• Tidak ada hasil yang ditemukan

Kiswahili ni lugha inayotumiwa na jamii ya watanzania na Kimakonde ni lugha inayotumiwa na Wamakonde wanaoishi Mtwara Kusini mwa Tanzania, Massamba na wenzake (1999) wanasema” Lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao TUKI (1981) inatoa maana ya lugha kuwa, “lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kabila fulani kwa ajili ya kuwasilana. Chomsky(1957) anasema kwamba“Lugha ni seti ya sentensi (zenye ukomo au zisizo na ukomo), na kila moja

ikiwa na urefu fulani na ikiwa imeunda seti za elementi ambazo zina maumbo “Mkondo huu umefuatwa na wanaisimu wengine Fergusson (1969) anaeleza lugha kama tukio la jamii ambapo Labov(1991) anaifafanua dhana ya lugha kama umbo la tabia za jamii.Wataalamu hawa wawili wanatoa fasiri hizi wakiegemea jamii kwa sababu wao ni wanaisimu jamii. Crystal (1997) anaeleza lugha kama elementi ya akilini ambayo hujidhihirisha nje ya mkusanyiko wa sentensi. Chomsy (1977) anabainisha lugha kama elementi ya kiakili ambayo mtu huipata kwa kujifundisha, na elementi hii hutumiwa na mzungumzaji pamoja na msikilizaji, pia anazungumzia muundo wa nje wa lugha, kwa maana ya mkusanyiko wa sentensi zinazoeleweka pasi na kurejelea sifa za kimiktadha.

Kutokana na fasili hizi za wataalamu hawa lugha ni utaratibu maalumu wa sauti za nasibu ambazo huhodhi maana katika jamii fulani.Sauti hizi hutumiwa na wanajamii hawa kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. Sauti hizi lazima ziwe za kutamkika. Aidha, lugha ni mfumo nasibu unaotumiwa na watu wenye utamaduni mmoja kwa minajili ya mawasiliano kati yao,na mfumo huu ndiyo huwatambulisha na kudumisha umoja wao.

Wamakonde ni wanajamii wenye utamaduni mmoja na wanazungumza lugha moja halikadhalika kimakonde kinazungumzwa na jamii moja yenye utamaduni mmoja na lugha moja, Inatumika zaidi katika mawasiliano katika nyanja mbalimbali. Lugha kwa upande wake na undani wake inahusisha na kuwasiliana kwa kusema na kusikia hizi ni sauti ambazo ni nasibu katika kuambatana kwazo na maana maalumu, naye Robert Lado (1964) anadai kuwa‘’lugha ni chombo cha kuwasiliana miongoni mwa binadamu wa jamii moja na utamaduni wao wa namna moja. Barber (1964) anasema kuwa, lugha ni utaratibu wa kupeana ishara unaotumia alama za sauti,ni utaratibu unaotumiwa na

kundi maalumu la watu kwa nia ya au madhumuni ya kuwasiliana kwa hoja ya kushirikiana katika jamii”. Nkwera (1979) anasema, ‘’Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana zilizokubaliwa na jamii ya watu zitumike katika kuwasiliana’’. Malmstron (1960) anaelezea kuwa lugha ni “utaratibu wa miundo,ni jumla ya mazoea ya tabia ambazo kwazo wakazi wa jamii fulani huhusiana na kuwasiliwana katika utamaduni wao.

Mawasiliano ya jamii hizi ni lazima yahusishwe na sauti, Msokile (1972) anadai kuwa“Lugha ni chombo cha kuwasiliana kwa binadamu wa utamaduni wa aina moja au tamaduni mbalimbali ikiwa watajifunza. Mawasiliano kati ya watu hawa yanazingatia mambo ya msingi, yakiwemo matumizi ya alama fulanifulani ambazo huandamana na sauti” kimsingi alama hizi ni nasibu katika kuambatana kwazo na maana maalumu na nasibu katika maumbo yake katika lugha fulani.

Mhina, na Kiimbila, wanasema ‘’Lugha ni utaratibu (mfumo) kamili wa sauti za kusemwa, sauti za nasibu,za watu wa utamaduni fulani, watumiao kupashana habari’’. Archbald,anadai kuwa ‘lugha ni umbo la asili lililoshonana sana ambalo ni kitendo kinachomhusu binadamu. Alama zake zinatokana na sauti zinazofanywa na ala za sauti” Naye Crystal (1992) anafasili lugha kama: “Mfumo wa sauti nasibu, ishara au maandishi kwa ajili ya mawasiliano na kujielezea katika jamii ya watu”. Katika fasili yake Crystal ametaja mambo kadhaa ya msingi kama ifuatavyo;

Mfumo-Kila lugha ina muundo. Kwa upande mwingine kila lugha ni kijisehemu tu cha miundo iliyopo katika jozi nzima ya miundo ya lugha duniani. Miundo hiyo kama vile jinsi maneno yanavyoundwa au jinsi vishazi vinavyofuatana, hufuata ruwaza maalumu.

Sauti Nasibu-Uhusiano baina ya sauti za maneno au umbo linalowakilisha alama katika lugha ya alama na ule wa maana inayowakilisha ni wakinasibu tu au ulitokana namakubaliano ya wanajamii wazungumzao lugha fulani. Sauti, Alama na Ishara-Kila lugha huteua sauti au ishara zinazowakilisha wazo au ujumbe fulani. Isharaza maandishi ni sehemu ndogo ukilinganisha na lugha zamazungumzo ambazo zipo takribani lugha zaidi ya 6800 za duniani.

Jamii ya Wanadamu-Ni watu tu ndio watumiao lugha na ni jamii zao pekee ndizo zinazoteua na kuyapa maana maneno wayatakayo na jinsi gani miundo ya lugha zao ziwe. Lugha za wanadamu zinatofauti za msingi dhidi ya njia nyingine za mawasilaiano za viumbe wengine.

Mawasiliano-Njia mojawapo ya kuelezea ni kwa namna gani lugha huitumikia jamii na kuwasaidia watu kuwasiliana yaani kutoa na kupokea ujumbe pamoja na kutolea hisia zao. Kwa kutumia lugha tunasema tunachotaka ili kukidhi mahitaji yetu. Kuandika, kusoma, kusema na hata kutumia mfumo wa ishara. Zote hizo ni njia za mawasiliano ya lugha.

Kujielezea-Pamoja na kuwa wanadamu hutumia lugha kwa mawasiliano kiujumla lakini ieleweke kuwa watu hutumia lugha kama njia ya kujitambulisha kama wanakundi jamii fulani mahsusi. Kwa mfano Wapemba au Wasiu.Wazo hili la lugha linatukumbusha migao mitatu ya lugha kulingana na Ferdinand de Saussure (1916). Saussure alidai kuwa lugha ipo katika viwango vya langage, langue, na parole.

Langage inarejelea lugha katika ujumla wake; yaani ni sifa zinazoitambulisha lugha

wote. Katika kiwango hiki Ferdinand de Saussure (ametejwa) anaendelea kusema kuwa upo uwezekano wa kuona sauti zote zinazotumiwa na mwanadamu katika jungu kuu moja. Kwa mfano, kusema kuwa sauti [a] ni vokali inayotumika katika lugha ya mwanadamu ni kauli ya langage.Hii ni kwa sababu sauti hii inapatikana katika lugha nyingi za ulimwengu. Sauti hizi huteuliwa na kila utamaduni na kupewa ruwaza na mpangilio fulani ambao hujulikana kama langue.

Langue ni mfumo wa sheria za matumizi ya lugha mahsusi.

Parole nayo ni matumizi ya mfumo wa lugha katika muktadha mahsusi. Swala hili

limeangaliwa kwa undani katika sehemu ya sarufi miundo. Watu hujifunza lugha japo huzaliwa na uwezo wa lugha. Kwa vyovyote vile tunavyoitazama lugha inatujuza kuwa lugha ina sifa zifuatazo:

(i) Lugha inahusisha sauti.

(ii) Lugha ina husisha sifa za unasibu. (iii) Lugha ni mali ya mwanadamu. (iv) Lugha ni mfumo.

(v) Lugha ni shughuli ya jamii.

(vi) Lugha hubadilika kwa sababu ni kiungo hai.

Inatupasa kuelewa kuwa lugha ni mkondo ambao ni changamano. Ina vitengo vingi ndani yake. Vitengo hivi hutokana na hali kuwa lugha husemwa kwa njia tofauti katika mahali tofauti, miktadha tofauti, na watu tofauti hata kama lugha ni ile ile. Kwamfano lugha ya Kiswahili husemwa kwa njia tofauti na watu tofauti katika mazingira na maeneo tofauti, hii inatokana na kuathiriwa na lugha za makabila, Kimakonde ni moja ya kabila ambalo lina athiri lugha ya kiswahili hata kinazungumzwa tofauti maeneo ya

Mtwara ambako huwa wanatumia zaidi sauti ya / n / sehemu ambayo inatakiwa kutumia sauti /m/ Lugha ya Kiswahili inayosemwa pwani ya Mtwara, sivyo inavyosemwa sehemu za bara kama Newala, Tandahimba na Mahuta. Tofauti huwa katika kiwango cha msamiati, matamshi, na miundo ya sentensi. Katika lugha ya Kimakonde kuna makosa ya kimuundo madhalani miundo yao ya sentensi hujitokeza kama vile Wale

vijana walionkaja jana wameondoka, badala ya wale vijana waliokuja jana

wameondoka, Tofauti nyingine zaweza kutokana na mambo kama vile umri, cheo,

elimu, urafiki na uwezo wa kiuchumi. Sifa hizi huathiri jinsi watu mbalimbali wanavyoteua msamiati, kutamka maneno, na kutunga sentensi.

Lugha vile vile huwa tofati kutegemea utendakazi wake. Davy na Crystal (1969) wameeleza swala hili kwa uwazi zaidi. Kulingana na wataalamu hawa lugha katika sekta mbalimbali za kutenda kazi huibua mitindo ya kipekee. Kuna lugha ya kidini, mazungumzo ya kawaida, sheria, michezo na nyinginezo. Kila lugha hujisimamia katika msamiati wake, sintaksia, na pia mofolojia yake. Jamii ya Kimakonde ina misamiati yake mingi sana ambayo huwa inaitumia ambayo huwa mara nyingi wanaihusihsa sana na lugha ya Kiswahili kwa mfano kuchepuka –kwenda kujisaidia haja ndogo, ngolombwe—mnyama swala, tawara—mnyama mbawala, ntesa— karanga, na katika kufanya hivvyo Kiswahili huwa kianaathiriwa.

Kwa ujumla wake lugha ni utaratibu (mfumo) maalumu wa sauti za nasibu zenye maana ambazo hutumiwa miongoni mwa binadamu kwa madhumuni ya mawasiliano miongoni mwao. Sauti hizo lazima ziwe za kutamkika. Kutokanana maana za wataalamu hawa, kuna mambo sita ya kuzingatia kama yalivyoonyeshwa, mambo hayo ni:

(i) Lugha ni Sauti za Kusemwa za Binadamu kwa Kutumia Ala za Sauti

Kimsingi hakuna kiumbe ambacho si binadamu kinachoweza kuzungumza lugha. Lugha ni chombo maalumu wanachotumia binadamu kwa lengo la mawasiliano. Lugha huambatana na sauti za binadamu kutoka kinywani mwake ambazo zina maana fulani.Binadamu hutumia mdomo, meno, ufizi, kaakaa laini, kaakaa gumu, koromeo n.k., kwa ajili ya kutolea sauti hizi. Kwa kawaida mtu ambaye hawezi kusema au kutoa sauti zenye maana huitwa bubu.

(ii) Lugha ni Sauti za Nasibu

Mwadamu hazaliwi na lugha isipokuwa huikuta katika jamii. Iwapo mwanadamu hazaliwi na lugha basi tunaweza kusema hukutana nayo kwa nasibu Upangaji wa sauti zitumikazo katika lugha na kuziweka katika mfumo wa mawasiliano hutegemea wale wanaoanzisha lugha inayohusika. Hakuna utaratibu maalumu wa mpangilio wa sauti ambao huwa tayari. Kwa hiyo wanaoanzisha lugha huzipanga sauti katika utaratibu ambao ni wa nasibu tu.

Massamba na wenzake (2013) wakifafanua dhana hii y sauti nasibu wanasema kuwa ni sauti ambazo uteuzi wake haukufanywa kwa kufuata mantiki au vigezo fulani maalum bali umetokana na makubaliano ya kimazoea tu ya watumiaji wa lugha inayohusika, na hii ndiyo maana sauti za lugha mbalimbali ama zinaweza kufanana sana au kwa kiasi fulani tu na zinaweza pia zikasigana sana au kwa kiasi fulani tu. Katika utaratibu huu lugha ya Kiswahili ina maneno na majina ambayo yameundwa kutokana na sauti mbalimbali za lugha ya kibantu Kimakonde kikiwemo. Hivyo muhimili mkuu wa lugha asili ni sauti na mihimili mingine ni uunganishaji wa sauti kuunda silabi au mofimu;

uunganishaji wa mofimu kuunda maneno na uunganishaji wa maneno kuunda tungo kubwa zaidi.

(iii) Lugha ni Sauti Zenye Utaratibu Maalumu

Sauti ya lugha yoyote huwa zimepangwa kwa kufuata utaratibu fulani uliokubaliwa na jamii hiyo ya watu. Kwa maneno mengine si kila sauti itokayo kinywani mwa binadamu ni lugha.Mtoto anapolia hatusemi anaongea au anazungumza. Utaratibu huo huitwa sarufi.Mfano : Hatusemi.

John embe ana.

Nimepoteza mimi kisu changu.

Jamii imepata kusema.

John ana embe.

Mimi nimepoteza kisu changu.

(iv) Lughani Sauti za Utamaduni wa Watu Fulani

Utamaduni ni mila desturi za maisha ya watu zilizojengwa tangu awali.Lugha inatawaliwa na maneno ya utamaduni wa watu hao.

(v) Lugha Ina Maana Fulani

Utaratibu wa kupangilia sauti peke yake hautoshi kukamilisha maana ya lugha.Sauti zinapowekwa kwenye muundo maalumu ndipo zinapokuwa na maana ambayo zimepangiwa katika lugha hiyo. Muundo huo unaitwa mpangilio wa fonimu, mpangilio wa fonimu hizi na maana zinazoambatana na mipangilio hii, ndiyo hasa vitu vinavyotofautisha lugha moja na nyingine. Kwa mfano neno “paba’’, mpangilio wake

haukubaliki katika Kiswahili kwa sababu neno halina maana yoyote katika jamii ya waswahili.

(vi) Lugha ni Sauti za Kueleza Wazo

Lugha ni sauti zinazomwezesha mwanadamu kupashana habari au kujuliana habari na wenzake. Kwa hiyo lugha lazima iwe ni sauti za nasibu za kusema na binadamu. Sauti hizo za binadanu ni lazima ziwe na utaratibu maalumu wa kuwasiliana, na kama hakuna utaratibu maalumu hiyo sio lugha. Sauti na milio iko mingi duniani, milio ile inayoweza kuwafanya binadamu wawsiliane ndiyo tunayoita lugha.