• Tidak ada hasil yang ditemukan

TANZANIA UNION MISSION OF SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH

N/A
N/A
Protected

Academic year: 2019

Membagikan "TANZANIA UNION MISSION OF SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH"

Copied!
11
0
0

Teks penuh

(1)

1

TANZANIA UNION MISSION OF SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH

SEMINA YA IDARA YA HUDUMA ZA WATOTO KANISANI NA: Winfrida Aneth Mitekaro

Kusudi kubwa la huduma za watoto ni kukuza imani ya watoto kuanzia wanapozaliwa hadi umri wa miaka 14. Wakati shule ya sabato inapotoa mafundisho ya dini ya watoto hao mara moja kwa wiki yaani siku ya sabato, Idara ya huduma za watoto inatoa huduma mbali mbali kwa muda uliobaki. Huduma hizo huwaongoza watoto kwa Yesu na kuwafanya wanafunzi wake katika maisha yao ya kila siku.

FALISAFA YA IDARA

Biblia inaweka wazi kuwa watoto ni wa pekee mbele za Mungu. Ikiwa utachunguza kile biblia isemacho kuhusu watoto utagundua kuwa utagundua mitizamo kadhaa.

Watoto ni zawadi toka kwa Mungu. (Kumb.7:13, Zab.127:3) Mungu anawapatia wazazi watoto kama ishara ya upendo na kulidhisha nafsi.

Watoto ni kitu cha kutamanika maana tumeangizwa kuwazaa. (Mw.9:7, Kumb. 6:3) Toka uumbaji mungu ametuagiza kuzaa watoto.

Watoto huleta furaha na mbaraka kwa watu wazima. (Hes. 5:28, Kumb. 28:4,11) Mungu anawapa wazazi faida nyingi zitokanazo na kuwalea watoto wao.

Watoto wanapaswa kufundishwa namna ya kukuza mahusiano yao na Mungu (

Kut.12:26,37,Kumb.6:1-7,Mith.22:6). Moja ya changamoto tulizonazo ni kuwarithisha watoto wetu imani kumuelewa Mungu.

Watoto ni wa thamani sana mbele za Mungu kiasi kwamba anatuamuru tuwalinde na kuwatunza. (1sam.20:42, Ezra 8:21) Wazazi wanapaswa kuhakikisha usalama wa watoto wao kimwili na kiroho.

Mungu anawapenda sana watoto hata anahakikisha kuwa wanaadibishwa.

(mith3:11,12; 13:24;19:18; Efeso 6:4).

Mungu anafurahia namna na haiba ya watoto na anatuomba tujifunze kutoka kwao. (math. 18:13, 19:14; Fil.2:15) Tabia hizo ni kama: Watoto husema kweli , ni

wanyenyekevu, huishi maisha rahisi na wanaamini. Mungu anazithamini sana tabia hizi.

Kama watoto ni wa Muhimu kiasi hiki mbele za Mungu, wanapaswa wawe wa Muhimu kwetu pia. Ni muhimu tukiwachukulia watoto kwa makini kama urithi toka kwa Bwana.

(2)

2 TAMKO LA UTUME WA IDARA YA HUDUMA ZA WATOTO

Utume wa Idara ya Huduma za Watoto ni kuwalea katika upendo, na huduma ya mahusiano na Yesu. Utume huu unatimizwa kwa kufanya ifuatayo:

Kwa kutoa huduma za neema:

Hapa watoto wote wanapitia uzoefu wa upendo usio na masharti wa Yesu, watoto huhakikishiwa kukubaliwa na kusamehewa, kujitoa upya kwa ajili yake na kukua katika imani.

Ni huduma jumuishi

Wajitoleao kuhudumia, na watoto wanaohudumiwa, wote wanathaminiwa na

kuhusishwa bila kujali utaifa wao , rangi, lugha, jinsia,umri,uwezo na hali yao ya kijamii na ya kiuchumi.

Kwa huduma ya uongozi

Wale wanaojitoa kuwahudumia watoto, wanatiwa shime, wanapata mafunzo na kuandaliwa vyema kwa huduma ya watoto.

Huduma ya utumishi

Watoto wanapata fursa ya huduma ya utumishi kwa watu ambao ni majirani zao, watu walio katika miji, na hivyo kuanzisha mtandao wa kuwafikia walio nje ili waweze kuendelea na maisha.

Huduma inayoshirikisha idara zingine

Huduma ya watoto hushirikisha idara nyingine kama vile , huduma za Familia, shule ya sabato, uwakili na nyingine ili kuendeleza malengo yetu yanayofanana.

Huduma salama

Ambapo makanisa (a) huchagua watu wenye viwango vya juu vya kiroho na waadilifu ili wajitolee kuwahudumia watoto. (b) Hupanga namna ya kuwalinda watoto kutokana na manyanyaso ya kimwili, kihisia na kiroho.

Huduma ya kiuinjilisti

(3)

3 HUDUMA YA YESU KWA WATOTO

Wakati wote wa huduma yake hapa Duniani Yesu alikuwa na nafasi ya kuwahudumia watoto.

Biblia pamoja na roho ya unabii vyote vinatueleza wazi jinsi alivyowathamini.

Huduma yake kwao ilihusisha mambo kama:

Aliwabariki na kuwaombea (Math19:4) Wakati akinamama walipoleta watoto wao wadogo kwa Yesu, badala yake wanafunzi wake waliwakemea. Ndipo akawawekea mikono, akawabariki na akawaombea. (Math. 19:14)

Aliwahakikishia kuwa ufalme wa mbinguni ni wao, (Marko10:15; Math 18:3) Yesu aliwatangazia nakuwahakikishia kuwa ufalme wa mbinguni ni wa watoto pia. Kwa hakika yeyote asiyeupokea ufalme wa mbinguni kama mtoto mdogo hataingia (marko 10:15). Hapa anatambua jambo la muhimu ili kuingia ufalme wa Mungu ni lazima tuamini na kuwa wanyenyekevu kama mtoto.

Wakati mwingine Yesu alipoulizwa na wanafunzi wake kuwa nani atakuwa mkuu katika ufalme wa mbinguni, alimchukua mtoto mdogo na kumweka katikati yao. Na akasema, Amini amini nawaambia msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Hapa pia Yesu anakazia umuhimu wa kujifunza toka kwa mtoto. Anataja moja ya tabia katika mathayo 18:4, Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.

Alijenga urafiki nao. Alifurahia mambo madogo waliyoyafanya kwake, hata maua

waliyo mlete. Ellen G. White anaandika “ Kama watoto walivyokusanya maua mwitu na

kujikusanya kumpa sadaka zao alizipokea kwa furaha, aliwatabasamia na kuonyesha furaha yake kwa kuona maua ya aina mbali mbali. __Upward Look, uk. 57.

(4)

4 MASHAURI YA ELLEN G. WHITE KWA HUDUMA YA WATOTO

Ellen G. white amepokea uvuvio mwingi kutoka kwa Mungu juu ya umuhimu wa watoto na malezi ya awali ya kuwaandaa kumpokea Yesu kama mwokozi wao. Anakubaliana na huduma kwa watoto. Yafuatayo ni baadhi ya mashauri yake.

“Umuhimu mkubwa unapaswa kuwekwa kwa watoto wa umri mdogo. Mafundisho ambayo mtoto anajifunza ndani ya miaka saba ya maisha yake ya kwanza yanaunda tabia kuliko

atakayojifunza katika maisha ya baadaye.”- Child guidance, p.193

“Bado ni kweli kuwa watoto huathiliwa/guswa zaidi na mafundisho ya injili; mioyo iko tayari kupokea mvuto wa Uungu na wana nguvu ya kutunza mafundisho waliyopokea. Watoto wadogo wanaweza kuwa wakristo, wakipata uzoefu kulingana na miaka yao. Wanahitaji kupewa elimu ya mambo ya kiroho na wazazi wanapaswa kuwapa fursa zote ili waunde tabia

inayofanana na tabia ya kristo”. Desire of Ages P. 515.

“Watoto wa miaka minane au kumi na mbili ni wakubwa wa kutosha kufundishwa juu ya somo

la dini ya mtu binafsi. Usimfundishe mtoto ukimwelekeza maisha ya baadaye ambapo unadhani kuwa atakuwa mkubwa wa kutosha kuungama na kuuamini ukweli. Wakielekezwa vizuri watoto wadogo wana namana sahihi ya kujitambua kuwa wako katika hali ya dhambi na njia ya wokovu kwa kupitia Yesu Kristo.” Testmonies Vol.1, p.400

“Kati ya watoto walioletwa kukutana naye, Yesu aliona wanaume na wanawake wapaswao kuwa warithi wa neema na watu wa ufalme wake, na ambao wangekuja kufa kwa ajili yake. Alijua kuwa watoto wangemsikiliza na kumpokea kama mkombozi wao, walikuwa tayari mno kuliko watu wazima ambao wengi wao walikuwa na hekima ya duniani na mioyo migumu. Katika mafundisho yake alijishusha mpaka kufikia mahali pao. Yeye jemedari wa mbinguni alijibu majibu yao na akarahisisha mafundisho yake ya muhimu ili kufikia kiwango cha kuelewa

cha utoto.” Evangelism, p. 579.

“ Katika kufunga taswira ya historia ya dunia hii, wengi wa watoto hawa na vijana

watawashangaza watu kwa ushuhuda wao wa kweli, ambao utatolewa kwa urahisi, lakini wenye roho na nguvu. Wamefundishwa kumcha Bwana na mioyo yao imelainishwa na kujifunza biblia kwa uangalifu na maombi mengi. Hivi karibuni, watoto wengi watawezeshwa na roho wa Mungu, na watafanya kazi ya kuitangaza kweli kwa ulimwengu, maana kwa wakati haiwezi kufanywa na washiriki ambao ni watu wazima.”Counsels to Teachers,pp 166,167.

“Wale wanaompenda Mungu wanapaswa kuwa na upendo wa kina kwa watoto na vijana. Kwa hao Mungu anaweza kufunua ukweli wake na wokovu. Yesu anawaita watoto wadogo

(5)

5

watoto…….Sadaka ya thamani kuliko zote watoto wawezazo kumpa kristo ni uchanga wa utoto wao.” Reflecting Christ,p. 373.

“ Yesu alipowaambia wanafunzi wake kutowazuia watoto kuja kwake, Alikuwa akiwaambia

wafuasi wake katika vizazi vyote_ kwa maofisa wa kanisa, wachungaji, wasaidizi na wakristo wote. Yesu anawakaribisha watoto, na anatusihi tusiwazuie kuja, ni kama vile anatuambia,

Watakuja kama hamtawazuia.” Desire of Ages,p. 517.

MALENGO YA IDARA YA HUDUMA ZA WATOTO

1. Kuwa kuza kiimani (nurture)

Watoto waelekezwe kumtambua Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Wamwelewe katika mtazamo wa Biblia kuwa Yeye ni mwenye upendo mwingi na anasamehe watu wote. Ili mambo haya yafanikiwe watoto wanapaswa kuwa na:

 Watoto wawe na bilblia na vitabu vya nyimbo na kununuliwa lesson zao  Watoto wawe na makambi yao

 Wawe na program mbali mbali kama za retreat n.k  Watoto waandaliwe somo kila sabato kabla ya Muhubiri

 Wahubiri wanapohubiri watambue kuwa watoto ni miongoni mwa wasikilizaji wao  Kuwe na darasa la ubatizo kwa ajili ya watoto waliofikia umri wa kubatizwa.

 Watoto washirikishwe katika mipango ya uamsho na matengenezo.  Wafundishwe kumtegemea Mungu na kuwa watu wa maombi.

2. Kuwawezesha

Kanisani

-Watoto washiriki kutoa huduma kwa watu wengine ndani ya kanisa kama vile kuhudumia wagonjwa.

-Wawe na kwaya yao

-Kila kanisa lianzishe chama cha wahubiri wadogo chini ya kiongozi wa idara hii. -Wahusishwe katika shughuli za kanisa kama vile kukusanya sadaka, kuomba, kusoma fungu na kusali katika kanisa lao mara moja moja

Nje ya kanisa

-Wafundishwe kuwapenda wageni -Kusalimia na kupokea watu wazima

- wajifunze kusema pole, asante na kuomba msamaha

(6)

6 3. Kufanya uinjilisti

 Kutembelea watoto wenzao kwa kusudi la injili

 Watoto waandikishe watu kwa masomo ya sauti ya unabii  Kupitia VBS watoto wawalete watoto wenzao kwa Kristo.

Majina ya mkuu wa idara ya watoto

 Mkuu wa idara ya watoto  Mkurugenzi wa idara ya watoto  Mratibu wa idara ya watoto

Kazi za Mkuu wa Idara ya watoto

 Yeye ni mjumbe wa baraza la kanisa

 Kuunda idara, Auelewe mtaala mpya wa Shule ya sabato ya watoto na kuufundisha  Kuandaa taarifa za conference

 Ni mjumbe wa kamati ya makambi  Kuandaa budget ya Idara

 Kufuatilia kalenda ya matukio yanayohusu watoto

 Adumishe mawasiliano kati ya conference na kanisa na wazazi.  Kutumia muda wa kutosha na watoto

 Kushirikiana na mkuu wa mtaa, mf. Katika huduma ya kuweka watoto wakifu  Awe na rekodi za watoto wote kanisani mwake

 Huratibu shughuli za watoto wakati wa huduma kuu

 Huwafuatilia watoto waliojitoa kwa bwana wakitaka kubatizwa  Ni mtetezi wa watoto kanisani

 Huhakikisha kuna kisa cha watoto kabla ya mhubiri

PROGRAM NA SHUGHULI ZA WATOTO

Ni muhimu sana kama tukipanga program zenye mafanikio kwa ajili ya watoto. Program hizi ndio nyezo za kuujenga mwili wa Kristo. Kamwe hatupaswi kupoteza mwelekeo wa utume wetu katika idara ya huduma za watoto: Kuwakuza watoto katika uhusiano na Yesu unaookoa. Kila program tunayoitoa yapaswa kuwaongoza watoto katika safari yao ya imani.

(7)

7 Siyo lazima tuwe na kila program tunazoziona katika makanisa mengine. Panga zile tu

unazoweza kumudu. Lakini zingatia pia kuwa kadiri ulivyo na program nyingi na kuzifanyia matangazo ndivyo utakavyovutia familia nyingi na ndivyo kanisa litakavyokua.

PROGRAM ZA WATOTO KANISANI

1. Shule ya Sabato ya Watoto

Kusudi: Ili kuwapatia watoto elimu ya kidini itakayowasaidia watoto kukuza mahusiano yao na Yesu. Huu ni wakati ambapo watoto wanajifunza maandiko, wanashirikiana na kuhusishwa katika kuwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo.

Maelezo: Saa nzima katika shule ya sabato, watoto watauhishwa kikamilifu katika kujifunza neno la Mungu kwa kutumia shughuli mbalimbali zitakazofanikisha kujifunza kwao kwa kutumia mwongozo wa kujifunza biblia.

Upekee wake: Hii ni huduma pekee inayowafikia watoto wa kiadventista. Inawapatia fursa kubwa ya kujifunza neno la Mungu na kuwasaidia kulihusianisha neno hilo na maisha yao ya kila siku. Wakurugenzi wa idara ya watoto wanapaswa kuhakikisha kuwa program zilizopo katika shule ya sabato zinazingatia umri.

2. Kanisa la Watoto

Kusudi: Kuwapatia watoto fursa ya kuabudu katika mazingira ya umri sahihi, wakijifunza katika viwango vyao vya kuelewa na kuhusishwa kikamilifu katika ibada.

Maelezo: Kanisa la watoto ni kwa ajili ya ibada ya watoto. Ibada hii huanza mara tu ibada ya watu wazima inapoanza. Hii inawahusu watoto wa miaka 2-8 ambao ni vigumu kwao kuketi na kusikiliza kwa muda mrefu. Ibada inapofanyika kuwe angalau na sabato katika mwezi ambapo watoto watajumuika na wazazi wao ili kujifunza namna ya kuketi katika nyumba ya ibada. Shughuli za ibada katika kanisa la watoto ni kama: Nyimbo za sifa, maombi, ushirika au shuhuda,kujifunza neno, mahubiri ya watoto, maigizo na njia nyinginezo zinazotuelekeza kwenye matumizi ya neno katika maisha yetu ya kila siku.

(8)

8 3. Mkutano wa Maombi wa Watoto

Kusudi: Kuwahusisha watoto katika uzoefu wa maombi.

Maelezo: Kuwe na somo fupi linalotoka katika maandiko ili kuimalisha imani na uelewa wa watoto juu ya umuhimu wa maombi. Program hii huhusisha nyimbo, maombi, na sanaa au ubunifu. Watoto wanaweza kukutana katika nyumba badala ya kanisani.

Upekee wake: Watoto wanapata fursa ya pekee ya kukua kiroho na kuwa na ushirika na wengine.

3. Darasa la Ubatizo la watoto

Kusudi: Kuwaandaa watoto ambao wameonyesha nia ya kubatizwa

Maelezo: Watoto wanajifunza misingi ya imani ya kikristo ya kanisa la waadventista wasabato, ili kuelewa uhusiano wao na wajibu wao kwa Mungu na jamii ya waumini.

Upekee wake: Masomo hayo ya ubatizo yameandaliwa kulingana na uelewa wa mtoto. Yanaweza kuchukua muda unaofaa kwa maandalizi ya ubatizo.

4. Kwaya ya Watoto

Kusudi: Kuwapatia watoto uzoefu wa kuabudu kwa njia ya uimbaji, kuwafundisha namna ya kuimba na kuwaelewesha kuwa uimbaji ni huduma ya muhimu katika uinjilisti.

Maelezo: Watoto wanaweza kuwa na kwaya ya kudumu au ikaandaliwa kulingana na matukio. Wakati mwingine program ya nyimbo inaweza kuandaliwa vizuri na ikahitimishwa kwa

kuwaalika watoto wengine na wazazi wao katika jamii kushuhudia program hiyo. Nyimbo, maombi na program yenyewe vyaweza kuwa ushuhuda mkubwa.

Upekee wake: Huduma hii inaleta pamoja shule za kanisa shule zingine na jamii pamoja.

5. Sabato ya Watoto

Kusudi: Kuwapatia watoto fursa ya kutumia vipaji vyao na talanta zao kwa kushiriki katika huduma ya ibada.

Maelezo: Hii ni program ya pekee kila mwaka sabato ya tatu ya mwezi wa kumi (oktober) ili kusisitiza mahitaji ya watoto na wajibu wetu kama kanisa katika kuyakidhi mahitaji

(9)

9 Upekee wake: Program hii maalum inatupatia fursa ya kuwaandaa watoto kuwa viongozi

kanisani. Watoto wanajisikia kama washiriki wa kanisa wanapohusishwa.

6. Mkutano wa watoto nje ya eneo la kawaid (retreat/kambi)

Kusudi: Ni kwa kusudi la kuwapatia watoto uinjilisti wa kiroho na utunzaji wa watoto katika katika mazingira ya kambi.

Maelezo: Watoto watakutana pamoja kwa muda wa siku 2-3 katika eneo la kambi au mahali pa utulivu palipochaguliwa kwa ajili ya kufanya shughuli zinazowatia moyo katika ukuaji kiroho, kimwili, kijamii na kiakili. Wazo kuu lichaguliwe na program itayarishwe ili kulenga wazo kuu. Masomo yanayotolewa yanaweza kuwa ni pamoja na uwakili, Urithi wa kiadventista, na kujifunza Biblia na mashujaa wa biblia.

Upekee Wake: Watoto wanapata fursa ya kukuza ujuzi wao wa uongozi, kiroho, kimwili, kiakili na kijamii. Katika program hii watoto wanajifunza katikati ya wiki na mwishoni mwa wiki (jumamosi na jumapili).

7. Mkutano wa uinjilisti wa watoto

Kusudi: Kuwasaidia watoto kujitoa kwa Yesu na kuulewa mpango wa ukombozi na misingi ya imani ya waadventista wasabato.

Maelezo: Wakati wazazi wanapohudhuria mikutano ya hadhara, watoto wanakusanywa na kufundishwa mfululizo wa kweli za biblia zinazoendana na umri wao. Program hizi zaweza kuhusisha hadithi za Biblia, mafundisho makuu, mafungu ya kukariri, nyimbo, maombi, ubunifu na sanaa.

(10)

10 8. Chama cha Wahubiri Wadogo

Kusudi: Kuwafundisha watoto wenye kipawa cha kuhubiri neno la Mungu.

Maelezo: Watoto wenye kipaji cha kufundisha hujiunga na chama hiki kinachokutana mara 1-2 kwa juma. Wanajifunza namna ya kuandaa mahubiri, namna ya kuhubiri na ujuzi mbalimbali wa kuongea katika hadhara. Baada ya miezi kadhaa ya mafunzo hawa wahubiri wadogo wanafanyia mazoezi ujuzi huu katika mazingira halisi kama kwenye ibada makanisani, mikutano ya hadhara, makanisa ya watoto n.k.

Upekee wake: Watoto wanafundishwa kama wahubiri wadogo wakati wakati bado wanapenda kufanya hivyo na wana kipaji hicho. Pia kuna fursa ya ushirika na uzoefu wa kiroho pamoja na wana rika wenzao.

9. Tamasha la uimbaji

Kusudi: Kuwapa watoto fursa ya kutumia taranta yao ya muziki katika kuimba na kutumia ala za muziki katika kumtukuza Mungu.

Maelezo: Watoto wanakusanyika kwa ajili ya kuimba nyimbo mbalimbali mchanganyiko. Watoto katika jamii pia wanaweza kualikwa katika program hii.

Upekee wake: Huduma hii huwaleta pamoja watoto wenye karama mbalimbali katika muziki ili zitumike katika sifa na shukrani kwa Mungu muumbaji. Inawapatia watoto nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za uimbaji na jinsi ya kufanya uinjiliti kwa njia ya nyimbo.

10. Kambi la watoto la kufurahia maumbile

Kusudi: Kuwapa shime watoto na kuwaongoza kufurahia maumbile ulimwenguni ambayo ni kazi ya mikono ya Mungu.

Maelezo: Watoto wapelekwe mahali penye maumbile mazuri kwa siku kadhaa na kushiriki katikashughuli zitakazowafanya wamtambue Mungu kama mbunifu mkuu na Muumbaji wetu.

Upekee wake: Watoto wanapata fursa ya kuuchunguza ulimwengu asili kupitia shughuli

(11)

11 MIKAKATI YA IDARA YA WATOTO 2011-2015

Kutokana na umuhimu wa idara hii kama tulivyouona hapo juu. Viongozi wa idara ya watoto katika kila kanisa wakishirikiana na idara zingene kama shule ya sabato, kaya na familia, vijana na Idara ya huduma za washiriki wameombwa kufanya yafuatayo.

 Kutoa elimu kwa wazazi juu ya utendaji kazi wa idara hii na kuwaomba watoe ushirikiano katika kutoa malezi ya kiroho kwa watoto wao.

 Kuhakikisha watoto wanapata lesson zao kulingana na umri wao ( Grace link curriculum)  Kila mtaa ualike mwalimu mzoefu na mpenda watoto kwa ajili ya mikutano ya makambi  Watoto watumie vitabu vyao vya nyimbo katika ibada badala ya kuimba pambio tu

wakati wote.

 Kila kanisa liweke mikakati ya watoto kuwa na kanisa lao ili kuboresha program za shule ya sabato ya watoto na ili mara mojamoja waabudu wenyewe na kupata chakula cha kulingana na umri wao.

 Kiongozi wa watoto ahakikishe watoto wanapata huduma ya kisa kabla ya muhubiri kusimama kila sabato watoto wanapokuwa wamejumuika katika ibada na wazazi wao.  Kiongozi wa idara akishirikiana na shule ya sabato ahakikishe kuwa watoto wanaanza na

shule ya sabato yao bila kuchangamana na watu wazima.

Referensi

Dokumen terkait

Kwa kuwa, wahusika wa aina mbalimbali hujitokeza katika kazi za fasihi na wahusika hao husawiriwa wakiakisi maisha ya wanajamii, hivyo, tumehamasika kufanya

i) Kwanza, utafiti huu una umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya ufundishaji na ujifunzaji wa mada zinazohusiana na isimu katika shule za sekondari kama mada za

Aidha, lengo la utafiti huu kama lilivyobainishwa katika sura ya kwanza ilikuwa ni kuchunguza dhima ya vipengele vya kimtindo katika tamthiliya za kihistoria kwa

Katika jamii ya wajita, majina ya asili hutolewa yakiwa na lengo la historia na matukio mbalimbali yaliyotokea kwa mtu mmoja mmoja au jamii, kwa mfano jina Nyabhita

Kwa kuunganisha mbinu hizo zote shirikishi za uthibiti wa wadudu na magonjwa, tunaiweka miti ya kahawa kuwa yenye nguvu na yenye afya kuthibiti wadudu na magonjwa, bila ulazima wa

Avondale University Avondale University ResearchOnline@Avondale ResearchOnline@Avondale Theology Papers and Journal Articles School of Ministry and Theology Avondale Seminary

Leadership and Personality Correlates of School Head Performance in the Seventh-day Adventist Church Northern Luzon Mission Marvin Nonoy B.. Campit Northern Luzon Adventist College

Conflict Management Practices of Seventh-day Adventist Church Members at the Workplace in Thailand Thitaree Sirikulpat and Paluku Kazimoto Asia-Pacific International University