• Tidak ada hasil yang ditemukan

Kwa kuelewa umuhimu wa kutumia mbinu nyingi za kukusanyia data, utafiti huu ulitumia mbinu tano ili kuchunguza maudhui na fani ya tondozi (Cohen na

Lawrence, 2000). Mbinu hizo, uchunguzi shirikishi, kushuhudia, usaili, usomaji wa matini na usikilizaji wa sidii na uangaliaji wa kanda ili kukusanya data. Matumizi ya mbinu hizo, kwa pamoja, yanatokana na ukweli kwamba kila mbinu ina ubora na udhaifu wake.

Kwa hiyo, kwa kuzitumia mbinu hizi pamoja zimetusaidia sana katika kukamilishana kupunguza sana udhaifu wa kutumia mbinu moja. Mbinu ya uchunguzi imetumika katika kuchunguza mabadiliko yaliyojitokeza katika tondozi za awamu tofauti zilizotumiwa katika utafiti huu; mbinu ya kushuhudia/kushiriki imetumika katika kuchunguza utendaji wa tondozi na matukio yanayofanyika katika jamii iliyotafitiwa. Mbinu ya usomaji matini imesaidia kutupa mwanga wa mambo mbalimbali yanayozungumzwa kuhusu tondozi. Mbinu ya usikilizaji na uangaliaji wa sidii na kanda imetusaidia kubaini vipengele mbalimbali vya kifani vinavyotumika katika tondozi. Aidha, matumizi ya mbinu hizo yamesaidia kutathimini mabadiliko katika tondozi, katika awamu tofauti za kihistoria katika maendeleo ya jamii. Maelezo zaidi yametolewa katika vipengele vinavyofuata hapa chini.

3.6.1 Uchunguzi Shirikishi

Hii ni mbinu ya kukusanyia data, ambayo mtafiti hukusudia kufanya uchunguzi wa jambo, hali au kitu na kulichunguza kama linavyotendeka. Mbinu ya uchuguzi shirikishi inahusu ukusanyaji wa data kwa kuchunguza na kumhoji mhusika.Kwa kutumia mbinu hii mtafiti alitembelea na kuhudhuria mikusanyiko zikiwemo sherehe na misiba. Mtafiti alishiriki kuimba na kucheza kwa baadhi ya tondozi. Hata hivyo, katika kuiongezea nguvu mbinu ya uchunguzi shirikishi, mtafiti alifanya mahojiano yasiyo rasmi na washiriki wa mikusanyiko. Mahojiano yasiyo rasmi, hayana kanuni,

juu ya idadi ya maswali au aina ya maswali. Aina ya maswali na idadi yake inaamuliwa na muktadha na hali halisi ya mkusanyiko. Kwa kutumia mbinu hii tumegundua mambo mengi yahusuyo jamii ya Wanyakyusa kwasababu walikuwa wanatenda mambo mengi bila kujua kama wanatafitiwa hivyo walikuwa huru kufanya mambo yao.

Mbinu hii imetusaidia kupata baadhi ya tondozi zinazoimbwa misibani na kwenye mikusanyiko kama vile harusi. Finnegan (1970) anasema tondozi wakati mwingine zilitumika katika sherehe za misiba na harusi. Hivyo kwa kutumia mbinu hii, pia tumebaini kuwa kuna baadhi ya nyimbo zinaimbwa katika miktadha yote ila baadhi ya maneno yanabadilika.

3.6.2 Kushuhudia

Zaidi ya kukusanya data kutoka katika kushiriki, katika utafiti huu pia tulitumia njia ya ushuhudiaji. Ushuhudiaji ni ukusanyaji wa data ambapo mtafiti huchunguza kwa kuangalia watafitiwa moja kwa moja bila kumuuliza mtu mwingine, (Kothari 1990: 96). Mtafiti hulazimika kwenda katika eneo husika na kushuhudia kile anachokitafiti. Hivyo katika utafiti huu tulienda katika maeneo husika ya jamii tuliyokuwa tunaitafiti. Katika maeneo haya tuliona mengi kwa macho yetu wenyewe. Mfano tulihudhuria tamasha kubwa la nyimbo za asili za Kinyakyusa. Tamasha hili lilihusisha wilaya za Kyela na Rungwe, tamasha hili liliandaliwa na mheshimiwa Tulia Akson Mwansasu wilayani Rungwe. Katika tamasha hili tulijionea mengi ambayokwa namna ya kawaida ukimuuliza muhusika angeshindwa kutoa majibu ambayo yangetosheleza kiu ya utafiti wetu. Ushuhudiaji pia umetusaidia kuona matendo halisi yanayofanywa na wasanii. Miongoni mwa wasanii walioshuhudiwa ni

Asamisye kutoka kijiji cha Bujesi, Uswege kutoka Itete, na vikundi kutoka Iponjola na kingine kutoka wilayani Kyela. Katika tamasha hili mtafiti aliwahoji wasanii wa nyimbo za tondozi waliokuwepo, hivyo pia kuna baadhi ya nyimbo tulizotumia katika utafiti huu zilirekodiwa na mtafiti wakati wa tamasha.

Vilevile ushuhudiaji ulifanyika katika mikusanyiko kama vile harusi na misiba, ambapo kwa jamii ya Wanyakyusa huwa na nyimbo za kusifu. Katika mikusanyiko hii pia tulishuhudia yale ambayo Wanyakyusa wanayaamini katika maisha yao ya kila siku. Mbinu hii imatusidia kubaini maudhuiya nyimbo za harusini na misibani kwa kipindi hiki yalivyo ukilinganisha na yale ya awamu zilizotangulia.

3.6.3 Usaili

Mbinu hii imetumika katika maeneo yaliyokuwa yanahitaji ufafanuzi wa kidhana na kiuchambuzi. Usaili ulitumika kuhoji wasanii wa tondozi walioteuliwa kwa ajili ya kukusanya data. Mahojiano yalifanyika kwasababu kuna mambo ya msingi ambayo wahusika walisaidia kutoa taarifa muhimu. Taarifa hizo ni zile ambazo, zinaweza zisijitokeze katika tondozi bali katika uzoefu wa maisha. Kwa mfano kipengele cha utungaji wa tondozi kinazingatia mambo gani? Majibu ya swali kama yalitakiwa kujibiwa na wasanii.Mahojiano mengi yalifanyika kwa wasanii kuhusu sanaa ya tondozi, kwasababu wao wanayajua mengi kuhusu sanaa hii.

Katika kundi hili la wasanii wapo wazee kuanzia miaka sitini na kuendelea, wapo watu wazima wenye umri wa miaka thelathini na tano mpaka hamsini na vijana wenye umri wa miaka kumi na nane mpaka thelathini na nne. Wasanii wazee tuliowahoji walikuwepo tangu kipindi cha ukoloni. Wazee watano walihojiwa wawili

kutoka wilayani Kyela ambao ni Singasipa Mwandulusya na Daimon. Wawili tuliwapata wilayani Rungwe ambao ni Mwabwalwa na Aliko Mwakisambwe ambaye pia ni msanii wa ngoma za asili. Mwingine ni Msanii Mwandwanga ambaye anaishi mpakani mwa Mbeya na Chunya. Tuliona njia hii inafaa sana kwa kundi hili kwasababu yale waliyoyaeleza ndiyo ambayo pia tuliyakuta yamesawiriwa katika tondozi zao. Hivyo basi tulitimiza azma ya data tulizokuwa tunazihitaji.

3.6.4 Usomaji wa Matini

Mbinu hii ni tumeitumia katika utafiti huu; vitabu, makala, tasnifu, matini za kielektroniki zimetumika kwa lengo la kuzifanyia uchambuzi. Mtafiti alipendekeza data hizi kwasababu ndani ya matini hizo ndimo kuna hazina kubwa ya maarifa. Kuna baadhi ya mambo muhimu ambayo hatukuweza kuyapata katika mahojiano, kushuhudia, kushiriki nakadhalika, tuliyapata katika matini andishi. Mbinu hii imetufaa sana kwasababu mpaka sasa kuna baadhi ya tondozi tulizozitumia katika kuchanganua data ni zile zilizorekodiwa miaka ya nyuma na waimbaji wa tondozi hizo. Waimbaji hao wengine walishafariki na wengine wamekuwa wazee na hawawezi kufanya kazi hiyo tena. Hivyo basi mbinu hii imetufaa sana katika utafiti wetu.

3.6.5 Usikilizaji wa Sidii na Uangaliaji wa Kanda

Mbinu hii imetumika kwa minajili ya kusikiliza nyimbo za kusifu, zilizorekodiwa katika kanda. Usikilizaji huo ulihusisha vipindi vya redioni katika vipindi vya burudani na uangaliaji wa sidii za picha. Pia kuna tondozi za awamu zilizopita nazo hatukuweza kuzipata uwandani, tondozi hizo tumezipata katika kanda za kaseti, video, vyombo vya habari na mitandao ya kielektroniki ni mbinu ambayo imetufaa

sana katika utafiti huu kwa sababu siyo rahisi kupata nyimbo nyingi katika matukio halisi yaani kwenye mikusanyiko kwa nyakati hizi kwasababu wasanii walio wengi wanafanya kama sehemu ya ajira. Hivyo tondozi nyingi zilisikilizwa katika redio kwenye kipindi cha Mkoa kwa Mkoa, tulisikiliza kipindi kinachorushwa na TBC taifa redio na televisheni vijulikanavyo kama Utamaduni wetu na Ngoma zetu.

Tondozi zingine tulizozisikiliza ni zile ambazo zimerekodiwa na waimbaji wenyewe, wengine baadhi ya wasanii hao wamefariki lakini tumezipata nyimbo zao katika kanda, wengine wangali hai lakini hawakuweza kuimba tondozi zote bali kwa kutoa kanda zao au sidii ambazo pia ni sehemu mojawapo ya kuwaingizia kipato, mfano nyimbo nyingi za msanii Mwandwanga tumezipata kwenye sidii ingawa msanii huyo yuko hai lakini hali yake ya kiafya si nzuri sana, na umri nao umeenda. Kwahiyo tondozi hizo zimesikilizwa na kufanyiwa upembuzi yakinifu kupitia kanda na sidii. Ili kujua tondozi hizi ni za awamu gani, baadhi ya wasanii kama vile Mwandwanga na Mwandulusya ambao ni wasanii wa muda mrefu, walieleza kuwa tondozi hizo waliziimba katika awamu fulani na hivyo waliweza kutupa picha kuhusu tondozi za kila awamu.