• Tidak ada hasil yang ditemukan

5.2 Fani ya Tondozi Wakati wa Ukoloni

5.1.2 Utendaji wa Tondozi

5.2.2.1 Fanani na Hadhira

Tondozi wakati wa ukoloni, na kabla ya ukoloni, ilikuwa na waimbaji wa aina mbili. Waimbaji kama kikundi na mwimbaji mmoja. Hiki ni kipindi ambacho jamii iliishi pamoja, kipindi ambacho, hata zana za utendaji kazi zilikuwa ni hafifu sana. Jinsi zote zilishiriki katika uimbaji. Rubanza (1994), Mulokozi (1996), Peek na Kwesi (2004) wanabainisha kwamba tondozi ziliimbwa na wanawake tu. Maelezo yao yanashadidiwa na Ndamugoba (1987) aliyefanya utafiti katika kabila la Wahaya akieleza kuwa, katika jamii hiyo wanawake ndiyo walioimba tondozi na wanaume walighani majigambo. Maelezo hayo yametiwa uyakini na utafiti huu kwasababu, katika jamii tuliyoitafiti, wanaume wanaoimba tondozi ni wengi kuliko wanawake, ingawa wanawake wanaoimba tondozi nao wapo.

Kwa hiyo jinsi zote ziliimba tondozi mpaka baada ya mgawanyo wa kazi ulipoingia. Mgawanyiko huu ulitambulisha kazi za kiume na kazi za kike. Wanawake wengi walihusika kuwasifu waume zao ambao waliweza kushinda vita, kuwinda na kulima

mazao mengi. Haya mara nyingi yalijitokeza baada ya waume zao kufanya vizuri. Wanaume nao waliwasifu wake zao kwa kuzaa watoto wengi na kuweza kuwalea vizuri, wanawake wachapakazi pia walisifiwa.

Jedwali Na. 5.2: Tondozi ya Kumsifu Mke

Na Kinyakyusa Kiswahili

1. Unkasi gwangu kimoghe ugwa bhusungu

Mke wangu mzuri aliyepevuka 2. Umoghela amisi kyeupe dawa Maji ya kunde cheupe dawa

3. Pakilo tala jha nkoloni Usiku anang`aa kama taa ya mkoloni 4. Ukwaka ulwa hela jha nkyunya Anang`aa kama hela ya chunya (dhahabu) 5. Aka ni koko nalimo Hana kovu hata moja

6. Ukwenda ikwinyonga ngati ijhongolo lya nkibhumba

Anatembea anajinyonga nyonga kama jongoo wa kwenye udongo wa mfinyanzi 7. Unkasi gwangu malangalanga Mke wangu msafi asiye na mawaa 8. Unkikulu bho jhu Luti Mwanamke kama Luti ( Luti katika jamii

hii ni mwanamke mwenye bidii ya kufanya kazi)

9. Akamanya ukwifuna Hajui kulinga 10. Pa kujhobha ikusopa limo limo

akamanya ukusipinya mu ndumbula kana Ng`onda

Kuongea kwake ni taratibu, hutoa neno moja moja hajui kuweka mambo moyoni mtoto wa Ng`onda

11. Amakosi matali ulwa twiga Shingo ndefu kama twiga 12. Ingiriri mmakosi ngati majhigha gha

kwa sumbi

Michirizi ya shingoni ni kama mawimbi ya ziwa Nyasa

13. Unkasi gwangu kimoghe ujhu aikulila ifwa jhangu, njobhe bho ngali ukufwa

Mke wangu mzuri atakayelia msiba wangu, niseme kabla sijafa

14. Aikumbyaghisya kumbulo bho mfwile, aikuti ukaghone ilumbu gwangu mwaibagisya

Atanifuta puani nikifa, atasema kwaheri kaka yangu mzuri

15. Kali ukumenye ukufwa , namanga linga tufwile tukunyalisya,

tukonangika

Hivi unajua kufa, kwasababu tukifa tunachefua, tunaharibika, tunachukiza 16. Tukusebhula kundomo ngati mbwa

jhifwilile panjila

Tunaharibika mdomoni utafikiri mbwa aliyefia barabarani

17. Kangi ndi nimwene mwa jhubha ugwa kibhili jho nkasi gwangu kana

Ng`onda, umpimba, umoloki, umpapa abhana, atuti kunsyila ni ngungwe

Tena niko peke yangu kwa mama yangu wa pili ni mke wangu mtoto wa Ng`onda, mzazi, aliyezaa watoto wengi, hatutamzika na kitoto cha ndizi

18. Imbeto syosa bhikuswigha ubhubhumbigwa bwake

Jedwali Na. 5.3:Tondozi ya Kumsifu Mume

Na Kinyakyusa Kiswahili

1. Undume gwangu kighane kyangu, unyambala gwa maka ikisu kyosa

Mume wangu, kipenzi changu, mwanaume mwenye nguvu katika mji wote

2. Ukufwana nsungu kumaso linga gumbwene

Ukimwangalia utafikiri mzungu usoni

3. Unyambala gwa mboto Mwakibete Mwanaume rijali Mwakibete 4. Akamolo imbobo, ikhubhomba

atikukatala

Siyo mvivu wa kazi, anafanya bila kuchoka

5. Ukulima ifyalo ifikafu nkisu iki Analima mashamba magumu katika mji huu

6. Ikubhomba imbombo atikukatala mbibhi

Anafanya kazi hachoki haraka

7. Umbili gwake mololo fijho nalinga ghunketile

Mwili wake ni laini sana hata ukimchunguza

8. Ukulya ifindu ifi kyala afipelile Anakula chakula kilichowekwa na mwenyezi mungu

9. Imyenda gyope gimbaghile Mwakibhete

Hata nguo zinampendeza Mwakibete

10. Kukuti nkikulu ikunyonywa undume gwangu

Kila mwanamke anamtamani mume wangu

11. Aka mwimi linga alinindalama ikusosya

Siyo mbahili akiwa ana hela huwa anatoa

12. Unyambala gwa maka amenye ukuswila abhana

Mwanaume mwenye nguvu anajua kulea watoto

13. Umwenda kimyeka mwaibhagisya Anatembea taratibu anapendeza 14. Akabhumanya ubwite ali nu

lutengano

Hajui ugomvi ni mtu wa amani

15. Kyala akutule kana Mbojha Mungu akusaidie mtoto wa Mboja

16. Aaah kyala akutule Aaah mungu akusaidie

Kwahiyo tunaona katika jamii ya Wanyakyusa, wanawake na wanaume walihusika katika uimbaji wa tondozi. Katika awamu hii, tondozi zililenga mambo halisi yaliyotokea katika jamii. Hata mtu aliposifiwa, alisifiwa kwa sababu alistahiki kupata sifa hizo kutokana na jamii hiyo inaona nini kwa muhusika. Kipindi hiki machifu walisifiwa kwa utendaji wao wa kazi, busara na hekima walizonazo (Finnegan, 1977).

Hadhira ya tondozi ilitegemea sana aina ya tondozi na muktadha husika. kwa mfano wakati wa mazishi, wakati wa sherehe na hata shughuli nyingine za kijamii. Kuna wakati hadhira pia walihusika kuitikia hata wakati mwingine kupiga makofi. Kwa mfano wakati wa tamasha lililoandaliwa na Mheshimiwa Tulia Akson Mwansasu wilayani Rungwe lililohusisha wilaya za Rungwe, Kyela na Halmashauri ya Busokelo.Kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu, mtafiti aligundua kuwa kuna uhusiano mkubwa wa utendaji wa msanii na ushirikishwaji wa hadhira.

Kuna wakati wasanii walipoingia kughani hadhira ikajikuta ikiambiwa piga makofi na ikashiriki kupiga makofi, walipoambiwa kina mama piga vigelegele wakapiga vigelegele na kuna wakati baadhi ya wasanii walipoingia kughani na kuimba hadhira ilikuwa haina ushiriki wa aina yoyote. Hivyo tulichogundua katika utafiti huu ni kuwa, hadhira inaweza kutumiwa na msanii kama atakavyo ilimradi hadhira hiyo inashirikishwa, na pia hutegemea sana vionjo na mbwembwe za msanii katika kuwashirikisha hadhira.