5.2 Fani ya Tondozi Wakati wa Ukoloni
5.2.1 Utungaji wa Tondozi
5.2.1.1 Utungaji wa Papo kwa Papo
Milman Parry (1928-1930) na mwanafunzi wake Albert Lord (1981), wameelezea utungaji wa papo kwa papo wa kazi za fasihi simulizi. Parry alianza kujiuliza ni kwa vipi tendi za Homer zilitungwa, je, zilikuwa simulizi au andishi? Parry alifanya uchunguzi katika jamii za Wayugoslavia ingawa uthibitisho wa dai hili ulikuwa haujatolewa. Samwel (2011) anasema Parry alianza kwa kuchunguza mishororo 25 ya mwanzo ya Iliad na Ulisei (odyssey) ili kuona ni kwa kiasi gani tungo hizo mbili ni za kifomula. Matokeo ya utafiti wake yalimshangaza. Aligundua kuwa takribani 70% ya mistari 27,000 katika tendi hizo ilikuwa ya kifomula, kutokana na hilo Parry akahitimisha kwamba tungo hizo ni nudhumu, ni simulizi (si andishi) na, niza kimapokeo.
Miaka michache baadaye baada ya kifo cha Parry miaka ya 1935, Lord aliundeleza utafiti wake na kutoa mchango wenye manufaa. Aliongezea kipengele cha “formulaic expression” kauli ya kifomula, katika nadharia ya fomula simulizi.
Alisema wakati mwingine hutokea watendi kutumia fomula bila kuzibadilisha, wakati mwingine, huweza kubuni na kutumia kauli zenye muundo wa fomula. Alielezea kauli za kifomula kuwa ni mshororo au kipande chenye umbile la fomula.
Mchango mahsusi wa Lord ni kwenye kipengele alichokiita “theme” na baadaye
kipengele hicho kikaitwa topo kwa Kiswahili. kwa maelezo ya Lord, theme ni kipengele kinachorudiwa rudiwa “repeated incidents and descriptive passages”. Tofauti na fomula, topo hailazimiki kufuata urari wa mizani au kujirudiarudia kwa neno, bali huwa na umbo zalishi lenye kubadilika kulingana na mazingira ya usimulizi. Kwa maelezo haya topo hutegemea sana muktadha na utendekaji wa tukio.
Topo humsaidia fanani kuijenga na kuisimulia kazi yake kwa haraka wakati wa utendaji, maana topo tayari zimo katika jadi na akili yake, anachohitaji ni kuziainisha, kuzirekebisha kidogo kulingana na mahitaji.
Wataalamu mbalimbali kama vile Jahn (1961) na (1968), Okpewho (1979) na Mulokozi (2002), walijaribu kuirekebisha kulingana mitazamo yao. Kwa maelezo ya Mulokozi (2002) akizungumzia enanga anasema maelezo ya fomula yaanzie katika ngazi ya maana. Fomula kama inavyotumika katika tendi za enanga ni wazo- kiini radidi la kidhahania na kimapokeo. Hivyo basi fomula hubainishwa kwetu kupitia sura mbalimbali wakati wa uwasilishaji. Maumbo hayo ameyaita alomofu (alloforma-Mulla). Dhana hii ya fomula kwa mujibu wa Mulokozi, ndiyo inayotumika katika utafiti huu inaboresha ufafanuzi wa awali wa akina Lord na Parry. Aidha Mulokozi anapendekeza dhana ya “Theme” iliyopendekezwa na Lord
na Parry, ambayo tayari inatumika kumaanisha dhamira/wazo kuu. Theme katika nadharia ya fomula simulizi iitwe topo. Mulokozi (2002: 132-135) anaifasili topo kwa kusema:
A traditional or Conventional stock incident or description which regularly reformulated in different stories and context by the oral bards to build up Oral narrative poems during performance.
Kitushi au sawiri ya kikaida ya kijadi ambayo husimuliwa na watendi simulizi wakati wa hadithi na miktadha mbalimbali ili kutunga tungo simulizi wakati wa utendaji.
Kwa jumla, msimamo wa Parry, Lord na wafuasi wao ni kwamba fomula na topo hazihusishi kukariri. Hii ina maana kazi za fasihi simulizi, zikiwamo tondozi, hutungwa papo kwa papo wakati wa utendaji wake. Huu ndiyo ukawa msingi unaotumiwa na wanafasihi kuwa tondozi zilikuwa zinatungwa papo kwa papo.
Kuna wakati wasanii hukatokea wakaenda mahali fulani ambapo wanatakiwa kughani au kuimba na muhusika hajawahi kumuona, wanapomuona tu kwa mara ya kwanza wanatunga papo hapo. Katika utafiti huu kati ya wasanii kumi ambao mtafiti alihojiana nao alipowauliza kuhusu utungaji wa tondozi wote kwa nyakati tofauti walijibu kuwa, wao huwa wanatunga kulingana na muktadha husika unawataka wao wafanye nini kwa wakati huo. Utungaji huu ulidhihirishwa wakati mtafiti alipokuwa akihojiana nao, baadhi yao waliweza kutunga tondozi kadhaa zilizomhusu mtafiti kwa nyakati tofauti. Wanachofanya ni kuuliza utokako, ukoo wako na majina yako baada ya hapo mengine yote wanayafanya wao kama wasanii. Mfano msanii Adamson kutoka kijiji cha Selya alimuuliza mtafiti majina yake na asili yake kisha akatunga tondozi hii papo hapo wakati wa mahojiano.
Jedwali Na. 5.1:Tondozi Inayohusu Watoto Yatima
Na Kinyakyusa Kiswahili
1. Mhh, ahaa Rose, itenga, kalapa, Itundu lya ng’ombe
Mmh, ahaa Rose, Itenga, Kalapa, Itundu lya ng’ombe
2. Linga gwisile kukajha kwa Selya, atukuponyagha twe bhana bha bhalondo Rose
Siku ukija nyumbani kwetu Selya tutakusalimia sisi watoto wa maskini Rose
3. Gwe gwa kubhusokelo, kwa Mwakaleli, kunjuni inyanga, kulisu ilyonywa, kuno bhafumile abhimbi bha kwanda Rose
Wewe wa Busokelo, Mwakaleli, kwenye ndege wazuri, majani mororo, kule walikotokea wasomi wa mwanzo Rose
4. Kusekondari jha Mwakaleli, kumaendeleo Rose
Kwenye sekondari ya Mwakaleli kwenye maendeleo Rose
5. Linga twaghanile munjila
gumbonyeghe, ne Mwamulangala, ne Kilembe, ne Mwailamula
Tukikutana njiani uwe unanisalimia, mimi ni Mwamulangala, mimi Kilembe, Mimi Mwailamula
6. Ngundendesyege pakumbonya, kangi ngaja ni lyojo, ngamanya ukujwegha na bhandu
Uwe unanibembeleza unaponisalimia, tena mimi sina hasira, sijui kupigizana kelele na watu
7. Gundendesyeghe bho ulu gwalindendesisye bho kumbapa
Unibembelezage kama vile
Rose Rose 8. Gwakolile indumbula mmabhoko,
undumegho alinkuti pamo unkasi gwangu ikufwa
Ulishika roho mkononi, mumeo alifikiri labda mke wangu atakufa
9. Po apa ngubhule unkasi gwangu jho kalebhela Ngondo, Musyani, Kifulagha, gwa mu Mbhighili
Ngoja nikuambie, mke wangu majina yake ni Kalebela, Ngondo, Musyani, Kifulanga mtoto wa Mbigili
10. Unkasi gwangu umpimba, untitu, imbaghi ngati kifigho kya ikanisa, mwe bhaputi mweee
Mke wangu mfupi mweusi na mwanya kama mlango wa kanisa, jamani
wachungaji mweee 11. Linga nfwile unkasi gwangu ise
akonyole ilisu, ambyagisye kumbulo
Nikija kufa mke wangu atakata jani na kunipangusa puani
12. Papo linga tufwile tukunyalisya, tukufwana mbwa jifwilile pa lami inditu
Kwasababu tukifa tunachefua, tunakuwa utafikiri mbwa aliyefia kwenye lami nyeusi.
13. Aikumbyagisya kumaso aikuti ufwile naloli Mwambapa, ufwile naloli Mwamulangala
Atanifuta usoni atasema, ni kweli umekufa Mwambapa, umekufa kweli Mwamulangala
14. Aikundwala kukajha, kwa Kasenga, kwa Mwaihojo, kwa Kaponela
Atanipeleka nyumbani kwa Kasenga, kwa Mwaihojo, kwa Kaponela
15. Aikukolela, ise ime pakyamba kya malajha, ikundwala unkasi
gwangu umpimba untitu
Atakuja kuita, atakuwa amesimama kwenye mlima Malaya, wakati
ananipeleka mke wangu mfupi mweusi 16. Umama gwangu ugwa kighili,
ugwa misimu, unganga gwa jadi amunkolelege kanunu mutunze ifyombo, isa kughomoka kunyuma nyuma
Mama yangu mwenye kichaa, mwenye nguvu za mizimu, mganga wa jadi, mtamshika vizuri mutunze na vyombo vyake atakuja atembee kwa kurudi nyuma nyuma
17. Bho ikuti findu fiki muti abhinile tukuntwala Kwitete kusipitali
Atakaposema ni kitu gani hicho, muje mumwambie anaumwa tunaenda naye hospitali ya Itete
18. Unkasi gwangu Kalebela Musyani Ngondo gwa Mumbighili
Mke wangu Kalebela Musyani, Ngondo wa Mbigili
19. Aikwima pakyamba kya Malaja bho bikuti fiki bhati
Atasimama kwenye mlima Malaya, watakapomuuliza ni nini tena 20. Aikuti ingongobhe jhangu jifwile
ulufwa, ingongobhe jha Mwaihojo jifwile ulfwa
Atasema jogoo wangu amekufa kideli, jogoo wa Mwaihojo amekufa sababu ya kideli
21. Bhati jifwile ingongobhe ijhi jhali kwa Mwandobo, kwa Kaponela,
Eti imekufa ngo’mbe yangu iliyokuwa kwa Mwandobo, kwa Kaponela, Kwa
kwa Mwakatumbula, Kwa Mwakilili, kwa Mwaisumo
Mwakatumbula, kwa Mwakilili, kwa Mwaisumo
22. Unkasi gwangu bho ikulila ikupikanika x 2
Mke wangu wakati analia kwa uchungu akijipigapiga
23. Kangi abhalumbu bhitu bhikulila bhikupikanika
Tena dada zetu wanalia na kujipiga piga
24. Aghunkolele umwanako, Tupilike Uje umwite binti yako Tupilike 25. Tupilike unka Mwamulenga, unka
Mwakitwange, unka Mwaihojo, unka Mwakasula, unka Mwakilili
Tupilike mke wa Mwamulenga, mke wa Mwaitege, Mwakasula, mke wa
Mwakilili 26. Auti ingongobhe jha Banyandobo
jifwile
Utasema jogoo wa watu wa Ndobo amekufa
27. Kangi jifiwile ulufwa ejhoo Tena imekufa kideli
28. Rose ahaa x 2 chunga sana yatima Rose ahaa x 2 chunga sana yatima
Hivyo katika utafiti huu tumebaini kuwa pale ambapo kulikuwa na utungaji wa papo kwa papo wa tondozi mtunzi aliongozwa na fomula na topo ambayo tayari anazo anachokifanya ni kuongeza yale ambayo kwa wakati huo yamejitokeza kwa muktadha aliopo.