• Tidak ada hasil yang ditemukan

MAFANIKIO 1. Elimu rika

Maeneo yanayolengwa ni maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo, sehemu za kazi na shule za msingi. Kwa upande wa elimu rika katika shule za msingi, semina na mafunzo yameendeshwa kwa vikundi vya walengwa. Mafunzo yaliendelea mwaka huu katika baadhi ya wilaya kwa kuanzisha elimu rika katika baadhi ya shule au kwa kuimarisha elimu rika iliyopo sasa katika shule za msingi, ingawa katika uwezo tofauti. Elimu Rika katika sehemu za kazi iliimarishwa kwa mafunzo ya siku 3 ya waelimishaji rika wote kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya. Pia, makampuni binafsi yaliendesha mafunzo chini ya msaada wa kiufundi wa mkoa na ushauri kutoka kwa waelimishaji wa waelimishaji waliopo katika mkoa.

Shughuli mbalimbali zilizokuwa zinaendelea katika maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo tofauti ziliimarishwa na kuendelezwa. Mradi uliendesha mafunzo kwa ajili ya wilaya za Mbeya Mjini na Vijijini kwa watu 39. Mafunzo yalitanguliwa na mkutano wa uhamasishaji kwa wafanyakazi na wamiliki wa mabaa. Ilifuatiwa na mkutano wa kutambulishana baina ya matabibu kutoka maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo na waelimishaji rika waliopata mafunzo,

2. Utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya uelimishaji

Kwa njia ya moja kwa moja au vinginevyo mradi huu unafikia jamii na unahitaji vifaa mbalimbali vya uelimishaji ili kuendelea kutoa elimu kwa watu. Jedwali la 4 (Ukurasa wa 10) linaorodhesha aina za vifaa vya elimu ya afya zilizotengenezwa na/au kusambazwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vipeperushi, vitabu, kalenda, mabango nk. Matangazo ya redio yaliyotengenezwa na kurushwa hewani hapo awali, yanaendelea kurushwa hewani mwaka huu. Vifaa vya elimu vimekuwa vikitakiwa na kuhitajika sana ndani na nje ya mkoa na vimekubalika katika jamii. 3. Maonyesho ya maigizo na filamu.

Vikundi 5

vilivyosajiliwa vya maigizo vimekuwa vikifanya maonyesho katika maeneo yao lakini vingine kama

KIHUMBE vimekuwa

vikifanya maonyesho hadi nje ya maeneo yao kwa mialiko maalumu. Idadi ya maeneo yaliyoonyesha michezo ya kuigiza ni 275 na yalihudhuriwa na watu 255,123 kutoka katika idadi iliyotegemewa ya watu 305,107.

Maigizo mengine huendeshwa katika maeneo tofauti kwa kutumia vikundi visivyosajiliwa vilivyopo katika kila wilaya. Wilaya

4. Mikutano /Mafunzo/Semina/Warsha

Chini ya kipengele hiki yafuatayo yalitekelezwa:

i) Mafunzo ya siku 5 ya kuendeleza elimu rika katika maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo Mbeya Mjini/Vijijini yaliyoenda sambamba na mkutano wa uhamasishaji kwa wamiliki na wafanyakazi wa mkoa na wanachama wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI ya Kata kutoka maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo;

ii) Kongamano la siku moja la wafanyakazi wa hospitali ya mkoa na familia zao lililofanyika Siku ya Familia duniani,

iii) Mkutano wa UKIMWI wa Arusha 2007;

iv) Uadhimishaji wa siku ya UKIMWI duniani, iliyoadhimishwa kimkoa Kyela; v) Hakuna mafunzo ya kuanzisha elimu rika kwa madereva wa teksi wa mji wa

Mbeya;

vi) Semina za uhamasishaji kwa Timu ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ili kuanzisha elimu rika UKIMWI makazini katika ngazi ya hospitali;

vii) Mkutano wa afya wa mkoa uliofanyika siku tatu kila baada ya miezi mitatu ambapo wanachama wa Timu ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya /Timu ya Afya ya Halmashauri ya Mkoa pamoja na wataalamu walikutana kwa lengo la kuboresha na kuimarisha huduma za afya katika Mkoa wa Mbeya. Huu

viii) Utoaji wa msaada wa kiufundi kwa sekta ya umma na binafsi kwa kupitia mafunzo/mikutano katika eneo la Virusi vya UKIMWI/UKIMWI. Warsha iliandaliwa Dar es Salaam kwa msaada wa Mfuko wa Dunia ili kupata taarifa ya maendeleo.

ix) Mkutano na watu wa vyombo vya habari kwa lengo la kuwapatia habari mpya kuhusu Virusi vya UKIMWI/UKIMWI.

5. Uhamasishaji wa Matumizi ya kondomu

Mkoa wa Mbeya una kondomu za bure na zinazouzwa zinazowafikia watu kupitia njia tofauti. Hii ni ili kuhakikisha kuwa kondomu zinapatikana muda wote ili watu wenye kushindwa kusubiri au kuwa waaminifu wapate matumizi sahihi na hakika ya kondomu. Jumla ya idadi ya kondomu zilizosambazwa ni kondomu 6,005,952.

6. Utafiti

Katika kutekeleza lengo lake la kufuatilia nyendo za janga, mradi umejihusisha na tafiti tofauti kwa miaka. Mara kwa mara, mradi umekuwa ukitoa taarifa za wagonjwa wa UKIMWI kwa Mradi wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na idadi iliyotolewa mwaka huu ya wagonjwa wa UKIMWI ni 1,408. Ukusanyaji wa takwimu unategemewa kuanza Januari, 2007

7. Huduma za Matunzo na Tiba

Huduma hii ilianzishwa Oktoba 2004 katika mkoa. Ujenzi wa uwezo kwa ajili ya wafanyakazi wa afya katika hospitali ya rufaa ya Mbeya uliendelea na vituo vinavyotoa huduma za matunzo na matibabu sasa hivi ni pamoja na hospitali za mkoa na rufaa, hospitali zote za wilaya, hospitali ya misheni ya Igogwe, hospitali ya Kilutheri ya Matema, hospitali na kituo cha Uhai Baptist, hospitali ya Mwambani, hospitali ya Isoko na hospitali ya Chimala. Jumla ya wagonjwa waliohudumiwa ni 13,911; waliopata dawa ya kuongeza kinga ya mwili ni 3,480, na waliotakiwa kupata dawa ya kuongeza kinga ya mwili ni 8,470.

Kupitia uraghibishi na uhamasishaji baadhi ya shughuli zilipata msaada na pesa kutoka Serikali za Mitaa. Shughuli zilizopata msaada wa pesa ni pamoja na usimamizi, elimu rika katika shule za msingi na maeneo yenye kasi kubwa ya maambukizo ya UKIMWI, maigizo na maonyesho ya filamu pamoja na matukio ya kitaifa kama Siku ya Ukimwi Duniani. Juhudi zinaendelea kupata msaada mkubwa zaidi.

10. Uboreshaji wa Usafi wa Vifaa vya Hospitali

Katika kuhakikisha kuwa watu hawapati maambukizo ya VVU kwa kupitia vifaa vya hospitali, vituo vyote vya afya huchemsha vifaa vyake kwa kutumia chombo maalumu cha kuondoa vijidudu vyote vya ugonjwa kwa kuchemsha au kwa kupasha moto. Pia, wafanyakazi wa afya walikuwa wanakumbushwa wakati wote kuhusu uwezekano wa kupata maambukizo wakati wanafanya kazi au uwezekano wa kumwambukiza Virusi vya Ukimwi mgonjwa kutoka kwa mgonjwa mwingine kwa bahati mbaya, hivi karibuni wafanyakazi wote kutoka hospitali ya mkoa ya Mbeya walihudhuria semina ya siku nne iliyohusu jinsi ya kudhibiti maambukizo.

11. Uzuiaji wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama Kwenda Kwa Mtoto

Mkoa uliweza kuongeza huduma hadi kuzifikia wilaya zote na jumla ya idadi ya vituo imefika 29 kutoka vituo 4 vilivyokuwepo kabla. Vyote vinasimamiwa mara kwa mara na wanawake wajawazito wanapata huduma ipasavyo. Jumla ya wanawake wajawazito 960 na watoto wachanga 1104 walipata dawa iitwayo “Nevirapine”. Jumla ya wanawake wajawazito waliopata ushauri nasaha na kupima Virusi vya UKIMWI ni 16,907 kati ya wanawake wajawazito 26,402 waliopata huduma ya awali ya kliniki. Wanawake wajawazito 2,145 waligundulika kuwa na virusi vya UKIMWI.

Waume pia wanazidi kuhusishwa. Jumla ya waume 653 walipima na 135 waligundulika kuwa na Virusi vya UKIMWI.

Huduma ya Uzuiaji wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto iliendelea na jumla ya wateja 2,409 walipimwa. 265 walijiandikisha kwenye idadi ya CD4 na 235 wanapata tiba ya vidonge vya kuongeza kinga ya mwili.

dalili za magonjwa. Mfumo wa kuagiza madawa wa mfumo wa pull umetumiwa mwaka mzima. Lakini bado kuna matatizo katika upokeaji wa bidhaa zilizoagizwa. 13. Ushauri Nasaha na Upimaji wa Hiari na Matunzo ya Nyumbani

Mkoa una vituo vya afya 117 vyenye kutoa huduma ya ushauri nasaha na kupima na jumla ya idadi ya washauri nasaha katika mkoa ni 234. Jumla ya idadi ya wateja walioshauriwa na kupima ni 55,098. Na katika hawa, 12,983 walikuwa na Virusi vya UKIMWI. Matunzo ya nyumbani yanatolewa kwa wateja 8,005. Kwa ujumla kuna idadi inayoongezeka ya watu wanaopata ushauri nasaha na kupima na matunzo ya nyumbani. Jamii nayo inazidi kujihusisha katika kutoa huduma ya matunzo na msaada abayo ni dalili ya kupungua unyanyapaa.

Kuhusiana na ujenzi wa uwezo, watoaji huduma ya matunzo ya nyumbani 80 kutoka katika jamii walipata mafunzo Rungwe na Mbozi kwa msaada wa ufadhili wa Walter Reed.

14. Usalama wa Damu na Maabara

Huduma ya usalama wa damu iliendelezwa na kila kituo cha afya ambapo damu ilipimwa kugundua kama ina Virusi vya UKIMWI. Huduma hii imekuwa ikiongezeka kasi mara kwa mara sambamba na uhamasishaji na uhusishaji wa jamii.

15. Kutembeleana na Matukio

n Nane Nane:- Wakati wa tukio hili Mradi wa kudhibiti UKIMWI Mkoa wa Mbeya (MRACP) waliandaa shughuli tofauti ikiwemo ushauri nasaha na upimaji wa hiari, huduma ya tiba ya magonjwa ya zinaa, uelimishaji, maigizo na maonyesho ya filamu. Jumla ya wateja 1331 walipata huduma za ushauri nasaha na kupima, na 109 waligundulika kuwa na Virusi vya UKIMWI.

MAPENDEKEZO

Dokumen terkait