4.4 Vigezo Vinavyotumika Kuteua Majina ya Asili katika Koo za Ginantuzu . 104
4.4.1.3 Majina ya Watu kwa Kigezo cha Vitendea Kazi Wanavyotumia
Kama tulivyobainisha hapo mwanzo kuwa baadhi ya majina ya asili katika koo za
Ginantuzu yanatokana na majina ya vitendea kazi wanavyotumia jamii husika. Mtafiti
amebaini kuwa, vitendea kazi ni mojawapo ya vigezo vya utoaji wa majina. Kwa
mujibu wa watafitiwa 28 kati ya 80 waliofikiwa na mtafiti kwa njia ya hojaji na
mahojiano kama ilivyoonesha katika Jedwali Na. 4.4 hapo mwanzo walisema kuwa,
utolewaji wa majina hayo hufungamana na muktadha maalum ambao unaweza kuwa
wa utumiaji au utengenezaji wa vitendea kazi hivyo.
Baadhi ya majina ya asili yaliyoshamili kutokana na vitendea kazi ni pamoja na
Magembe, Isonga, Kasheto, Koloboi, Mapanga, Mbasa, Ilanga, Chenge, Nhunda,
Nungu, Machimu, Izengo, Kisabo, Cheyo, Buta, Mawe, Lukago, Kasuka, Sululu na
Lubiga. Miongoni mwa majina haya, majina yaliyoweza kupatikana karibu kila kata
na kila kijiji ni pamoja na Magembe, Isonga, Ilanga, Kasuka, Mbasa/shoka, Lukago,
Kisabo na Mawe.
Hata hivyo kwa mujibu wa watafitiwa walieleza kuwa utoaji wa majina kwa watoto
kwa kuangalia kigezo cha vitendea kazi umepungua kwa kiasi kikubwa kwani watoto
wanaozaliwa kipindi hiki wanapewa majina yasiyo ya asili na kuacha majina ya asili.
Mtafitiwa mmoja alidai kuwa majina hayo yamepungua kutokana na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia kwani baadhi ya vitendea kazi vilivyokuwa vinatumika kutolea
majina kwa sasa zimebadilika. Kubadilika huku kumeathiri kwa kiwango kikubwa
utoaji wa majina kwa kigezo cha vitendea kazi. Hapa chini ni ufafanuzi wa baadhi ya
majina yaliyotokana na kigezo cha vitendea kazi.
1. Magembe (majembe) Jina hili lilitolewa kutokana na upatikanaji wa kitendea
kazi hicho au kutokana na wazazi wa mtoto huyo kuwa
watumiaji wazuri wa kitendea kazi hicho kwani katika jamii ya
2. Isonga (mshale) Hili ni jina ambalo alipewa mtoto wa kiume na wazazi wake
ambaye alizaliwa kipindi cha kutengeneza mishale au wakati
mwingine mshale husika ulikuwa na athari yoyote katika
kuzaliwa kwa mtoto husika. Wakati mwingine mtoto aliweza
kupewa jina hilo kuashiria ushujaa atakaokuwa nao hapo mbele
kwa sababu mshale ulikuwa silaha za kivita.
3. Ilanga (fimbo) Jina hili alipewa mtoto wa kiume aliyezaliwa kipindi cha
kutayarisha fimbo kama silaha. Wakati mwingine fimbo hiyo
iliathiri kwa njia moja au nyingine katika kuzaliwa kwa
mwanzilishi wa jina hilo. Mzee Manyatula mmoja wa watafitiwa
alisema kuwa, baba yake aliitwa jina la Ilanga baada ya mama
yake kushindwa kujifungua chini ya usimamizi wa wakunga wa
kike mpaka wanaume wakiwa na fimbo kumchalaza mpaka
akajifungua salama. Baada ya kujifungua wanawake wenzake
wakawa wanamtania kuwa ‘kujifungua kwako mpaka fimbo’ na mtoto huyo aliyezaliwa aliitwa ‘Ilanga’ ikimaanisha fimbo.
4. Kasuka (jembe) Jina hili alipewa mtoto wa kiume na wazazi wake kipindi cha
kutayarisha majembe tayari kwa kilimo. Wakati mwingine jina
hili aliweza kupatiwa mtoto kama ishara ya ukulima hodari hapo
mbeleni.
5. Mbasa (shoka) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume ambaye alizaliwa wakati
mama yake akifanya kazi ya kusena au kupasua kuni au kukata
miti porini kwa kutumia kitendea kazi hicho. Kama yalivyo
kutabiri uchapakazi wa mtoto huyo hapo mbeleni kama kilivyo
kifaa chenyewa.
6. Lukago (zindiko) Jina hili alipewa mtoto wa kiume ambaye kuzaliwa kwake
kulikuwa na matatizo yaliyosababishwa na mama kukanyaga
mitego. Hivyo ili kuzaliwa salama ilibidi kufuata miamba wa miti
shamba (wanganga) kwa ajili ya kutegua mitego hiyo na baada ya
kuzaliwa mtoto huyo alipewa jina hilo la zindiko yaani Lukago ili
asiathirike tena na mitego mingine.
7. Kisabo (kibuyu) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume ambaye alizaliwa
kipindi mama yake akiwa ama anatengeneza kibuyu au kipindi
cha uvunaji wa vibuyu au wakati wa kiangazi kikali ambapo
akina mama wakati wote walikuwa wanatembea na vibuyu kwa
ajili ya kutafuta maji. Wakati mwingine jina hilo lilitokana na
tabia ya mama kuwa anapendelea kubeba kibuyu wakati wa
kufuata maji kipindi cha ujauzito wa mtoto husika.
8. Mawe (mawe) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume ambaye ama mama yake
alishikwa na uchungu akiwa mlimani au alizaliwa wakati mama
yake akiwa anasaga unga katika mawe kwani kipindi cha zamani
mashine za kusaga unga zilikuwa ni mawe makubwa
yaliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa na kutumiwa kama
mashine zilizoendeshwa na akina mama peke yao. Wakati
mwingine mtoto aliweza kupewa jina hilo kutokana na mama
yake kutokuwa na tatizo lolote kipindi chote cha ujauzito wa
9. Chenge (kijinga cha moto) Jina hili alipewa mtoto wa kiume na wazazi wake
ambaye alizaliwa ama kwa wakunga waliomhudumia mzazi
kutumia kifaa hicho (chenge) kama nyenzo ya kupata mwanga
kwa ajili ya kuona kutokana na ukosefu wa taa kipindi hicho au
wakati anazaliwa mtoto huyo kulikuwa na vimulimuli vingi nje
vilivyojulikana kwa jina hilo la chenge vilivyotumiwa na
wachawi au miujiza fulani kuleta athari fulani.
10. Izengo (miti ya kujengea) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume ambaye
alizaliwa katika kipindi cha kuandaa miti ya kujengea nyumba
ama amezaliwa sehemu ambayo miti hii ya kujengea nyumba
imekusanywa na kuhifadhiwa. Kwa mujibu wa watafitiwa
walisema kuwa hapo zamani nyumba karibu zote zilijengwa kwa
kutumia miti. Sayansi ya kutumia matofari ya udongo na saruji
haikuwepo kabisa.
Kutokana na orodha ya majina yaliyowasilishwa hapo juu inadhihirisha kwamba
baadhi ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu yanayotumika maana zake
zinahusiana na majina ya vitendea kazi ambazo zilipatikana kwa wingi katika
mazingira wanamoishi waanzilishi wa majina hayo. Matokeo ya utafiti huu pia
yanadhihirisha kuwa vitendea kazi ni kigezo muhimu kilichozingatiwa katika
kumpatia jina mtoto aliyezaliwa katika koo za Ginantuzu. Katika sehemu hii,
kupatikana kwa majina haya kwa kutumia kigezo cha vitendea kazi vilivyopatikana
katika mazingira waishio, kulitimiza moja ya lengo mahususi la utafiti huu lililolenga
Ginantunzu. Aidha, kupatikana kwa data hizi kunadhihirisha kufaa kwa nadharia ya
uumbaji ambayo imetumiwa na mtafiti kama mwongozo wakati wa kukusanya na
kuchambua data za utafiti huu.