• Tidak ada hasil yang ditemukan

Somo elimu na jukumu la mshiriki

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "Somo elimu na jukumu la mshiriki"

Copied!
6
0
0

Teks penuh

(1)

KICHWA CHA SOMO: ELIMU YA KIKIRISTO NA JUKUMU LA MSHIRIKI TEXT: LUKA 17:7 – 10

Mkurugenzi wa elimu-WTF Pr.Emmanuel Allen Senguo

UTANGULIZI:

Kwa kila jambo Yesu alikuwa anaona mbele kile ambacho kilikuwa kinaenda kutokea. Kwa sababu hiyo Yesu alikuwa tayari amelitangulia lile ambalo lilikuwa linaenda kutokea kwa wanafunzi wake au lile ambalo lilikuwa linaenda kutokea kwa washiriki wake au kwa watendakazi wake.

Tukumbuke kuwa maneno haya Yesu aliyatoa wakati alipokuwa karibu sana na kifo chake.

Yesu aliona ni vyema awajulishe wanafunzi wake jambo ambalo lilikuwa ni la muhimu sana kwa kila muumini anayejiita yeye ni mwanafunzi wa Yesu yeye ni mshirika na Yesu, yeye ni mafanyakazi na Yesu, yeye ni mtenda kazi na Yesu na anayejiita kuwa yeye ni Mkristo na Mwandiventista wa kanisa la wa Adventista wasabato.

Katika kilele hiki cha mwisho cha maisha ya Yesu, anatoa agizo linalohusinan na utume wetu kwake.

Katika mwaka huu wa uamsho na matengenezo katika elimu ni pamoja na kufahamu kile Yesu alichokifundisha kwa wanafunzi wake katika Luka 17:7-10.

V 7 “Lakini ni nani kwenu mwenye mtumwa aliye naye au achungaye ng’ombe atakaye mwambia mara arudipo kutoka shambani njoo upesi keti ule chakula?”

V 8 “Je hatamwambia, nifanyie tayari chakula nile; jifunge unitumikie hata niishe kula na kunywa ndipo nawe utakapo kula na kunywa?”

V 9 “Je, atampa asante Yule mtumwa kwasababu amefanya aliyoagizwa?” V 10 “Vivyo hivyo nanyi mtakapokwisha kufanya yote mliyoagizwa, semeni sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya yaliyotupasa kufanya.

(2)

- Kwa wale wote wanaosema sisi ni washiriki na watendakazi na

wanafunzi wa Yesu, ni lazima wafahamu vile Yesu anavyowatambua na anavyotaka wawe.

- Yesu anawatambua kama watumwa tena wasio na faida.

- Hatutaweza kuunga mkono na kushiriki vyema katika njia hii ya

uinjilisti kupitia elimu kama hatutajitambua kuwa sisi ni watumwa wa Bwana wetu Yesu Kristo.

- Hatutaweza kutoa michango yetu, sadaka zetu ili zijenge shule kama dhana ya kuwa mtumwa wa Yesu kristo haitakuwepo ndani ya fikra zetu.

- Yesu anapoelezea maisha ya mtumwa alitaka wanafunzi wake watende kazi kama watumwa wa Bwana wa dunia hii wanavyotenda.

- Historia inaonyesha kuwa katika utawala wa kirumi mtumwa hakuwa mtu wa muhimu sana kwa Bwana wake.

- Kulikuwa hakuna usawa kati ya Bwana na mtumwa wake. Mtumwa alifananishwa kama chombo kinachoishi chenye jukumu la kufanya kazi ya aina yeyote ile.

- Mtumwa hakuwa ni mtu ambaye ni bora bali ni kitu tu.

- Mtumwa hakuwa na haki yeyote kwa Bwana wake, hata hivyo bwana wake alikuwa na uwezo wa kumfanya lolote apendalo liwe jema au baya, hata akitaka kumuua bado bwana wake alikuwa na huo uwezo wa kumtenda mtumwa wake.

- Maisha ya uhai au kifo yalikuwa juu ya bwana wake.

- Na ilikuwa ni kawaida mtumwa amalizapo kazi yake alikuwa anatupwa akafie huko!

- Mtumwa hakua na haki ya kuchagua nifanye lile niache hili, hakuwa na haki kukubali au kukataa kazi yake ilikuwa ni kutenda kile ambacho bwana wake amemuamuru bila kujali anapenda au hapendi.

- Mtumwa alikuwa hana uhuru wa kufanya vile apendavyo yeye. Hivyo alikuwa ni mtu ambaye siku zote hakutenda kama vile apendavyo bali kama vile bwana wake apendavyo.

- Yesu anapokuwa anaeleza maisha ya mtumwa, anaonyesha hakuna shukrani yeyote ambayo mtumwa angapewa kwa sababu yeye alikuwa anatekeleza wajibu wake aliopewa na bwana wake.

- Kazi ya mtumwa wa Yesu ni sawa naya bwana wa dunia hii, japo wanatofautiana.

(3)

1. Bwana wa dunia hii ni mwanadamu

2. Mwanadamu ni mkorofi hana huruma ni mkatili na muuaji

1. Bwana huyu yeye ni Yesu na ni wa mbinguni

2. Yesu anahuruma, upendo na si mwepesi wa hasira. 3. Yesu ukimtumikia

unapata mibaraka tele 4. Yeye anapenda haki 5. Kwa Yesu mwisho wake

ni uzima wa milele.

Kuna faida kubwa kuwa mtumwa wa Yesu Kristo.

Sisi tulio watumwa wa Bwana wetu Yesu Kristo chimbuko la uzima wetu, inatupasa tuishi na kutenda kulingana na nuru hii ambayo Yesu ameifunua kwetu. Inatupasa tuwe na tabia ya kusema sisi tuwatumwa wasio na faida, tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Kama sisi washiriki endapo tutakubali kuwa watumwa wa yesu kristo ,na kufanya wajibu wetu kama watumwa wake, ndipo kazi ya Mungu

itakapofanywa kwa moyo wote na matunda yake yatakuwa makubwa.

Moja ya jukumu ambalo Mungu ametupatia kama njia ya kufikishia wengine habari njema ya wokovu ni njia ya Elimu. EG White katika kitabu chake cha elimu ya kweli anasema “ kwa kuwapenda watoto wake, baba yetu wa

mbinguni ndiye aliyetoa elimu”( EG White, elimu ya kweli Uk 12). Dada White anendelea kusema, “Hivyo kadri ambavyo zama zingeendelea dunia yote ingejaa kaya na shule ambazo maneno na matendo ya Mungu vingesomwa, na ambapo wanafunzi zaidi na zaidi wangekamilishwa kuakisi kwa zama zote mwangaza wa ujuzi wa utukufu wa Mungu.”(EG White elimu ya kweli Uk 13).

- Moja ya swali ambalo unaweza kujiuliza ni hili, ni kwanini Mungu anawatumia wanadamu kama wajumbe wake? Jibu ni hili “Mungu hategemie mwanadamu kuendesha kazi yake. Angaliwaweka malaika kuwa mabalozi wa ujumbe wake. Angaliweza kuwajulisha upendo wake , kama alivyotangaza kutoka mlima wa Sinai kwa sauti yake

(4)

- Kama mshiriki wa imani wa kanisa la waadventista wa sabato, ni vyema kulitambua hili, unapokuwa unatoa mali zako, muda wako, talanta yako katika kujenga shule, moja kwa moja unashiriki mibaraka ya Mungu na kuwa mtenda kazi pamoja naye.

- Tusisahau kuwa sisi tu watumwa wa Bwana wetu Yesu Kristo. Na sifa mojawapo ya mtumwa ni kwamba yeye hana nafasi ya kuchagua. Shida tuliyonayo ni kwamba tunataka kubagaini na Mungu tunataka kumchagulia Mungu cha kufanya. Na ndio maana utaona, baadhi ya watu utawakuta wanasema, kama ni kijijini mimi siendi, mimi sitoi sadaka yangu kama ni kiasi hicho, mimi nataka kwenda huku; ukishakuwa mtu wa namna hiyo basi wewe hujui maana ya kuwa mtumwa wa Mungu.

- Inapendaza sana kusikia W.T.F ilipokuwa inatanganza ujenzi wa shule, washiriki walijitoa kwa wingi katika ujenzi wa shule. Makanisa yalitoa vyakula, vijana wa kike na wakiume walishiriki kutengeneza zege la kuweka lenta, huku wamama wakibeba mifuko ya cement, huku

nyimbo za furaha zikiimbwa za kumtukuza Mungu na wenye karama za ujenzi kufanya kazi ya kujenga bila malipo. Kila mmoja akiona ni

mibaraka ya pekee kushiriki kutenda kazi pamoja na yesu.

- Mitume walipotambua wao ni watumwa wa Bwana Yesu, utendaji wao wa kazi ulikuwa na mafanikio makubwa sana na Bwana aliwabariki kwa maana walikuwa wanafanya kama wajibu wao.

- Kila anayekubali kuwa ni mtumwa wa Yesu Kristo, UTII ni wa lazima bila kujali tunapenda au hatupendi! Bila kujali wakati unaofaa au usiofaa. Na ndio maana Yesu anatuhitaji tuwe na hisia za utumwa katika kutangaza habari njema ya wokovu kwa njia ya ujenzi wa shule mahali ambapo itarudisha ile twasira ya sura ya Mungu iliyopotea. - UTII wetu kwa Mungu sio swala la kupewa zawadi (japokuwa Mungu

anatuheshimu sana tunapokuwa tukifanya kazi chini ya mamlaka yake), na anataka utii wetu kwake uwe ni swala la wajibu.

- Watiifu katika kristo hawana haki ya kuchagua kile ambacho Bwana Yesu anawataka wafanye kazi na wajibu wao ni kutii na kusema niko hapa nitume mimi Bwana.

- Mungu anatumia viongozi wake kutupatia majukumu ya kutenda. Na ndio maana kitabu cha Mithali 8: 4, Mfalme Sulemani anasema “Enyi watu, nawaita ninyi”, na sauti yangu ni kwa wanadamu”.

(5)

- Kwa WTF ,kilio chao ni michango kwa ajili ya ujenzi wa shule. Kwa hiyo magoli uliyopewa na utakayopewa na viongozi wako, tambua hiyo ni sauti ya Mungu ikizungumza nawe. Na kama umtumwa wa Yesu Kristo, kazi yako ni kutii na kutekeleza kama wajibu wako. Ndicho Yesu

alichokuwa anawaambia wanafunzi wake, ambao kwa leo ni mimi na wewe.

- Neno “Wosia na Faida” lisije kutafsiriwa kuwa hatuna faida yeyote mbele za Mungu. Tuna faida kubwa sana mbele za Mungu na msalaba ni jibu la yote.

- Neno “ Wosia na Faida” inamaanisha hakuhitajiki chochote (without need) Ndipo kazi ya Mungu itendeke. Kwa maana nyingine kama ingekuwa lugha ya leo tungesema hakuhitajiki kitu kidogo ili kazi ifanyike, hakuhitajiki hongo ili kazi ya Mungu ifanyike.

- Kufanya tunafanya kwa maana ni wajibu wetu na kwasababu tu watumwa wa Bwana wetu Yesu Kristo, na kazi yetu ni kutii (jina la Bwana lipewe sifa).

- Hata hivyo fungu hili lisingeweza achwa peke yake tukizingatia ya kwamba Mungu anatuheshimu sana, bila kufikiri kuhusu malipo, tunu au zawadi.

- Luka 12:37 anasema “Heri watumwa wale ambao Bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amini nawaambieni, atajifunga na

kuwakaribisha chakulani atakuja na kuwahudumia”. Hakuna tunu iliyokubwa kama ya kuhudumiwa na Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme.

- Mathayo 25:23 – “Yesu atasema vyema mtumwa mwema ulikuwa mwaminifu kwa machache nitakuweka juu ya mengi. Ingia katika furaha ya Bwana wako”.

- Kuna watu wanasema tumetoa sana na tumechangia ujenzi wa

mashule sana, kwa hiyo hatutoi tena kama wewe ummoja wao, habari njema ndio hii, wewe unaposema nimetoa sana, Yesu anasema

“umekuwa mwaminifu kwa machache . hata kama umeshawahi kujenga shule yote peke yako, bado kwa Yesu hayo ni machache. Maana yake nini? Maana yake ni kwamba haitafikia siku ya kukoma kutoa mpaka mkuu wa watoaji kupita wote Yesu Kiristo atakaporudi, (jina la Bwana lipewe sifa).

(6)

MWISHO.

Kamwe tusisahau ya kwamba hata mali ya mtu iwe ndogo au nyingi kiasi gani na tukumbuke ya kwamba mali ile ni amana. Nguvu zetu, akili zetu, muda wetu, talanta, fursa na mali, itatupasa kutoa hesabu mbele za Mungu kwa ajili ya vitu hivyo. Yule ambaye amepokea nuru ya upendo wa Kristo, huwa chini ya wajibu mkuu wa kuangaza nuru ya mbaraka kwa roho zingine zilizomo gizani ambazo kwa uwepo wa taasisi zetu (shule) Yesu

anathihirishwa.

Kama tunavyoendelea kupokea mibaraka ya Mungu, ndivyo inavyotupasa kuendelea kutoa. Wakati mtoaji wa mbinguni atakapokoma kutoa kwetu, ndipo nasi tutakapoacha kutoa kwa sababu hatutakuwa hatuna kitu cha kutoa. Pale Mungu atakapoacha kutoa pumzi yake kwako, ndipo kutoa kwako kutakoma.

Hebu Mungu atusaidie tunaposhiriki pamoja naye katika kueneza injili kwa njia ya elimu na ujenzi wa shule kwa kutoa mali zetu, muda wetu, vipaji vyetu, wengi waliogizani wakapate nuru ya kumjua Yesu. Nasi kama

Referensi

Dokumen terkait

peningkatan konsentrasi minyak terlarut pada pengamatan V, ternyata pada pengamatan yang sama kepadatan mikorba relatif rendah. Kondisi ini dimungkinkan terjadi karena pasokan

Berdasarkan latar belakang, maka permasalahan dalam penelitian ini adalah alfamart sebagai pasar retail modern kurang memperhatikan tentang penataan ruang kawasan strategis yang

carpocapsae yang diinokulasikan pada media cair senyawa humik tidak mampu bertahan hidup sampai dua minggu setelah inokulasi, bahkan dalam 10 hari setelah

Temperature-Responsive Fluorescence Polymer Probes with Accurate Thermally Controlled Cellular Uptakes.. ACS

Penelitian Yang Relevan Dalam penelitian tentang Pembelajaran Tema dan Amanat Novel Matahari di Atas Gilli karya Lintang Sugianto dengan Metode Kontekstual untuk Siswa SMA Kelas

1.3 Tujuan Penelitian Berdasarkan rumusan masalah yang telah dipaparkan di atas, tujuan dari penelitian yang akan dicapai adalah mendeskripsikan analisis tema dan amanat novel 5

kalsium dalam tiap air minum berbeda-beda dan dapat menyebabkan perbedaan pada ekskresi kalsium urin serta berhubungan dengan kejadian kristaluria yang merupakan awal