Kwa kawaida, data za utafiti wa kimaelezo hupatikana katika muundo wa maneno na
siyo namba (idadi). Ili kuhakikisha kuwa data za utafiti huu ni thabiti na halali kwa
kiwango cha kuridhisha, mbinu tofautitofauti za kukusanya data zilitumiwa. Katika
utafiti huu mtafiti alitumia mbinu ya hojaji na mbinu ya mahojiano kwa kukusanya
data za msingi kwenye uwanda wa utafiti. Mtafiti alitumia mbinu hizi mchanganyiko
kwa lengo la kupata matokeo yaliyo bora. Kama walivyobainisha na Best na Khan
(1993) kwamba, mbinu moja haijitoshelezi katika kupata data zinazoaminika na
kukubalika katika utafiti. Lengo la mtafiti kutumia mbinu hizi ni kwamba; Kwanza,
ni kupata uthabiti wa matokeo ya utafiti aliokusudia kuufanya. Pili, mbinu hizi
zilimsaidia kukusanya data kwa haraka na kwa wingi. tatu, mbinu hizi zilimsaidia
3.7.1 Hojaji
Hojaji ni miongoni mwa mbinu zinazotumika kukusanyia data. Kwa mujibu wa
Kothari (2004) hojaji ni mbinu ya kukusanyia data ambapo mtafiti huandika maswali
na kisha kuyapeleka kwa watoa taarifa ili wayajibu na baadae kumrudishia mtafiti
yakiwa tayari yemeshajibiwa. Mbinu hii ilitumiwa sana kwa watafitiwa lengwa ambao
wanajua kusoma na kuandika. Aidha, mbinu hii ilitumika ili kuhakiki, kulinganisha,
na kuthibitisha data zilizotokana na mapitio ya nyaraka ili kupata mtazamo kuhusu
makundi ya majina ya asili, vigezo vilivyotumika kuteua majina ya asili na miktadha
ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu.
Mbinu hii ilitumika kujibu maswali yote matano ya utafiti wetu, Hojaji ilitumika kwa
Sampuli ya jamii ya Ginantuzu wenye umri wa kuanzia miaka 25 – 85 ambao idadi
yao walikuwa 40, yaani vijana 20 wenye umri wa miaka 25-54 kwa uwiano sawa wa
kijinsia na wazee 20 wenye umri kuanzia miaka 55-85 kwa uwiano sawa wa kijinsia.
Mbinu hii iliwapa fursa watafitiwa hao kutoa maelezo ya kina na yenye hoja za
kitaaluma. Mbinu ilimsaidia mtafiti kupata taarifa mbalimba kuhusu makundi ya
majina ya asili, vigezo vilivyotumika kuteua majina ya asili na miktadha mbalimbali
ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu kupitia maswali yote yaliyoandaliwa na
mtafiti. Faida zifuatazo tulizipata kwa kutumia mbinu hii:
(i) Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kwa kuwa ina gharama ndogo na ni rahisi kutumika
kupata taarifa nyingi kwa muda mfupi.
(ii) Mbinu hii iliweza kuibua taarifa nyingi na ilimsaidia mtafiti kukusanya data
(iii) Mbinu hii ilimpa mtafitiwa uhuru wa kujieleza na kujaza kile anachokifahamu
kulingana na uwezo, uelewa na tajiriba yao kuhusu maswali aliyoulizwa kwenye
hojaji.
(iv) Mbinu hii ilikuwa na hojaji iliyoandaliwa ikiwa na orodha ya maswali sawa na
yanayofanana kwa watafitiwa wote ili kumsaidia mtafiti kufanya ulinganifu wa
majibu kutoka kwa watafitiwa.
Aidha aina ya data zilizokusanywa katika njia hii ya hojaji ni data za msingi. Hapa
mtafiti aliorodhesha maswali aliyotaka yajibiwe na watafitiwa na kuyapeleka
uwandani. Maswali hayo yote yalilenga kujibu vipengele vya makundi ya majina ya
asili katika koo za Ginantuzu, vigezo vilivyotumika kuteua majina ya asili katika koo
za Ginantuzu na miktadha ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Majibu ya
maswali hayo yaliweza kutimiza malengo mahususi matatu ya utafiti. Katika njia hii,
jumla ya watafitiwa 40 tu kutoka katika vijiji vyote 10 ndio waliohusishwa, kwa kuwa
ndio waliokuwa wanajua kusoma na kuandika. Aidha watafitiwa wote 40 walirejesha
majibu yao, tena kwa wakati uliopangwa. Pamoja na mafanikio makubwa
yaliyopatikana katika mbinu ya hojaji kulikuwa na kasoro zifuatazo kama baadhi ya
watafitiwa uandishi wao ulikuwa haufahamiki. Pia watafitiwa ambao walikuwa
hawajui kusoma na kuandika walishindwa kutoa taarifa za utafiti. Kutokana na
watafitiwa kutojua kusoma na kuandika, mtafiti alitumia mbinu ya mahojiano ili
kuweza kuziba kasoro hizo ziliyojitokeza.
3.7.2 Mahojiano
Mahojiano (usaili) ni majibizano ya ana kwa ana, simu, dijitali au barua pepe kati ya
watu wawili au zaidi kwa lengo la kukusanya taarifa au maoni kuhusu suala fulani la
kufanywa kwa simu, dijitali au barua pepe, uulizaji wa maswali ya ana kwa ana au
majadiliano ndio uliotumika zaidi katika utafiti huu. Aidha aina ya data
zilizokusanywa katika njia hii ya mahojiano ni data za msingi. Katika mbinu hii,
wahojiwa 20 wenye umri kati ya 25-54 na wahojiwa 20 wenye umri kati ya 55-85
kutoka sampuli ya watu 40 walifikiwa na mtafiti. Mbinu hii ilitumiwa kwa watu 40.
Mtafiti aliichagua njia hii kwa sababu zifuatazo:
(i) Mbinu hii ilitoa fursa kwa watafitiwa ambao hawajui kusoma na kuandika
kuweza kushiriki katika kutoa taarifa za kutosha na za kina kuhusu utafiti.
(ii) Mbinu hii ilimsaidia mtafiti kupata taarifa nyingine ambazo zisingepatikana kwa
mbinu ya hojaji.
(iii) Mbinu hii ilitoa fursa ya kuuliza maswali ya ziada na kujibu maswali
tokezi/ibukizi yaliyojitokeza katika mahojiano kati ya mtafiti na mtafitiwa.
(iv) Njia hii pia ilimsaisia mtafitiwa kuelewa swali ipasavyo kwani ni mbinu pekee
inayotoa fursa kwa mtafiti kutoa maelezo zaidi kwa swali ambalo halikueleweka
kwa mtafitiwa.
(v) Njia hii inatoa mwanya kwa maswali mengine ya kujieleza yaani maswali
ambayo yako nje ya yale yaliyoulizwa (maswali ibukizi).
(vi) Mbinu hii ilimpa fursa mtafitiwa kueleza hisia zake binafsi kuhusu mada
inayotafitiwa.
Mbinu ya mahojiano ilimwezesha mtafiti kukusanya data zilizohusiana na makundi ya
majina, vigezo walivyotumia kuteua majina na mazingira yanayopelekea watu
kupewa majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Hivyo basi, mchakato wa mahojiano
upatikanaji wa watafitiwa. Mahojiano yaliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili kwa
watafitiwa wanaoweza kutumia lugha ya Kiswahili. Watafitiwa walioshindwa
kutumia lugha ya Kiswahili mahojiano yaliendeshwa kwa lugha ya Ginantuzu kwa
kuwa mtafiti naye ni mzungumzaji wa lugha ya Ginantuzu. Data zilizopatikana katika
mbinu hii zilinukuliwa na kuhifadhiwa kwa lugha ya Kiswahili kwa njia ya
maandishi.