SURA YA KWANZA UTANGULIZI
1.1Utangulizi
Utafiti huu ulihusu athari ya lugha mama (Kisukuma) katika kujifunza lugha ya Kiswahili.
Utafiti huu ulifanyika kwa kuzingatia malengo ya utafiti huu na mapitio yanayohusiana na athari za lugha mama katika kujifunza lugha ya kiswahili. Uliangalia tafisiri za dhana hii ya lugha ya Kisukumana jinsi ilivyoathiri katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Utafiti ulieleza maana juu ya lugha, lugha ya Kiswahili na lugha yaKisukuma.
Massamba na wenzake (2009), Wao wanasema lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano baina yao. Madai ya wataalamu wa isimu na Lugha kuwa, Lugha ni mfumo wa sauti nasibu yanatokana na sababu tatu.
Kwanza kabisa asiliya binadamu anapozaliwa huwa hana lugha bali huikuta katika jamii husika, hivyo basi hukutananayo kwa nasibu tu. Pili upangaji sauti zitumikazo katika lugha na kuziweka katika mfumo wa mawasiliano hutegemea wale wanaoanzisha ile lugha inayohusika maana hakuna mpangilio maalumu wa sauti ambao huwa tayari kwa hiyo wanaoanzisha lugha huzipanga sauti katika utaratibu ambao ni nasibu tu. Na tatu hata pale sauti zinapokuwa zinapangwa kuwa bado maneno yale kuwa sehemu kubwa sana kuwa ni nasibu tu kwa sababu dhana zinazowakilisha na maneno hakuna uhusiano wa moja kwa moja hivyo ni nasibu.
TUKI (2004) wanasema Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambayo hutumiwa na watu wa taifa au kundi fulani kwa ajili ya kuwasiliana baina yao.
TUKI (1990) Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana kuwasiliana.
Nkwera(1979) Ametoa maana ya lugha kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na zilizokubalika na jamii ya watu zitumike katika kuwasiliana.
Robert (1964) maana ya lugha kwake, lugha ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa binadamu wa jamii moja na tamaduni moja. Au Lugha ni mfumo wa mawasiliano ambao hutumia mpangilio wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi kama mofimu, maneno,na sentensi.
Kwa ujumla lugha ni mfumo wa sauti, ishara, nasibu zilizokubaliwa na jamii fulani yenye utamaduni sawa kwa madhumuni ya kuwasiliana, kuelewana na kushirikiana katika upashanaji habari.
Kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili (2004) imejaribu kueleza maana ya lugha ya Kiswahili, inasema Kiswahili ni lugha ya kibantu yenye asili ya mwambao wa Pwani ya Afrika Mashariki yenye lahaja mbalimbali ambayo hutumiwa na watu wengi wa Pwani ya Afrika mashariki na kati.
Mekacha (2011) Lugha ya Kisukuma nilugha moja wapo ya lugha za kibantu zinazopatikana hapa nchini Tanzania, lugha hii huzungumuzwa katika mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, Geita, na Simiyu. Lugha hii ni moja wapo ya lugha za mbali ya Niger- congo kutoka makala ya Williamson na Roger Blench. Heine naNurse (2000) lugha za kibantu zinasemekana kuwa zaidi ya miamoja na wasemaji wa lugha hiyo wanakadiliwa
kuwa asilimia 95 ya watanzania wote. Ngonyani (1994) wazungumzaji wa lugha za mbali yaani kibantu ndiyo wanaokalia maeneo karibu yote hapa nchi ya watanzania, anaendelea kuripoti kuwa utafiti wa pekee wa isimulinganishi uliompa na uliopata kufanywa kuhusu lugha nchini Tanzania ni ule wa Nurse, ambaye kwa kutumia mbinu za kitakwimu ya kulinganisha maumbo na maana za maneno ya lugha mbalimbali za kibantu, alizigawa lugha zote za kibantu katika kanda sita,kulingana na jinsi zinavyofanana. Lugha ya kisukuma aliiweka katika kanda ya kaskazini na mashariki mwa Tanzania ambayo, kanda hii ilijumuisha lugha kama kisukuma, kinyaturu, kinyamwezi na kisumbwa. Wasukuma wanajishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kama vile, kilimo cha mahindi, pamba, mpunga, mtama na alizeti na ufugaji,ufugaji mkuu ni ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Mila, desturi na utamaduni ni kama kuoa na kuolewa, kwa wasukuma, mwanaume anayetaka kuoa, wazazi wake huongea na wazazi wa msichana, wazazi hawa wakishakubaliana, wazazi wa msichana hupanga mahari ambayo kwa asilimia zote ni mifugo kama ng’ombe, mbuzi, na kondoo. Wasukuma pia wanaamini juu ya Mungu wa kweli ambaye ni Mungu muumba mbingu na nchi ambaye ndiye anayewapa uwezo wa kiroho na kimwili katika dini zote yaani ukristo na uislamu.
1.2Usuli wa Utafiti
kila jamii huwa na lugha mama ambayo hutumika katika mawasiliano ya kila siku.
Kutumia lugha mama husaidia sana katika kuleta maendeleo ya Taifa kwa ujumla maana hurahisisha katika kuwasiliana na kuelewana kwa haraka zaidi. Hata hivyo ni vigumu sana kwa jamii kutumia lugha zaidi ya lugha moja katika mawasiliano,ni lazima pawepo na lugha teule inayowaunganisha kwa pamoja watu hao, mfano Tanzania kuna lugha nyingi sana lakini lugha teule inayowaunganisha ni lugha ya kiswahili.
Mhulu (2005) yeyé anasema lugha mama hutumika katika shughuli za mawasiliano ya kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kijamii kwa ujumla. Kwa kawaida watu wanapotumia lugha sawa huwasaidia kuelewana wao kwa wao na kuwawezesha katika kufanikisha mambo yao kiuchumi, kibiashara na kitamaduni katika jamii husika ambavyo ni tofauti na kutumia lugha zaidi ya moja. Matumizi ya lugha zaidi ya moja katika jamii kwa upande mwingine husababisha utata mwingi kwa jamii na kudumaza maendeleo ya jamii kwa ujumla. Mfano mataifa kama France, Japan, na China yameendelea sana kutokana na mchango mkubwa wa matumizi ya lugha mama.
Mekache (2011) yeyé anasema sera ya lugha ni dhana inayohusu mpango wa utekelezaji wa yale yanayohusu lugha ambazo huwa zimechaguliwa ili kutekeleza majukumu mbalimbali katika Taifa au jamii. Yaani será za lugha ni maamuzi juu ya matumizi ya lugha fulani katika jamii fulani. Será ya lugha hulenga kufanya mambo kama haya.
Kwanza kutoa mwongozo kuhusu utaratibu wa matumizi mema ya lugha, pili kutoa mwongozoufaao wa matumizi ya lugha fulani fulani katika jamii, tatu kutoa ushauri kwa watawala kuhusu utumiaji mwema wa lugha katika jamii husika.
Será ya lugha huambatana na kuchukuana na mahitaji ya kisiasa kiuchumi na kijamii ya wakati fulani husika. Kutokana na hali hii será ya lugha haijaribu kueleza mkondo wa kijumla unaokwenda na fikira pamoja na matendo ya wanajamii kupitia mifumo mbalimbali. Hivyo basi kila hatua za maendeleo ya kijamii,kisiasa, kiuchumi na kitamadunizinazoipitia jamii fulani huweza pia kuathiri na kutawala sera ya wakati huo, kwa mfano ikiwa utawala uliopo ni wa kidemokrasia, sera ya lugha kwa wakati huo itahusisha watu wengi wakiwemo wataalamu. Kwa upande mwingine ikiwa utawala ni wa kiimla, será ya lugha itakuwa ya mtu mmoja na utekelezaji wa mpango wa lugha utakuwa ni maagizo au amri.
1.3Tatizo la Utafiti
Athari ya lugha ya kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili ni tatizo kubwa kwa watoto wa kisukuma wanaojifunza lugha ya kiswahili. Wasukuma wengi waliojifunza na wanaojifunza lugha ya kiswahili kuna athari zinazojitokeza katika nyaja kama matamushi, uchanganyaji wa sauti wakati wa kuzungumuza pamoja na kuweka mkazo pasipohitaji.Kutokana na hayo yote kuna umuhimu wa kuchunguza na kubaini chanzo na asili ya adhari hizo. Utafiti huu ulisaidia kubaini athari hizo na jinsi ya kuwasaidia kwa wale wanaojifunza lugha ya kiswahili.
1.4Malengo ya Utafiti
Utafiti huu uligusa malengo mawili.
1.4.1Lengo Kuu
Kuchunguza athari za kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili
1.4.2 Malengo Mahususi
1. Kubainisababu za athari kwawanafunzi kuathirika kwa kisukuma katika kujifunza Kiswahili.
2. Kubaini mbinu za kutumia ili kuwasaidia wananafunzi wanaojifunza lugha ya Kiswahili kama lugha yao ya pili.
1.5 Maswali ya Utafiti
1.Kwa nini wanafunzi wameathiriwa na kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili?
2.Mbinu gani zitumike ili kuwasaidia wanafunzi walioathiriwa na kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili?
1.6Umuhimu wa Utafiti
Lugha ya kisukuma ni muhimu sana katika jamii ya Kisukuma, kwasababu huwasaidia sana katika kuwasiliana wao kwa wao katika shughuli za kiuchumi, kisiasa na kijamii na pia husaidia kuhifadhi utamaduni wa Kisukuma. Umuhimu wa utafiti huu alitarajia kubaini mambo yanayoleta athari kwao katika kujifuza lugha ya Kiswahili kama lugha yao ya pili.
Utafiti huu uliohusu athari za Kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili, utawasaidia wasukuma wenyewe wanaojifunza lugha ya kiswahili, wanazuoni wajishughulishao na lugha vile vile kwa wanafunzi katika vyuo na shule za sekondari katika kujifunza na utafungua milango kwa tafiti nyingine kwa watafiti wengine watakao jihusisha na athari za lugha mama katika kujifunza kiswahili pia utatoa mwanga kwa kwa wataalam kuhusu lugha ya kisukuma na tamaduni zake. Utafiti huu utajaza mapengo yaliyoachwa na wanazuoni na watafiti ili kupata utata uliopo kuhusu athari za kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili. Utafiti huu ulisaidia kupata njia nyingine za kuwasaidia wasukuma wakati wanapojifunza lugha ya kiswahili.
1.7 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu ulijikita katika lugha ya kiswahili na kisukuma, kufafanua na kuchambua athari mbalimbali za kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili na maana ya lugha ya kiswahili na kisukuma kwa ufupi na kivipi kisukuma kimeathiri lugha ya kiswahili na kuzingatia zaidi nadharia ya mawasiliano.
1.8 Kiunzi cha Nadharia
Wamitila (2011:22), anaeleza kwamba nadharia ni mawazo, dhana au maelezo yanayotolewa kuelezea hali fulani, chanzo chake, utendakazi wake na mwingiliano wake wa ndani na nje. Lugha ni muhimu katika jamii za ulimwengu.
Nadharia ni istilahi ya kijumla inayomaanisha miogozo inayomwelekeza msomaji wa kazi ya fasihi ili kuifahamu kazi ya fasihi katika vipengele vyake vyote.
Utafiti huu uliongozwa naNadharia ya mawasiliano, iliyoshika kasi na kupanuka nchini Uingereza katika miaka ya 1970. Paul M, Musau, LeonardM, Chacha (2001) Lengo kuu la nadharia hiini kukuza uwezo wa kuwasiliana, lakini siyo kukuza ujuzi wa miundo au vipengele vya lugha tu. Inakusudiwa kukidhi matakwa ya wale wanaojifunza lugha ya pili katika kuwasiliana. Mawasiliano yanahusu mambo mengi kama vile kusababisha mambo fulani yafanyike, kuboresha mahusiano kati ya watu, na kuonesha hisia za watu na ubunifu wao. Kadharika nadharia hii ilikusudiwa kuimalisha mbinu za ufundishaji ambazo zitasisitiza uhusiano uliopo kati ya miundo ya lugha na mawasiliano, hivyo nadharia hii imemsaidia sana mtafiti kumuongoza na kusimamia misingi na mipaka ya nadharia hii.
Nadharia ya mawasiliano ina mihimili ifuatayo
Maana ya miundo husisitizwa kwani lengo kubwa la nadharia ni mawasiliano. Kwa mjibu wa nadharia hii, madumuni makuu ya lugha ni kuwasiliana, kwani lugha ni mfumo wa kueleza maana.
Vipashio vya lugha siyo vile vya sarufi na kimuundo tu, lakini pia vile vya kimawasiliano.
Matamushi yanayoelekezwa na watu wengi katika mazungumzo ndiyo lengo kuu. Lengo siyo matamshi yanayofanana nay ale ya wazawa wa lugha.
Muktadha hupewa nafasi muhimu katika ufundishaji, kwa mfano maneno mapya au miundo Fulani ya kisarufihuwekwa katika muktadha wa mawasiliano.
Matumizi ya lugha kwa wingi hupendekezwa darasani kwani nadharia hii husisitiza kuwa mtu hujifunza lugha vizuri kwa kuitumia.
Kusoma na kuandika kunaweza kuanza katika siku za mwazo na kuendelea ikiwa ni muhimu.
Nadharia ya mawasiliano ilipendekeza ufundishaji ambao unatumia shughuli zinazoendeleza mawasiliano. Hii ni kwasababu wafuasi wa nadharia hii wanaamini kuwa ujifuzaji wa lugha huendelezwa na vitendo au shughuli zinazoelekeza mawasiliano badala ya ukaririshaji wa miundo. Vitendo kama vile ulinganishaji wa picha, maelezo yanayo husu ramani, mazungumzo ya vikundi, uigizaji, michezo, mijadala na usomaji wa magazeti, vitabu.
1.9Hitimisho
Kulingana na malengo ya utafiti huuulikamilishwa na majibu ya maswali ya utafiti. Utafiti ulifuata mbinu zote zilizobainishwa ili kuhakikisha majibu yanatoa taarifa sahihi ya maswali yaliyoulizwa na kukamilisha malengo ya utafiti ili kuweza kubaini Athari za kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili utangulizi uliwezesha utafiti kuingia Sura iliyofuata kueleza mapitio ya machapisho.
SURA YA PILI
MAPITIO YA MACHAPISHO
2.1 Utangulizi
Utafiti ulipitia mapitio yaliyohusina na athari za lughakatika lugha ya Kiswahili vile vile uliangalia uhusiano wa Kiswahili na lugha za kibantu. Utafiti uliangalia athari za lugha nyingine katika lugha ya Kiswahili pamoja na mbinu zilizotumika katika kuwasaidia watu wale.Yafuatayo yalikuwa mapitio ya utafiti huu najinsi yalivyo msaidia mtafiti katika utafiti wake.
2.2Mapitio ya Machapisho
Rugatiri Mekacha (2011), lugha moja huathiriwa kutokana na muktadha wa matumizi yake. Rugatiri anabaini kuwa lugha ya Kiswahili hutumiwa hasa katika shughuli za kijamii zaidi kama vile ofisini, shuleni, sehemu za kazi, biashara, na sehemu ambazo kuna makabila mengi ndipo Kiswahilihutumika. Watu wanapokuwa nyumbani kwao kwa asilimia kubwa hutumia lugha zao za asili.
Rugatiri anaendelea kusema, matumizi ya lugha katika maeneo mbalimbali, kama maeneo ya nyumbani na miongoni mwa wanafamilia, taratibu za matumizi ya lugha haziamuriwi moja kwa moja na sera za lugha, bali mufumo wa uhusiano wa jamii, kulingana na hali hii inaweza kuwa ni sababu kubwa kwa mtumizi walugha fulani kuathiwa na lugha nyingine.
Mfano yawezekana wasukuma ikawa ni sababu moja wapo ya kuwaathiri wao katika kujifuza lugha ya Kiswahili. watafiti wengi wameripotikwamba kwa jumla na kwa kawaida mawasilianino yanayofanyika nyumbani miongoni mwa wanafamilia wa familia moja,ndugu na marafiki na ndugu wa karibu hufanyika kwa lugha ya kijamii
(Abdulaziz(1972, Brauner na wenzake 1978, Mekacha 1993, Ngonyani 1994,). Hata hivyo ripoti hizo na hasa ya ile ya Msanjira zinaeleza kwamba katika hali hiyo ya jumla kuna tofauti zitokanazo na mahali watu wanapoishi
Tofauti ya matumizi ya lugha ni baina ya mjini na vijijini Msanjila (1999), na kama inavyoelezwa na Mekacha (1993a) anasema hii haitokani na ukaribuau umbali wa kijiografia wa eneo moja kutoka jingine. Hapa anahalisi na kusema kwamba hatimaye lugha huenea kwa mchakato wa mkabala wima. Hii ina maana kwamba lugha huenea kutokana na wasemaji wake kuwa na nguvu za kiuchumi, kijamii na kisiasa kiasi cha kuathiri jamii-lugha nyingine kutumia lugha yao. Hapa tunaona kwamba kwa matumizi ya lugha asilia nyumbani husababisha kuathiri lugha nyingine katika kujifunza. Mfano watoto wa kisukuma hutumia lugha ya kisukuma kwa mda mwigi wakiwa nyumbani pia hata wakiwa shuleni hutumia lugha ya kisukuma badala ya lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili hutumika pale tu wakiwa darasani wanasoma lakini wakitoka hutumia lugha yao ya kisukuma.
Brauner na wenzke (1978), takwimu zinaonyesha kwamba hadi hivi sasa bado asilimia 75 na 80 ya wantanzania wote wanatumia lugha zao katika mawasiliano wakiwa nyumbani kwao. Kutawala kwa matumizi ya lugha hizo katika eneo hilo kunatokana na siyo tu na mahitaji ya kimawasiliano yaani haja ya watu kuwasiliana kwa lugha wanayoifahamu vema zaidi,bali pia ukweli kwamba lugha hizo zimefungamana na utamaduni na maisha ya jamii na ni kigezo mojawapo cha kizitambulisha.
Habwe (2010) wanasema, kwa muda mrefu, elimu imetegemewa kama nguzo ya uhai wa binadamu. Kila mtu na kila nchi imetafuta maarifa na kuzua mbinu mbalimbali za kujiboresha na kuiboresha jamii kupitia kwake. Ufanisi wa shughuli hizi zote umetegemea pakubwa mchango wa lugha.
Lugha imepewa kipaumbele katika mitaala ya shule na vyuo vikuu ulimwenguni. Kwa mfano nchi ya Tanzania na Kenya kiingereza na Kiswahili zinafundishwa kama masomo ya lazima. John Habwe anaendelea ksema kuonyesha umuhimu wa lugha na elimu. Lugha ndiyo nguzo kuu ya elimu kwasababu ndiyo chombo cha mawasiliano kwa binadamu.
Kufaulu shughuli yoyote ya kielimu hutegemea sana lugha.
Rugatiri Mekacha (2011),wao wanaonesha uhusiano wa Kiswahili na lugha zingine za kibantu. Madai kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya kibantu yanatokana na uhusiano uliopo baina ya lugha ya Kiswahili na lugha zingine za kibantu. Wanaisimu maarufu kama Carl mainhoff na Malcom Guthrie wamedhihirisha kuwa lugha ya Kiswahili ina sifa zinazofanana na zile za kibantu. Sifa hizo zimebainishwa kwa kutumia vigezo Fulani vya kiisimu. Vipengele hivyo ni kama
Msamiati wa lugha, kwa uchunguzi wa msamiati wa msingi wa lugha ya Kiswahili na ule wa lugha za kibantu umeonesha kuwa na ufanano, msamiati wa msingi na ule unao husu vitu vilivyo vya kawida na vya asilia katika mazingira,majina ya sehemu za mwili na shughuli za kila siku za kijamii. Mfano katika jedwali hapo chini linaonesha uhusiano wa Kiswahili na lugha nyingine za kibantu.
Kiswahili Kisukuma Gikuyu Lubukusu Zulu
Ulimi Lulimi Rurimi Lulimi ulimi
Cheka Kuseka theka Chekha hleka
Maji Minze maii Kamechi -
Maumbo ya maneno, lugha ya Kiswahili inamaumbo ya maneno yanayofanana ya yale ya za kibantu. Maneno katika lugha hizi hujengwa kwa viambishi, mfano
Kiswahili Zulu Kisukuma Gikuyu
M-tu Mu-ntu Mu-ntu Mu-ndu
U-limi U-li-limi Lu-limi Ru-rimi
Kitu kingine kinachoonesha uhusiano wa lugha ya Kiswahili na lugha zingine za kibantu ni Mfumo wa sauti, sauti za irabu na za konsonanti za lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu zinafanana sana kwa kiasi kikubwa. Vile vile hizi zinafanana katika mpangilio wake wa sauti na muundo wa silabi. Kwanza hakuna maneno yenye silabi funge yaani yanayoishia na konsonanti. Maneno mengi katika lugha hizi huishia na irabu, mfano,(I, KI, KKI, KK1/2II).
Kutoka na maelezo haya yanaonyesha uhusiano wa lugha hizi yaani lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za kibantu.
Kutoka baadhi ya vipengele hapo juu, ni baadhi ya sehemu katika lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu, ndiyo vipengele kwa kiasi kikubwa vinavyoathiri lugha ya Kiswahili mfano kama mfumo wa sauti, mofolojia, semantiki, sintaksia.
Lugha ya Kiswahili na jamii ya Tanzania. Mvung (2010) anasema, wanalugha wamejaribu kueleza lugha ni nini, na kwa ujumla, wengi wao walioeleza lugha husema kuwa ‘lugha ni utaratibu halisi wa matumizi ya viungo vyetu vya sauti ambao kwa fikra huzungumzwa kati ya binadamu hasa katika jamii husika. Kutokana na hali hii, mzungumzaji wa lugha huathiriwa na lugha ambayo huitumia kwa mda mwingi. Mfano, hii inaweza kuwa sababu kwa wazungumzaji wa kisukuma kuathiriwa na lugha yao kwa kuitumia kwa mda mwingi wakiwa nyumbani na wanapokuwa katika jamii inayowazunguka. (J. Hughes). Na E.
Sapair (1949) anasisitiza sehemu ya utamaduni katika lugha akisema, “lugha ni utaratibu halisi kwa kila uelewano halisi katika kuzingatia maana na matumizi ya utamaduni uliopo.
Ikiwa ni kwa njia ya mazungumzo au katika hali iliyo badala ya mazungumzi yaani fikra.
Katika maana zote mbili, twaona kuwa lugha ni muhimu katika kuelewana na kufikiri, na kwamba hakuna lugha yenye tofauti na nyingine. Lugha zote zina uwezo wa kuelezea mambo yote yote yanatokanayo na utamaduni wa watu wanaotumia lugha hiyo. Ikiwa utamaduni utabadilika, lugha pia hubadilika ili kulingana na mahitaji ya utamaduni. Hivyo lugha na utamaduni huambatana.
Lucius (1978) yeye anamini kwamba, kanuni na misingi ya lugha ndizo zinazotawala lugha za walimwengu wote kwa ujumla. Kila lugha kuna kanuni na misingi maalumu inazozihusu lugha Fulani tu; ambayo huifanya lugha hiyo iwe tafauti nalugha zingine.
Misingi na kanuni hizo maalumu inakuwa pia katika lugha yetu ya Kiswahili.
Mfano wataalamu wa kigeni walitumia kanuni na misingi ya lugha zao ili kuelezea sarufi ya Kiswahili. Maelezo mengine licha ya kutokuwa sahili, pia yamekuwa yakipotosha ukweli. Kwa mfano katika kitabu cha sarufi cha Broomfield kuna maelezo yanayosema
“sentensi kamili ni lazima na mtendaji na kitendo chake (subject and predicate). Kauli hiyo imethibitiswa na wazalendo wa isimu ya lugha ya Kiswahili kwamba si ya kweli hata kidogo. Mathalani katika vifungu vifuatavyo. Waswahili kwenye mazungumzo yao husema;
Asante sana Haya twende Mkubwa haya
Nahisi njaa.
Ndiyo!
Njoo hapa Yeye mwongo.
Vifungu hivi vya miundo ya maneno yaweza kuwa ni sentensi; yaani ni taarifa kamili katika lugha ya mazungumzo kwa mjibu wa kanuni na misingi ya matumizi ya kila siku ya lugha yetu ya Kiswahili (uk 1). Lugha huathiriwa kutokana na matumizi ya watu na jinsi anavyoitumia na kwa kiasi gani mtu huyo ameathiriwa na lugha yake ya kila siku. Kama tunavyoona makabila mengi hapa nchini yalivyoathiriwa na lugha zao za kwanza wakiwemo wasukuma, ambapo wakati wa kuzungumza lugha ya Kiswahili hujikuta wameingiza kanuni na misingi ya lugha yao. Hatima yake huathiri pia lugha ya Kiswahili wakati wanapozungumza maana hutumia lafudhi ya kisukuma hii ni kwa sababu lugha ya Kiswahili ina kanuni na misingi yake katika uundaji wa maneno na jinsi ya utamkaji wake vile vile hata lugha ya kisukuma pia inakanuni zake ambazo zinapaswa zifuatwe wakati wa kuzungumza na kuunda maneno.
Lucius anaendelea kusema kwamba Kiswahili kina misingi na kanuni zake mahususi ambazo hukitambulisha kwamba ni lugha maalumu ya kibantu. Misingi na kanuni hizo hazimo katika lugha nyingine za walowezi huku kwetu na hata katika baadhi ya lugha za kibantu (uk 3). Pia anaundelea kusema kuwa, kuna baadhi ya maneno yaliyomo kwenye kamusi la kiswahili la F. Johnson. Lafudhi ya matamushi yake inapotoshwa na athari ya dini za walowezi hao kushindwa kuyatamka sahihi maneno ya Kiswahili. Matharani matamshi ya maneno yafuatayo yana athari hiyo ya lafudhi ya dini za wageni walowezi.
Athari/ kiingereza Lafudhi/ kibantu
Majambo Mambo
Motokaa Motokari/ mtukari
Ngombe/ gombe ng’ombe
Tofauti Tafauti
Vielelezo Vielezo/vielezeo
Mwavuli Mwamvuli/mwemvuli
Basi, mifano hiyo iliyotajwa ni baadhi tu miongoni mwa maneno mengi ambayo lafudhi yake ya kibantu imepotoshwa; hata hivyo tukazoea kuyaona matamshi hayo ni sahihi
Si lugha za kigeni tu ambazo zimeathiri lugha ya Kiswahili, pia hata lugha za kibantu ambazo zinaizunguka lugha ya Kiswahili. Mfano kama lugha ya kisukuma ni lugha mojawapo ambazo zimeathiri lugha ya Kiswahili katika matamshi na lafudhi yake. Kama tunavyoelewa kuwa lugha ya Kiswahili kwa watanzania wengi ni lugha yao ya pili, hivyo wakati wa kuzungumza, hawayatamki maneno ya lugha ya Kiswahili ipaswavyo; hii ni kutokana na athari za lugha mama maana hutumia lafudhi ya lugha yao ambapo hujikuta wanatamka maneno ya tafauti ni inavyotakiwa kutamkwa. Mfano katika maneno haya.
Athari/ kisukuma Lafudhi/ Kiswahili
Nilikwendaga nilienda/ lilikwenda
Zaifu dhaifu
Lafuzi lafudhi
Kulaga Kula
Kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa kila lugha ina misingi na kanuni zake katika utamkaji na uunaji wa maneno mfano katika lugha ya kisukuma sauti {dh} Haipo badala yake hutumia sauti {z}. ni thahili kuwa kila lugha utawaliwa na kanuni zake. Mfano; hata lugha ya Kiswahili ina utaratibu na kanuni zake. Basi, kanuni ya pekee ya lugha ya Kiswahili ni
kuwa na uwezo wa neno kujitosheleza na kujieleza lenyewe bila ya msaada wa maneno mengine. Kujitosheleza kwa neno la Kiswahili ni kutokana na kunyambulika kwake.
Uwezo huo wa kunyambulika hufanyika kwa kuongeza viambishi vya mofimu mwanzoni ama mwishoni mwa shina la neno hilo. Viambisho vya mofimu vinapobadilishwa katika muundo wa neno hilo, basi, dhana ya maana ya neno hilo pia hubadilika na kueleza hisia nyingine. Mifano ifuatayo inaeleza uwezo wa maneno ya viarifa vya Kiswahili kunyumbulika na kubadili pia dhana ya maana ya neno hilo.
Viambishi vya mofimu vya hisia za wakati Kuimba - ngeli ya kiarifa Aimba - tendo latendeka sasa
Anaimba - tendo linalotendeka Aliimba - tendo lililotendeka
Angeimba - tendo lingetendeka kwa sharti fulani Miundo ya maneno mawili, hisia ya neno moja
Mwana –mwali Mwana –hewa Mwana –mume Mwana –sayansi
Mwana –damu Mfua –chuma
Kulingana na mifano hiyo ni baadhi tu ambayo inaonyesha kujitosheleza kwa maneno ya lugha ya Kiswahili na jisi ya vipashio hivyo vinavyobadili maana katika utumizi wake.
Rocha (2011) lugha mama na lugha ya pili, kwa watanzania wengi lugha mama ndiyo lugha ya kwanza kujifunza maana huzaliwa na kuikuta katika jamii yake na lugha ya Kiswahili huwa ni lugha yake ya pili kwa mjibu wa wantanzania wenyewe. Si watanzania wote kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili, wengine ni kama lugha yao mama maana huzaliwa na kuikuta katika mazingira yao. Hali hii imechaniwa sana na kupanuka sana kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili katika nchi yet. Ni wazi kuwa watu wengi wanaozaliwa mijini lugha yao hasa ni Kiswahili hata kama akiwa wazazi wake wanazungumza lugha zao za makabila. Kiasi kikubwa kilichobaki kwa matumizi ya makabila, hasa ni vijijini maana Kiswahili hakitumiki sana kama mijini. Kwa wantanzania wengi wanajifunza kama lugha yao ya pili, lakini hata hivyo lugha ya Kiswahili hutambuluka kama lugha ya taifa katika nchi ya Tanzania. Sababu ni kwamba lugha hii huwaunganisha watanzania wote maana hata shughuli zote za kiserkali hutumia Kiswahili katika mawasiliano yao.
Hivyo lugha mama hubakia kutumika wao kwa wao wanaielewa lugha hiyo kama matumizi ya nyumbani rafiki na ndugu zake tu na vijana wanaoielewa ile lugha. Maana lugha ya Kiswahili imeteuliwa kutumika kwa niaba ya lugha nyingine hapa nchini. Wakati wa kujifunza lugha ya Kiswahili kama lugha lugha yao ya pili huwa tayari walishaathiriwa na lugha zao za kwanza kutokana na kuwa mzungumzaji wa lugha hiyo kwa muda mwingi.
Kotokana na hali hii mzungumzaji huwa mahili kuzungumza lugha yake tafauti na lugha ya Kiswahili. Hali hii husababishwa sana na misingi na kanuni za lugha fulani maana huwa tayari mifumo yote ya utamshi wa maneno huwa umezoea kutamka maneno ya lugha hiyo, lakini mzungunzaji anapoongea lugha ya Kiswahili kama lugha yake ya pili hujikuta anatumia kanuni na kanuni za lugha ile ndiyo maana kunakuwepo utafauti wa kutamka na lafudhi kwa mzungumzaji .
Rocha anaendelea kusema, hata kipidi cha utawala wa mjerumani Kiswahili kilipewa nafasi ya kutumika katika ngazi za chinimfano “akida na wajumbe” kwa ajili ya kutasiri.
Hata baada ya uhuru hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere aliteua lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya taifa baada ya uhuru wa Tanganyika, ambapo hali hiyo ilichangia kwa kisasi kikubwa kwa lugha ya Kiswahili kuenea kwa kasi hapa nchini. Kwa upande wa Tanzania bara Kiswahili kabla ya uhuru kilikuwa hakitumiki sana kama upande wa pwani ya Tanzania maana kwa kiasi kikubwa lugha ya Kiswahili ilikuwa haitumiki sana makabila ndiyo yalikuwa yanatumika sana. Kutokana na uteuzi huo wa lugha ya Kiswahili kutumika katika shughuli zote za kiserkali ilisaidia sana katika kukieneza Kiswahili kwa maeneo ya Tanganyika bara.
Richa ya kufanya hivyo lakini bado kuna athari zinazojitokeza kwa wazunguzaji wa lugha ya Kiswahili maana kwa wengi wao Kiswahili huwa kama lugha yao ya pili kujifunza ambapo kuna kuwepo kwa athari ndogodogo zinazojitokeza kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili ndiyo maana kunakuwepo na utafauti wa utamukaji wa maneno ya Kiswahili na dosari hizo hujitokeza hasa katika matamshi na lafudhi anayotumia mzungumuzaji wa Kiswahili.
Dixon (1992) yeye anamini kuwa, uhusiano wa lugha ni baina ya kati ya jamii husika au wazazi na watoto na dungu katika ukoo. Lugha inaweza kukua au kuanguka au kuathiriwa ni kutokana na kuwepo na matumizi ya lugha nyinginekatika jamii hiyo. Kwa mfano Tannzania tuna lugha nyingi sana za makabila kwa makadilio ni zaidi ya lugha za makabila 300, zinapatikana katika jamii ya watanzania lakini kutokana na ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimechukua nafasi kubwa sana katika jamii ya Tanzania katika mawasiliano ya kiuchumi, kiuchumi na katika mawasiliano ya kila siku. Hususani lugha za makabila matumizi yake kwa kiasi kikubwa imebakia maeneo ya vijijni. Watu wengi wa vijijini
wameathiriwa sana na lugha hizi za makabila katika sehemu husika, hii ni kutokana na matumizi ya lugha hiyo kwa wakati mwingi. Pia anaendelea kusema kuwa, kukua, kubadilika au kufa au kuathiriwa kwa lugha husika, hii huweza kusababisbwa na shughuli ambazo zinatendeka katika eneo hilo. Mfano shughuli za kilimo, biashara na shughuli za kiserkali.
Idarus,(2005) katika Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili chuo kikuu Dar es salaam, wao wamejaribu kueleza makosa mbalimbali yanayofanywa mara kwa mara katika matumizi ya kiswahili. Ambapo utafiti huo ulifanyika jijini Dar es salaam Januari na Oktoba (1979).
Uteuzi wa eneo hilo ni sababu yao ilikuwa ni kwamba, mji wa Dar es salaam katika mji huo kuna watu wanaotoka katika kila mkoa wa Tanzania na nchi za jirani na nyingine wanaotumia lugha ya kiswahili katika shughuli zao zote. Kwa hiyo basi, wao wanasema kuwa athari ya lugha mbalimbali katika lugha ya kiswahili inaonekana. Athari hizo zinachangiwa na vitu vingi kama vyombo vikuu rasmi vya habari vinatumia lugha ya kiswahili na kuathiri mamilioni ya watanzania, viko Dar es salaam (magazeti, radio, na ofisi kuu zote za kiserkali)
Utafiti huo ulifanywa kwa watu wa aina tofauti walio mjini humo mfano wafanyakazi, wafanya biashara, watu ambao wametoka katika jamii tofauti tafauti
Katika utafiti wao walibaini vyanzo mbalimbali ambavyo huathiri lugha ya kiswahili.
Baadhi ya hayo ni;- vipindi mbalimbali vya radio, msimamo wa watu kuhusu lugha maalum, pia wameonesha athari zinazojitokeza kama katika makosa ya kuunda sentensi, msamiati. Makosa haya yanaweza kuwa ni chazo cha kuathiri lugha fulani kikwemo kisukuma.
2.3 Hitimisho
Utafiti huu ulitumia wataalamu katika mapitio yahusuyo athari ya lugha na watalaamu walioongelia lugha kwa ujumla.Mapitio ya machapisho yalielezea jinsi gani lugha
huathiriana pia yalitoa msaada zaidi ya kuelewa maada hii ya athari ya lugha mama (kisukuma) katika kujifunza Kiswahili. Sura hii iliwezesha utafiti kuingia Sura iliyofuata.
SURA YA TATU MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Utafiti ulifafanua na kubainisha mbinu zilizotumika katika utafiti uliohusu athari za lugha ya kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili. Utafiti huu ulifanyika mawandani na maktabani. Mbinu zilizotumika katika utafiti huuziliwezesha kukamilisha kukusanya data za msingi na fuatizi zilizokamilisha malengo na kujibu maswali ya utafiti.
3.2 Mbinu za UkusanyajiData
Ukusanyaji wa data ulifanyika katika mkoa wa Tabora wilayani Igunga. Utafiti ulikusanya data katika Kata ya Igunga mjininavijijini. Ukusanyaji huu wa data ulitumia wiki mbili kuanzia tarehe 01/09/2013 hadi tarehe 14/09/2013.
Utafiti huu ulitumia mbinu ya hojaji na dodoso katika kukusanya data. Utafiti ulitumia mbinu ya dodoso kwa sababu hukusanya data kwa watafitiwa wengi kwa muda mfupi.Mbinu ya hojaji ilitumika kwa walimu ili kupata data sahihi kwa sababu waalimu ni wataalamu wanao uwezo wa kujieleza.Mbinu ya maktabani ilitumikakwa kusoma vitabu na makala zilizohusiana na athari za lugha na jinsi zilivyoathiri lugha ya Kiswahili, utafiti pia ulipendekeza mbinu za kutumia ili kuwasaida watu hao. Mbinu hizi za ukusanyaji wa data zilimsaidia kukusanya taarifa za kutosha katika utafiti.
3.2.1 Hojaji
Baraza la Kiswahili la Zanzibar (2010) hojaji ni karatasi ya maswali ya utafiti kuhusu jambo maalumu.
Utafiti ulitumia mbinu hii kwa watafitiwa.Maswali yaliandaliwa kwa ajili ya kujibiwa na watafitiwa. Mbinu hii iliitumika katika kukusanya data zilizohusiana na utafiti huu, maswali yaliyoandaliwa kwenye karatasi kwa ajili ya kujibiwa na watafitiwa. Uhojaji huu ulitumika kwa wote ambao wanajua kusoma kwajinsia zote yaani wanaume na wanawake.
3.2.2 Dodoso
Utafiti uliandaa dodoso za aina tatu. Aina ya kwanza kwa ajili ya wanafunzi na dodoso aina ya pili kwa ajili ya wazazi na dodoso ya tatu ni kwa ajili ya walimu. Utafiti Uliandaa dodoso zenye maswali ya aina mbili. Aina ya kwanza ni dodoso zenye maswali funge na aina ya pili ni dodoso zenye maswali ya wazi. Utafiti aliuliza maswalikwawatafitiwa kwa mdomo. Njia hii ilitumika kwa wote ambao wanajua kusoma na wasiojua kusoma. Jinsia, umri na kiwango cha elimu kilizingatiwa ili kuleta usawa na uwiano katika kuwauliza watafitiwa maswali hii ilisaidia utafiti kupata taarifa sahihi kuhusiana na mada.
3.2.3 Mbinu ya Maktabani
Utafiti ulitumiambinu ya maktaba katika kukusanya data, kutoka katika vitabu na makala.
Utafiti ulitumia maktaba ya chuo kikuu cha Jordan na katika maktaba ya mkoa wa Morogoro wakati wa kukusanya taarifa zake.
3.3Vyanzo Vya Taarifa
Baraza la Kiswahili la Zanzibar (2010) Data ni mkusanyiko wa taarifa za kiuchunguzi wa kitaalamu unaopelekea usahihi wa jambo. Mtafiti alitumia aina mbili za data yaani data za msingi ambazo alizipata kutoka kwa watafitiwa, na data fuatizi kutoka maktabani ili kukamilisha utafiti.
3.3.1 Data za Msingi
Benard (2012) data za msingi ni zile anazozipata mtafiti moja kwa moja kutoka kwa watafitiwa, utafiti hutumia mbinu kama dodoso, hojaji na mahojiano ya makundi katika kukusanya taarifa (ty).
Utafiti ulitumia data za msingi kwa kiasi kikubwa katika utafiti. Taarifa hizo zilikuswanywa kutoka kwa watafitiwa kuhusiana na athari za Kisukuma katika kujifunza lugha ya kiswahili.Data za msingi ilisaidia kukusanya na kupata taarifa sahihi kuhusiana na mada, kama tunavyoelewa kuwa taarifa hizi hupatikana mpaka mtafiti awatembelee watafitiwa ili aweze kupata taarifa juu ya kile alichokusudia kutafiti. Hata hivyo mtafiti aliwatembelea watafitiwa na kuweza kukusanya taarifa zake zinzohusana na maada yake.
3.3.2 Data Fuatizi
Benard (2012) anasema, data fuatizi ni taarifa ambazo tayari zilishakusanywa na watu wengine (ty). Taarifa hizo utafiti ulizitumia katika utafiti, ambapo data hizo zilipata katika makala, vitabu na magezeti hasa zile ambazo zilizohusiana na athari za lugha mama katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Hivy wakati wa utafiti, ulijaribu kusoma na kuchambua kazi za waandishi hasa zile ambazo ziliendana na maada ya utafiti. Kabla ya kufanya utafiti, ulipitia vitabu na majarida ili kuona watafiti walivyotatua na kutoa maoni juu ya yale na mbinu gani zilitumika juu ya lugha ya Kiswahili.
3.4 Sampuli na njia za Usampulishaji
Taasisi ya uchunguzi waKiswahili Dar es salaam (2004) Sampuli ni kitu kimoja kati ya vingi vya aina ile ile kinachukuliwa kama mfano mzuri wa vitu hivyo.
Sampuli ni kitu kimoja kinachochaguliwa katika vitu vingi kwa ajili ya kuviwakilisha vile vingi.
Usampulishaji ni kile kitendo cha kuchagua kitu kimoja kati ya vingi vya aina ile ile kinachukuliwa kama mfano mzuri wa vitu hivyo kwa kuviwakilisha.
Sampuli ni sehemu ya idadi maalumu ya watu ambayo mtafiti ataitumia katika ukusanyaji wa taarifa zitakazomsaidia kufikia malengo yake ya utafiti. Usampulishaji utatumika
katika kukusanya taarifa ambapo kila kipengele kitakachofaa kwa kutoa taarifa kuhusu athari za lugha ya kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili kitapewa nafasi ya kutumika kama sampuli na kuambatanishwa ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa. Kila nukuu itakayotumika kama sampuli itapewa msimbo ili kuepuka uchanganyaji wa taarifa zitakazokusanywa na mtafiti.
Sampuli nasibu, sampuli nasibu tabashi, na sampuli kusudiozitatumika kwani ndiyo njia zinazofaa na huru ambazo zitampa mtafiti uhuru wa kuchagua nukuu itakayofaa kutumika kama taarifa na kuchambuliwa ili kukidhi malengo na majibu ya maswali ya mtafiti.
3.5 Mbinu ya Uchambuzi Data
Data zitafafanuliwa kwa mkabala wa kiidadi au takwimu pia atatumia njia ya maelezo katika kuzichambua na kuzibainisha data. Taarifa zitapangwa kulingana na malengo ya maswali ya mtafiti, kwa sababu mtafiti atataka uchanganuzi wa data hizo uendane na malengo ya utafiti sambamba na kujibu maswali ya utafiti. Data zote yaani data fuatizi zitanukuliwa pale itakapobidi ili kuthibitisha na kushadadia data za msingi.
Nadharia ya mawasiliano, itakua ndio mwongozo mzuri kwakua ndio utakaompa mtafiti uwezo wa kumudu mada hii na kwenda mbele katika kuifafanua. Nadharia ya mawasiliano itasaidia utafiti katika kuchanganua athari za lugha ya Kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili.
3.6 Vifaa katika Ukusanyaji Data
Vifaa vilivyotumika katika kukusanya data ni pamoja na shajara, kalamu na penseli kwa ajili ya kunukuu data za msingi, data fuatizi na vipengele muhimu kutoka katika maandiko vitakavyohusu mada ya utafiti huu. Pia mwandishi alitumia kompyuta na kinyonyi kwa
ajili ya uchapaji na utunzaji wa kumbukumbu za utafiti. Utafiti wa mawandani, pia mtafiti alitumia tepu rekoda, picha pale inapobidi ili kunasa maneno baadhi ya watafitiwa.
Vifuatavyo ni vifaa vilivyotumika katika utafiti huu na matumizi yake.
1 Rimu 1 Kuandaa pendekezo
Kuandika ripoti Madodoso
2 Kalamu 5 Kuandaa pendekezo
Kuandikia ripoti Kurekodi data
Shughuli nyinginezo za Mtafiti
3 Penseli 5 Kuchorea majedwali katika ripoti ya Utafiti 4 Kinasa sauti Kuirekodia matamshi ya watafitiwa
5 Shajara Kuandikia kumbukumbu za Mtafiti
6 kinyoyi Kuhifadhi data za awali pamoja na data za kuperuzi 7 marejeo Yalitumika kwa ajili ya kumpatia mtafiti maarifa na pia
kujua ni sehemu gani haijatafitiwa na ni kiasi gani mada yake imetafitiwa
8 Mkoba Kubeba vifaa na zana za utafiti
9 Kikokotoa Kimetumika katika uchanganuzi wa data
10 Dodoso Kukusanyia data
11 Kitanakilishi mpakato
Kwa ajili ya kuchapa kazi
3.7Eneo la Utafiti
Ngure, (2011:198) aneleza kwamba inabidi kuamua ni wapi utakusanya data unayohitaji?
Mjini au kijijini, karibu ama mbali, wazazi wako ama mwalimu watasaidia kutambua msimulizi afaaye.Mtu huyu huenda atapatikna mjini au kijijini.Apatikanapo si hoja, bora awe fanani wakutoa habari ya kutegemewa. Huenda mwalimu wako akapendekeza uikusanye data yako katika eneo lililo karibu na shule yenu, ama unapokwenda likizo.
Jamii inayozungumzia lugha unayoielewa. Mtafiti atafanya utafiti wake mawandani na maktabani.
3.7.1 Uwandani
Kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili (2004) mawanda ni eneo ambalo mtu au akili inaweza kutalii.
Utafiti huu utafanyika katika Mkoa wa Tabora katika Wilaya ya Igunga. Wilaya ya Igunga ni miongoni kati ya Wilaya za Mkoa wa Tabora Nchini Tanzania. Wilaya ya Igunga inapakana naWilaya ya Nzega upande wa magharibi na Wilaya ya Iramba upande wa mashariki.
Mtafiti alienda kuwatembelea watafitiwa kwa ajili ya mahojiano nao kuhusu baadhi ya vipengele vinavyohitajika kufafanuliwa na watafitiwa ili kusaidia katika utafiti.
3.7.2 Maktabani
Kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili (2004) maktaba ni chumba au nyumba mnamohifadhiwa vitabu ambamo watu huruhusiwa kuvisoma au kuviazima kwa muda.
Maktaba ni eneo jingine ambalo utafiti ulikusanya data kutoka katika vitabu na makala.
Utafiti huu ulifanyika katika maktaba ya chuo kikuu cha Jordan na katika maktaba ya mkoa wa Morogoro. Eneo hili ililiupa utafiti uwezo wakupata mapitio ya kutosha.
3.8 Hitimisho.
Ushilikiano wa utafiti na watafitiwa ilisaidia kukusanya taarifa zilizokusudiwa na kusaidia katika utafiti na kufanikisha kubaini athari za lugha ya Kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili.
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NAUCHAMBUZI DATA
4.1 Utangulizi
Sura hii ilihusisha taarifa zilizokusanywa wakati wa utafiti huu. Sehemu hii ilihusisha uwasilishaji wa data, na uchambuzi wa data. Taarifa hizi zilihusisha makundi matatu,
Makundi hayo ni walimu, wanafunzipamoja na wazazi. Utafiti ulifanikiwa kwa kiasi chake wakati wa kukusanya data zilizohusiana na mada ya utafiti kwa kupitia Jumla ya idadi ya watafitiwa 91, katika idadi hii, Walimu walikuwa 12 wanafunzi walikuwa 46 na wazazi walikuwa 33.
4.2 Athari ya Lugha ya Kisukuma Katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili
Lugha mama ina athari nyingi wakati wa kujifunza lugha yingine. Mtu anayejifunza lugha, hukumbana na vikwazo na changamoto nyingi zinazoweza kumuzuia wakati wa kujifunza na kuwasiliana. Mawasiliano yanapokesekana katika upande moja basi huashira kuna mapungufu katika mawasiliano kama data zifuatazo zilivyochanganuliwa.
4.2.1Kutomuelewa Mwalimu Wakati Anafundisha
Mawasiliano ni nyanja mhimu kwawatu katika kuwasiliana ndani ya jamii, Chacha (2001) anaeleza kuwa lengo kuu la nadharia ya mawasiliano ni kukuza uwezo wa kuwasiliana.
Hivyo athari ya lugha ya kisukuma hupelekea kukwamisha lengo la mawasiliano. Chanzo cha data hii ni kutoka kwa watahiniwa wanafunzi na walimu waliojibu hojaji iliyohusu athari zipi zinazojitokeza kwa wanafunzi wa kisukuma wanapojifunza lugha ya Kiswahili.
Idadi ya walimu na wanafunzi ilikuwa 56 na kati ya hao waliojibu ni 34 ambayo ni sawa na 62%.
Jedwali
Idadi ya watafitiwa walioshiriki wasioshiriki
56 34 22
Utafiti ulibaini kuwa mwalimu anaposhindwa kupokea au kufikisaha ujumbe uliokusudiwa kwa wanafunzi wake hii husababisha kutoelewana baina ya mwalimu na mwanafunzi wakati wa ujifunzaji, hii hutokana na athari alizonazo mwalimu au
mwanafunzi mwenyewe. Wasukuma wengi huwa wameathiriwa na lugha yao kutokana na matumizi ya lugha hiyo kwa muda mrefu.
Rocha (2011) anaeleza kuwa wabantu wengi wameathiriwa na lugha mama, hii ni kutokana na matumizi ya lugha mama.
4.2.2Athari Katika Matamshi
Data hii ni kutoka kwa watahiniwa wanafunzi na walimu waliojibu hojaji iliyohusu athari zipi zinazojitokeza kwa wanafunzi wa kisukuma wanapojifunza lugha ya Kiswahili.
Jedwali
Idadi ya watafitiwa waliosema Ambao hawakusema
56 40 16
Takwimu hii ilionesha wazi kuwa matamushi ni athari mojawapo inayokwamisha mawasiliano baina ya wale wanaopashana habari maana matamshi ni msingi mkubwa wa mawasiliano, mtu anaposhindwa kutamka vema huweza kuathiri mawasiliano baina ya watu, muzungumzaji anaposhindwa kutamka maneno inavyotakiwa hukwamisha mawasiliano kutopokelewa kwa msikilizaji. Leonard (2001) anahusisha umhimu wa mawasiliano ni kukuza uwezo wa kuwasiliana, lakinisiyo kukuza ujuzi wa miundo au vipengele vya lugha tu, hivyo matamshi ni msingi muhimu sana katika mawasiliano, hii ina maana kuwa unapojifunza lugha pia matamushi ya sauti lazima ujifunze ili katika mawasiliano pasiwepo na kutoelewana pande mbili. Hii ni mifano kutoka kwa watafitiwa jinsi athiri ya kisukuma katika Kutamka maneno ya Kiswahili
Kisukuma Kiswahili Fasaha
Baazi Baadhi
Ninazani Ninadhani
Azari Atheri
Karamu Kalamu
Matamushi ni utaratibu utumikao katika utoaji wa maneno ya binadamu. Neno matamushi kwa watu wengi walilihusisha na maneno mabaya, lakini katika lugha huwa na maana ya utoaji wa maneno husika, ambavyo kama Nkwera (1979) anaeleza kuwa muhimili wa mawasiliano mazuri ni utoaji wa matamushi yanayoeleweka kwa msikilizaji.Yule (2010) anaendelelea kusema kuwa matamushi ni utamkaji wa sauti za binadamu kwa kuzingatia mkutadha wa mazungumuzo. Lucius (1978) yeye anamini kwamba, kanuni na misingi ya lugha ndizo zinazotawala lugha za walimwengu wote kwa ujumla. Kila lugha kuna kanuni na misingi maalumu inazozihusu lugha fulani tu; ambayo huifanya lugha hiyo iwe tafauti nalugha zingine. Misingi na kanuni hizo maalumu inakuwa pia katika lugha yetu ya Kiswahili.
4.2.3Kuongeza Viambishi Visivyohitajika
Mawasiliano husababisha mambo Fulani kufanyika, Paul (2001) anasema dhamira ya mawasiliano yanahusu mambo mengi kama vile kusababisha mambo Fulani yafanyike ili kukidhi matakwa ya mawasiliano baina ya wazungumzaji mfano kutumia mbinu mbadala katika kuwasiliana, mbinu za ufundishaji. Wazungumzaji wa lugha ya kiswahili walioathiriwa wasukuma huongeza viambishi mahali pasipohusika wakati wa kuzungumza lugha ya Kiswahili lengo lao ni kukuthi mazungumzo ya wakati huo. Chanzo data hii nikutoka kwa watafitiwa walimu waliojibu dodoso iliyouliza athari zipi zinazojitokeza wakatiwa kujifunza kiswahili. Hii ni baadhi ya mifano iliyotolewa kutoka kwa watafitiwa.
Utafiti huu ulibaini kuwa wasukuma wengi huogeza vitamkwa visivyo vya lazima katika maneno ya lugha ya Kiswahili kama mifano ya badhii ya maneno yaliyooneshwa na watafitiwa katika utafiti huu.
Maneno ya Kiswahili Vitamkwa vinavyoongezwa na wazungumzaji wa Kiswahili.
Kucheza Kucheza –ga
Lima Lima –ga
Kimbia Kimbia –ga
Nuna Nuna –ga
Kunywa Kunywa –ga
Pata Pata –ga
Mzungumzaji wa Kiswahili fasaha anaposikia utamkaji wa maneno ya Kiswahili kwa namna hii, hugundua moja kwa moja kuwa, anaye zungumza si mumahili katika lugha ya Kiswahili. Ni rahisi sana kwa anayejua kutambua na kubashili kuwa mzungumzaji huyu ni mtu aliyeathiriwa na lugha ya kisukuma. Mtaalamu wa kiswahili hugundua kwasababu, huwa tayari anajua sauti za lugha ya kiswahili zinatamkwaje na mahali pakutamkia.
Utofauti hujitokezapale mzungumzaji anapotamka sauti za Kiswahili maana hutumia matamshi na lafudhi ya lugha ya kisukuma. Mzungumzaji wa lugha ya kisukuma hutumia nguvu sana wakati wa kutamka maneno hivyo hivyo wakati wa kuzungumza lugha ya Kiswahili hutumia nguvu ile ile, ndiyo maana wanaongea maneno kwa kuweka mkazo hata pasipohitajika. Utofauti huu huleta mabadiliko katika matamshi ya lugha ya Kiswahili kutokana na athari kubwa ya lugha ya Kisuma kwa mzungumzaji. Mtu anayeweza kutambua Utofauti huu ni lazima awe anaifahamu lugha ya Kiswahili kifasaha, Kihore(2009) alieleza kuwa utaratibu wa mpangilio wa viambishi huhusu viambishi hupangwa katika mfuatano unaotupatia silabi zinazokubalika katika lugha kama mifano hapa chini;
Anapika a-na-pik-a
a- Ikiwakilisha nafsi ya tatu umoja -na- ikiwakilisha njeo ya wakati uliopo
-pik- ikiwakilisha mzizi wa neno
-a- ikiwakilisha kiambishi tamati
Mifano hii kila kiambishi katika neno kinamaana kulingana na mkutadha wa matumizi yake, mtaalamu Idarus(2005) anaonyesha athari zinazojitokeza katika lugha ya kiswahili baada ya mtu kuathiriwa na mambo kadhaa wa kadhaa. Idarus ametaja athari hizo ni kama;
kuongeza vitamkwa maneno, sauti pasipohitajika, msamiati wa lugha, makosa ya muundo wa sentensi, makosa katika matamushi. Hii ni wazi kuwa lugha ya kisuma imeathiri katika lugha ya kiswahili.utafiti huu ulionyesha kuwa, walioathiriwa na lugah ya kisukuma wengi wao ni kutoka vijijini. Mfano katika wilaya ya Igunga ni maeneo kama Mwanzugi, Isakamaliwa, Mwashoma, Ipumbulya, Makomero. Mambo mengi sana walibaini watafitiwa kuhusu kuathiriwa kwao.
4.2.4 Msamiati
Matumizi ya lugha zaidi ya moja katika jamii husababisha mwingiliano katika msamiati wa lugha katika jamii husika. Chanzo data ni kutoka kwa watafitiwa wanafunzi na walimu waliojibu dodoso iliyohoji kuwa athari zinazojitokeza katika lugha ya kisukuma na kiswahili.
Jedwali
Idadi ya watafitiwa ndiyo hapana
56 40 16
Msamiati ni isitali iliyomuhimu sana katika kuwasiliana, mzungumzaji anatakiwa awe makini katika uteuzi wa msamiati unaoendana na muktadha wa mazungumzo, uteuzi wa msamiati kwa kuzingatia utumizi wake huboresha mawasiliano baina ya wazungumzaji, kama nadharia ya mawasiliano ilivyoelezwa na mwasisi, Musau (2001) kuwa mawasiliano huboresha mahusiano kati ya watu. Hii inaweza kuboreshwa endapo matumizi ya msamiati
yatazingatiwa wakati wa mazungumzo.Maelezo haya pia yanasawili mtazamo wa Rugatiri (2011), anaeleza kuwa msamiati ni nyanja muhimu katika kuwasiliana, hii ina maana kuwa msamiati ndio unaonogesha mawasiliano.
4.3Sababu Zinazochangia Kuwaathiri Wasukuma Wakati wa Kujifunza Lugha ya Kiswahili
4.3.1Lugha Mama
Chanzo cha data hii ni watahiniwa wanafunzi waliojibu hojaji iliyouliza sababu zinazochangia kuwaathiri wasukama katika kujifunza Kiswahili. Utafiti huu ulionesha kuwa wanafunzi wawapo Shule wanatumia lugha ya Kisukuma zaidi katika kuwasiliana wao kwa wao kuliko lugha ya Kiswahili hii inadhihiriswa na taarifa kutoka kwa watafitiwa(wanafunzi), kama jedwali linavyosawili.
Jedwali
Idadi ya wanafunzi Kiswahili Kisukuma
46 17 29
Matokeo yalikuwa 36.95% ya watafitiwa ilionesha wanatumia lugha ya Kiswahili na 63.04% ya watafitiwa walijibu Kisukuma kinatumika katika mawasiliano Shuleni na kiswahili hutumika tu hasa wakiwa darasani. Nadharia ya mawasiliano kama ilivyoasesiwa na Paul (2001), lengo kuu ni kukuza uwezo wa kuwasiliana na kukidhi matakwa ya wale wanajifunza lugha ya pili katika kuwasiliana. Wanafunzi wawapo darasani hujifunza lugha ya kiswahili ili kuweza kuwasiliana na Watanzania na siyo kwa kabila la wasukuma pekee.
Mawazo ya Mbunda (1996) alionesha katika kujifunza Kiswahili ambayo ni lugha ya pili kwa watanzania wengi, wanafunzi wa makabila wanashindwa kumudu Kiswahili kutokana na athari ya lugha mama. Vile vile Tuntufye (1972) naye anaendelea kusema kwamba
makabila mengine hushindwa kutamka maneno ya Kiswahili kutokana na athari ya lugha ya kwanza.
Wanafunzi wawapo nyumbani wanatumia lugha ya Kisukuma wanapowasilana nawazazi.
Chanzo cha data hii ni watafitiwa wanafunzi waliojibu hojaji iliyouliza wawapo nyumbani hutumia lugha ipi katika kuwasiliana na wazazi wao
Jedwali
Idadi ya wanafunzi kiswahili kisukuma
46 16 30
Wanafunzi 30 ambao ni sawa na 65% walijibu kwamba, lugha ya kisukuma ndiyo inatumika katika mawasiliano ya nyumbani. Wanafunzi 16 ambao ni sawa na 35%
walisema Kiswahili kinatumika katika mawasiliano ya nyumbani.Maelezo haya yanashadadiwa na nadharia ya mawasiliano Shanon –weaver kuwa lengo lake pia ni kuboresha mahusiano ya watu na mawasiliano huweza kuathiriwa na muktadha ya matumizi, kama lugha ya Kisukuma inavyokuza uhusiano wao na kuathiri kiswahili.Mekacha (2011), anasema lugha moja huathiriwa kutokana na muktadha wa matumizi yake. Lugha ya Kiswahili hutumiwa hasa katika shughuli za kijamii zaidi kama vile ofisini, shuleni, sehemu za kazi, biashara, na sehemu ambazo kuna makabila mengi ndipo Kiswahili hutumika ili kuwakutanisha. Watu wanapokuwa nyumbani kwao kwa asilimia kubwa hutumia lugha zao za asili. Dixon (1992) yeye anamini kuwa, uhusiano wa lugha ni baina ya kati ya jamii husika au wazazi na watoto na ndugu katika ukoo.
4.3.2Matumizi ya Lugha Zaidi ya Moja Katika Jamii
chanzo data ni kutoka kwa watafitiwa walimu, wazazi na wanafunzi waliojibu hojaji iliyouliza unapotumia lugha zaidi ya moja, mfano lugha ya kisukuma na lugha ya Kiswahiliau kiswhili na kiigereza, kuna athari zinazojitokeza.
Jedwali
Idadi ya watafitiwa ndiyo hapana
91 75 16
Idadi ya watafitiwa 75 ambayo ni sawa na 82% walisema ndiyo, sababu kuu ni kwamba lugha ya kwanza ambayo mtoto hujifunza kwa mara ya kwanza, hujenga mizizi na msingi katika nyanja zote za mfumo wa sauti. Anapoanza kujifunza lugha nyingine, huwepo na athari ambazo hujitokeza katika ujifuzaji wa lugha nyingine. Leonard (2001), Nadharia ya mawasiliano kama wasisi walivyosema kuwa lengo kuu ni kukuza uwezo wa kuwasiliana.Kuwa na lugha zaidi ya lugha moja husababisha lugha moja kuathiriwa kama kiswahili kilivyoathiriwa na lugha ya Kisukuma. Mekacha (2011), anasema lugha moja huathiriwa kutokana na muktadha wa matumizi yake. Lugha ya Kiswahili hutumiwa hasa katika shughuli za kijamii zaidi kama vile ofisini, shuleni, sehemu za kazi, biashara, na sehemu ambazo kuna makabila mengi ndipo Kiswahili hutumika ili kuwakutanish
4.3.3Mazingira
Chanzo data hii ni watafitiwa walimu waliojibu dodoso iliyohusu mazingira yanaweza kuwa ni sababu moja wapo kuwaathiri wasukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili
Idadi ya walimu ndiyo hapana
12 12 0
Utafiti huu ulionyesha kuwa mazingira ni mojawapo ya chanzo cha kuwaathiri, nadharia ya mawasiliano lengo inakusudiwa kukidhi matakwa ya wale wanaojifunza lugha ya pili katika kuwasiliana kama, Poul (2001), anasema muktadha hupewa nafasi muhimu katika
ufundishaji, hivyo mwanafunzi anapojifunza lugha fulani, mazingira ni muhumu kuangaliwa. Mawazo haya yanaelezwa pia na Mekacha (2011), anasema lugha moja huathiriwa kutokana na muktadha wa matumizi yake, mojawapo ya athari inayochangia ni mazingira yanajumuisha nyumbani pamoja na jamii yake inayowazunguka. Idarus (2005) katika Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili chuo kikuu Dar es salaam, yeye pia anasema, maeneo yanayochangia ni pamoja na mazingira. Mtu aliyezaliwa katika jamii fulani, ambapo jamii hiyo hutumia lugha ya jamii wakati mwingi, inakuwa ni vigumu sana kuwa mzungumuzaji mzuri wa lugha ya pili kwa sababu lugha ya kwanza huitumia kwa muda mwingi. Mazingira ya kijijini wasukuma wengi huwa wameathiriwa na lugha mama, maana matumizi ya lugha ya kiswahili ni kidogo sana, mawasiliano mengi hufanywa kwa kutumia lugha mama.
Wazazi wanapotumia lugha ya kisukuma kwa muda mwingi, huchangia kuwaathiri watoto wao wakati wanapojifunza lugha ya nyingine. Chazo cha data hii ni kwa watahiniwa wazazi waliojibu dodoso ya swali wanatumia lugha ipi katika kuwasiliana na watoto wao.
Jedwali
Idadi ya wazazi kiswahili kisukuma
33 08 25
Wazazi (Watafitiwa) 25 ambao ni sawa na asilimia 85 walijibu kwamba kuzungumza sana na watoto wao (wanafunzi) kisambaa kunasababisha washindwe kutamka baadhi ya matamshi ya Kiswahili sanifu. Na wazazi (Watafitiwa) wanne (08) ambao ni sawa na 15%
walijibu hawazungumzi kiswahili na watoto wao. Nadharia ya mawasiliano hukusudia pia kuboresha mahusiano kati ya watu na kuonyesha hisia za watu. Rocha (2011) lugha mama na lugha ya pili, kwa watanzania wengi lugha mama ndiyo lugha ya kwanza kujifunza maana huzaliwa na kuikuta katika jamii yake na lugha ya Kiswahili huwa ni lugha yake ya
pili kwa mjibu wa wantanzania wenyewe. Si watanzania wote kuwa lugha ya Kiswahili ni lugha ya pili, wengine ni kama lugha yao mama maana huzaliwa na kuikuta katika mazingira yao. Wazazi wengi hawazungumzi lugha ya Kiswahili na huzungumza lugha mama kwa muda mwingi sana na watoto wao kwa sababu hawawezi kuongea Kiswahili sanifu hii ni kutokana na athari ya lugha mama kwakuitumia muda mwingi.Kingine kilichobainika ni kwamba, wazazi hawa hawahimizi watoto wao kuongea lugha ya Kiswahili kwa wakati wote. Hii ni kutokana na athari waliyonayo wazazi wao katika kuzungumza lugha ya Kiswahili.
4.4mbinu za kupunguza athari za lugha ya kisukuma wakati wa kuwasiliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili
Lugha mama ndiyo chazo cha athari kwa wazungumzaji wa lugha ya kiswahili kwa kiasi kikubwa. Matumizi ya lugha mama yaani kisukuma kwa muda mwingi, mwanafunzi huathiriwa sana katika kujifunza lugha nyingine maana lugha yake huwa tayari ishajenga mizizi katika utamkaji wa sauti za lugha hiyo. Jinsi ya kuwasaidia kwa wale tayari walishaathirika na lugha ya kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili ni pamoja na mambo haya:-
4.4.1 Wafundishwe Lugha ya Kiswahili Tangu Utotoni
Chanzo data ni kutoka kwa walimu waliojibu dodoso iliyohusu mbinu za kuwasaidia walioathiriwa na kisukuma. Utafiti huu ulionesha kuwa msingi bora wa kuwa mahiri katika lugha huanzia utotoni, lugha inapaswa kufundiswa tangu mtotoni, hali ambayo itamsaidia katika mawasiliano kwa badae, kama nadharia ya mawasiliano inavyoeleza kuwa nadhariailikusudia kuboresha mahusiano kati ya watu (Paul,2001) hii itatokea endapo
aliyejifunza lugha tangu akiwa mtoto, na hii itamsaidia kuwa na uhusiano mzuri yeye na lugha anayoitumia katika mawasiliano. Serkali lazima itilie mkazo katika matumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa kwa nchi ya Tanzania. Vile vile hamasa kwa wazazi au walezi zitolewe ili waweze kutumia lugha ya Kiswahili katika kuwasiliana na wanao na kuondoa imani potofu kuwa mtoto anapojifunza lugha ya Kiswahili ndiyo chanzo cha kupoteza utamaduni wao. Wazazi wao wakifanya hivi! Itawasaidia sana wanao kuwa wazungumuzaji wazuri wa lugha ya Kiswahili.
4.4.2Waelekezwe Matamshi Ya Kiswahili
Matumizi mazuri ya matamushi katika mawasiliano huonesha uhusiano mzuri baina ya miundo ya lugha na mawasiliano, Chacha (2001) nadharia ya mawasiliano ilikusudiwa kuimalisha mbinu za ufundishaji ambazo zitasisitiza uhusiano uliopo kati ya miundo ya lugha na mawasiliano. Utafiti huu ulionesha kuwa endapo wataelekezwa vizuri, tatizo katika matamushi litapungua, kama Habwe (2010) wanasema, kwa muda mrefu, elimu imetegemewa kama nguzo ya uhai wa binadamu. Kila mtu na kila nchi imetafuta maarifa na kuzua mbinu mbalimbali za kujiboresha na kuiboresha jamii kupitia lugha. Ufanisi wa shughuli hizi zote umetegemea pakubwa mchango wa lugha. Lugha imepewa kipaumbele katika mitaala ya shule na vyuo vikuu ulimwenguni kote.
4.4.3 Kuanzisha Mihadhara
Hii itasaidia sana kwa wale wanaojifunza lugha ya Kiswahili. Kwanza itawajengea uwezo mkubwa wa kuzungumuza lugha ya Kiswahili na hali ya kusimama mbele ya watu na kuzungumuza bila uoga. Watu wengi wanakosa uwezo wa kuzungumuza mbele ya watu
kutoka na kutokuwa na mazoea ya kuzungumza lugha yoyote mbele ya watu, ili kuendeleza mawasiliano, Msau (2001) mijadala, michezo, usomaji wa magazeti huendeleza mawasiliano na kukuza lugha kwa mzungumzaji. Mihadhara hii ikishaanzishwa shule za wilaya ya Igunga, wasukuma wanaweza kuwa zungumuzaji wazuri wa lugha ya Kiswahili.
Utafiti ulikusudiwa kuwa edapo wasukumawatajengewa utamaduni wakusoma vitabu vya hadithi, majarida, na vipeperushi vyinavyohusiana na lugha ya Kiswahili vitawasaidia katika kuborasha lugha ya Kiswahili katika kuwasiliana. Usomaji wa vitabu na majarida husaidia sana kwa mwanafunzi katika kuelewa na kumsaidia kuelewa lugha ya Kiswahili.
Faida nyingi sana mtu aliyesoma majarida na vitabu anazipata, kwaza mwanafunzi kuwa msomaji mzuri, pili humujengea hali kuwa na msamiati mingi, kusoma kwa haraka, kuweza kufasili maneno magumu yaliyotumika katika hadithi hiyo, uwezo wa kuelewa jinsi ya kuunda sentensi za Kiswahili, kumjengea kuwa mtamkaji mzuri wa maneno ya lugha ya Kiswahili kama inavyostahili kutamkwa. Jamiii zetu, watu wao hawana hali au mazoea ya kusoma vitabu vya hadithi na majarida ya Kiswahili kutokana na hali hii mtu anakosa umahili wa kutosha na kuwa mzungumzaji mzuri wa lugha ya Kiswahili. Ushauri watu wawe na mazoea ya kusoma vitabu na majarida mbalimbali.
Kiswahili ni lugha muhimu sana katika jamii ya wasukuma kwa sababu inawasaidia kuwaunganisha katika nyanja mbalimbali kama kujuana na watu wengi, kusoma na kusikiliza taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari vile vile katika makongamano na mikutano inayofanyika katika maeneo yao na nje ya pale walipo. Data hii ni watahiniwa wazazi, wanafunzi waliobaini umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika jamii ya watanzania kwa kuonesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika mawasiliano, Chacha (2001)
alibainisha lenngo la nadharia ya mawasiliano kuwa ni kukuza uwezo wa kuwasiliana, kama lugha ya Kiswahili ilivyo na umhimu katika jamii ya Tanzania.
SURA YA TANO HITIMISHO LA UTAFITI
5.1 Utangulizi
Sura hii ilihitimisha utafiti huu unaohusu athari za lugha ya kisukuma katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Sura hii ilionesha Utangulizi, Muhtasari wa utafiti huu, mchango wa utafiti, vikwazo, mapendekezo na hitimisho kuhusiana na utafiti huu.
5.2Muhtasari Wa Utafiti
Katika sura ya kwanza mtafiti alitoa maana mbalimbali ya vipengele muhimu vilivyotumika katika utafiti huu kwa kuelezea nini maana ya lugha kulingana na wataalamu jinsi wanavyoelewa juu ya lugha, maana ya lugha ya kiswahili pamoja na lugha ya kisukuma. Sura ya kwanza pia utafiti ulieonyesha nadharia iliyotumika katika utafiti huu pamoja na malengo ya utafiti, tatizo la utafiti, umuhimu wa utafiti.
Sura ya pili ilihusu juu ya mapitio ya vitabu teule vilivyohusiana na maada ya utafiti yaani vitabu vyote vilivyotumika katika tasnifu yake, ni vile vilivyohusiana na athari ya lugha katika lugha ya kiswahili, na si katika kiswahili tu hata katika lugha nyingine ambavyo viliongelea juu ya athari ya lugha.
Katika sura ya tatu utafiti alionyesha mbinu za utafiti ambazo utafiti ulitumia wakati wa kukusanya data. Utafiti huu ulifanyikia mawandani na maktabani. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu, ziliwezesha utafiti kukusanya data za msingi na fuatizi ili kukamilisha malengo na kujibu maswali ya utafiti.
Sura ya nne utafiti ulichambua data ili kupata majibu juu ya maswali ya utafiti kama yalivyoandikwa katika sura ya kwanza. Mwisho kabisa ni sura ya tano ambayo ni hitimisho ya utafiti huu kwa kufanya muhtasari na mapendekezo katika athari ya lugha ya kisukuma katika kufifunza lugha ya kiswahili.
5.3 Mchango wa Utafiti
Utafiti huu ulifanyika ili kuibua ari za watafiti wengine na hasa katika kutafiti athari za lugha katika lugha ya kiswahili mfano Idarus,(2005) aliye tafiti juu ya makosa yanayofanywa na wazungumzaji wa lugha ya kiswahili na kubaini athari zilizojitokeza katika kiswahili.
Utafiti huu utatoa mchango mkubwa kwa watafiti wengine kuhusiana na athari za lugha juu ya lugha ya kiswahili.
5.4 Mapendekezo
Wazazi waelimishwe juu ya umuhimu wa lugha ya Kiswahili ili waone umuhimu wa kuwa zungumza na kuwasiliana nao kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Lugha ya Kiswahili ina
matumizi makubwa na muhimu. Wazazi wakijua umuhimu wa Kiswahili watakuwa makini katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
Kutokana na matumizi ya lugha mama kwa muda mwingi kwa watoto wa kisukuma, ni dhahiri kuwa matumizi hayo huathiri ufasaha wa lugha ya kiswahili.
Hivyo basi, mapendekezo ya mtafiti ni kwamba ili kuwa na lugha ya Kiswahili sanifu kuna haja ya kufanya tafiti za kina zaidi za kubainisha athari na mbinu za kuwasaidia kwa wale wanaojifunza lugha ya Kiswahili.
Vilevile itakuwa ni vema zaidi kama mashirika na taasisi mbalimbali za ukuzaji wa lugha hii ya Kiswahili kama vile Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TAKILUKI pamoja na vyama mbalimbali vya kiswahili wakahamasisha matumizi fasaha ya lugha hii ya Kiswahili, pamoja na kujitokeza wafadhili mbalimbali ambao watawafadhili watafiti ambao watajishughulisha na uchunguzi huu.
5.5 Vikwazo vya Utafiti
Utafiti ulipata tabu ya usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika ukusanyaji wa data. Hii ni kwa sababu maeneo mengi ya Igunga barabara zake siyo nzuri. Kutokana nahali hiyo ya ubovu wa barabara kuna baadhi ya sehemu usafiri kama magari na pikipiki haziwezi kufika. Kutokana na sababu hiyo mtafiti alilazimika kutembelea kwa miguu jambo ambalo lilimfanya mtafiti atumie muda mwingi. Pia kutembea huko kwa miguuu kulisababisha uchovu kwa mtafiti na kushindwa kufanya baadhi ya shughuli za kiutafiti pindi anaporudi kutafuta data.
Utafiti ulipata kikwazo katika suala la marejeleo. Vipo baadhi ya vitabu ambavyo utafiti ulilazimika kuvinunua kutokana na kutopatikana kwake.
Kikwazo kingine ni muda ambao ulitarajiwa kwa ajili ya maandalizi ya ripoti ulikuwa finyu ukilinganisha na uaandaji wa ripoti yenyewe kama inavyojulikana wandaaji wa ripoti ni kazi kubwa.
Uhaba wa fedha ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa utafiti. Utafiti hujapata msaada wakutoshawa kifedha ambao ungemsaidia katika shughuli mbalimbali za utafiti wa mada hii. Utafiti ulilazimika kutumia fedha nyingi ambazo pia zilikuwa hazitoshi katika shughuli za utafiti kama kukusanya data, kununua marejeo, kuchapisha na kurudufisha ripoti, kununua kama vipaza sauti na gharama za uchapaji vilimgharimu sana utafiti wa mada hii. Gharama za usafiri, malazi na makazi kwa muda wote wa kukusanya data ilikuwa pia ni kikwazo kikubwa kwa utafiti.
5.6 Hitimisho
Utafiti huu kwa ujumla umefanikiwa kufumbua chanzo cha tatizo la Athari za lugha ya Kisukuma katika Kujifunza lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi wa Shule za sekondari Tabora kuwa ni tatizo linalosababishwa na mambo kadhaa.
Wanafunzi wa shule za sekondari hutumia sana Kisukuma katika mawasiliano yao.
Hutumia Kisukuma wawapo nyumbani huongea lugha hiyo na wazazi wao. Wanafunzi pia hawa wawapo shuleni hutumia lugha ya Kisukuma wakati wanawasiliana wao kwa wao.
Ili kupunguza tatizo hili ni lazima serikali itilie mkazo katika matumizi ya lugha ya kiswahili, waelekezwe wanafunzi juu ya matamshi, na kuanzishwa kwa midahalo ihusuo kiswahili shuleni.
Marejeo
Ayubu Mukhwana – P. I. Ribemwangi (2011), Isimuujamii.
Baraza la Kiswahili la Zanzibar (2010) Kamusi la Kiswahili Fasaha, Oxford University Press.
Benard Witek na Edmord Ouma Ogalo (2012) Topographical Norms, Salvatorianum, morogoro.
C. K. Omari – M. V Mvungi (1981) Urithi wa Utamaduni wetu Tanzania, Tanzania Publishing House Dar es salaam.
Carless, D (2008) students use of Mother Tonque in the task based classroom. EL. T Journal62.
David P. B. Massamba (2009) Kamusi ya Isimu naFalsafa ya Lugha, TUKI Publication Dar es salaam.
John Habwe – Assupta. K. Matai – Jakton Nyonje (2010) Darubini ya Isimujamii kwaShule na vyuo, Phoenix Publishers, Nairobi.
Habwe John (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili,Phoenix Publishers, Nairobi.
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Oxford University Press, Dare As Salaam.
Lucius M Thonya (1978) Misingi ya Kiswahili, Mhenga Publishing Consultants Company Limited.
Mhilu G. D (2005), Language Its Nature and Use
Musau, Paul M, Chacha, Leonard M, (2001) Mbinu za Kisasa za Kufundishia Kiswahili Upili na Vyuo, Nairobi, Kenya Literature Bureau.
Nkwara F Michael (1979) Ukombozi wa Wanadamu; Kitabu cha nne, 1-6: Kitabu cha Mwalimu Pamoja na Silabasi; Kiada.
N. D Tuntufye (2010) Jinsi Ya Kufundisha Kiswahilidarasani, Tanzania Publishing House;
Dar es salaam
Paul. M,. Musau, Leonard M, Chacha (2001), Mbinu za kisasa za kufundishia Kiswahili.
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar es salaam (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la pili, Oxford University Press.
Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili chuo kikuu Dar es salaam, (2005),makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa kiswahili, Oxford University Press
Wamitila K.W, (2011) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi, Nairobi Focus Publication Ltd
Rocha (2011) Kiswahili Past Present and Future Horizoni, Nairobi University Press Yule George (2010) The Study Of Language