4.4 Vigezo Vinavyotumika Kuteua Majina ya Asili katika Koo za Ginantuzu . 104
4.4.6 Kigezo cha Tabia na Matendo ya Mtu
Majina yanayotokana na tabia na matendo ya mtu kwa kawaida huakisi mienendo ya
wahusika. Mienendo hiyo hujumuisha ubishi, ukarimu, ukaidi, ufuska, majivuno,
usafi, hasira, upole, uchoyo, ukali, wema, ulevi ama ukorofi. Watafitiwa 7 ambao ni
sawa na asilimia 8.75 walibainisha kuwa tabia na matendo ya mtu ni mojawapo ya
Tabia na matendo hayo yalifanywa na waanzilishi wa koo husika katika jamii. Tabia
na matendo katika jamii yalitofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine kama
anavyodai Adrey (1970) kwamba, kila mtu katika jamii ana tabia na matendo
yanayoweza kumtofautisha na wengine. Salapion (2011) naye katika utafiti wake
alishadidia haya kwa kusema kuwa, majina yanayotokana na tabia kimsingi huakisi
mienendo ya wahusika. Alitolea mifano michache ya majina katika jamii ya wahaya
ambayo yanatokana na tabia kama vile ‘Karikwera’ yaani mtu msafi asiye na doa na
‘Izooba’ yaani mtu mzuri na mwenye haiba. Hata katika koo za Ginantuzu kama ilivyoelezwa hapo mwanzo kuwa baadhi ya majina ya asili yanatokana na tabia na
matendo ya watu wa jamii hiyo. Utafiti umebaini kuwa katika koo za Ginantuzu, kuna
majina ya asili yenye maana yatokanayo na tabia na matendo ya watu. Tabia na
matendo ya wazazi ama ndugu wa karibu wa watoto hao ndizo zilizopelekea watoto
hao kuitwa majina hayo. Kwa mujibu wa watafitiwa waliofikiwa na mtafiti kwa njia
ya mahojiano na hojaji walieleza kuwa, tabia na matendo katika jamii yaliyopelekea
kupatikana kwa majina hayo mara nyingi yalikuwa yanaakisiwa kutoka kwa wazazi
wa watoto hao na si watoto wenyewe. Ingawa kwa kiasi kidogo yalifanywa na watoto
wenyewe lakini zaidi yalitoka kwa wazazi. Kwa mfano jina ‘Machilu’ au ‘Buchilu’ ni jina ambalo alipatiwa mtoto kutokana na tabia yake ya kupenda kulialia sana bila
sababu wakati wa utoto wake. Baadhi ya majina yanayotokana na tabia na matendo ya
mtu ni pamoja na Malaya, Kilekawanzile, Kuyela, Lusumbula, Masemba, Kabudi,
Mayombo, Kilila, Nhonge, Mnyumba, Mahela, Walwa, Kasabuku, Ngokolo, Maseko,
Nkali, Mkali, Buyegi, Nkwabi, Butogwa, Long’we na Mayuma. Hapa chini ni
ufafanuzi wa maadhi ya majina yaliyotokana na tabia na matendo ya watu
1. Ngokolo (mvivu) Hili ni jina ambalo alipatiwa mtoto wa kiume ambaye
mwanzilishi wa jina hilo alikuwa na tabia ya uvivu wa kufanya kazi.
Wazazi wa mtoto huyo waliamua kumpa mtoto wao jina hilo ili asije
akarithi tabia na matendo ya mwanzilishi wa jina hilo. Wakati
mwingine jina hilo lilitolewa kwa mtoto huyo kama kuweka
kumbukumbu ya mwanzilishi wa jina hilo lisije likapotea.
2. Kuyela (mtembezi) Jina hili hupewa mtoto wa kiume ambaye wazazi wake
aumwanzilishi wa jina hilo alikuwa na tabia ya utembezi kupita kiasi.
Tabia hii ya utembezi katika koo za Ginantuzu ilipigwa vita sana
kwani mtembezi daima katika jamii alionekana kutokuwa na kitu
chochote cha kiuchumi kwani muda wake mwingi aliiutumia
kutembea badala ya kufanya kazi inayozalisha mali. Hivyo jina hilo
lilitolewa kwa mtoto kama kukemea hali hiyo isijirudie tena kwa
mtoto aliyepewa jina hilo.
3. Masemba (vituko/utani) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume na wazazi
wake ambaye alikuwa na vituko sana au mwazilishi wa jina hilo
alikuwa na vituko vingi vyenye kuchekesha katika maisha yake. Watu
wenye vituko katika jamii ya Ginantuzu kwa kiasi kikubwa
walipendwa sana na walitakiwa sana kuwepo katika shughuli yoyote
iliyokuwa inafanywa kwa jumuia. Hivyo mtoto aliweza kupewa jina
hili kama ukumbusho wa mwanzilishi huyo.
4. Mayombo (mwenye vurugu) Jina hili hupewa mtoto wa kiume ambaye wazazi
Kutokana na majibu wa watafitiwa walisema kuwa katika jamii yao
kama zilivyo jamii nyingine kulikuwapo na watu ambao walipenda
sana kufanya vurugu nje au ndani ya jamii yake. Watu kama hao
walipewa jina hilo kama ishara na utambulisho kwa jamii husika.
Hivyo ili kutunza kumbukumbu ya mtu huyo jina lake lisipotee katika
ukoo watoto wengine waliweza kupatiwa jina hilo kwa ajili ya
ukumbusho.
5. Kilila (kulia) Hili ni jina analopewa mtoto wa kiume ambaye alikuwa na tabia
ya kulialia bila sababu wakati wa utoto wake. Wakati mwingine jina
hili hupewa mtoto kama jina la ukoo ambapo mwanzilishi wake
alikuwa na tabia hiyo ya kulialia bila sababu ya msingi. Jina hili
wakati mwingine huitwa ‘Machilu’ likiwa na maana hiyo hiyo ya kulialia bila sababu ya msingi.
6. Mnyumba (nyumbani) Jina hili alipewa mtoto wa kiume ambaye mwanzilishi
wa jina hili alikuwa na tabia ya kukaa ndani ya chumba au nyumbani
kwake tu. Katika koo za Ginantuzu wanaume walikuwa wanatakiwa
kukaa nje wakati wote na sio ndani ya chumba au mwanaume
alitakiwa wakati mwingine atoke nje ya familia yake kwa ajili ya
kukutana na wanaume wenzake kwa kubadilishana mawazo. Hivyo
kwa mwanaume ambaye hakuwa na tabia hizo alipewa jina hilo ili
kusadifu tabia na matendo aliyo nayo kwa jamii husika.
7. Walwa (pombe) Hili ni jina analopewa mtoto wa kiume jina ambalo
kiasi kwamba alikuwa hawezi kukosekana mahali palipo na pombe.
Wakati wowote mtu huyo anapohitajika na jamii, mahali pa
kumtafutia ilikuwa ni vilabuni. Watu wengine wenye tabia na
matendo kama haya walipewa jina la ‘Mahela’ likiwa na maana ya machicha ya pombe ya kienyeji. Watu hawa wakati mwingine
walikuwa mafundi wa kutenganisha pombe na machicha ya pombe
hivyo ikapelekea kupatiwa jina hilo la Mahela.
8. Nkwabi (mtafutaji mali) Jina hili alipewa mtoto wa kiume akirithi kutoka kwa
wazazi/ waanzilishi. Mwanzilishi wa jina hili alipewa kutoka na tabia
ya utafutaji mali kwa njia halali. Katika jamii ya Ginantuzu mtu kama
huyu alipendwa na kila mtu mwenye moyo wa utafutaji mali.
Utafutaji mali ulikuwa ni msingi wa maisha katika koo za Ginantuzu
hivyo jina kama hili lilipendwa na jamii na linapatikana kwa wingi
katika koo za Ginantuzu mpaka sasa.
9. Mkali (ukali) Hili ni jina analopewa mtoto wa kiume jina ambalo limetokana
na mzazi au mwanzilishi wa jina hilo kuwa na tabia ya ukali wakati
mwingi. Tabia kama hii haikukubalika katika koo za Ginantuzu. Mtu
aliyeonekana kuwa na tabia hiyo ya ukali bila ya kuwa na sababu za
msingi aliweza kupewa jina hilo kama kusadifu tabia aliyonayo.
10. Mayumila (kutoa kitu bila kipimo maalum) Jina hili lilitolewa kwa mtoto wa
kiume akirithi kutoka kwa mwanzilishi aliyekuwa na tabia nzuri
iliyokubalika kwa jamii kiasi kwamba alikuwa anatoa kitu chochote
ilikuwa inamilikiwa na wachache sana. Wachache hawa walipewa
jina hili kama zawadi ya kusadifu tabia na matendo waliyo nayo.
Watu wengingi jina hili lilifupishwa na kuitwa ‘Mayuma’.
Kutokana na ufafanuzi wa majina hayo hapa juu, utafiti umebaini kuwa tabia na
matendo ya mtu ni kigezo kilichotumiwa na koo za Ginantuzu kutolea majina katika
jamii yao na majina hayo huwa na maana tu kwa jamii ya Ginantuzu. Mtoto
anayepewa jina la aina hiyo kutambuliwa kuwa yeye ni Mnyantuzu kutokana na jina
la Ginantuzu linalomtambulisha kwa jamii yake. Katika sehemu hii, kupatikana kwa
majina haya kwa kutumia kigezo cha tabia na matendo ya mtu aliyonayo katika jamii
anamoishi kunatimiza moja ya lengo mahususi la utafiti huu lililolenga kuonesha
vigezo vinavyotumika katika kuteua majina ya asili katika koo za Ginantunzu. Aidha,
kupatikana kwa data hizi kunadhihirisha kufaa kwa nadharia ya uumbaji ambayo
imetumiwa na mtafiti kama mwongozo wakati wa kukusanya na kuchambua data za
utafiti huu.