• Tidak ada hasil yang ditemukan

Taarifa ya Tathimini na Ufuatiliaji wa Hali ya UKIMWI Mkoani Shinyanga

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2021

Membagikan "Taarifa ya Tathimini na Ufuatiliaji wa Hali ya UKIMWI Mkoani Shinyanga"

Copied!
19
0
0

Teks penuh

(1)

TAARIFA YA TATHIMINI NA

UFUATILIAJI WA HALI YA UKIMWI

MKOANI SHINYANGA

TA

CAID

S

TU ME YA K U D H IBIT IUK IMW ITAN ZANIA C OMM IS S IO N F O R A ID S May 2011

(2)

YALIYOMO

SHUKURANI ... 4

HALI YA VVU NA UKIMWI MKOANI SHINYANGA ... 5

VICHOCHEO VYA MAAMBUKIZI ... 11

CHANGAMOTO ... 15

(3)

MAJEDWALI

Jedwali 1: Kiwango cha Maambukizi Kiwilaya ... 6 Jedwali 2: Idadi ya vituo vya Afya vinavyotoa Huduma

za VVU na UKIMWI 2010... 7 Jedwali 3: Hali Ya Maambukizi Ya VVU ... 8 Jedwali 4: Huduma za Utambuzi wa VVU

kwa Watoto Wachanga (HEID) ... 8 Jedwali 5: Huduma za Tiba na Matibabu ... 9 Jedwali 6: Huduma Majumbani ... 9 Jedwali 7: Watoto yatima na Wanaoishi katika

(4)

SHUKURANI

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania inapenda kutoa shukurani kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa kukubali ombi la Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania pamoja na wadau wengine kufanya ziara mkoani Shinyanga kwa lengo la kuangalia na kuchambua hali ya UKIMWI kwa njia ya mijadala na kutumia taarifa zilizopo.

Shukurani zinatolewa pia kwa viongozi wa Halmashauri ya Manisipaa ya Shinyanga, Maswa, Kahama na Bariadi. Tunatoa shukurani kwa Kamishina wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI, uongozi wa Wiraza ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Baraza la Watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) kwa kukubali kwao kushiriki katika zoezi hili.

Utafiti huu usingefanikiwa bila ya ushirikiano na wadau mbalimbali Mkoani na kwenye Halmashauri zilizotembelewa. Tume inawashukuru Mratibu wa Mkoa wa Shinyanga na Waratibu wa Mwitikio wa Taifa wa kudhibiti maambukizo ya VVU na UKIMWI katika Halmashauri,vivyo hivyo kwa watumishi wa Tume.

Vile vile shukurani zinatolewa kwa wale wote waliosaidia kupatikana kwa taarifa mbalimbali, ikiwa ni pamajo na viongozi wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya, watoa huduma za afya, viongozi wa kisiasa hususani waheshimiwa madiwani, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wadau wa maendeleo, watu maarufu, wahudumu katika sehemu za vileo na nyumba za kulala wageni, kamati za Mwitikio wa Taifa za kudhibiti VVU na UKIMWI katika Halmashauri, Kata, Vijiji na wananchi kwa ujumla.

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa “Tanzania bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana”

Dr. Fatma H. Mrisho Mwenyekiti Mtendaji

(5)

SURA 1

HALI YA VVU NA UKIMWI MKOANI SHINYANGA

Ufuatiliaji na tathmini ya hali halisi ya UKIMWI mkoani Shinyanga ulifanyika Mei 2011 ukijumuisha watumishi kutoka; Tume ya Kudhibiti UKIMWI, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Baraza la Watu wanaoishi na VVU na Vyombo vya Habari

Mkoa wa Shinyanga upo Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania na Kusini mwa ziwa Victoria kati ya longitudo 20 15ʹ na 40 30ʹ kusini na longitudo 310 14ʹ na 350 11ʹ Mashariki. Mipaka ya Mkoa wa Shinyanga inatengenezwa na ile ya mikoa ya Mwanza, Kagera na Mara kwa upande wa Magharibi, Manyara na Singida kwa upande wa Mashariki na kwa upande wa Kusini ni Mikoa ya Kigoma na Tabora. Mkoa una jumla ya kilometa za mraba 50,781 na Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya watu 3,692,941.

Kiutawala Mkoa wa Shinyanga unatengenezwa na Halmashauri za Wilaya saba (7) na Halmashauri ya Manispaa moja (1), Tarafa 27, Kata 160 na Vijiji 869. Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa Mikoa yenye rasilimali nyingi zinazochangia katika pato la Taifa. Miongoni mwa rasilimali hizo ni pamoja na madini ya Almasi na Dhahabu. Pia Mkoa ni maarufu kwa zao la pamba na ufugaji wa ng’ombe.

Mtu mwenye maambukizo ya VVU alitambuliwa mwaka 1986 Mkoani Shinyanga kwa mara ya kwanza. Kufikia mwaka 1988, takribani wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga zilikuwa zimeripoti kuwa na wagonjwa wa UKIMWI. Kiwango cha maambukizo ya VVU Mkoa wa Shinyanga ni asilimia 7.4 (THMIS, 2007/08). Mkoa Shinyanga ni miongoni mwa Mikoa nane (8) yenye maambukizo ya juu ya VVU zaidi ya kiwango cha Taifa cha asilimia 5.7. Mikoa mingine ikiwa ni pamoja na Iringa, Mbeya, Dar es Salaam, Mara, Tabora, Mwanza na Pwani. Wilaya ya Kahama, ndiyo inayoongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya VVU ya asilimia kumi (10%) kwa takwimu za upimaji wa hiari za mwaka 2010.

(6)

Jedwali 1: Kiwango cha Maambukizi Kiwilaya Halmashauri KIWANGO 2008 (%) 2009 (%) 2010 (%) Kahama 9.6 7.8 10 Maswa 8.5 0.8 7.5 Bukombe 8.0 11.5 8.0 Shinyanga MC 7.4 7.4 8.4 Shinyanga DC 5.3 6.1 10.9 Kishapu 4.0 7.9 4.4 Bariadi 3.3 6.7 6.9 Meatu 2.4 2.3 6.7

(Chanzo: Takwimu Mpango wa Upimaji VVU kwa Hiari Shinyanga 2009/2010) Mkoa wa Shinyanga una jumla ya vituo vya afya 343 na takribani kila kituo cha afya kinatoa huduma mbalimbali za zinazohusiana na VVU na UKIMWI kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali 2:

Wajumbe wa KONGA (Council for People Living with AIDS) wilaya ya Maswa katika mjadala na watumishi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI

(7)

Jedwali 2: Idadi ya Vituo vya Afya Vinavyotoa Huduma za VVU na UKIMWI 2010

DISTRICT HFs CTC VCT PITC PMTCT HEID TB/

HIV HBC STI RPR Bariadi 63 5 29 7 53 2 7 19 38 40 Bukombe 33 5 12 5 19 3 5 18 18 19 Kahama 53 5 25 36 39 4 10 35 45 39 Kishapu 55 6 6 5 40 4 7 12 22 15q Maswa 41 5 17 5 38 3 6 9 30 39 Meatu 41 5 30 5 39 2 1 18 33 7 Shinyanga DC 33 4 26 8 26 2 3 16 25 33 Shinyanga MC 28 6 17 5 12 5 5 11 15 12

Katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2009, kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu waliopata ushauri nasaha na kupima kwa hiari kilikuwa asilima sita (6%). Katika kipindi hicho hicho, kiwango cha maambukizi ya VVU kwa akina mama wajawazito waliojitokeza kupata huduma ya kuzuia mamabukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto kilikuwa takribani asilimia nne (4%).

Mpango wa damu salama umeonyesha kushuka kwa kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wanaojitolea kutoa damu salama, kutoka asilimia nne (4.1%) mwaka 2008 hadi kufikia asilimia mbili (2.5%) kwa mwaka 2009.

(8)

Jedwali 3: Hali Ya Maambukizi Ya VVU

2008 2009

Huduma Pima +ve % Pima +ve %

Ushauri nasaha na

upimaji hiari (VCT) 151590 9988 6.6 156261 10442 6.7

Kuzuia mamabukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)

88617 3949 4.5 125586 4857 3.9

Huduma ya damu salama (Safe Blood Transfusion)

18354 751 4.1 33871 835 2.5

Jedwali 4: Huduma za Utambuzi wa VVU kwa Watoto Wachanga (HEID)

2009 2010

Jumla ya waliopima

Wenye VVU (%) Jumla ya

waliopima

Wenye VVU (%)

428 8.9 (38/428) 1150 11.04 (127/1150)

Takwimu za kutambua maambukizi ya VVU mapema kwa mtoto mchanga zilizopatikana katika halmashauri nne (4) zilizotembelewa zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha mwaka 2009 na 2010, kiwango cha huduma hizi bado kiko chini. Kati ya watoto 428 waliozaliwa na mama wenye virusi vya VVU, takribani asilimia tisa ya watoto hao walikutwa na VVU, licha ya huduma hii kuendelea kuwafikia watoto wachache zaidi kama ilivyoripotiwa katika majadiliano na wadau wa sekta ya afya.

(9)

Jedwali 5: Huduma za Tiba na Matibabu 2008 2009 Jumla waliosajiliwa kwa matibabu Walio katika matibabu % ya walio katika tiba Jumla walio sajiliwa Walio katika matibabu %yawalio katika tiba Huduma za matibabu 23518 9169 25.2 32696 15067 42.14

Juhudi za serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo zinaendelea kote nchini ili kuhakikisha kuwa watu wenye VVU na UKIMWI wanapata huduma za matibabu kulingana na miongozo. Idadi ya wagonjwa waliosajiliwa na kupata huduma za matibabu katika hospitali na vituo vya afya pamoja na zahanati imekuwa ikiongezeka toka asilimia inshirini na tano (25.2%) mwaka 2008 hadi kufikia asilimia arobaini (42.14%) mwaka 2009

Jedwali 6: Huduma Majumbani Idadi ya watoa huduma majumbani ambao wamepata mafunzo Idadi ya wagonjwa waliofikiwa Idadi ya watoa huduma wa kujitolea ambao wamepata mafunzo Idadi ya vifo iliyotokea majumbani 2008 2009 2008 2009 2010 2008 2009 2008 2009 157 294 9178 23885 24112 402 553 461 251

Huduma za tiba na matunzo majumbani nazo zimekuwa zikiongezeka na idadi ya wagonjwa waliofia nyumbani ilipungua toka 461 mwaka 2008 hadi kufikia 251 mwaka 2009. Idadi ya wagonjwa waliofikiwa nayo imekuwa ikiongezeka toka 9178 mwaka 2008 hadi kufikia 23885 mwaka 2009 na 24112 kufikia mwaka 2010.

(10)

Jedwali 7: Watoto yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu Watoto yatima na waliopo katika mazingira magumu 2009

Wakiume 33632 (49.7%)

Wakike 34065 (50.3%)

Jumla 67696 100

Takwimu za mkoa wa Shinyanga kuhusu watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu nayo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Kiwango cha watoto hawa, yaani wa kiume na kike takribani kinalingana katika mkoa huu

(11)

SURA 2

VICHOCHEO VYA MAAMBUKIZI

Ili kufahamu vichocheo vikubwa vya maambukizi ya VVU mkoani Shinyanga, timu ya TACAIDS ilikutana na wadau mbalimbali wa UKIMWI na kubainisha vichocheo vifuatavyo:

MIKUSANYIKO YA KIJAMII NA SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Mikusanyiko mbalimbali ya kijamii na kiuchumi hasa inayofanyika wakati wa usiku imeonekana kuchangia kwa kiwango kikubwa ufanyaji wa ngono isiyo salama na kupelekea uwezekano mkubwa wa kupata maambukizo ya VVU. Mikusanyiko hiyo ni pamoja na minada, mikesha ya harusi, mbio za mwenge wa uhuru, makambi ya kidini, uvaaji wa mavazi yanayoonyesha maungo ya mwili na ulevi wa kupindukia. Tamaa za kipato na umasikini uliokithiri imeonekana pia ni moja ya vichocheo.

Biashara ya kuonyesha picha za ngono kupitia mikanda ya video kwa lengo la kupata kipato ilionyesha kuchochea kufanya ngono isiyo salama baada ya kuangalia picha hizo. Tabia inayoendelea ya kuoa wake wengi na kurithi wajane kwa mila za kisukuma, imeendelea kuwa ni kichocheo cha maambukizi ya VVU hasa pale ambapo anayerithiwa alifariki kwa UKIMWI.

Tabia ya wazazi kuona aibu kukaa na watoto wao kuzungumzia masuala yanayohusiana na ngono imeendelea kuwa ni kichochea cha maambukizi ya VVU. Mama Amina Salama-mzee maarufu toka kijiji cha Malampaka alisisitiza “ni mwiko na aibu kubwa kwa wazazi kuzungumzia masuala ya kujamiiana kama moja ya vyanzo vya maambukizi ya VVU” ukweli na ujumbe kuhusu UKIMWI huachiwa watoto watafute wanakoweza.

Waendesha magari makubwa wamekuwa ni kikwazo kikubwa katika mapambano ya maambukizo ya VVU na UKIMWI, kutumia vipato vyao kwa kuwa na wapenzi wengi kitu ambacho huchochea maambukizi ya VVU hasa maeneo ya Kagongwa na Isaka katika wilaya ya Kahama.

(12)

(i) Ngoma za utamaduni wa jamii ya kisukuma

Baadhi ya ngoma za utamaduni za jamii ya Wasukuma huambatana na matukio yanayochochea kufanya ngono zisizo salama mfano ni ngoma za “Bukango” kwa ajili ya matambiko ya wazazi waliozaa watoto mapacha au mtoto aliyetanguliza miguu.

“Bukango” Na uwezekano WA maambukizi ya VVU: Bwana Ghireka na Bwana Mashenene

Bwana John Ghireka ni mwanaharakati katika mapambano ya UKIMWI wilayani Maswa katika kijiji cha Malampaka, ni kiongozi wa kikundi kinachoitwa Huruma group. Bwana Ghireka kwa masikitiko alielezea jinsi ngoma ya Bukango inavyochochea na kutia hamasa watu kufanya ngono isiyo salama, alisisitiza “kwa mila za kisukuma, watoto mapacha ni ishara ya laana katika familia, hivyo wanapozaliwa mapacha wanalazimika kutakaswa ili kuondoa hiyo laana. Sherehe za kutakasa hukesha kwa takribani siku 3 hadi 5 mara moja kwa mwaka kwa kula na kunywa pombe kulingana na uwezo wa waandaji. Kila usiku unapoingia washiriki wanaruhusiwa kuchagua mwenza wao bila kujali ni mwenza wa nani katika kundi la washiriki. Katika mazingira hayo, Bwana Ghireka alilisisitiza “hakuna cha kinga utaipata wapi? Hapo ni peku peku tu”. Inapofika asubuhi washiriki hupongezana kwa mkesha uliopita.

Bwana Mashenene ni DAC wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na yeye alikuwa na haya ya kuongeza kuhusiana na Bukango “pamoja na dhana ya kutakasa watoto mapacha, lengo lingine kubwa ni kuendelea kutafuta watoto wengine mapacha ili ngoma hiyo iendelee kuchezwa kila mwaka, na kwa sababu hiyo matumizi ya kondomu hayapo kabisa”

“Mbina ya Salasini” ni ngoma za usiku za kimila ambazo hufanyika Mei 30 ya kila mwaka, ni ngoma ya kusherehekea mavuno ambayo watu hukesha katika mashindano ya ngoma na nyimbo. Mkesha huo huambatana na vitendo vya ngono zisizo salama. “Chagulaga” ni tukio jingine linalotokea mara baada ya kukamilika kwa ngoma ambayo huwa ni matokeo ya sherehe mbalimbali vijijini. Wanaume huchagua wasichana wa kufanya nao ngono aidha kwa makubaliano au hata kwa

(13)

lazima inapobidi pale ambapo muafaka haujafikiwa. Jamii hukaa kimya na kuchukulia ni sehemu ya mila na desturi za wasukuma.

“Bukwilima” wakati wa kutoa mahari bwana harusi na bibi harusi huambatana na kundi kubwa la wanaume na wanawake wapatao hamsini (50) hadi mia moja (100) ambao husindikiza wachumba kwa ajili ya sherehe za kutoa mahari. Sherehe hizi hudumu kwa muda wa siku moja hadi mbili, vitendo vya ngono hufanywa kwa kiasi kikubwa baina ya wanawake na wanaume katika kundi hilo. Kwa upande wa wasichana, kuteuliwa kushiriki katika kundi hilo ni fahari katika jamii na hupata Baraka zote za wazazi. Binti au msichana ambaye hakuteuliwa kushiriki katika sherehe hiyo wazazi hudiriki kumpeleka kwa mganga wa kienyeji ili akafanyiwe tambiko la kuondoa nuksi.

(ii) Utandawazi:

Utandawazi ulionekana kuwa ni kitu kizuri na cha maendeleo katika jamii, lakini umeathiri mienendo ya jamii hasa ya vijana, mfano matumizi ya mitandao mbalimbali inayolenga kuangalia picha za ngono ambazo hatimaye huamsha hamasa ya kufanya ngono. Matumizi ya simu za kiganjani zimechangia na kurahisisha mawasiliano kati ya mtu na mtu na hasa vijana ili kufanikisha azma zao za kufanya ngono.

(iii) Imani potofu baina ya jamii

Imani potofu kwa baadhi ya watu imekuwa in kichocheo cha maambukizi ya VVU ikiwa ni pamoja na vitendo vya ngono zembe kwa baadhi ya watu wakiamini tayari kuna dawa zinazozuia makali ya UKIMWI (ARVs) na hivyo maisha bado marefu. Uwepo wa kondomu umechangia kwa kiasi kikubwa kufanya mapenzi kiholela ambapo mara nyingine watu hawazingatii matumizi sahihi ya kondomu. Dawa za kienyeji zinazotolewa kwa njia ya ‘vikombe’ zimesababisha baadhi ya watu kuendelea na ngono zisizo salama kwa imani kuwa dawa imekwishapatikana.

Baadhi ya watu wenye umri mkubwa hufanya mapenzi na watoto wenye umri mdogo kwa imani kuwa wao ni salama zaidi hali ambayo imesababisha wengi wa watoto kuambukizwa VVU na pia kupata mimba

(14)

za utotoni. Pia ilionekana kuwa, uwezekano wa watoto waliozaliwa na VVU wa kuwaambukiza watu wazima ni mkubwa kutokana na imani hiyo hiyo kwamba watoto wako salama. Tabia ya mtu mmoja kuwa na idadi ya wapenzi wengi kwa wakati mmoja nayo kilionekana ni kichocheo cha maambukizi ya VVU.

Inakadiriwa kuwa katika mkoa wa Shinyanga kiwango cha “ujinga” kinafikia 35%, Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ujinga na kutokuwa na elimu ya stadi za maisha katika jamii ya watu wa Shinyanga husababisha ugumu kwa kiasi kikubwa katika mapokeo ya elimu ya VVU na UKIMWI. (iv) Mahusiano ya kijinsia

Katika jamii ya watu wa kabila la kisukuma mahusiano ya kijinsia yameonekana bado ni kikwazo cha maendeleo na yanachangia sana katika kuongeza maambukizi ya VVU hasa maeneo ya vijijini. Mfumo wa mwanaume kumkandamza mwanamke humfanya mwanaume kuwa na maamuzi ya mwisho kwa kila jambo, mwanamke huwa ni mnyonge siku zote katika maamuzi muhimu ya kiuchumi na kijamii. Mfano, katika jamii ya kisukuma, mwanaume ni mwenye maamuzi ya mwisho katika mapato yote yatokanayo na kazi walizozifanya pamoja kama mazao ya kilimo na mifugo pamoja na mahari zinazotokana na kuoza mabinti zao humilikiwa na wanaume.

Kutokana na ukubwa wa mfumo wa kumkandamiza mwanamke, kumesababisha wanawake kuogopa kuwa wawazi pale wanapopimwa na kubainika wameambukizwa VVU hushindwa kuwaeleza waume zao wakiogopa vipigo na hata wakati mwingine ndoa kuvunjika, huku baba akiendelea kueneza VVU kwa vile hataki kupima kujua afya yake. Watoto wa kike kunyimwa haki ya kupata elimu na kutumika kama sehemu ya kipato cha familia kutokana na mahari inayolipwa wanapoolewa. Inapofikia mwanaume kuhitaji kuongeza mke aidha kwa kuoa au kurithi mjane, mwanamke hashirikishwi zaidi ya kuletewa mwenzi wake. Vitendo vya ukatili kwa wanawake hasa ubakaji katika migodi ni vikubwa vinavyompelekea mwanamke kuwa katika hatari ya maambukizi ya VVU.

(15)

SURA 4

CHANGAMOTO

Katika juhudi za kupambana na tatizo la UKIMWI, mkoa wa Shinyanga unakumbana na changamoto zifuatazo:

Huduma hafifu za utambuzi mapema wa VVU (HIED) kwa watoto wachanga waliozaliwa na mama wenye VVU.

Watoaji huduma waliohojiwa katika vituo vya kutolea huduma walikiri kuwa tatizo hili ni kubwa sana katika mkoa huu. Mara kadhaa vitendea kazi (DBS) kwa ajili ya huduma hii vimekuwa vinakosekana, kuchelewa kupatikana kwa majibu ya vipimo hivyo ambapo wakati mwingine huchukua miezi mitatu hadi sita, majibu kupotea, majibu kuchanganywa na kupelekwa sehemu nyingine. Hali hii ya udhaifu katika mfumo wa utoaji wa huduma inachangaia kwa kiasi kikubwa sana kuufanya mpango wa kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto kutokidhi kwa kiwango mahususi malengo yaliyokusudiwa. Pia udhoofu wa huduma hii umeelezwa kuwa ni kikwazo kikubwa kwa akina mama wanaojitokeza kupata huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Kukosekana mara kwa mara kwa vitenganishi kwa ajili ya kupima VVU kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma.

Hii inakwamisha jitihada za wananchi kujitokeza kupima VVU na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa harakati za kupambana na VVU na UKIMWI mkoani Shinyanga.

Kukosekana kwa dawa za kutibu magonjwa nyemelezi katika vituo vya kutolea huduma.

Hii inapotekea husababisha adha kubwa na mahangaiko kwa wagonjwa wasio na uwezo wa kununua dawa hizo katika maduka ya dawa. Dawa za kutibu magonjwa ya zinaa nazo zimekuwa zikikosekana mara kwa mara katika baadhi ya vituo vya kutoa huduma za afya.

(16)

Lishe duni

Lishe duni miongoni mwa wagonjwa wa UKIMWI inachangia kwa kiasi kikubwa sana kudhoofika kwa afya za wagonjwa na hatimaye hufariki.

Elimu kwa walemavu,

Elimu ya VVU na UKIMWI imekuwa hailengi makundi ya walemavu na hivyo kuwaacha wakiwa hawana elimu hiyo muhimu. Katika majadiliano na kundi la walemavu, kundi hili lilidai kuwa elimu ya VVU na UKIMWI haina budi kulenga kundi hili kwa kuangalia mahitaji yake halisi, mahitaji hayo ni kama vile elimu kwa vipofu, viziwi na bubu, walemavu wa viungo na mahitaji mengine. Pia jitihada za kupeleka elimu ya VVU na UKIMWI zielekezwe katika maeneo ya vijijini.

Umaskini;

Kiwango cha umasikini ni kikubwa katika jamii hii licha ya kuwepo kwa shughuli za uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga. Takribani 80% ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga ni wakulima na wafugaji ambao mara kwa mara huathirika katika mavuno kutokana na kuwepo kwa ukame wa mara kwa mara katika mkoa wa Shinyanga.

Mifumo ya Kuratibu shughuli za UKIMWI.

Udhaifu katika mifumo ya kuratibu shughuli za UKIMWI katika ngazi za kata na vijiji na vitongoji unachangia kwa kiasi kikubwa sana katika kukwamisha utekelezaji wa shughuli za VVU na UKIMWI katika jamii. Kuendelea kuwepo kwa unyanyapaa miongoni mwa jamii katika eneo hili kunasababisha pia kukwamisha jitihada za kupambana na VVU na UKIMWI.

Udhaifu wa Asasi za kiraia.

Imefahamika kuwa asasi zinazojishughulisha katika kutoa huduma kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu zinauwezo mdogo. Mahitaji kwa watoto hawa ni makubwa kuliko uwezo wa asasi kukidhi mahitaji hayo.

(17)

Upatikanaji na ugawaji wa Kondomu.

Mkoa wa Shinyanga ni mkubwa sana kwa eneo na wenye miundombinu mibovu. Hali hii inasababisha ugumu katika ugawaji wa mipira ya kiume (Kondomu). Hata hivyo hakuna utaratibu mzuri wa kuhakikisha maeneo yote ambayo vitendo vya ngono vimekithiri kuna Kondom za kutosha.

Tohara kwa wanaume,

Wanaume katika jamii ya kisukuma hawafanyiwi tohara. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali ni dhahiri kwamba tohara kwa wanaume inapunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU kwa asilimia 60. Kitendo cha kutofanya tohara kinachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa maambukizi ya UKIMWI katika jamii. Mila na desturi zilizopitwa na wakati,

Mila na desturi za jamii ya wasukuma katika eneo hili zilitajwa kuwa zinachochea maambukizi ya UKIMWI katika jamii.

Matumizi ya ARV

Wenye VVU kukimbilia kutumia dawa za kienyeji na kuchelewa kwenda hospitali hadi afya inapodhoofika kwa kuwa na mawazo potofu ya kulogwa. Wagonjwa wanaotumia ARVs wakinenepa au kupata nguvu, hufikiria kuwa walilogwa, badala ya kujichunga kwa kufanya ngono salama, hufanya ngono zembe hivyo kujidhoofisha na kuambukiza wengine.

Mmomonyoko wa maadili katika jamii

Kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi, suala mojawapo linalotajwa kusababisha maambukizi ya VVU mkoani Shinyanga ni mmomonyoko wa maadili katika jamii. Sehemu kubwa ya wanajamii wazee kwa vijana hawana malengo katika maisha na hawajali kuhusu kufikia malengo katika maisha yao. Watu hawapendi kujishughulisha na kazi za uzalishaji bali kukaa vijiweni au majumbani na hivyo wana muda wa kutosha wa kufikiria kufanya mambo ya tabia mbaya kama ngono.

(18)

SURA 5

MAPENDEKEZO

I. Huduma za utambuzi kwa watoto wenye VVU.

Jitihada za makusudi zifanyike ili kuboresha upatikanaji wa huduma za utambuzi mapema wa VVU kwa watoto waliozaliwa na mama wenye VVU. Jitihada hizi pia ni vyema zikashirikisha kikamilifu wadau wa maendeleo waliopo katika mkoa wa Shinyanga ambao wanajishughulisha na utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI. Serikali kuu nayo haina budi kuona uwezekano wa upatikanaji wa huduma hizi katika hospitali za mikoa ili kuboresha upatikanaji wa huduma hii kwa jamii. Akina mama wajawazito waendelee kuhimizwa kutumia huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto licha ya changamoto zinazojitokeza katika huduma hii.

II. Vitenganishi

Halmashauri iweke mikakati mahususi ya kuhakikisha kuwa vitenganishi kwa ajili ya huduma za upimaji hiyari zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma ili wananchi waweze kupata huduma hii. Dawa kwa ajili ya magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa wa UKIMWI ni vyema jitihada za makusudi katika ngazi ya halmashauri na Serikali kuu zikafanyika ili kuweza kunusuru maisha ya wagonjwa wa UKIMWI na hasa wale ambao hawana uwezo wa kumudu kununua dawa hizi toka maduka ya dawa. Pia haina budi kuhakikisha kuwa dawa za kutibu magonjwa ya zinaa zinapatikana katika katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuweza kuzuia maambukizi ya VVU.

III. Elimu ya UKIMWI kwa makundi yote

Juhudi za makusudi zifanywe katika ngazi ya Halmashauri na serikali kuu ili kuhakikisha kuwa elimu ya VVU na UKIMWI inakidhi mahitaji ya kundi la walemavu. Pia ni vyema elimu ya VVU na UKIMWI ikaelekezwa zaidi katika maeneo ya vijijini.

(19)

IV. UKIMWI na umaskini;

Serikali ya mkoa na Halmashauri ya manispaa haina budi kubuni mikakati mahususi ya kupunguza umasikini na kukuza kipato cha wananchi kulingana na sera na miongozo ya kitaifa ya kupunguza umasikini na kukuza uchumi.

V. Kuboresha kamati za UKIMWI

Halmashauri kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI iendelee kuimarisha uwezo na utendaji kazi wa kamati za UKIMWI za kata na vijiji ili ziweze kukidhi matakwa na kuweza kuratibu vyema shughuli za VVU na UKIMWI katika jamii.

VI. Kushirikisha asasi za kijamii

Asasi za kijamii zina nafasi kubwa ya kuongezea nguvu za serikali katika kuboresha utoaji wa huduma kwa kijamii. Serikali kwa kushirikiana na asasi mbalimbali kuendelea na jitihada kutoa huduma za elimu, afya na malezi kwa watoto yatima na wale walio katika mazingira magumu.

VII. Mila na desturi

Mkoa wa shinyanga ni miongoni mwa mikoa ambayo ina mila na desturi potofu na zinazoweka mazingira hatarishi kwa maambukizi ya VVU. Serikali za mitaa kwa kushirikiana na serikali kuu iweke jitihada za makusudi kutoa elimu kwa jamii namna mila na desturi zinavyoweza kuiweka jamii katika hatari ya kupata VVU na hivyo kuepukana na mila na desturi hatarishi.

Referensi

Dokumen terkait

Kutokana na mifano hiyo, utafiti huu ulibaini kuwa msanii wa riwaya teule anatumia utamaduni wa Kikerewe kuibua dhamira ya ukarimu na uchoyo na tafsiri yake katika jamii ya

Usawiri wa taswira ya mwanamke katika kazi za fasihi umejitokeza tangu pale tu mwanadamu alipoumbwa na kuanza kuandaa na kushiriki katika shughuli mbalimbali

Aliyetia saini yake hapa chini, anathibitisha kuwa, amesoma tasnifu hii iitwayo “Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kufanya tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Emmanuel Mbogo kwa kulinganisha tamthiliya ya Ngoma ya Ng’wanamalundi (1988)

Nitoe rai kwa wadau wote kushirikiana na kulitumia Baraza katika kuratibu, kutetea na kuwafikia WAVIU pale walipo katika mwitikio wa kitaifa wa shughuli za UKIMWI

kumuweka sawa mgojnwa wa UKIMWI, kwa kiwango gani na kitu gani ni muhimu kuzingatiwa katika maisha.. Dira

Kutokana na ukweli kwamba lugha ya Kiswahili na Kiyao zinatumiwa pamoja kwa muda mrefu hususani maeneo ya Wilaya za Songea, Tunduru na Namtumbo katika mkoa wa

jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao TUKI (1981) inatoa maana ya lugha kuwa, “lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au