• Tidak ada hasil yang ditemukan

5.2 Fani ya Tondozi Wakati wa Ukoloni

5.1.2 Utendaji wa Tondozi

5.2.2.3 Matumizi ya Lugha

Ushairi ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo au wazo kwa njia ya mkato na kwa namna inayoteka hisia za msomaji au msikilizaji. Maneno ya shairi huteuliwa kimakusudi na kimahususi ili yaweze kujenga taswira maalumu akilini mwa msomaji na msikilizaji. Maneno hayo hupangwa yaweze kutoa mdundo fulani, shairi hilo linapoimbwa, kusemwa au kughaniwa au kusomwa (Njogu na Chimerah, 1999).

Maadam ushairi hutumia lugha, asili yake inaambatana na chanzo cha lugha (Kahigi, 1975). Matumizi ya lugha kama ilivyo katika vipengele vingine, hukua na kupanuka kulingana na maendeleo yaliyofikiwa katika jamii. Lugha na ushairi viliambatana na

harakati za uzalishaji mali ili kuweza kuyatawala mazingira ya awali. Watu wa awali baada ya kuvuka hatua ya uhayawani na kuwa viumbe razini waliishi pamoja (Senkoro, 1988). Kubuniwa kwa lugha ndiko kulikomfanya mtu afaulu katika kuyamudu maisha na kuyakabili mazingira yake. Ushairi wa mwanzo ulikuwa nyimbo za kazi. Nyimbo hizo ziliambatana na ngoma pamoja na sanaa za maonyesho. Watu walivyozoea kukaa pamoja na kutumia zana za kazi ndivyo walivyoendelea kutunga na kuendeleza lugha iliyoiga mazingira. Maneno yaliiga mazingira na sauti za uzalishaji mali. Maneno kama vile kata, piga, lima, vuna na mengineyo yaliiga vitendo vyenyewe (Kahigi, 1975). Kila shughuli ilitungiwa nyimbo zilizoelezea hisi, mawazo na mielekeo yao kijamii. Nyimbo hizo zilikuwa zikitungwa papo kwa papo kulingana na matakwa ya mazingira. Nyimbo hizo zilitungwa kwa mujibu wa haja, huku ikikuza maadili yao.

Lugha iliyotumika katika kipindi cha maendeleo ya awali yaani kabla ya ukolonihaikupiga hatua kubwa kama lugha iliyotumika baada ya ukoloni na wakati huu. Ilikuwa ikifuatia sauti na mapigo ya zana za kazi, hata hivyo ilikidhi haja za watu katika mazingira hayo. Senyamanza (2015: 203) akimnukuu Eaton, (1966) anasema;

….. from the cave to artificial dwelings human beings started to work together. These were productive development for their needs….at work or hunting men communicated by signs combined with noises out of which grew the complexities of spoken languages and the various mens of communication in dispensable to working together.

Kutoka mapangoni mpaka katika makazi ya kujengwa mwanadamu alianza kuishi na kufanya kazi pamoja. Hii ilikuwa ahatua ya maendeleo ya uzalishaji wa mahitaji ya lazima……katika kazi au uwindaji mwanadamu aliwasiliana kwa ishara na kelele ambazo baadaye zilizalisha lugha ya mawasiliano kwaajili ya kazi.

Kama alivyosisitiza Eaton (1966) kuwako kwa jamii kulilazimisha kuwepo kwa mawasiliano. Mawasiliano haya yalikusudiwa kuendeleza kazi. Lugha iliyotumika haikuwa imeendelea kama inayotumika wakati huu. Mwanadamu alivyoendelea kuishi na kupambana na mazingira yake, hisi zake kuhusu sanaa ziliingia na kujikuta katika matumizi ya lugha kisanaa. Lugha za makabila kutokana na kuwa na mwingiliano wa chini zilitumika. Aidha Kiswahili kilikuwa katika hatua za chini na kilikuwa katika ukanda wa pwani.

Hata hivyo kadri muda ulivyosonga mbele na jamii kadri ilivyopiga hatua ya maendeleo, matumizi ya lugha nayo yalipanuka kutoka katika dhima ya mawasiliano na kuwa lugha kwa ajili ya Sanaa. Kutokana na hali hii nyimbo zilizoimbwa na tondozi zikiwemo, zilitumia lugha ya kawaida; lugha ambayo haikuhitaji kuingiza mafumbo mengi na lugha zenye mkanganyiko wa matumizi ya mbinu za kisanii. Kilichobainika sana katika utunzi wa tondozi za awali ni maudhui kuliko fani, tofauti na sasa ambapo fani hutumika zaidi ili kuweza kuipamba kazi ya fasihi. Kwa mfano tondozi hii ya kumsifu chifu Mwakatumbula wa eneo la Masoko ilijulikana kwa jina la Umpandapanda gwa nkisitu.

Kutokana na jamii nyingi kuishi katika maeneo ya aina fulani yenye mila na tamaduni za aina moja zilizowaongoza katika maeneo yao, lugha za makabila zilitumika sana. Hali hii ilitokana na kuwepo kwa mwingiliano wa kitamaduni kutokana na jamii nyingi kutegemea rasilimali za kuendesha maisha yao kutoka katika maeneo yao. Matumizi ya lugha za makabila ndiyo yaliyozoeleka katika maeneo yote kabla ya ujio wa kigeni. Mwingiliano wa kijamii ulianza kujitokeza kwa kasi baada ya ujio wa wakoloni.

Jedwali Na. 5.4:Tondozi ya Kumsifu Chifu wa Masoko

Na Kinyakyusa Kiswahili

1 Mwee bhamyitu, ndagha x 2 Jamani ndugu zangu nashukuru x 2 2 Nisile ne mwininu Nimerudi mimi mwenzenu

3 Mbujhile kukajha, eeenamaah ndagha mwee

Nimerudi nyumbani, eeenamaah nashukuru jamani.

4 Numwe bha tata na bha jubha mughonile

Nanyi kina baba na kina mama hamjambo

5 Ndagha mulindilile Nashukuru kwakulinda mji 6 Ikisu kya Mwakatumbula, malafyale Mji wa Mwakatumbula, chifu 7 Ndagha mwee, ndagha x 4 Nashukuru jamani nashukuru x 4 8 Mwakatumbula ugwa Mmasoko

umwana gwa bhanyafyale

Mwakatumbula wa Masoko aliyetoka ukoo wa kichifu

9 Ugwa maka, untali mu mwanya Mwenye nguvu, mrefu kuliko wote 10 Umwene kisu kya Mpunguti,

Mungaseke, Mumbambo, Mbunya Kisughusughu

Mwenye maeneo ya Mpunguti, Mungaseke, Mbambo, ukoo wa Kisugusugu

11 Ikisu kya bhanyambala bha tata Mji wa mashujaa baba zangu 12 Namanga bhali bhifyusi Tena walikuwa wasafi

13 Ndagha mwee ndagha x 4 Nashukuru jamani, nashukuru x 4 14 Mwakatumbula bha jubha undongosi

gwa Mmasoko

Mwakatumbula kina mama kiongozi wa Masoko

15 Uju ali na abhakikulu bhingi abhanunu Aliyeoa wake wengi wazuri 16 Abhabhombi bha mbombo abholoki

abha bhapapile abhana abhingi mwee abhehe.

Wachapa kazi wazazi waliozaa watoto wengi jamani wake wa machifu 17 Ndagha bha tata na numwe bhajubha Nashukuru kina baba nanyi kina mama 18 Nine linga nali nkabhi Na mimi ningekua tajiri

19 Linga nali ni ndalama eeeh Ningekuwa na hela eeeh 20 Linga nali ni kyuma ne mwininu Ningekuwa na mali jamani

21 Neghagha undenga Ningeoa binti kutoka nyumba ya chifu 22 Uji afumile mu nyumba jha Kalasya Aliyetoka kwenye nyumba ya Kalasya 23 Kalasya umwehe ugwa makeketa

mmakosi

Kalasya mke wa chifu mwenye shingo yenye pingili

24 Neghagha umwana gwa malafyale Ningeoa mtoto wa chifu 25 Umwana gwa Mwakatumbula Mtoto wa Mwakatumbula

26 Ndagha mwe bha tata munyambilile Nashukuru akina baba mmenipokea 27 Kangi mumbele ni kisu Tena mmenipa na eneo

28 Kyala antule Mwakatumbula Mungu amsaidie Mwakatumbula 29 Ammongelesyepo amasiku Amuongezee siku za kuishi 30 Aaaaaaaah Mwakatumbula Aaaaaaaah Mwakatumbula

Wakati huo lugha moja ya mawasiliano ilihitajika sana. Kwa ujumla awamu hii ya kabla ya ukoloni lugha kuu ilikuwa ni lugha ya makabila. Hata baada ya ujio wa wakoloni katika maeneo ya vijijini lugha ya makabila iliendelea kutumika. Lugha hii imeonekana kuendelea kutumika katika maeneo mengi tuliyofanyia utafiti pengine kwasababu tondozi hizi huimbwa kwa kutumia lugha ya makabila. Kana kwamba haitoshi hata zile tondozi zinazotumia lugha ya Kiswahili bado zina mchanganyiko wa lugha ya kikabila, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya maneno ya kikabila huleta maana zaidi yakitumika hivyo bila kutafsiriwa.