• Tidak ada hasil yang ditemukan

Athari za Lugha Mama (Kimakonde) katika Ufundishaji

Chanzo cha data hii ni watafitiwa walimu waliojibu hojaji iliyouliza matatizo ambayo mwalimu anakutana nayo anapofundisha wanafunzi wamakonde lugha ya Kiswahili.Utafiti huu unaonesha kwamba wanafunzi wanapokuwa shuleni wanatumia lugha mama ya Kimakonde zaidi katika kufanya mawasiliano ya wao kwa wao kuliko lugha ya Kiswahili. Hii inachangia kuleta ugumu katika kuitumia lugha ya Kiswahili na hivyo kusababisha iwe ngumu kufundisha watoto kujifunza lugha ya Kiswahili darasani. Walimu walijibu swali lilillo taka waeleza athari zinazotokana na lugha mama katika ufundishaji, majibu yalikuwa kama ifuatavyo kuhusu matumizi ya Lugha mama;

Jedwali Na. 4.10: Athari Ya Lugha Mama Katika Ufundishaji

Idadi ya walimu Waliosema Athari ya Lugha Mama Ambao hawakusema

30 22 08

Kielelezo Na. 4.5: Athari Ya Lugha Mama Katika Ufundishaji Chanzo: Uwandani 2017

Watafitiwa 22 sawa na 59% walieleza kuwa wanafunzi wengi wana mazoea ya kuzungumza Kimakonde zaidi kuliko Kiswahili, hii inatokana na kukosekana kwa

0 5 10 15 20 25

baadhi ya misamiati ya lugha ya Kiswahili katika lugha ya Kimakonde na athari za kimatamshi zinazotokana na ndimi za wahusika kuathiriwa na lugha mama na kusababisha kukosekana baadha ya sauti zifuatazo;

/m/ na /r/ / l/,/ na / ʃ / ,/ Ɵ/ na /ð/ / z / na / h /n/

Na kwa kukosekana kwa msamiati wa kutosha wa lugha ya kiswahili,hali hii huwafanya wahalalishe msamiati wa kimakonde kuwa misamiati ya kiswahili na hivyo kutumia maneno yasiyosanifiwa na yanayofahamika na wao wenyewe tu na hii husababisha mtu mwingine nje ya kabila lao hasiweze kuelewa na tatizo hili wanalokutana nalo walimu piapale wanafunzi wanapokuwa darasani na matumizi ya misamiati ya kimakonde zaidi wakati walimu wengi wanaofundisha si wamakonde na hii huwapa changamoto sana wanapokuwa darasani wanafundisha.Walitoa mifano ya maneno hayo kuwa ni;

Jedwali Na. 4.11: Linaloonyesha Athari za Msamiati wa Kimakonde Na Msamiati wa

Kimakonde

Maana yake kwa Kiswahili

1 Kuchonyota Maumivu ya sehemu katika mwili kama mguu

2 Kibadanga Msukule

3 Kukakachala Kukakamaaa kwa kitu

4 Unyala Fangasi

5 Kuchopika Upishi wa kuchemsha bila kiungo chochote

6 Kifuku Masika

8 Wepo Wewe

9 Chikandanga Chakula Mseto(unga wa muhogo na mizizi kwa Kimakonde Ming’oko)

10 Mmbomba Suruali

11 Chanchupi Ndege shorwe

12 Kututusa Kubebelea/kusombelea kitu kama kifusi au mchanga

13 Kugumia Kupiga yowe

14 Kukalambala Mtu aliyekomaa/kushupaa

15 Kituku Njiwa

16 Kuhemwa Kushangaa

17 Kulambila Kusema uongo

Chanzo: Uwandani 2017

Watafitiwa walifafanua kuwa matumizi ya lugha ya Kimakonde ni makubwa sana kuanzia nyumbani hadi shuleni.Wanafunzi wanapata nafasi ndogo ya kujifunza lugha ya Kiswahili wanapokuwa darasani tu. Hii haitoi fursa ya wao kufanya mazoezi mengi ya kujifunza Kiswahili. Mbunda (19960 anasema kujifunza Kiswahili ambayo ni lugha ya pili kwa watanzania weng ni ngumui; wanafunzi wa makabila wanashindwa kumudu Kiswahili kutokana na athari za lugha mama.

Walimu watafitiwa walieleza tatizo jingine wanalokutana nalo wakati wa ufundishaji kuwa ni makosa ya kimatamshi kwa wanafunzi wa kimakonde wanapojifunza lugha ya kiswahili.

Jedwali Na. 4.12: Athari ya Matamshi Wakati wa Kufundisha Kiswahili Idadi ya watafitiwa Walimu waliosema Wasiosema

30 26 04

Kielelezo Na. 4.6: Athari ya Matamshi Wakati wa Kufundisha Kiswahili Chanzo: Uwandani 2017

Mchanganuo wa unaonyesha kuwa walimu 26 sawa na 86% walisema kuwa wanafunzi wa Kimakonde matamshi yao yameathirika sana na lugha ya kimakonde na matamshi ni moja ya njia kuu ya mawasiliano kati ya mwalimu na mwanafunzi. Matamshi yasipokuwa sahihi kwa neno linalokusudiwa matokeo wakati mwingine maana inaweza kuwa tofauti na maana uliyokusudia na hii husababisha ujumbe kufika kwa msikilizaji au mpokeaji ukiwa tofauti na kusudio na hivyo kusababisha jambo kutotekelezeka kwa usahihi au kutekelezwa tofauti. Umuhimu wa mawasiliano ni kukuza uwezo wa kuwasiliana, ujuzi wa miundo na vipengele vya lugha (Leonard, 2001). Hivyo mawasiliano fanisi yanategemea matamshi sahihi ya maneno. Hivyo mtu anapojifunza lugha ya pili, jambo la msingi ni lazima ajifunze matamshi sahihi ya sauti ya lugha husika.hii itasaidia kurahisisha mawasiliano ya pande mbili ya kutoelewana na kusababisha ujumbe husifike kwa usahihi. Ifuatayo ni mifano ya watafitiwa walimu, inayoonesha athari ya lugha ya Kimakonde inavyoathiri watoto katika kutamka maneno ya Kiswahili;

Waliosema Wasosema

Jedwali Na. 4.13: Matamshi ya Lugha ya Kimakonde na Kiswahili Kimakonde Kiswahili Annjambo hamjambo Fezea fedheha Ansini hamsini Selasini thelathini Balabala barabara Ntoto mtoto Samanini themanini Zarau dharua Baazi baadhi Nnazamilia ninadhamiria Nnazani ninadhani Chanzo: Uwandani 2017

Kutokanan na mifano hiyo hapo juu inaonyesha wazi kuwa katika ufundishaji walimu wanapata ugumu katika kufanya mawasiliano na wanafunzi wao. Muhuimili wa mawasiliano mazuri ni utoaji wa matamshi yanayoeleweka kwa msikilizaji. (Mkwera 1979), Lucius (1978), anaamini kuwa kanuni za msingi ya lugha ndizo zinazotawala lugha za walimwengu wote kwa ujumla. Hii ina maana kwamba kila lugha ina kanuni na misingi yake maalumu ambayo inahusu lugha hiyo tu na si lugha nyingine. Hali hii hufanya lugha hiyo ionekane tofauti na lugha nyingine, kama lugha ya Kimakonde na Kiswahili.Hii ndiyo sababu wamakonde wanapata ugumu wa kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa kutumia kanuni za Kimakonde. Sababu nyingine eneo la kijiografia anakotoka huyo mtu, kabila lake, kundi lake la kijamii (kundirika) kwa mfano msanii, mwanasiasa, mcheza mpira wa miguu, elimu aliyonayo na wakati mwingine ulemavu wa viungo kithembe, mwanya. Hizi zote zinaweza kusababisha watu watofautiane

katika matamshi.Walipoulizwa swali kuwa wanafunzi wanaowafundisha wana uwezo wa kuzungumza kiswahili fasaha; majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Jedwali Na. 4.14: Idadi ya Wanafunzi Wanaozungumza Kiswahili

Idadi ya walimu Ndiyo Hapana

30 01 29

Kielelezo Na. 4.7: Idadi ya Wanafunzi Wanaozungumza Kiswahili Chanzo: Uwandani 2017

Kama mchanganuo wa jedwali unavyoonesha hapo juu walimu 29 sawa na 97% wamesema hapana; wakiwa na maana kwamba wanafunzi wanaowafundisha hawana uwezo wa kuzungumza Kiswahili fasaha, na mwalimu 1 sawa na 3% amesema ndiyo, akiwa na maana kwamba wanafunzi wanaowafundisha wana uwezo wa kuzungumza Kiswahili fasaha. Mgawanyo huu unaonyesha kwamba athari ya lugha ya Kimakonde katika Kiswahili inazidi kuonekana ni kubwa na jitihada za makusudi zinahitajika. Swali lilikuwa na sehemu mbili, swali liliuliza kuwa je wanafunzi wanaongea Kiswahili fasaha, jibu lilihitajika liwe ndiyo au hapana na endapo ni HAPANA atoe sababu; Jedwali Na. 4.15: Waliojibu na Wasiojibu Kuhusu Matumizi Fasaha ya lugha ya

Kiswahili

Idadi ya Walimu Waliojibu Wasiojibu 0 5 10 15 20 25 30 Ndiyo Hapana

30 25 5

Chanzo: Uwandani 2017

Data zinaonyesha kuwa Watafitiwa walimu 25 sawa na 83% walitoa sababu,na walimu 5 sawa na 17% hawakujibu,Moja ya sababu ni kwamba wanafunzi wameathiriwa sana na lugha mama kiasi wanashindwa kuongea Kiswahili chenye matamshi, lafudhi ya Kiswahili,sehamu kubwa ya matamshi yao yameelekea zaidi kwenye matamshi ya lugha yao ya Kimakonde, walitoa mifano ya sentensi.

Jedwali Na. 4.16: Mifano ya Athari za Lugha ya Kimakonde Kimatamshi Athari za Kimakonde Kiswahili fasaha

Watoto tano wanaimba Watoto watano wanaimba

Kesho nitajilawa kwenda shambani Kesho nitadamka/kuamka asubuhi na mapema

Ally wamemwita na mama Ally ameitwa na mama Ashura ana domo sana Ashura ni mgomvi sana Chanzo: Uwandani 2017

Watafitiwa waliulizwa kuhusu kama wanafunzi wanachanganya lugha ya kimakonde na kiswahili waliweza kutoa majibu kama ifuatavyo.

Jedwali Na. 4.17: Tatizo la Kuchanganya Lugha

Idadi ya walimu Waliojibu Wasiojibu

Kielelezo Na. 4.8: Tatizo la Kuchanganya Lugha Chanzo: Uwandani 2017

Kielelezo kinaonyesha watafitiwa 15 sawa na 50% walisema kwamba wanafunzi huwa wanachanganya lugha ya Kimakonde na Kiswahili wakati wa kuzungumza. Hii huwasababishia mawasiliano yao kutokuwa ya moja kwa moja wanapowasiliana na mwalimu na hata watu wengine. na 15 sawa na 50% hawakusema.Watafitiwa walitoa mifano ifuatayo;

Jedwali Na. 4.18: Athari za Kuchanganya Lugha ya Kimakonde na Kiswahili

Na: Kimakonde Kiswahili

a. Wepo idaa Wewe njoo

b. Tunakatambogakwa chipula Tunakata mboga kwa kisu c. Yule wanchema Daudi Yule wanamuita Daudi

Chanzo: Uwandani 2017

Utaratibu huu wa uzungumzaji wa kuchanganya unasababisha kiswahili kinachozungumzwa kisiwe cha ufasaha.Matokeo yake kinakuwa Kiswahili kilichochanganyika na kimakonde jambo ambalo linafanya kiswahili kiathirike na kipoteze sifa na uasili wake. Chanzo cha data zifuatazo ni watafitiwa walimu wa shule

0 2 4 6 8 10 12 14 16 Waliojibu Wasiojibu

za msingi waliojibu hojaji iliyowataka kutaja sababu nne zinazochangia kuwaathiri wanafunzi wa Kimakonde katika kujifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili. Majibu yalikuwa kama ifuatavyo;

Jedwali Na. 4.19: Athari za Kushindwa Kujifunza Kiswahili

Idadi ya walimu Waliojibu Wasiojibu

`30 27 3

Kielelezo Na. 4.9: Athari za Kushindwa Kujifunza Kiswahili Chanzo: Uwandani 2017

Mchanganuo katika kielelezo unaonyesha kwamba watafitiwa walimu 27 sawa na 90% wamezianisha sababu nne zinazochangia kuwaathiri wanafunzi wa Kimakonde katika kujifunza Kiswahili kama lugha yao ya pili na walimu 3 sawa na 10% hawakujibu.Watafitiwa waliweza kuzianisha sababu hizo kuwa ni watafitiwa walitakiwa kujibu kuhusu ni sababu zipi ambazo zinachangia wanafunzi washindwe kuzungumza Kiswahili,watafitiwa walimu walifafanua kuwa mazingira wanayoishi wanafunzi yamezungukwa na wanajamii wa asili wa lugha yao moja ya kimakonde ambayo wanaifanya lugha yao kuu ya mawasiliano ambayo ni Kimakonde(lugha jamii) Idadi ya waliojibu ni kama ifuatavyo:

0 5 10 15 20 25 30 Waliojibu Wasiojibu

Jedwali Na. 4.20: Wanafunzi Kushindwa Kuzungumza Kiswahili

Idadi ya walimu Waliojibu Wasiojibu

`30 19 11

Kielelezo Na. 4.10: Wanafunzi Kushindwa Kuzungumza Kiswahili Chanzo: Uwandani 2017

Kama kielelezo kinavyofafanua walimu 19 sawa na 63% wametoa sababu kuwa katika mazingira wanayoishi kunakosekana na maingiliano /mwingiliano wa watu wa makabilia mengine katika maeneo ya wamakonde ambapo huchangia wamakonde kushindwa kuzungumza kiswahili na badala yake wanawasiliana zaidi kwa lugha yao ya kimakonde. Hii huchangia kwa kiasi kikubwa kwa vizazi vya watoto vilivyozaliwa na vinavyoendelea kuzaliwa kushindwa kujifunza lugha ya pili ya Kiswahili. Mtafiti alipokuwa uwandani aliweza naye kushuhudia hilo kwa watoto na hata wazazi, wote ni wamakonde na wanaongea Kimakonde, walimu 11 sawa na 37% hawakujibu.

Watafitiwa wengine wapatao 13 sawa na 43%walitoa sababu ya kuwa jamii za kimakonde wanapenda kuishi maeneo /mazingira ya kwao zaidi bila kutengeneza

Waliojibu Wasiojibu

utamaduni wakutembeleana kama kwa kufanya biashara, sherehe, kilimo na makabila mengine ambayo Kiswahili kimeshamiri.haya yote huwza kusababisha kuwepo kwa lugha moja itakayoweza kuwaunganisha watu wote wenye utamaduni na lugha mbalimbali kama umuhimu wa swala hili unavyoonyeshwa na Kiango (2002), anasema mtu binafsi hutoka kwenye jamii inayozungumza lugha tofauti na lugha ile ya kwao.hali hii itamlazimisha mtu kujifunza lugha ya jamii ile ya pili ili aweze kuwasilianan nao.Maingiliano hayo yangewafanya wachangamane na kuweza kujifunza lugha ya Kiswahili vizuri.

Tatizo jingine lililoelezwa ni mila na desturi za kimakonde huwa hazitoi kipaumbele katika kujifunza lugha ya kiswahili.Mazingira wanayoishi wazazi hutumia lugha mama zaidi na tatizo linaanzia hapo. Data zimeonyesha kuwa wanafunzi walio wengi wanaporudi toka shule yaani wanapokuwa nyumbani, huwa hawatumii tena lugha ya Kiswahili katika mawasiliano kati yao na wazazi wao, salaamu na mazungumzo mengine hutakiwa kufanyika kwa lugha ya kimakonde. Hii husababisha swala la kusalimia kwa wageni liwe linafanyika kwa kilugha kwa kuamini kwamba wote ni wamakonde na hii hufanya salaamu ya heshima kwa wakubwa itolewayo kwa kiswahili yaani ‘Shikamoo’, kuonekana kwa wamakonde kuwa haina uzito wowote au haina maana yoyote dhidi ya salamu zao za kilugha.

Kimakonde kimekuwa ni lugha ya familia, koo na jamii.kwa maana hiyo familia na koo nyingi za kimakonde, hakuna anayeruhusiwa kutumia Kiswahili katika kuwasiliana wawapo nyumbani.kwa namna moja au nyingine limekuwa kama swala la lazima kwa msukumo wa kuonekana kama unaringa pale unapoongea Kiswahili, unasaliti kabila lako, na kuonekana huna kabili. Wamakonde huipenda lugha yao ikiwa pia kama njia

ya kufanya mawasiliano yao kuwa siri mbele ya mgeni.Mtafiti akiwa maskanini aliweza kuishuhudia hiyo kupitia kwa wanafunzi na wazazi pale walipokuwa wanataka kupeana ufafanuzi wa juu ya umuhimum wa utafiti huu kwao walitumia kilugha mzaidi, na kwa kufanya hivi hujikuta wanawaambukiza watoto wao tabia hii. Jambo hili huwanyima watoto hao muda wa kutosha kujifunza na kuzungumza Kiswahili katika mazingira wanayoishi.

Licha ya hayo, pamoja na wanafunzi kufundishwa kiswahili,hukosa muda wa kukifanyia mazoezi kwa kukizungumza kwa hiyo wakati mwingine huweza kusahau msamiati, matamshi au maanana matumizi ya baadhi ya maneno. Rocha (2011), anasema kuwa wabantu wengi wameathiriwa na lugha mama, hii ni kutokana na matumizi ya lugha mama. Idarus (2005), ametaja athari zinazojitokeza katika lugha ya Kiswahili baada ya mtu kuathiriwa na mambo kadhaa kuwa ni pamoja na kuongeza vitamkwa ama sauti pasipohitajika, msamiati wa lugha, makosa ya muundo wa sentensi na makosa katika matamshi. Paul (2001), anaeleza kuwa muktadha hupewa nafasi muhimu katika ufundishaji, hivyo mwanafunzi anapojifunza lugha fulani, mazingira ni muhimu kuangaliwa. Idarus (ameishatajwa.), katika Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili anaendelea kueleza kuwa maeneo yanayochangia ni pamoja na mazingira. Dixon (1992), anaeleza kuwa uhusiano wa lugha ni baina ya jamii husika au wazazi, watoto na ndugu katika ukoo.Lugha inaweza kukua kuanguka au kuathiriwa kutokanana kuwepo na matumizi ya lugha nyingine katika jamii hiyo.

Tatizo jingine ambalo lilionekana kusababisha ni, uhusiano na mwingiliano mkubwa wa lugha hizi mbili unachangia kwa sehemu kubwa sana ukizingatia lugha ya kiswahili ni zao la lugha za kibantu hivyo maeneo mengiyamekuwa yanafanana kwa kiasi fulani

kiasi kwamba mzungumzaji anashindwa kugundua tofauti na kushindwa kuona makosa na kuyasahihisha. Watafitiwa waliulizwa kuhusu namna wanavyowasaidia wanafunzi wanaotumia lugha ya Kimakonde kama lugha yao rasmi ya mawasiliano wakati wa kujifunza lugha ya Kiswahili.majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Jedwali Na. 4.21: Watafitiwa Waliojibu na Wasiojibu Kuhusu Namna Walimu Wanavyowasaidia Wanafunzi

Idadi ya Walimu Waliojibu Wasiojibu 30 30 0

Data zinaonyesha kuwa walimu 30 sawa na 100%, waliweza kutoa majibu yao tofautitofauti ambayo yaliweza kujibu swali hili kama ifuatavyo; Katika kuwasaidia huwa wanawapa mazoezi mengi yatakayowawezesha kuwa na uwezo wa kuzungumza Kiswahili kama;

(i) Kuwaimbisha nyimbo nyingi za Kiswahili

(ii) Kuwapa mazoezi ya kutunga sentensi mbalimbali

(iii) Kuwapa mazoezi ya kusimulia adithi fupi za Kiswahili na kuwapa vitabu vya kusoma hadithi

(iv) Kufanya ziara ya kwenda shule jirani na wakati mwingine maeneo ya watu wengine tofauti.

(v) Kujenga utaratibu wa kutoa zawadi kwa wale wanafunzi wanaoongea Kiswahili tangu asubuhi hadi jioni.

(vi) Kuwashuhulisha mara moja pale wanapokosea (vii) Kutoa msisitizo wa wanafunzi darasani

(ix) Kuanzisha midahalo ya kujadili Kiswahili

Na waliweza kueleza mafanikio ambayo wanayapata kuwayapo mabadiliko ambayo yanaonekana kwa baadhi ya watoto baada ya kutumia njia hizi kwa wapo ambao walianza shule hawajui Kiswahili kabisa lakini sasa wanaweza kuongea kidogo. Kutokana na data hizi mtafiti ameona kwamba njia hizi zilizo tumiwa na walimu kuwa zikitiliwa mkazo katika shule zinaweza kusaidia kupunguza tatizo hili au kama si kulimaliza kabisa.

Chanzo cha data zifuatazo ni watafitiwa wamilisi wa lugha (wazazi/walezi na wazee) na wanafunzi wa shule za msingi wanaozungumza Kimakonde na waliojibu hojaji iliyouliza iwapo yeye ni mzungumzaji mzawa wa lugha ya Kimakonde. Watafitiwa walijibu kama ifuatavyo;

Jedwali Na. 4.22: WatafitiwaWazawa wa Lugha ya KImakonde

Watafituwa (waliojibu) Ndiyo Hapana

Wamilisi 15 05

Wanafunzi 35 03

Kielelezo Na. 4.11: Watafitiwa Wazawa wa Lugha Ya KImakonde Chanzo: Uwandani 2017 0 5 10 15 20 25 30 35 40 NDIYO HAPANA Wamilisi Wanafunzi

Taarifa katika jedwali hapo juu zinaonyesha kwamba watafitiwa wamilisi 15 ambao ni sawa na 75% na wanafunzi 35 sawa na 92% walisema NDIYO wakati huo wamilisi 5 sawa na 25% na wanafunzi 3 sawa na 8% walisema HAPANA. Mgawanyo huu unaonyesha kwamba waliosema ndiyo ni wengi zaidi, hii ina maana kwamba maeneo aliyopita mtafiti (uwandani) wenyeji wengi ni wamakonde. Kutokana na hali hii mtafiti ameona kwamba inatoa nafasi kubwa kwa lugha ya Kimakonde kuathiri lugha ya Kiswahili.Walipoulizwa ni lugha gani wanaitumia zaidi katika mawasiliano wanapokuwa nyumbani. Majibu yalikuwa ifuatavyo:

Jedwali Na. 4.23: Kuonyesha Lugha Wanayotumia Zaidi

Wahusika Kiswahili Kimakonde Majibu Yote

Sawa

Wanafunzi 5 30 3

Wamilisi 2 14 4

Kielelezo Na. 4.12: Lugha Wanayotumia Zaidi Chanzo: Uwandani 2017

Kama mchanganuo hapo juu unavyoonesha, wanafunzi 5 sawa na 13% walijibu kuwa wanatumia sana Kiswahili katika mawasiliano, wanafunzi 30 sawa na 79% walijibu kuwa wanatumia Kimakonde kufanya mawasiliano na wanafamilia na wanafunzi 3 sawa na 8% walijibu kuwa majibu yote ni sawa. Na kwa upande wa wamilisi/

0 5 10 15 20 25 30

mchanganuo unaonyesha wamilisi 2 sawa na 10% wanatumia lugha ya Kiswahili, wamilisi 14 ambao ni sawa na 70% wanaongea sana kimakonde na wamilisi 4 sawa na 20% wanaonyesha kuwa majibu yote sawa. Katika mchanganuo wa data hizi inaonyesha kuwa lugha ya kimakonde ndiyo iliyokuwa na mashiko katika kufanya mawasiliano katika maeneo yale ya vijiji vyao. Swali hili lilihusisha wanafunzi wa shule ya msingi na wamilisi wa lugha ya kimakonde ambapo walitafakari kuwa maoni kuhusu mbinu au hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wa Kimakonde kusifiwa kiswahili sanifu. Yafuatayo ni majibu yaliyotolewa.

Jedwali Na. 4.24: Wazazi Wanajukumu la Kuwasaidia Wanafunzi Kuongea Kiswahili

Na Waliojibu Wasiojibu

Wamilisi wa lugha 18 2

Wanafunzi 32 6

Kielelezo Na. 4.13: Wazazi Wanajukumu la Kuwasaidia Wanafunzi Kuongea Kiswahili

Chanzo: Uwandani 2017

Kama kielelezo kinavyoonyesha, kundi la kwanza la wamilisi linaonyesha kuwa waliojibu ni 18 ambao ni sawa na 90% walitoa maoni kuwa wazazi wanajukumu kubwa la kuwasidia watoto wao kutumia Kiswahili mara kwa mara hasa wanapokuwa shuleni

0 5 10 15 20 25 30 35 Waliojibu Wasiojibu Wamilisi wa lugha Wanafunzi

na nyumbani kwa sababu kuifahamu lugha hii itawasaidia kujifunza na masomo mengine vizuri. Walieleza kuwa wazazi wanatakiwa wawe mtari wa mbele kuzungumza Kiswahili wanapowasilianan na watoto wao, kufanya jitihada za kukieneza Kiswahili kwa kutoa elimu kwa wenzao kuhusu umuhimu wa lugha hii kwao na pia kuacha kasumba za kubeza lugha ya Kiswahili. Kuhusiana na mbinu au hatua za kuchukua katika kuwasaidia watoto wa Kimakonde wamilisi 2 hawakujibu sawa na 10% na kwa upande wa wanafunzi mchanganuo wao ni kama ifutayo wanafunzi 32 walitoa maoni na mbinu za kutumia sawa na 74% na wanafunzi sawa na 16% hawakusema chochote katika swali hili.

4.5 Mikakati ya Kufanya ili Kupunguza Athari za Lugha ya Kimakonde