• Tidak ada hasil yang ditemukan

B. JITENGE ILA USIJITENGE - KANUNI SABA ZA UINJILISTI WA MTU MMOJA MMOJA

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "B. JITENGE ILA USIJITENGE - KANUNI SABA ZA UINJILISTI WA MTU MMOJA MMOJA"

Copied!
5
0
0

Teks penuh

(1)

KANUNI SABA ZA UINJILISTI KWA MTU MMOJA-MMOJA (YOHANA 4:1-26)

UTANGULIZI

1. Wengi wetu tunaweza tukawa tunatamani kuwafikishia wenzetu injili ya Yesu inayookoa… a. Wengine wanashindwa namna au jinsi ya kufanya mazungumzo.

b. Au hawajui jinsi ya kuwa na mawasiliano stahiki ktk kujifunza Biblia

-- hii hupelekea watu wengi kujisikia vibaya na kukata tamaa ya kufanya kazi ya ushuhudiaji

2. Lakini yapo mambo ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa Yesu, Mkufunzi wa ajabu wa Waalimu wa Biblia.

a. Alihusika sana na uinjilisti wa mtu mmoja -mmoja na hawa ule wa hadhara b. Mfano mzuri ni ule tunaouona pale katika kisima cha Yakobo - Yoh 4:1-26

[Tukimtazama Yesu, vizuri katika kile alichokitenda hapa, tutapata kanuni saba zitakazo tusaidia katika kuwafikia watu wengine kwa ajili ya kazi ya utume wa injili kama Yesu anavyotuagiza, na

tukumbuke kuwa: Njia pekee ya kuwafikia watu inaoweza kuleta mafaanikio, ni ile aliyoitumia Yesu Kristo. Kristo alichangamana na watu kama mtu aliyehitaji aliyewatakia mema. Aliwahurumia, akawapatia mahitaji yao na akahakikisha wamemuamini (Wamempokea/wamemkubali). Ndipo akawaambia sasa mnifuate. Kazi hii ikifanyika namna hii kwa nguvu ya maombi, nguvu ya upendo wa Mungu na nguvu ya ushwawishi, kazi hii haiwezi kuacha kuzaa matunda. (The Ministry of Healing, Uk. 143, 144)

I. WASILIANA NA WATU KTK MAMBO YA KIJAMII

A. TUSIJITENGE NA JAMII FLANI YA WATU...

1. Wayahudi walijitenga sana na Wasamaria ila Yesu aliwaendea - Yoh 4:1-6 a. Wayahudi wengi waliwatenda jeuri Wasamaria na kujitenga nao b. Lakini Yesu na wanafunzi wake, alipita kwao na kujenga uhusiano c. Yesu alifanya hivyo pia kwa Petro, yakobo na Yohana - cf. Luk 5:29-32

2. Ikiwa watu hawaji kwa Kristo, ni kwa kuwa sisi hatuendi kwao

a. Hatuwezi tukavua samaki kwa kukaa tu ndani ya chombo, ikiwa samaki hawaji chomboni basi tuondoke twende mahali palipo na samaki

b. Tatizo si kwamba hakuna udongo au mahali pa kuotesha mbegu, ila badala yake mbegu bado tumezitunza katika ghala - cf. Hag 2:19

B. JITENGE ILA USIJITENGE

1. Ni kweli, imetupasa kutengana – 2 Kor 6:14-18

2. Lakini hii haina maana kuwa hatutakiwi kuwa pamoja nao

(2)

C. TUMIA FURSA ZA MAMBO YA KIJAMII...

1. Huenda ni katika taasisi za elimu

a. Vijana wahusike kuwashuhudia wengine juu ya upendo wa yesu bila kujali umri wao b. Vijana wanafursa nzuri Zaidi ya kuwashuhudia wenzao juu ya upendo wa Mungu 2. Huenda ni katika eneo la kazi na uko na wafanyakazi wenzako

a. Sehemu kubwa ya maisha yetu tuko na wafanyakazi wenzetu, hivyo tusipoteze fursa ya kuajulisha pendo la yesu

b. Tuna fursa na uwezo mkubwa wa kuwavuta kwa Yesu hasa kwa kuwa mfano Bora 3. Pale nyumbani, wapo majirani zako

a. Uwafahamu majirani zako

b. Wale walio karibu nasi Zaidi kunaweza kukawa na ugumu lakini bado inawezekana kuwafikia - e.g., Math 13:54-58; Yoh 7:5; Mat 1:14

[Kumbuka Yesu alisema enendeni ulimwenguni kote..." (Mk 16:15). Tunatakiwa kwenda mahali watu walipo! Yesu alikwenda mpaka Samaria, hakusubiri Wasamaria waje kwake…]

II. ANZA KWA MAMBO AMBAYO MNAFANANA (Jenga Daraja)

A. MAMBO YANAYOFANANA HUJENGA DARAJA LA MAHUSIANO...

1. Zingatia maneno ya kwanza ya Yesu kwa yule Mwanamke - Yoh 4:7-8 a. Amekuja kuchota maji

b. Yesu alikuwa na kiu

c. Maneno yyake ya kwanaza yaliwaleta katika kitu ambacho wote walikihitaji 2. Tambua umuhimu wa kujenga wahusiano mapema ktk mazungumzo

a. mazungumzo ya maana si rahisi, hasa yale yanayohusika na wokovu b. Mambo yanayowafananisha, hupelekea mazungumzo yenye maana

c. Wakati daraja linapojengwa vizuri, ni jambo rahisi sana kufanya mazungumzo ya kiroho na mtu husika

B. MAMBO YANAYOTUFANYA TUIFANANE NI MENGI

1. Mambo ya kifamilia na wanafamilia

2. Shughuli mbalimbali za bibafsi na za kijamii 3. Uzoefu unaofanana ktk maisha

4. Imani zinazofanana n.k.

(3)

III. JENGA HITAJI LA KUSIKILIZWA

A. KUPITIA MATENDO/KWA VITENDO... (Fanya jambo ambalo si la kawaida)

1. Mfano wa Yesu - Yoh 4:9

a. Ni mwanaume lakini anazungumza na mwanamke

b. Ni Rabi wa kiyahui lakini anazungumza na mwanamke, mdhambi c. Ni myahudi lakini anazungumza na Msamaria

-- Alimjengea hitaji la kusikiliza kwa Yeye kuzungumza naye. 2. Tunaweza kufanya jambo flani ambalo si la kawaida

a. Tunaweza kuwa mfano bora kwa matendo yetu b. Fika mahali wanapofanyia ibada (msikitini/kanisani) c. matendo ya huruma na rehema kwa wote (Hata waovu)

d. Kwa kuvuka mipaka ya kijamii hasa kuwaendea wanaofikiriwa vibaya e. Kuonesha mfano wa tumaini letu na Imani yetu - e.g., 1Pet 3:1-2,15

B. KUPITIA MANENO YETU

1. Mfano wa Yesu mwenyewe - Yoh 4:10-14

a. Maneno yake Yesu yalipelekea kuwapo kwa hitaji la mazungumzo ya kiroho b. Alimuongoza kwa kusema kitu ambacho si cha kawaida kwake (maji ya uzima 2. Kwa kupitia maneno yetu

a. Tunaweza kuzungumza maneno au kuleta maswali ambayo yatatupeleka kwenye mjadala wa mambo ya kiroho

1) Mfano: Unadhani mwisho wa matukio haya ya kutisha ktk dunia ya leo utakuwa ni nini?

2) Hivi unajua hayo yamezungumzwa ktk Biblia… Ungependa tuyachunguze? b. Mafunzo ya mwanzoni yanatakiwa kuwa yale ambayo wote mnakubaliana nayo

1) Anza nay ale mnayokubaliana nayo ili kujenga urafiki na kuaminiana

2) ndivyo walivyofanya Mitume wa yesu - e.g., Ac 13:16-22

IV. USIENDE MBALI GHAFLA TENA KWA HARAKA

A. ANZA KWA KILE AMBACHO YUKO TAYARI KUKISIKILIZA...

1. Angalia mazungumzo ya Yesu na Mwanamke - Yoh 4:15-16 a. Alihitaji maji ya Uzima

b. Yesu aliona hitaji la kwenda taratibu na kuimarisha kwanza msingi 1) Mwanamke alihitaji kwanza kumwamini kama Masihi

2) Alijenga kwanza ushahidi kuwa Yeys ndiye c. Kwa hiyo badala ya kumweleza juu ya Maji ya uzima

1) Anamwambia amlete mume wake

2) Jambo hili lilimhakikishia huyu mwanamke kuwa Yesu alikuwa nabii 2. Wakati mwingine watu hawaelewi kile wanachohitaji kwanza

a. Watataka kuzungumzia mada flani kwanza

(4)

B. BAADHI YA MIFANO

1. Wapo wanaotamani kujifunza Ufunuo wakati wanahitaji kujua kwanza Biblia ni kitabu gani, na vitabu vyote kwa ujumla vinazungumzia nini?

2. Wengine wanataka kuzungumzia juu ya sabato wakati bado hawajaelewa juu ya uumbaji 3. Anza kwanza na mafundisho rahisi (anza na maziwa) - cf. 1Co 3:1-2

V. USIMLAUMU MTU BILA SABABU

A. MFANO WA YESU

1. Angeweza kukazania uzinzi wa Yule Mwanamke - Yoh 4:17-18

2. kama alivyosema alikuja kuuokoa ulimwengu, si kuuhukumu - cf. Yoh 3:17

3. Sio kwamba ulimwengu hautahukumiwa bali kitu cha kwanza ni wokovu - cf. Yoh 12:46-48

B. KATIKA UINJILISTI TUNAOFANYA

1. Tunatakiwa kuhubiri juu ya dhambi lakini lengo si kuhukumu ila kuokoa – 1Kor 5:12-13 2. Lengo ni kuwaelekeza watu msamaha ambao Mungu anaweza kuutoa- cf. 2Kor 5:18-20

a. Mungu anatafuta upatanisho na wadhambi

b. kazi yetu ni kuwaelekeza namna ya kupata upatanisho

VI. USIHAME-HAME MADA KUSUDIWA

A. KWA HABARI YA YULE MWANAMKE MSAMARIA...

1. Alihama kutoka mambo yanayomuhusu mpaka mahali pa ibada - Yoh 4:19-20

2. Yesu alijibu swali lake huku akimrejesha ktk mada kusudiwa iliyofundisha kuwa yesu ni nani na nini anaweza kutoa - Yoh 4:21-25 (cf. Yoh 4:10)

B. KUWA IMARA KWA KILE ULICHOKUSUDIA

1. Tafuta kujenga makubaliano kabla hujaenda kwa jambo jingine

2. Unapotoka kwa mambo ya kawaida na kwenda kwa mambo asiyofahamu c. Zungumzia jambo moja kwa wakati mmoja

c. Usihame mpaka mmekubaliana juu ya mada flani husika

3. Mfano: Ikiwa lengo ni somo la dhambi ni nini, epuka kujadili mambo ya vyakula safi na visivyo safi - cf. Pr 15:28

VII. SASA ZUNGUMZA WAZIWAZI

A. MFANO WA YESU...

(5)

B. Mfano leo hii...

1. Ukitaka kuazniasha msomo ya kujifunza Biblia d. Tafuta marafiki (katika jamii)

c. Angalia mambo mnayofanana sana

d. Uwe makini katika mambo ambayo yatapelekea mazungumzo ya kiroho, onesha Imani yako kwa matendo yako

e. Achana na ubishi usio na maana, sisitiza imani zinazofanana f. Wasifie kwa mambo mema na watie moyo kuelekea uelekeo sahihi g. Uwe na lengo moja la msingi: watie moyo kujifunza Biblia

i. Waulize ikiwa watapenda kujifunza juu zaidi mambo ya Biblia ii. Matazame Akwila na Prisla na Apolo - Mat 18:24-26

h. Sasa anza nao mafundisho rahisi kutoka katika Biblia 2. Mtakapokuwa katika kujifunza Biblia zingatia yafuatayo

a. Endelea kudumisha mahusiano ya kijamii

b. Endelea kudumiasha makubaliano na mambo mnayofanana c. Endelea kufafanua kwa undani Zaidi juu ya kile anachofahamu d. Songa mbele kutoka mafundisho ya kawaida kuelekea magumu zaidi e. Sisitiza juu ya ujumbe wa injili wala si mapungufu aliyonayo mtu f. Lengo ni moja, wajulishe hitaji la wokovu Mk 16:15-16; Kol 1:5-6 g. Watake kufanya maamuzi kwa kila jambo wanalolielewa; Mfano

1) Je, huoni mambo haya ndiyo kweli yote na mapenzi ya Mungu? 2) Je, kuna nililolisema lakini bado haujalielewa?

3) Je, kuna mambo ambayo nimekufundisha kinyume na neno la Mungu?

4) Unaonaje kama utachukua hatua ya kufuata kile ambacho tumejifunza pamoja maana ndiyo mapendi ya Mungu???

HITIMISHO

1. Matokeo ya Yesu kuzungumza na yule Mwanamke ilikuwa kuzungumza na watu wengi Zaidi katika mji uliokuwa jirani - Yoh 4:39-42

2. Hii inaonesha ubora wa uinjilisti wamtu mmoja mmoja

a. nani ajuaye kuwa mmoja unayemfundisha, anaweza kuleta wengi kwa Kristo? b. Huyo mmoja anaweza kuwa mbegu moja itakayozalisha mbegu nyingine nyingi Tukielewa umuhimu wa uinjilisti wa aina hii, tutakubaliana na maneno ya Yesu:

“Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi

nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa

yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno”. (Yoh 4:35)

Kwa kufuata Mfano wa Yesu, tunaweza kutumika vizuri Zaidi katika kufanya kazi ya Mungu hasa ya ushuhudiaji wa Pendo lake kwa watu wengine.

CONTACT ME PLEASE:

Pr. ALMODAD AMOS Mobile phone: +255 657 87 89 87

Referensi

Dokumen terkait

Jamii na watu walioathiriwa na mikasa, wakiwemo walio katika hatari ya kuathirika zaidi, wanachukulia kuwa usaidizi na ulinzi wanaopokea umetolewa kwa wakati unaofaa.. Jamii na

Usawiri wa taswira ya mwanamke katika kazi za fasihi umejitokeza tangu pale tu mwanadamu alipoumbwa na kuanza kuandaa na kushiriki katika shughuli mbalimbali

Kutokana na ukuaji mkubwa wa mawasiliano katika ulimwengu wa sasa, kumekuwa na athari pia za matumizi ya lugha. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili, matumizi ya Kiswahili

Muhtasari wa somo la Kiswahili (2016:2), ufundishaji wa somo la Kiswahili katika elimumsingi umelenga kumwezesha mwanafunzi, kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika kwa

Utafiti huu ulilenga tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Shaaban Robert kwa kuangalia vipengele vya Fasihi Simulizi ndani ya riwaya ya Adili na

Pia Buberwa (2010) alifanya utafiti wake mkoa wa Kagera, hususani katika katika wilaya ya Bukoba, alimakinika katika kuchunguza majina ya maeneo katika jamii ya

Kutokana na ukweli kwamba lugha ya Kiswahili na Kiyao zinatumiwa pamoja kwa muda mrefu hususani maeneo ya Wilaya za Songea, Tunduru na Namtumbo katika mkoa wa

Kama Mzee wa kanisa lazima ujifunze na kuelewa utume wa kanisa lako, kazi zako na muundo wa uongozi pamoja na ngazi zake katika kanisa la Waadventista Wasabato.. Asante