti kwa jamii.

ix. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …….

4. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Utandaaji

Watandaaji ni washiriki ambao kwa sababu mbalimbali hawawezi kuhudhuria daima vipindi vya Shule ya Sabato. Wanaweza kuzuiwa

na:-a. Matatizo ya usafiri b. Ugonjwa

c. Uzee

d. Hali zisizoepukika nyumbani

Kiongozi huyo huchaguliwa wanapokuwepo watandaaji zaidi ya watatu. Wasipozidi watatu, hutunzwa na Karani wa Shule ya Sabato au Msaidizi.

Baadhi ya majukumu yake:

i. Hufanya kazi chini ya Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ushirika

ii. kuwasiliana na washiriki wasioweza kuhudhuria Shule ya Sabato iii. kuwasiliana na Mchungaji, Mzee / Wazee wa Kanisa, Msaidizi wa

Shule ya Sabato – Ushirika, na yeyote anayeweza kutoa habari za wale wanaopaswa kuandikishwa katika utandaaji.

iv. Kudumisha mawasiliano na watandaaji kwa kuwatembelea ikiwezekana, au barua au simu.

v. Kuhakikisha watandaaji wanapata miongozo ya kujifunza Biblia, somo la nchi za mbali, bahasha za matoleo, vifaa vingine vya Shule ya Sabato vinavyotakiwa ili wapate Baraka zote za Shule ya Sabato.

vi. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya kitengo chake

vii. Kutoa taarifa kamili ya watandaaji na matoleo yao kwa Karani wa Shule ya Sabato mwisho wa juma, mwezi na robo.

viii. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato ……

5. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Ukarimu

Baadhi ya majukumu yake:

i. Kufundisha kutoa semina, na kusimamia mabawabu / wakaribishaji.

ii. Kupanga na viongozi wa migawanyo kuhakikisha kuwa somo la misheni lipo katika programu ya Shule ya Sabato.

(21)

iv. Kupanga na kuhimiza programu ya kuwakarimu wageni milo, ama majumbani au kanisani.

v. Kukuza mpango wa ufuatiliaji kwa wageni wote wanaohudhuria Shule ya Sabato ikijumuisha – kadi, barua, simu na / au kutembelea.

vi. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango kuhusu ukarimu.

vii. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …..

6. Kiongozi Msaidizi wa Shule ya Sabato – Utume

Ulimwenguni

Baadhi ya majukumu yake:

i. Kupanga pamoja na viongozi wa migawanyo kuhakikisha kuwa somo la misheni lipo katika programu ya Shule ya Sabato

ii. Kuratibu programu ya Shule ya Sabato ya 13, kutangaza sadaka ya 13 Sabato moja kabla ili kuwatayarisha watoaji.

iii. Kuhudhuria baraza la Shule ya Sabato na kutoa taarifa juu ya shughuli na mipango ya ukuzaji wa utume ulimwenguni.

iv. Kuwa tayari asubuhi ya Sabato …….

7.

Majukumu ya Karani wa Shule ya Sabato:

i. Kuifahamisha Shule ya Sabato kuhusu maendeleo, mwenendo, mipango, na mafanikio yaliyofikiwa kwa kutoa taarifa wakati wa taratibu za kawaida.

ii. Kugawa na kukusanya makadi ya madarasa, bahasha za sadaka na makadi ya taarifa ya huduma yangu kwa Yesu.

iii. Kukagua makadi, kujazia majina yaliyopungua, kuhesabu na kutunza kumbukumbu za fedha.

iv. Kukabidhi fedha zote za Shule ya Sabato kwa mtunza hazina wa Kanisa

v. Kupata na kutunza risiti za fedha alizokabidhi mhazini

vi. Kuingiza mapema takwimu zote za wiki katika kitabu cha taarifa cha Shule ya Sabato. Taarifa za washiriki na mahudhurio ziingizwe kwa uangalifu mkubwa.

vii. Kutengeneza taarifa kamili na sahihi ya robo ya Shule ya Sabato kwenye fomu ya taarifa na kutuma kwa wakati Konferensi, kupitia kwa Mchungaji wa mtaa.

viii. Kutoa taarifa fupi kila robo na ya mwaka kwenye kitabu cha majina ya washiriki wa Shule ya Sabato.

ix. Kuhakikisha majina ya wana madarasa wote kwenye kitabu kikuu cha majina ya washiriki wa Shule ya Sabato kila mwaka au makadi ya madarasa kila robo.

x. Kutunza miniti za vikao vya mabaraza ya Shule ya Sabato.

xi. Kuhifadhi vyema taarifa zote katika faili na kuzikabidhi kwa atakayeingia baada yake.

(22)

xiii. Kuomba vifaa vinavyotolewa bure toka idara ya Shule ya Sabato ya Konferensi.

xiv. Kuona kwamba wasaidizi wanajua na kufanya vyema kazi zao, hasa karani anapokuwa hayupo. Washirikishe wakati upo ili wafanye vyema wakati haupo.

8.

Majukumu ya Makarani wasaidizi wa Shule ya Sabato:

i. Kuzitenda kazi za karani wakati asipokuwepo.

ii. Kutenda kazi kila sabato chini ya maelekezo ya karani mkuu, katika kuyatimiza majukumu kama

vile:-a. Kusaidia kugawa na kukusanya vifaa

b. Kushiriki katika kuwajibika kuvitunza vifaa c. Kuhesabu sadaka ya Shule ya Sabato

d. Kutunza kumbukumbu

e. Kubeba wajibu wa shughuli maalumu kama atakavyopangiwa na karani.

9. Wajibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Biblia wakati wa Likizo (VBS Director):

Ni wajibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Biblia wakati wa Likizo kufanya

yafuatayo:-i. Kuongoza katika kuipangilia Shule ya Biblia wakati wa likizo.

ii. Kuihamasisha Shule ya Biblia wakati wa likizo wakati wa Shule ya Sabato

iii. Kufanya ushirikiano na viongozi wasaidizi, walimu, na wasaidizi wengineo kuwafikia watoto kwa ajili ya Yesu

iv. Kukurugenzi (direct) Shule ya Biblia wakati wa likizo, akitumia vifaa vinavyopatikana. Kama vile, masomo ya Shule ya Sabato ya watoto mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu.

v. Kupanga utaratibu mzuri wa kufuatilia ili chochote kisipotee. Hii ni pamoja na kutembelea nyumba za wanafunzi wa VBS, na kuwaalika watoto washiriki katika programu zingine zinazopangwa kuleta roho kwa Yesu, kama vile:

a. Shule ya Sabato

b. Matawi ya Shule ya Sabato

c. Wakati wa hadithi (huripotiwa kama tawi la Shule ya Sabato) d. Vyama vya biblia vya ujirani (huripotiwa kama tawi la Shule ya

Sabato)

e. Vyama vya watafuta njia f. Vyama vya wavumbuzi g. Shule ya Kanisa

h. Kambi la vijana i. Huduma za ibada.

B. SIKU MAALUM:

(23)

i. Siku za kufanya maamuzi (Decision days) ii. Sabato za kupandisha daraja (Promotion days) iii. Sabato za Rale za Shule ya Sabato (Rally Days)

iv. Sabato za Wageni (Community Guest Days)

 Siku hizi maalumu ni za muhimu sana kwa ajili ya kushughudia na malezi

 Ipangwe programu fupi, ya kuvutia, na ya kiroho … ili kuwavuta kuhudhuria tena au kujiunga na kanisa.

 Uchaguzi wa mahubiri, mfundishaji, na kwaya ufanywe kwa uangalifu mkubwa ili kukidhi kusudi la program. Mwaliko wa wahudumu hao ufanwe mapema kwa kadri iwezekanavyo kwa kufuata taratibu zilizopo.

I. Siku za kufanya maamuzi (Decision days)

 Wadogo kabisa (division ya Chekechea na Shule ya Msingi), mara mbili kwa mwaka.

 Watoto wakubwa / vijana wadogo, mara moja kwa mwaka

 Kusudi ni kuwavuta watoto na vijana wadogo kufanya maamuzi kumfuata Yesu

 Dakika 20-25 zafaa kwa ajili ya programu wakati wa Shule ya Sabato.

II. Sabato za kupandisha daraja (Promotion days)

 Kila mtoto awe radhi kupanda daraja (darasa) au la, hakuna kulazimisha

 Ni vyema wazazi kualikwa kuhudhuria.

III. Sabato za Rale za Shule ya Sabato (Rally Days)

 Kusudi: kuwaleta washiriki wasiohudhuria Shule ya Sabato kama wageni maalum siku hiyo.

IV. Sabato za Wageni (Community Guest Days)  Kusudi:

1. Kulitambulisha Kanisa la Waadventista wa Sabato kwa jumuia iliyo karibu nalo na

2. Kuongoa roho

 Ujumuikaji pamoja, mlo uwepo.

JINSI YA KUANDAA SIKU MAALUM

(maelezo ya jumla)

Idara ya Shule ya Sabato itayarishe mapema:

1. Itangaze siku maalum

2. Washiriki wote wahusishwe kualika

3. Kutuma kadi za mwaliko kwa washiriki wa zamani walio katika jumuia 4. Teua kamati ya kufuatilia mwaliko, kwa simu, ana kwa ana, barua, n.k. 5. Weka bango mbele ya Kanisa

6. Itangazwe katika matangazo ya Kanisa ya kila juma 7. Teua kamati ya ukaribishaji

(24)

9. Chagua nyimbo zifaazo kwa tukio. Ikiwezekana zichapishwe, nakala za kutosha zipatikane

10. Kwaya iandaliwe vyema. Nyimbo za kufaa tukio ziandaliwe 11. Uwe na zawadi kwa wageni

12. Wafanye wageni wajisikie wamethaminiwa. Wakaribishwe Sabato inayofuata

13. Tuma barua za shukrani kwa wale walioleta wageni

14. Andikisha washiriki wapya wa Shule ya Sabato haraka iwezekanavyo.



Hakikisha kwamba kila mgeni aliyealikwa amepata

barua / simu au kufikiwa na mtu katikati ya juma

linaloishia siku maalum.

Kuandaa kalenda kwa ajili ya Siku Maalum

Siku Maalum

Tare

he

Wahusika

Siku za Kufanya maamuzi

Siku ya kupandisha daraja

Sabato za Rale za Shule ya Sabato

Sabato ya Wageni

PROGRAMU ZA SHULE YA SABATO

Programu za kawaida za Shule ya Sabato zapaswa zitumie muda usiopungua dakika tisini (K–K. 8–9). Sehemu ya kwanza ya Shule ya Sabato yapasa kuanza saa tatu kamili asubuhi. Utaratibu huu utakuwa tofauti katika siku maalum za Shule ya Sabato.

A.

Dakika 15 za kwanza

(3:00 – 3:15) zitumike kwa kumsifu Mungu kwa nyimbo. Huu ni muda mzuri wa Kanisa lote kuimba. Nyimbo mpya zifundishwe, zinazoimbwa vibaya zirekebishwe, na za zamani ziimbwe pia, na pawepo mchanganyiko mzuri wa angalau wimbo mmoja wa kwaya au kikundi.

(25)

vipengele mbalimbali vya Shule ya Sabato, na taarifa za ukuaji na maendeleo Shule ya Sabato. Zingatia mashauri

yafuatayo:-1. Mkuu wa Shule ya Sabato au mmoja wa wasaidizi wake ndio wanaopaswa kuwa wenyeviti wa programu hii, na wasiuache wajibu huu kwa mshiriki mwingine yeyote, hata kama ni kikundi kimealikwa kuendesha Shule ya Sabato.

2. Kila mhusika awepo mahali pake kwa wakati. 3. Kila mhusika awe mwenye mwonekano mzuri. 4. Tumia lugha tamu iliyo fasaha na ya kuvutia.

5. Wakaribishaji wajae tabasamu na uangalifu katika kuwakaribisha watu. 6. Pangilia programu yako, kila mmoja ajue cha kufanya kwa wakati

husika.

7. Uwe mwanana, ruhusu waabuduo kupumzika katika Nyumba ya Mungu kwa kutowatwika malaumu, amri, maagizo mengi, au maswali mengi. 8. Epuka kutumia vifupisho visivyo rasmi – kama “S/S”, “SDA”, “Lesoni”

“Wasabato”, n.k.

UKUZAJI:

unapaswa kulenga moja ya malengo manne ya Shule ya Sabato ambayo ni

1. Kujifunza maandiko matakatifu 2. Ushirika

3. Kuifikia jamii inayotuzunguka, na 4. Kukazia utume ulimwenguni

Ukuzaji waweza kuwa juu ya

yafuatayo:-1. Mahudhurio kwenye Shule ya Sabato 2. Usomaji wa Biblia wenye mafanikio 3. Kukariri mafungu

4. Ushuhudiaji kwa majirani zetu 5. Madarasa ya watu 6 hadi 8 6. Sabato ya wageni

7. Sabato za kupandisha darasa

8. Kuanzisha na kuendesha tawi la Shule ya Sabato 9. Sabato ya Rale za Shule ya Sabato

10. Ununuzi na usomaji wa miongozo ya kujifunza Biblia 11. Siku za kufanya maamuzi

12. Matangazo ya Shule ya Sabato

 Anayepangwa kutoa ukuzaji, aelezwe mada ya kushughulikia.  Huu si muda wa kuhubiri.

TAARIFA ZA SHULE YA SABATO

(26)

UANDAAJI WA TAARIFA

Yafuatayo ni muhimu kuhusishwa katika taarifa:

1. Mahudhurio kwenye Shule ya Sabato, yakionesha wageni walioshiriki, washiriki waliowahi na waliochelewa.

2. Taarifa za ushuhudiaji.

3. Taarifa za wenye miongozo ya kujifunza Biblia na ambao wameisoma.

4. Taarifa fupi za darasa la waalimu na idadi ya madarasa ya Shule ya Sabato yaliyoendeshwa.

UTOAJI WA TAARIFA Yafuatayo yazingatiwe:

1. Kila taarifa ilinganishwe na iliyotangulia na ioneshe kama kuna kukua, kudumaa, au kurudi nyuma.

2. Tumia mchoro kuonesha picha ya maendeleo

3. Si lazima kutoa taarifa linganifu kila Sabato, lakini ni lazima iandaliwe kila Sabato. Usipitishe mwezi bila kutoa taarifa linganifu.

4. Kila mwisho wa robo, taarifa ya robo nzima, ile inayokwenda Fildi / Konferensi, ikijumlisha nyongeza ya mambo yanayohusu Kanisa mahalia, itolewe mbele ya washiriki kwa namna ya kuvutia.

C. Dakika 60 zinazofuata

(3:34 – 4:45) zitumike kwenye madara ya Shule ya Sabato. Kila darasa liwe na watu wasiopungua 6 na wasiozidi 8. Kila darasa liwe na viongozi watatu. Mwalimu, Mratibu na Katibu.

Dakika 20 au 25 za kwanza zitumike kwa shughuli za darasa kwa karani kutoa kwa kifupi picha ya maendeleo ya darasa, kuchukua mahudhurio, na kupanga namna ya kutembelea waliokosekana. Na kwa mratibu kuchukua taarifa za ushuhudiaji na kuhimiza ushuhudiaji.

Dakika 35 au 40 zitumike kujadili somo la juma hilo.

MUHIMU:

Imesisitizwa sana kuwa kila Sabato tuwe na muda

usiopungua dakika 30 za kujifunza Biblia kupitia mwongozo wa

kujifunza Biblia.

………

………

………

………

………

VITABU VYA REJEA:

<> Kanuni za Kanisa, Toleo la 17, 2005. <> Sabbath School Handbook .

(27)

KAMATI YA UWAKILI NA MAENDELEO

A. WAJUMBE WAKE:

1. Idadi ya wajumbe inategemea ukubwa wa Kanisa. Katika makanisa madogo pengine kazi za kamati hii hufanywa na baraza la Kanisa moja kwa moja.

2. Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-a. Mwenyekiti wa kamati

b. Mzee wa Kanisa

c. Mtunza hazina wa Kanisa d. Karani wa Kanisa

e. Kiongozi wa uwakili (Katibu)

f. Na wengine watakaoonekana kuhitajika

3. Mwenyekiti wa kamati hii anachaguliwa kama ofisa wa Kanisa kwa kazi hii, naye ni mjuzi hasa wa miongozo ya Kanisa.

B. SIFA ZA WANAKAMATI:

1. Wawe watu waliojitoa kikamilifu katika kutekeleza wajibu wa Kanisa 2. Wawe na uzoefu au ujuzi wa kupanga mikakati au shughuli za

maendeleo

3. Wawe tayari kutoa muda wao na nguvu zao nyingi kwa faida ya utumishi wa Kanisa

4. Wawe watu wenye mvuto mzuri kwa washiriki wenzao 5. Juu ya yote wawe mawakili waaminifu

C. KAZI ZA KAMATI:

1. Kubuni njia za kuendeleza familia Kanisa ili izidi kukua katika neema-kiroho, kijamii, kimwili, na kiuchumi.

2. Itawaelimisha washiriki namna ya kuishi kwa kujitosheleza kiuchumi kama familia binafsi nyumbani mwao, na kama Kanisa la Kristo katika ngazi zote.

3. Itawaelimisha washiriki kujua na kutekeleza wajibu wao kama mawakili wa Mungu na watumishi wa Kristo.

4. Itawaelimisha washiriki namna ya kuongeza si matoleo ya zaka na sadaka tu, pia kuinua kipato chao ili hali yao ya uchumi iinuke.

(28)

6. Itahamasisha utekelezaji wote wa mipango yote ya maendeleo kanisani – kama ujenzi wa makanisa, ujenzi wa Nyumba za watumishi, upatikanaji wa vifaa vya kufanyia uinjilisti, na program zingine za huduma kwa jamii.

7. Itabuni mbinu na njia za kuongeza mawakili waaminifu kanisani – watoaji wa zaka na sadaka kwa uaminifu, na wenye moyo wa kujitoa zaidi katika kuendeleza kazi ya Mungu.

8. Itabuni mbinu na njia za kuongeza mawakili waaminifu kanisani – watoaji wa zaka na sadaka kwa uaminifu, na wenye moyo wa kujitolea zaidi katika kuendeleza kazi ya Mungu.

9. Itabuni utaratibu wa kutambua vipawa na talanta mbalimbali za washiriki wa Kanisa, na kuviingiza katika utumishi wa injili na maendeleo ya Kanisa.

10. Itapokea na kufanyia kazi mipango na mikakati mbalimbali ya idara ya uwakili kutoka Fildi au Konferensi na kutoa taarifa juu ya maendeleo ya utekelezaji wake

11. Itafanya kazi zingine zote ambazo mkutano wa mashauri ya Kanisa utaitaka ifanye.

D. JINSI YA KUFANYA KAZI ZAKE:

Kamati hii inazo sehemu tatu za utendaji zitakazojulikana kama vikundi vya utekelezaji wa kamati.

1. KIKUNDI CHA ELIMU:

Kikundi hiki kitashughulikia program zote na majukumu yote yanayodai elimu

a. Kupendekeza masomo wa ajili ya washiriki mwaka hadi mwaka b. Kuendesha na kusimamia utolewaji wa elimu kwa washiriki yenye

lengo la kuwakomaza kiakili, kiroho na kimwili

Mwenyekiti: Karani wa Kanisa

2. KIKUNDI CHA BAJETI NA FEDHA:

Kikundi hiki kinasimamia program zote zinazohusu fedha – utaratibu wa kuingia na kutoka kwa kufuata sera za Kanisa na kutawala fedha na bajeti

a. Kuandaa jicho la Kanisa na kuhakikisha kuwa linajazwa na linafanya kazi yake.

b. Kutoa taarifa kwa mshiriki mmoja juu ya matoleo yake kwa kufuatana na matoleo yake na ujazwaji wa jicho la Kanisa.

c. Kuhakikisha kuwa washiriki wana bahasha kwa ajili ya matoleo yao na kuwaelimisha juu ya matumizi yake.

d. Kugawa mifuko kwa washiriki kwa ajili ya zaka ya vitu halisi (mahindi, maharage, n.k.)

Mwenyekiti: Mhazini wa Kanisa.

(29)

Program zote za kuhamasisha washiriki na kueleza mipango ya kazi zinazotekelezwa na kikundi hiki, mfano:

a. Kupendekeza mambo ya kufanyika kwa kuyawekea kipaumbele b. Kupendekeza magoli ya utendaji wa mwaka

c. Kupendekeza kalenda ya kazi za Kanisa ikionyesha tarehe za kuanza na tarehe za kumaliza

d. Kupendekeza matendo ya kufanywa na Kanisa na gharama zote zitakiwazo kuyakamilisha na mahali pa kuzitoa.

e. Watatathmini waaminifu katika matoleo na kupendekeza njia za kuboresha uaminifu katika matoleo

Mwenyekiti: Katibu wa Uwakili.

E. UTENDAJI NA UTEKELEZAJI:

1. Mipango yote na maazimio yote ya kamati yanafikiwa kwa pamoja na hatimaye Kanisa linayapitisha kama maazimio yake. Baada ya hatua hii, hatua za utekelezaji zaweza kuendelea kwa kutumia vikundi husika na program. Yaani, kila kikundi kinaweza kukaa na kutekeleza maazimio yanayokihusu bila kusubiri kamati yote.

2. Wajumbe wa kamati hii huwa watano au zaidi, itajengwa katika vikundi vya utekelezaji kuzingatia uwezo wa wajumbe.

3. Kamati yote inakaa pamoja angalau mara moja kwa mwezi, siyo kwa robo. Vikao vya maendeleo vinakutana kila baada ya muda mfupi.

IDARA YA UWAKILI NA MAENDELEO

Idara ya Uwakili na maendeleo ilianzishwa ili kutimiza mpango wa utaratibu wa utoaji wa ukarimu wa Mungu popote kwa Kanisa lake. Kwa kuwa wajibu wa uwakili wa mwanadamu wahusu utawala mzima wa maisha, wazo la uwakili hutia nguvu uangalifu hasa wa matumizi ya hekalu la Mungu, wakati, uwezo, na mali aliyonayo.

A. Sifa Za Katibu Wa Uwakili:

1. Awe kiongozi wa kiroho

2. Awe ni mtu mwenye mazoea ya kutimiza kanuni za uwakili wa kikristo 3. Awe anaufahamu mpango wa Kanisa wa mali na wa kiroho

4. Awe tayari kujitolea kwa wakati wake, kupanga kuinua na kuongoza katika Nyanja alizopewa za wajibu wake akishirikiana na mkurugenzi wa uwakili wa fildi / konferensi, Mchungaji wa mtaa na baraza la Kanisa. 5. Katibu wa uwakili anafanya kazi kati ya idara ya uwakili ya fildi /

konferensi na Kanisa katika kutimiza wajibu wake wa kuelimisha, atatekeleza mpango wa elimu ya kawaida ya idara ya uwakili kama inavyotolewa na kupanuliwa kwa vipindi vyake ili kutimiza haja inayoendelea kuongezeka.

(30)

sadaka, na kufundisha njia za msingi ya uwakili wakati wa huduma ya siku ya Sabato au wakati mwingine wowote.

B. Majukumu ya Katibu wa Uwakili Kanisani:

1. Yeye ni katibu wa kamati ya uwakili kanisani

2. Husaidiana na mzee wa Kanisa kuandaa taarifa ya uwakili kwenda fildi / konferensi kila mwezi, na kumkabidhi mchungaji wa mtaa kwa tarehe husika.

3. Kulinda na kulifanyia kazi “Jicho La Kanisa”

4. Kuandaa taarifa ya mshiriki mmoja mmoja na kumtumia

5. Kuhamasisha washiriki kurudisha zaka na kutoa sadaka kwa uaminifu huku yeye akiwa kielelezo

6. Kuandaa na kuwasilisha taarifa kwa baraza la Kanisa mara moja kila robo

7. Kuhakikisha kwamba kila mipango na mikakati ya kamati ya uwakili ya Kanisa inatekelezwa na wahusika kama ilivyoamriwa na kupitishwa katika kamati ya uwakili ya Kanisa.

8. Kumsaidia Mchungaji / Mzee wa Kanisa katika kutekeleza mipango mbalimbali ya uwakili toka fildi / konferensi / Union / divisheni.

9. Kuhakikisha kuwa elimu ya uwakili inatolewa kanisani kwa washiriki wa rika zote na yeye mwenyewe akiwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.

10. Kutembelea washiriki katika harakati za kukuza elimu ya uwakili katika maisha yao.

11. Kuhakikisha kuwa kupindi cha somo la matoleo cha kila Sabato kina mhudumu na anafanya kazi yake inavyostahili.

12. Kutayarisha na kusimamia semina za namna ya kujiajiri.

13. Kuratibu na kusimamia juma la uwakili kama linavyoonyeshwa katika kalenda ya matukio ya mwaka.

14. Utunzaji siri wa washiriki, upendo, uaminifu na uadilifu, umakini na uyakinifu, vyapasa kuuzunguka utendaji wa Katibu wa Uwakili na kamati yake.

Ujumbe maalum:

“Wakati watakapoamka na kuweka

maombi yao, utajiri wao, na nguvu zao zote na mali zao zote

miguuni pa Yesu, kazi ya kueneza ukweli

itashinda”

(4T.475).

JICHO LA KANISA

Kifaa muhimu kwa ajili ya huduma ya mchungaji / mzee wa Kanisa / mtunza hazina na katibu wa uwakili wa kanisa.

A. Mambo ya kuzingatia katika kulijaza na kulifanyia kazi jicho la Kanisa:

(31)

1. Viongozi wa Fildi / Konferensi / Union / Mchungaji Wa Mtaa 2. M(wa)zee wa Kanisa hilo

3. Mtunza Kanisa wa Kanisa hilo 4. Katibu wa uwakili wa Kanisa hilo

B. Jicho la Kanisa liwe na sehemu kuu tatu:

1. Orodha ya washiriki walioko kanisani, likianza na maofisa wa Kanisa hilo 2. Orodha ya wale ambao hawana ushirika kanisani hapo – wamehamia

karibuni na hawajaleta ushirika wao

3. Orodha ya wanafunzi wa darasa la ubatizo.

C. Matumizi ya jicho la kanisa:

1. Husaidia kujua maendeleo ya kiroho ya washiriki, Tendo la urudishaji wa zaka na sadaka ni moja ya mazoezi muhimu ya kiroho ambayo hudhihirisha uhusiano uliopo kati ya mtoaji na Mungu wake. Utoaji wa uaminifu huashiria kuwepo kwa uhusiano bora wa kiroho kati ya mtoaji na Bwana Mungu. Utoaji wa uaminifu huashiria kuwepo kwa uhusiano bora wa kiroho kati ya mtoaji na Bwana Mungu. Kwa mantiki hiyo, utoaji huwa ni pima joto la kiroho.

2. Husaidia katika kutoa taarifa ya maendeleo ya washiriki waaminifu kila robo.

3. Humsaidia mchungaji au mzee wa Kanisa, kujua wadhaifu na kuwasaidia, na kuwajua waaminifu na kuwatia moyo.

4. Hutumika wakati wa uchaguzi wa maofisa wa Kanisa 5. Husaidia kujaza kadi za ushirika na zile za ubatizo

6. Husaidia kutoa taarifa kwa mshiriki mmoja mmoja juu ya matoleo yake kwa muda uliokusudiwa.

7. Humsaidia mtunza hazina kutoa taarifa za washiriki kila mwezi kwa mchungaji wa mtaa wakati anapopokea taarifa za matokeo

8. Huweza kutumika katika uchambuzi wa mahesabu, kama nyenzo ya

udhibiti wa ndani wa fedha.

REJEA

:

Uwakili ni Mtindo wa Maisha-TUM.

IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA

Lengo kuu : Kuimairisha familia kama kituo cha ufundishaji wa nidhamu.  Huduma za familia hulenga watu katika mahusiano. Huhusika na mahitaji

ya wale waliooana, wazazi na watoto, mahitaji ya kifamilia kwa waseja na watu wote katika mzunguko huo mpana wa familia.

 Malezi ya waumini wote kanisani hayawezi kufanikiwa nje ya kaya na familia

A. Majukumu ya Kiongozi wa Huduma za Familia na kamati

yake:

1. Kuanisha familia zilizopo (fomu maalum zaweza kutumika).

(32)

3. Kutembelea wajane na wagane mara kwa mara kwa sababu ya matatizo ya upweke wao na kiwasaidia kutatua matatizo yao.

4. Kuombea familia mbalimbali katika maombi yake ya faragha

5. Kutia moyo kila familia kuimaisha ibada za familia (madhabahu ya nyumbani). Malezi ya familia hayawezi kukamilika kama familia hazijilishi kiroho.

6. Kuratibu vijana na watoto wa familia ambao hawajajiunga na vyama vinavyosaidia watoto na vijana kiroho, kuwashauri (kwa kushikisha na wazazi) kujiunga na vyama husika.

7. Kulisaidia Kanisa kuishi kama familia yenye upendo, kwa kushughulikia maafa, misiba, harusi, magonjwa, kati ya jamii ya waumini.

8. Kuweka ratiba ya kula pamoja kikanisa, kuimba, kutoa visa, kama njia ya kuleta furaha na amani kati ya washiriki. Wanaweza kushirikisha waimbaji na utaratibu huu wafaa mara moja kwa robo.

9. Idara ina jukumu la kuangalia kuwa kaya na familia hazisumbuliwi na ukabila, au tabaka la utajiri na umaskini.

10. Idara inahusika vile vile kuzungumzia unyanyasaji unaofanywa na watu katika kaya na familia.

11. Jukumu lingine la idara ni kufuatilia habari zinazojulikana za waumini, kushughulikia kiroho kwanza kabla ya kukatwa na Kanisa.

12. Idara vile vile ina jukumu lingine zito la kuangalia baadhi ya mila zinazotaabisha familia na kaya.

13. Idara iwe na lengo la kutia moyo watu wote kujiunga na huduma zilizomo kanisani. Idara inapswa kuangalia afya ya Kanisa kiroho na kimwili sawa na wazazi wanavyoangalia afya za watoto na familia nyumbani.

14. Kuandaa mipango / malengo na bajeti ya idara.

15. Kiongozi wa idara ana wajibu wa kuhudhuria baraza la Kanisa.

B. MIPANGO NA MALENGO YA IDARA YA HUDUMA ZA FAMILIA (Baadhi):

1. Vijana kufundishwa unyumba ipasavyo kabla ya kufunga ndoa.

2. Kuwasaidia (kuwashauri) vijana kupima Ukimwi kabla ya kuoana.

3. Kuwaona watu ambao wamerudi nyuma kiroho kwa sababu zinazochangiwa na migogoro katika kaya / familia.

4. Pawepo na lengo la kuwatembelea wajane na wagane kila robo.

5. Kuhamasisha washiriki kutoa michango kwa familia zilizo na dhiki.

 Zaidi soma Kanuni, 2005, 9-38, 39)

IDARA YA HUDUMA ZA UCHAPISHAJI

(33)

Inalisaidia kanisa la pale pale katika ukuzaji mauzo, na usambazaji wa magazeti na vitabu vingine vya utume vinavyouzwa. Idara hutenda kazi na mchungaji, na idara za kanisa katika kupanga njia za hatua kwa hatua za kuwashirikisha washiriki wa kanisa katika kuyatimiza malengo hayo.

“Ziko sehemu nyingi ambako sauti ya mchungaji haiwezi kusikika, sehemu zinazoweza kufikiwa kwa machapisho yetu tu-vitabu, vipeperushi na vijizuu vilivyojazwa na kweli za Biblia ambazo watu wanazihitaji” (Colporteur Ministry, p.4)

Baadhi ya majukumu ya Mratibu wa Huduma za Uchapishaji wa kanisa: 1. Kuandaa wainjilisti wa vitabu (kwa kuhamasisha na kutoa mafunzo). Idara inahusika katika kutoa semina za uinjilisti wa vitabu ili kuandaa watu watakaojitoa kwa kazi hiyo. Kupitia Kamati ya Huduma za Uchapishaji, Idara hupendekeza washiriki wa Kanisa wenye vipawa kutenda kazi ya uinjilisti wa vitabu. Ni jukumu la idara kuhamasisha washiriki wakiunge katika kazi ya uinjilisti wa vitabu.

2. Kuweka kiwango na kuisimamia kazi ya kusambaza vitabu na magazeti. Kazi ya kusambaza machapisho yetu ni kazi ya kila mshiriki.

3. Kuumba shauku kubwa miongoni mwa washiriki wa Kanisa kujipatia, kusoma na kuvithamini vitabu vya Ki-adventista vilivyothibitishwa na viatabu vya roho ya unabii ambayo huliainisha Kanisa la Waadventista wa Sabato kama la unabii wa wakati wa mwisho.

4. Kuanzisha mafunzo ya uinjilisti kwa njia ya vitabu. Hii itasaidia washiriki wa Kanisa kupata ufahamu kimawazo na kithiolojia wa asili na utume wa huduma ya vitabu kama shughuli ya kimishonary ya Kanisa mahalia.

5. Kuendeleza na kutekeleza mikakati ya usambazaji vitabu ya washiriki wa Kanisa wenyewe.

6. Kupanga, kutekeleza, kuratibu na kuhakiki shughuli za huduma ya vitabu.

7. Kushauriana na kushirikiana na baraza la Kanisa kuhusu mipango na shughuli za huduma ya vitabu.

8. Kuandaa mikutano ya huduma za vitabu kwa ajili ya Kanisa mahalia na kupata muwezeshaji kutoka ngazi za juu za Kanisa.

9. Kukuzia ununuaji na usomaji wa vitabu vya roho ya unabii kwa ajili ya malezi na ukuaji binafsi wa kiroho.

(34)

11. Kuelimisha kwa kutoa mafunzo, kuongoza na kuelekeza Kanisa kenye uinjilisti ulio hai kwa njia ya vitabu na kaika kufahamu asili yake.

12. Kuandikisha washiriki wa Kanisa katika kazi ya vitabu kupitia kwa timu zilizoundwa au kupitia kazi ya mtu mmoja mmoja.

13. Kuagiza vitabu kulingana na vinavyohitajika kupitia kwa katibu wa huduma za washiriki.

14. Kutoa taarifa za shughuli za huduma ya vitabu kwenye baraza la kanisa na mkutano wa mashauri ya Kanisa.

15. Kuwasilisha taarifa konferensi kupitia kwa Mchungaji wa Mtaa.

 Baraza la Huduma za Uchapishaji-Knn, 2005, 9-61….

IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

Idara ya Huduma za Wanawake ipo kwa ajili ya kuunga mkono, kutia moyo, na kutoa changamoto kwa wanawake Waadventista wa Sabato katika mwenendo wao wa kila siku kama wanafunzi wa Yesu Kristo na kama washiriki wa Kanisa la ulimwenguni. Utume wa Huduma za Wanawake kwa maana pana, ni sawasawa na ule wa wakristo wote – ule wa kumwiinua Kristo katika Kanisa na ulimwenguni.

A. Malengo – Huduma hii inajaribu:

1. Kuendeleza ukuaji kiroho na kufanyika kwa moyo mpya miongoni mwa wanawake.

2. Kusisitiza kwamba wanawake ni wa thamani isiyoweza kukadirika kwa sababu ya kule kuumbwa na kukombolewa kwao, na kuwapatia nyenzo kwa ajili ya utumishi kanisani.

3. Kuhudumia kwa uchambuzi mpana wa mahitaji ya wanawake kwa mahitaji yote, kuchukulia kwa unyeti wake mitazamo ya tamaduni nyingi na makabila mbalimbali

(35)

5. Kuwashauri na kuwatia moyo wanawake Waadventista wa Sabato, kwa kuanzisha njia za wao kujihusisha na Kanisa ili wafikie uwezo wa kufaa kwao katika Kristo.

6. Kutafuta njia na jinsi ya kutoa changamoto kwa kila mwanamke Mwadventista Msabato ili atumie karama zake kuchnangia talanta za wengine kadri wanavyofanya kazi bega kwa bega kuendeleza utume wa Kanisa kwa dunia yote.

B. Sifa Za Kiongozi Wa Huduma Za Wanawake

Mwanamke aliye mwepesi wa kuhisi, anayejali, anayejisikia kuwa na mzigo wa huduma na matatizo ya wanawake. Awezaye kuwatia moyo wanawake wengine waendeleze karama zao za kiroho. Awe anaayeweza kufanya kazi vizuri na wanawake kanisani, mchungaji, na baraza la Kanisa.

C. Baadhi Ya Majukumu Ya Kiongozi Wa Huduma Za Wanawake

1. Yeye hutumika kama mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Wanawake 2. Huhimiza mawazo na mipango ambayo hutumia kwa kiwango cha juu

michango ya wanawake kwa utume wa Kanisa.

3. Kuona kwamba malengo ya idara, kama yalivyoanishwa hapo juu, yanatekelezwa.

(36)

MUUNDO WA IDARA YA HUDUMA ZA WANAWAKE

IDARA YA MIRATHI NA WOSIA

(Ezekieli

3:16-21)

Referensi

Dokumen terkait

Kwa mujibu wa Nadharia ya Fasihi Linganishi, mtafiti amebaini kuwa katika riwaya ya Utengano, wanawake walikuwa ni tegemezi zaidi kwa wanaume tofauti na riwaya ya Kamwe si mbali

Kwa kuwa, wahusika wa aina mbalimbali hujitokeza katika kazi za fasihi na wahusika hao husawiriwa wakiakisi maisha ya wanajamii, hivyo, tumehamasika kufanya

Inakadiriwa kuwa katika mkoa wa Shinyanga kiwango cha “ujinga” kinafikia 35%, Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ujinga na kutokuwa na elimu ya stadi za maisha katika jamii

Kaida hii ya lugha ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa lahaja za Kiswahili (Mdee, 1998). Kama tulivyokwishaeleza katika usuli, tafiti nyingi zilizokwishafanywa kuhusu lahaja

Kwa mujibu wa data zilizopatikana, kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi kina dhima zifuatazo za kisarufi ; dhima ya kiima ambayo ni neno, kirai au kishazi ambacho

Kutokana na ukweli kwamba lugha ya Kiswahili na Kiyao zinatumiwa pamoja kwa muda mrefu hususani maeneo ya Wilaya za Songea, Tunduru na Namtumbo katika mkoa wa

Kama sisi washiriki endapo tutakubali kuwa watumwa wa yesu kristo ,na kufanya wajibu wetu kama watumwa wake, ndipo kazi ya Mungu?. itakapofanywa kwa moyo wote na matunda yake

Watoto wasio na fursa ya kuwa kanisani, huelekezwa kwa pendo la Yesu kupitia huduma za ushuhudiaji kama vile: Masomo ya Biblia Nyakati za likizo, matawi ya shule ya sabato ya