4.4 Vigezo Vinavyotumika Kuteua Majina ya Asili katika Koo za Ginantuzu . 104
4.4.8 Kigezo cha Ujio wa Vitu Vipya
Jedwali namba. 4.24 hapo juu linaonesha kuwa watafitiwa 5 ambao ni sawa na
asilimia 6.25 wamesema kuwa baadhi ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu
hutolewa kutokana na ujio wa vitu vipya. Utafiti unaonesha kuwa ujio wa vitu vipya
ni mojawapo ya vigezo vya utoaji wa majina katika koo za Ginantuzu. Kwa mujibu
wa watafitiwa waliofikiwa na mtafiti kwa njia ya mahojiano walisema kuwa, ujio wa
vitu vipya umekuwa ukitumika sana kutolea majina katika koo za Ginantuzu. Vitu
hivyo vipya vinaweza kuwa viumbe hai au viumbe visivyo hai.
Majina ya watu yanayotolewa kwa kigezo hiki yanatolewa kwa watoto wadogo na
mengine yanatolewa kwa watu wazima kulingana na athari ya kitu hicho katika jamii
husika. Watafitiwa hao walidai kuwa majina haya hutolewa kwa watu kutokana na
kuingia kwa vitu vipya au utawala mpya ambao haukuwepo katika jamii husika.
Watafitiwa pia walisema kuwa lengo la kupatiwa watoto majina hayo ni kuweka
kumbukumbu katika jamii juu ya ujio wa vitu hivyo au utawala huo.
Baadhi ya majina ya asili yaliyoshamiri kutokana na ujio wa vitu vipya ni pamoja na
Tegisi, Mashini, Keya, Dafu, Sikania, Pajero, Nyerere, Ng’winyi, Magufuli, Maseyi, Sadam na Osama. Miongoni mwa majina haya, majina yaliyoweza kupatikana karibu
kila kata na kila kijiji ni pamoja na Mashini, Tegisi, Nyerere, Sadam, Giligita na
Osama. Hata hivyo kwa mujibu wa watafitiwa walieleza kuwa utoaji wa majina kwa
watoto kwa kutumia kigezo cha ujio wa vitu vipya umepungua kwa kiasi kikubwa
kwani watoto wanaozaliwa kipindi hiki wanapewa majina yasiyo ya asili na kuacha
1. Tegisi (basi) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume baada ya ujio wa basi
yaani gari la abiria. Jina hilo kwa mujibu wa watafitiwa walisema kuwa
mtoto aliweza kupewa jina hilo aidha kwa sababu alizaliwa kipindi cha
ujio wa mabasi hayo au alizaliwa kipindi mama yake akiwa katika basi
akielekea hospitalini kwa ajili ya kujifungulia na akajifungulia humo
humo kwenye basi la abiria kabla ya kufika hospitalini.
2. Nyerere (Rais kwa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) Jina hili
alipewa mtoto wa kiume ambaye alizaliwa kipindi cha utawala wa
kiongozi huyo. Kwa mujibu wa watafitiwa walisema kuwa kutokana na
utawala wa kiongozi huyo kuwa mzuri watoto wengi waliozaliwa
kipindi anaanza kutawala walipewa jina hilo kama ukumbusho kwa
jamii husika. Jina hilo hadi sasa bado linatolewa kwa watoto kutokana
na kurithi kutoka kwa waanzilishi wake.
3. Ng’winyi (Mwinyi Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania awamu ya
pili) Jina hili pia alipewa mtoto wa kiume aliyezaliwa kipindi cha
utawala wa Ali Hassan Mwinyi kama ukumbusho kwa jamii husika.
4. Mashini (mashine) Hili ni jina alilopewa mtoto wa kiume mwanzoni mwa ujio wa mashine za kusaga na kukoboa. Kwa mujibu wa watafitiwa
walisema kuwa hapo mwanzo hapakuwepo na mashine za kusaga unga
na kukoboa nafaka. Kazi hizo zote zilifanywa na wanajamii husika kwa
kutumia nyenzo mbalimbali kama mawe na vinu. Baada ya ujio wa
mashine hizo ilikuwa ni jambo geni sana na watu kipindi hicho
waliweza kukusanyika kwenye mashine hiyo ili kuangalia utendaji kazi
walipatiwa jina la Mashini wakiashiria kuwa watakapokua watoto hao
watakuwa wanafanya kazi kama ilivyo mashine. Kwa hiyo mtoto
aliyepewa jina la Mashini jamii ilitarajia mtoto huyo awe mchapa kazi
sana kama ilivyo mashine.
5. Maseyi (aina ya trekta) Jina hili alipewa mtoto wa kiume ambaye alizaliwa
kipindi cha ujio wa trakta aina ya Massey Furgason. Chombo hiki cha
kilimo hapo mwanzo kiliwashangaza jamii ya Ginantuzu kwa utendaji
kazi wake kwani chombo hiki kiliweza kulima hata kwenye ardhi
iliyoshindikana. Kutokana na chombo hiki, watoto waliozaliwa kipindi
hiki walipewa jina hilo kama ukumbusho. Jina hili halikutolewa kwa
watoto tu bali hata watu wazima walijibatiza kwa jina hili na wengine
wakitumia jina la Giligita ikiwa na maana ile ile ya Trekta.
6. Osama (Kiongozi wa mtandao wa Alkaida) Hili ni jina alilopewa mtoto wa
kiume aliyezaliwa kipindi cha utawala wa mtu huyo. Wakati mwingine
watu wazima walijipatia jina hilo ili kuonesha ubabe alio nao mtu
huyo. Mtu ambaye alionesha hali ya ubabe kipindi kile alistahiri
kupatiwa jina hilo kulingana na matendo aliyokuwa anayafanya.
7. Magufuli (Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
Hili ni jina ambalo watoto wa kiume waliozaliwa katika kipindi hiki
cha utawala wa Rais Magufuli wamepewa. Kulingana na majibu ya
watafitiwa walisema kuwa wameamua kutoa jina hilo wakiwa na imani
kuwa hata watoto wao baada ya kukua watakuwa na msimamo na
yalipatikana kwa watoto karibu kila kata na kijiji kilichofikiwa na
mtafiti hasa kwa watoto waliozaliwa kipindi hiki.
Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha kuwa ujio wa vitu vipya wakati mtoto
anazaliwa ni kigezo kingine kilichozingatiwa katika kumpatia jina mtoto anayezaliwa
katika koo za Ginantuzu. Katika sehemu hii, kupatikana kwa majina haya kwa
kutumia kigezo cha ujio wa vitu vipya katika jamii kunatimiza moja ya lengo
mahususi la utafiti huu lililolenga kuonesha vigezo vinavyotumika katika kuteua
majina ya asili katika koo za Ginantunzu. Aidha, kupatikana kwa data hizi
kunadhihirisha kufaa kwa nadharia ya uumbaji ambayo imetumiwa na mtafiti kama
mwongozo wakati wa kukusanya na kuchambua data za utafiti huu.