4.5 Miktadha ya Majina ya Asili katika Koo za Ginantuzu
4.5.4 Muktadha wa Kudokeza Udunishaji
Udunishaji ni hali ya kukifanya kitu kuwa na thamani ndogo yaani kukiteremsha kitu
unaotumika kuelezea majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Jedwali namba 4.28
linaonesha uwepo wa majina ya asili yanayodokeza muktadha wa udunishaji.
Watafitiwa kupitia njia ya hojaji na mahojiano walisema kuwa, katika koo za
Ginantuzu yapo majina ambayo walipewa baadhi ya watu kwa kudokeza muktadha
wa udunishaji. Baadhi ya majina hayo ni pamoja na Budulungu, Ndalahwa, Shunula,
Buga, Butule, Ntengo, Ding’ho, Galedi, Golomanda, Holohondo. Bukela, Ng’holo, Shagembe, ng’olo, Sagala, Ng'oba, Nhungo, Ngokolo na Mnyumba. Watafitiwa waliendelea kusema kuwa jamii katika koo za Ginantuzu ziliweza kuwadunisha
wahusika wa majina hayo kwa kuwapa majina ya vitu ambavyo havikuwa na thamani
kwao. Lengo la kuwapa majina hayo ilikuwa kuwafanya wahusika wa majina hayo
wasiwe na tabia na matendo ya majina ya vitu hivyo ambavyo havikukubalika katika
jamii. Miongoni mwa baadhi ya majina yaliyotajwa, majina yaliyoonekana kutumika
zaidi katika koo za Ginantuzu ni pamoja na Budulungu, Nhungo, Bukela, Galedi,
Shunula, Ntengo, Holohondo, Golomanda/Goma, Ng’holo/Makolo, Shagembe, ng’olo, Ng'oba, Ngokolo na Mnyumba. Ufafanuzi wa baaadhi ya majina haya ni kama ifuatavyo:
1. Budulungu (ng’ombe) Maana halisi ya jina hili ni ng’ombe mkubwa ambaye
hakuwa na afya nzuri katika kundi la ngombe wengi tangu akiwa ndama.
Jina hili lilitolewa kwa mtoto wa kiume akirithi kutoka kwa mwanzilishi
kwa kuashiria afya yake kutoridhisha katika ukoo au jamii yake kwa
ujumla. Lengo la kupewa jina hili ni kwa ajili ya kuondokana na tatizo
hilo linalomkabili. Jina hilo linaweza kuwa la kuitwa, kutaniwa au kujiita
mwenyewe. Ingawa imani ya jamii katika koo za Ginantuzu ni kuwa jina
kumkinga asipatwe na hali ambayo hawaihitaji kwani mwenye jina
akuapo hufanya juu chini asisadifu jina husika. Kwa kufanya hivyo
watakuwa wamemwokoa kwa njia moja au nyingine mhusika wa jina hilo.
2. Nhungo (mnyama) Maana halisi ya jina ni mnyama pori jamii ya mbwa. Tabia
ya mnyama huyu huwa anajisaidia haja kubwa sehemu moja tu kwa
mwaka mzima na anausingizi sana wakati wa mchana na ni msahaurifu
kweli na kumbukumbu kidogo. Mnyama huyo hata akiwa mbali hukata
majani na kuziba sehemu ya haja kubwa lengo lake asije akajisaidia
sehemu nyingine. Akifanya hivyo hujitahidi kukimbia ili afike sehemu
anakojisaidia. Mnyama huyo kwa jamii ya Ginantuzu humwona kama
akili zake sio nyingi kwani angeweza kujisaidia sehemu nyingine tu. Jina
hili katika koo za Ginantuzu hupewa mtoto wa kiume ambaye anaonekana
ana akili na matendo yanayofanana na mnyama huyo. Lengo pia la
kupewa jina hili ni kumfanya mtoto huyu asifanane na mnyama huyo.
3. Bukela (-a kukosa kitu) Hili ni jina analopewa mtoto wa kike na wazazi wake
kama kiashirio cha mtoto kutokuwa na akili nyingi. Jina hilo hupewa
mtoto huyo baada ya kumwona makuzi ya akili ya mtoto huyo hayapo
sawa na umri wake.
4. Holohondo (panzi jike) Maana halisi ya jina hili ni panzi jike isiyo na mayai.
Kwa kuwa panzi katika koo za Ginantuzi kilikuwa ni kitoweo na panzi
aliyekuwa na thamani sana kwao alikuwa ni panzi jike mwenye mayai
maarufu kama bundikili au buki, panzi jike aliyekosa mayai hakuwa na
mayai. Hivyo basi jina hili aliweza kupewa mtoto wa kiume ambaye
aliashiria kutokuwa na thamani katika familia au jamii yao. Kwa hiyo
muktadha wa jina hili ni mtu yeyote ambaye hakuwa na msaada katika
jamii au familia.
5. Ngokolo (mzembe) Mzembe katika koo za Ginantuzu alionekana kuchukiwa
na watu wote katika ukoo na hata jamii nzina. Jina hili alipewa mtoto wa
kiume ambaye alionekana kuwa mzembe kwa kila hali. Lengo la kupewa
jina hili ni kumtaka ajirekebishe na tabia ya uzembe huo kwani mtu
mzembe katika jamii hiyo alionekana kutokuwa na chochote katika
familia yake. Hali hiyo ilimfanya awe ombaomba wakati wote hali
iliyochukiwa na kila mmoja wakati huo. Mtu mwenye tabia kama hiyo pia
aliweza kupewa jina la Mnyumba yaani mtu anayependa kukaa nyumbani
tu bila kufanya kazi au Ng’olo ikiwa na maaana ya mzembe wa kufanya
kazi yoyote.
6. Makolo (Kondoo) Jina hili alipewa mtoto wa kiume ambaye aliashiria kuwa
mpole kupita kiasi. Mtu ambaye alionekana kuwa hana mchango wa
mawazo katika familia yaani yeye kila kitu anachoambiwa anakubali tu
alifananishwa na kondoo na wakati mwingine alipewa jina la Ng’holo
ikiwa na maana ya kondoo ikidokeza muktadha wa mtu mpole kupita
kiasi.
Jedwali Na. 4.28: Majina Yanayodokeza Uduni
Na. Jina Jinsi Maana yake
1 Budulungu Me Ng’ombe
2 Buga Me Ndege
3 Bukela Me Asiye na akili
4 Butule Me Panzi
5 Ding’ho Me Harufu ya samadi
6 Galedi Me Takataka
7 Golomanda Me Panzi
8 Holohondo. Me Panzi
9 Mnyumba Me Mtu akaaye ndani daima
10 Ndalahwa Me Mdharauliwa
11 Ng’holo Me Kondoo
12 Ng’oba Me Mwoga
13 Ng’olo Me Mzembe
14 Ngokolo Me Mzembe
15 Nhungo Me Mnyama pori jamii ya mbwa
16 Ntengo Me Mtu anayekaa sehemu moja kuhama mpaka aondolewe
17 Sagala Me Hovyo
18 Shagembe Me Buu la nzi linalopatikana kwenye vumbi linyonyalo damu
19 Shunula, Me Mtu akaaye mdomo wazi muda mwingi
Chanzo: Data ya Uwandani – 2017
Data iliyowasilishwa katika Jedwali namba 4.28. hapa juu inadhirisha uwepo wa
majina yaliyotokana na muktadha wa kudokeza udunishaji. Aidha katika jedwali
namba 4.28. hapo juu linaonesha kuwa, majina mengi yaliyokusanywa na mtafiti
akiongozwa na nadharia ya uumbaji kutoka uwandani yameonesha kutumika kwa
wanaume tu. Sababu nyingine ya kutopatiwa majina yanayodokeza uduni ni kulingana
na asili ya mwanamke anavyothaminiwa katika jamii. Hivyo basi, kupatikana kwa
majina ya nayotokana na muktadha wa kudokeza udunishaji kunatimiza moja ya lengo
za Ginantuzu. Aidha, kupatikana kwa data hizi kunadhihirisha kufaa kwa nadharia ya
uumbaji ambayo imetumiwa na mtafiti kama mwongozo wakati wa kukusanya na
kuchambua data za utafiti wake.