• Tidak ada hasil yang ditemukan

4.5 Dhamira Zilizojitokeza Kutoka katika Tamathali za Semi

4.5.1.1 Dhamira ya Uongozi Mbaya

(q) Imani za kidini.

(r) Upendo kwa viumbe hai. (s) Umuhimu wa ndoa. (t) Uasharati.

(u) Umuhimu wa elimu. (v) Ukombozi.

4.5.1.1 Dhamira ya Uongozi Mbaya

Dhamira hii ya uongozi mbaya ni miongoni mwa dhamira zilizoibuliwa na mtafiti kwa kupitia data alizozikusanya za tamathali za semi mbalimbali kutoka katika riwaya ya Kichwamaji na riwaya ya Vuta n’kuvute na kisha kuziorodhesha kwa njia ya majedwali tisa. Uongozi mbaya ni ile hali ya kiongozi au mkubwa wa sehemu yoyote katika taasisi za umma au taasisi binafsi kutumia vibaya madaraka yake juu ya wale anaowaongoza. Data zinazoonesha dhamira ya uongozi mbaya kama zilivyoorodheshwa kutoka katika riwaya ya Kichwamaji.

Jedwali Na. 4.3.1.1 linaoonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashibiha kwa kulinganisha vitu viwili vyenye sifa tofauti kwa kutumia kiunganishi ili kuipamba kazi ya fasihi na kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Ukurasa wa 1: Wazee kwa vijana, wake kwa wanaume. Wote kama wagonjwa wangojeao kumuona daktari. Data hii inaonesha dhamira ya namna baadhi ya viongozi wasiowajali raia wanapokuja ofisini na kuwaacha wakisubiri kwenye bao kwa muda mrefu.

Pia katika ukurasa wa 7 kutoka jedwali hili namba 4.3.2.1 linaonesha data ya tamathali ya semi ya tashihisi kwa kuipa sifa ya kibinadamu kitu kisicho na sifa hio

kwa lengo la kuipamba kazi ya fasihi ambapo ametumia neno zero na kupewa tabia ya kibinadamu ya kucheka: Sababu yenyewe ilikuwa kwamba mwalimu alimwekea zero kubwa yenye macho mawili na meno yakimcheka. Data hii inaonesha dhamira ya baadhi walimu wakiwa kama ni viongozi wa madarsa wakitumia vibaya taaluma yao kwa wanafunzi ambapo hupelekea kurudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa wanafunzi.

Jedwali Na. 4.3.5.1 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tafsida kwa kupunguza ukali wa maneno kwa kutumia neno nilimpa vibao badala ya neno kumpiga vibao na kuibua dhamira ya uongozi mbaya. Ukurasa wa 80: Nilipomkaribia nilimpa vibao viwili vitatu akaanguka chini. Data hii inaonesha dhamira ya baadhi ya kina kaka wanavvyowalea vibaya wadogo zao wakiwa kama viongozi ndani ya familia kwa kutumia nguvu badala ya kuwaelimisha pindi wanapokosea.

Jedwali Na. 4.3.8.1 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya dhihaka kwa lengo la kumuweka mtu katika hali ya duni kupita kiasi. Ukurasa wa 2: Wazee wengine hawana akili hata kidogo! Anaingia humu na fimbo! Anafikiri humu kuna vita. Data hii inaonesha dhamira ya baadhi ya viongozi wasiojali utu wa mtu na hata kuwakemea na kuwakaripia watu wazima wanaotembea kwa mkongojo pindi wanapokuja ofisini mwao.

Data zinazoonesha dhamira ya uongozi mbaya kama zilivyoorodheshwa kutoka katika riwaya ya Vuta n’kuvute.

Jedwali Na. 4.3.1.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashibiha kwa lengo la kufananisha vitu viwili vyenye sifa tofauti kwa kutumia kiunganishi. Katika tamathali hii ya tashibiha mwandishi amelinganisha mvumo wa sauti ya mtu kama mlio wa sauti ya tarumbeta. Ukurasa wa 66: Aligonga mlango na suti nene iliyovuma kama mlio wa tarumbeta ilijibu come in. Hii ni data inayoibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kuonesha baadhi ya viongozi wa taasisi za umma wanavyotumia vibaya uongozi wao kwa kuwatisha watumishi wadogo wadogo.

Jedwali Na. 4.3.2.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tashihisi ilivyotumika na kuibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kukipa uwezo wa kibinadamu kitu kisicho na uwezo huo. Ukurasa wa 135: Juu ya dari yalining’inia mapankaboi mawili na yanapowashwa hulifukuza joto lote… Data hii imetumia neno pankaboi ambalo limepewa uwezo wa kibinadamu wa kufukuza kitu na ilhali halina uwezo huo. Pia data imeibua dhamira ya uongozi mbaya unaofanywa na baadhi ya wakuu wa idara kwa kujipendelea wao peke yao mabo mazuri katika ofisi zao bila ya kuwajali watumishi wengine.

Jedwali Na. 4.3.4.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya mubalagha kwa kuyakuza mambo kuliko vile yalivyo yani kwa kutia chumvi. Ukurasa wa 135: Ilikuwepo meza kubwa ya mzunguko wa yai na meza hio imezungukwa na viti vizuri vyenye mto laini ambayo mtu angeliweza kuikalia hata kutwa bila ya kuchoka. Data hii ya tamathali ya semi ya mubalagha imeibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kuonesha baadhi ya viongozi wa taasisi za

umma wanavyojipendelea wao kwa kujiwekea vifaa bora vya kazi bila ya hata kuwajali watumishi wengine.

Jedwali Na. 4.3.7.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya shitizai / kejeli kwa kutumia maneno yenye kuleta maana kinyume iliyokusudiwa ama maana kinyume na ukweli ulivyo. Ukurasa wa 181: Inspekta Wright amesimama mbele ya mlango wa ile nyumba, akamkaribisha kwa kumkejeli. Karibu bwana kubwa. Data hii ya tamathali ya semi ya shitizai / kejeli imeibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kuonesha namna baadhi ya viongozi wa serikali au taasisi za umma wanavyotumia vibaya madaraka yao kwa kuwadharau na kuwakejeli watu wengine.

Jedwali Na. 4.3.10.2 linaonesha data zilizokusanywa za matumizi ya tamathali ya semi ya tabaini kwa kutumia maneno yanayosisitiza jambo kwa njia ya ukinzani. Ukurasa wa 85: Koplo Matata alitoka kwa haraka na kiasi cha kufumba na kufumbua alirudi na jalada mkononi na kumkabidhi Inspekta Wright. Data hii ya tamathali ya semi ya tabaini imeibua dhamira ya uongozi mbaya kwa kusisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani pale aliposema kiasi cha kufumba na kufumbua alirudi na jalada… data hii inaonesha namna baadhi ya viongozi wanavyotumia vibaya madaraka yao kwa kuwatuma kwa njia isio sahihi watumishi wa umma.