• Tidak ada hasil yang ditemukan

4.5 Dhamira Zilizojitokeza Kutoka katika Tamathali za Semi

4.5.1.2 Dhamira ya Mapenzi Nje ya Ndoa

umma wanavyojipendelea wao kwa kujiwekea vifaa bora vya kazi bila ya hata kuwajali watumishi wengine.

Jedwali Na. 4.3.7.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya shitizai / kejeli kwa kutumia maneno yenye kuleta maana kinyume iliyokusudiwa ama maana kinyume na ukweli ulivyo. Ukurasa wa 181: Inspekta Wright amesimama mbele ya mlango wa ile nyumba, akamkaribisha kwa kumkejeli. Karibu bwana kubwa. Data hii ya tamathali ya semi ya shitizai / kejeli imeibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kuonesha namna baadhi ya viongozi wa serikali au taasisi za umma wanavyotumia vibaya madaraka yao kwa kuwadharau na kuwakejeli watu wengine.

Jedwali Na. 4.3.10.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tabaini kwa kutumia maneno yanayosisitiza jambo kwa njia ya ukinzani. Ukurasa wa 85: Koplo Matata alitoka kwa haraka na kiasi cha kufumba na kufumbua alirudi na jalada mkononi na kumkabidhi Inspekta Wright. Data hii ya tamathali ya semi ya tabaini imeibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kusisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani pale aliposema kiasi cha kufumba na kufumbua alirudi na jalada… data hii inaonesha namna baadhi ya viongozi wanavyotumia vibaya madaraka yao kwa kuwatuma kwa njia isio sahihi watumishi wa umma.

4.5.1.2 Dhamira ya Mapenzi Nje ya Ndoa

Dhamira ya mapenzi nje ya ndoa imeibuliwa na mtafiti kupitia data alizozikusanya za matumizi ya tamathali za semi mbalimbali. Mapenzi nje ya ndoa ni ile hali ya mtu

aliyeoa au kuolewa akawa anafanya mapenzi kwa mtu mwingine, ilhali yeye ni mke au mume wa mtu. Waandishi wote wawili wametoa dhamira zinazohusu mapenzi nje ya ndoa. Miongoni mwa tamathali za semi zilizoibua dhamira hizo ni kama zifuatazo:

Data zinazoonesha dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kama zilivyoorodheshwa kutoka katika riwaya ya Kichwamaji.

Jedwali Na. 4.3.1.1 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashibiha kwa kulinganisha vitu viwili kwa kutumia kiunganishi. Ukurasa wa 2: Watu tulikua tumekaa nje tuliweza kusikia sauti yake ikinguruma kama samba. Data hii ya tamathali ya semi ya tashibiha imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kutumia ulinganishi wa ungurumaji wa sauti ya mwanamme kwa mwanamke wa nje kama mngurumo wa samba. Data hii inaonesha namna baadhi ya wanaume wanaotoka nje ya ndoa zao kwa kuwafuata wanawake na kuwatia maneno ili wakubaliwe jambo lao.

Jedwali Na. 4.3.4.1 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya mubalagha kwa kuyakuza mambo kuliko vile yalivyo kwa kuengeza chumvi. Ukurasa wa 70: Tulikwenda kwa vidole mpaka mlango wa nyuma, tukajibanza ukutani. Data hii ya tamathali ya semi ya mubalagha imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kuonesha namna watu wanavyoenda kwa hawara wao kwa njia ya kificho sana. Data hii imeonesha baadhi ya wanaume wanaowaendea wanawake wa nje ya ndoa zao kwa kificho sana.

Jedwali Na. 4.3.5.1 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tafsida kwa kuficha matusi na kupunguza ukali wa maneno. Ukurasa wa 19:

Niliona wazi kwamba Manase alikuwa akijaribu kufanya mambo yasiyofaa. Data hii ya tamathali ya semi ya tafsida imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kuficha matusi na kutumia maneno laini kwa kusema kufanya mambo yasiyofaa. Data hii inaonesha namna baadhi ya wanaume wanaofanya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kuwaacha wake zao na kuwaendea wanawake wa nje. Data zinazoonesha dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kama zilivyoorodheshwa kutoka katika riwaya ya Vuta n’kuvute.

Jedwali Na. 4.3.1.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashibiha kwa kulinganisha vitu viwili kwa kutumia kiunganishi ili kuipamba kazi ya fasihi na kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Ukurasa wa 150: Tumbo lilikwisha kuwa kubwa limeumuka kama aliyemeza hamira. Data hii ya tamathali ya semi ya tashibiha imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kulinganisha ukubwa wa tumbo na umezaji wa hamira. Data hii inaonesha namna madhara yanayopatikana iwapo mwanamke atafanya mapenzi nje ya ndoa yake kwani hukosa msaidizi wa kumsaidia katika kulea mimba.

Jedwali Na. 4.3.2.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashihisi kwa kukipa uwezo wa kibinadamu kitu au kiumbe kisichokuwa na sifa hiyo. Ukurasa wa 105: Aliwaza labda amweleze au aiweke siri ile moyoni mwake huku ikimla na kumtafuna pamoja na kumuondolea raha ya maisha. Data hii ya tamathali ya semi ya tashihisi imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kuipa neno siri uwezo wa kibinadamu wa kula na kutafuna na kumuondolea raha ya maisha kwa mpenzi wake wa nje. Data hii imeonesha namna

baadhi ya madhara wanayoyapata wapendanao wanaofanya mapenzi nje ya ndoa kwa kutokuwa na raha ya maisha.

Jedwali Na. 4.3.4.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya mubalagha kwa kuyakuza mambo kuliko vile yalivyo kwa kutia chumvi. Ukurasa wa 21: Salum alimtumbulia macho Yasmin akaanza kumchunguza tokea utosini hadi dole gumba halafu akamuuliza; hujambo dada? Data hii ya tamathali ya semi ya mubalagha imetoa dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kuonesha baadhi ya wanaume wanaowafuata wake za watu bila ya kujali kuwa wanawake hao wanawaume zao.

Jedwali Na. 4.3.9.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali za semi ya takriri kwa kuyarudia rudia maneno zaidi ya mara moja kwa ajili ya kusisitiza jambo. Ukurasa wa 77: Denge unataka nikuimbie kweli? Ala! Sasa unafikiri nakufanyia mzaha? Ngoja usiwe na haraka, iko siku nitakuimbia. Iko siku nitakuimbia… Data hii ya tamathali ya semi ya takriri imeibua dhamira ya mapenzi ya nje ya ndoa kwa kuyarudia rudia baadhi ya maneno; “…iko siku nitakuimbia. Iko siku nitakuimbia…” kwa kusisitiza namna baadhi ya wanandoa huwakimbia waume zao na kwenda kwa wanaume wa nje na kuwafanyia mambo makubwa ikiwemo ya kuwaimbia.

Jedwali Na. 4.3.10.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tabaini kwa kusisitiza jambo kwa kutumia maneno kinzani ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Ukurasa wa 74: Mwisho Bwana Raza alimwomba mjomba wa Yasmin aseme na mpwawe, amlani shetani, awaze nyuma na mbele na arudi. Data hii ya tamathali ya semi ya tabaini inaonesha dhamira ya mapenzi ya nje

ya ndoa jinsi yanavyoathiri wapendanao na kufanya baadhi ya wanandoa hao kuathirika kisaikolojia.