2.5 Kiunzi cha Nadharia
2.5.1 Nadharia ya Uumbaji
Nadharia ya Uumbaji iliasisiwa na mwanaisimu wa Kimarekani Edward Sapir (1958)
na kuendelezwa na mwanafunzi wake Benjamin Lee Whorf (1958) ambaye baadaye
mwanafunzi huyo alidai kuwa ni yake na akaiita Dhanio la Whorf. Mpaka sasa
wataalam wengi wa isimu wanaiita kama nadharia jumuishi ya Sapir - Whorf.
Kimsingi nadharia hii inahusu lugha na utamaduni. Sapir aliamini kuwa upo uhusiano
wa lugha na jamii na kusema kuwa lugha hutawala fikra za wazungumzaji wake na
kuwapa namna ya kuusawiri ulimwengu wao. Sapir (keshatajwa) anaendelea kwa
kusema kwamba lugha ndio msingi wa kuuelewa ulimwengu. Unapojifunza lugha ni
na dunia kama ilivyoratibiwa na wasemaji wake. Binadamu huuona ulimwengu
kupitia taratibu zilizowekwa na lugha yake ya kwanza. Ni vigumu kuchukua jina la
mtu kutoka katika jamii fulani na kumpa mtu wa jamiilugha nyingine kwa sababu jina
la jamii moja hufungamana na imani hiyo ambayo huambatana na utamaduni wa jamii
husika. Kutokana na maelezo hayo watu wenye misingi tofauti ya lugha hawapati
picha sawia ya ulimwengu. Ulimwengu tunamoishi kwa kiasi kikubwa umejengwa
kupitia lugha za jamii fulani. Jamii zinatofautiana katika kujenga fikra na mawazo
kutokana na vitu mbalimba katika lugha husika kama ilivyo kwa majina ya asili ya
jamiilugha moja na nyingine ulimwenguni hususani Barani Afrika. Sapir (1921)
anaeleza kuwa, wanadamu hawaishi katika ulimwengu dhahiri wala wa pekee bali
wanazungukwa na shughuli za kijamii na kuzama katika ulimwengu wa lugha ambao
ndio njia pekee ya kujieleza katika jamii. Lugha huakisi ulimwengu halisi kwa kiasi
kikubwa na ulimwengu wa lugha umefungamana na tabia za lugha ya kundi au jamii
fulani. Watu huona, husikia na huwa na tajiriba ya mazingira yao kwa kuchukulia
kuwa lugha zao hufafanua na kuelezea tajiriba zao na hivyo, huathiri maisha yao.
Maoni ya Sapir yaliungwa mkono na Whorf aliposema kuwa wazungumzaji wa lugha
zilizo na sarufi tofauti huelekezwa na sarufi za lugha zao kwa njia tofauti ya kuyaona
mambo hayo. Whorf alifanya utafiti kwa kuchunguza lugha ya mzungumzaji mmoja
wa lugha ya Hopi aliyekuwa anaishi katika jiji la New York Marekani. Katika utafiti
huo alithibitisha kuwa wazungumzaji wa lugha ya Hopi hawazingatii sheria katika
upande wa nyakati (njeo) wanapozungumza, kwa hiyo ni lazima watu hao
wanausawiri wakati tofauti na watu wengine. Whorf (keshatajwa) alidai kuwa
wazungumzaji wa lugha fulani huzungumzia vitu fulani kwa urahisi kwa vile wana
Wataalamu hawa mwishoni waliungana na kuunda nadharia iliyojulikana kwa jina la
Nadharia ya Uumbaji ya Sapir- Whorf. Wataalamu hawa kwa pamoja wanadai kuwa,
muundo wa lugha huathiri jinsi ambavyo wazungumzaji wa lugha hiyo huufasiri
ulimwengu na kuathiri pia mielekeo ya maisha yao. Mawazo yao yaliungwa mkono na
Wardhaugh (1986) aliposema kuwa jamii fulani hutumia lugha kwa njia ambayo
inaashiria wanachoamini katika utamaduni wao. Kwa maelezo ya wataalamu hao ni
dhahiri kuwa, jamii fulani hutumia majina ambayo yanaashiria na kuakisi utamaduni
wa watu hao.
Sapir na Whorf wanaendelea kusema kuwa, kuna uhusiano uliopo baina ya lugha na
mawazo yaeleayo akilini mwa watu wa jamii moja itumiayo lugha. Lugha ina jukumu
na jukumu hilo sio tu kama njia ya kutolea mawazo, bali kama kifaa cha kujengea
wazo katika mawasiliano yetu. Lugha ndio msingi wa kuelewa ulimwengu wa jamii
husika. Lugha za jamii yakiwepo majina yanasaidia kufahamu utamaduni, historia,
mazingira, hali za kiuchumi na kisiasa katika jamii husika. Nadharia hii pia inasisitiza
kuwa lugha hufungamana na jamii na bila jamii hakuna lugha. Kwa vile majina ya
watu ni kipengele cha lugha ni dhahiri kuwa majina ya asili nayo yana uhusiano na
jamii husika. Nadharia hii ya Uumbaji imejengwa katika mihimili/ misingi ifuatayo:
(i) Lugha ndio msingi wa kuuelewa ulimwengu. Unapojifunza lugha ni kama
unatawaliwa na lugha hiyo. Hata dunia utakayoiumba akilini mwako itatokana
na dunia kama ilivyoratibiwa na wasemaji wake.
(ii) Fikra za mtu yeyote huamuliwa na lugha anayozungumza. Hii inamaanisha
kuwa, watu wanaufasili ulimwengu kulingana na jinsi unavyoendelezwa na
(iii) Lugha huathiri namna watu wanavyoumba ulimwengu wao. Hivyo, watu
wanaozungumza lugha fulani huuona na kuufasili ulimwengu tofauti na
wanaozungumza lugha nyingine.
(iv) Hakuna jamiilugha mbili zinazoweza kuwa sawa, hivyo, hata maana ya majina
katika jamii mbalimbali haziwezi kuwa sawa. Nadharia inasisistiza kuwa kama
wazungumzaji wa jamiilugha fulani hawatakuwa tayari kudumisha lugha yao ya
asili iliyobeba amali za jamii, kuna kila dalili kwamba utambulisho wa
jamiilugha inaweza kupotea.
Ikiwa tabia za watu huathiriwa na lugha yakiwemo majina, basi ni vigumu
wanaotumia majina ya lugha nyingine kuelewana na kuafikiana maishani. Ikiwa
tutafuata usemi huu, basi ni wazi kwamba lugha zetu za kwanza yakiwepo majina
ambayo tunatumia kufikiria ndiyo yaliyo na nguvu juu ya fikra, matendo na
utamaduni wetu. Tunapotumia majina mengine basi hatuna budi kuyapa kipaumbele
majina ya asili ambayo huumba fikra zetu.
Kwa kuwa hii ni nadharia na nadharia ni mwelekeo wa imani, wapo pia wanaopinga
nadharia hii ya Uumbaji ya Sapir-Whorf na wanatoa sababu zifuatazo:
(i) Nadharia ya Sapir-Whorf inafanya watu kuwa watumwa wa lugha zao ambazo
zinadaiwa kudhibiti fikra zao
(ii) Wanaanthropolojia wa utamaduni wamekubaliana kuwa watu wana uwezo wa
kitu kinachozungumzwa hata ingawa msamiati unaotumiwa ni tofauti. Kwa
mfano Wamarekani wana msamiati mwingi wa magari, lakini haimaanishi watu
(iii) Kama tungekuwa watumwa wa lugha zetu yakiwepo majina basi watu wawili
wanaoishi nyumba moja na wanaotumia majina ya asili wangefikiri sawa.
Licha ya pingarnizi hizi, nadharia hii inafaa sana katika utafiti huu. Sapir (1958) anaserna kuwa, lugha huwa kizuizi cha kuleta maendeleo, hasa masharnbani, kwa vile watu wengi warnepuuza dhima ya lugha katika kuleta maendeleo. Anadai kuwa, kusipokuwepo na uelewano baina ya rnzungurnzaji na mpokeaji habari, hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana. Maoni hayo yanaungwa mkono na Musau (1999) aliposerna kuwa, rnaturnizi ya lugha za kwanza yanaweza kuleta maendeleo mcngi ya uchurni katika jarnii zetu. Anaserna mtaalamu wa kilimo anahitaji kuwafunza wakulima njia bora ya kilimo kwa kutumia lugha yao ya kwanza wanayoifahamu vizuri.
Kutokana na majina haya ya asili tunaweza kusema kwamba jina linatunza historia ya
jamii kwa usahihi kuliko hata maandishi ya vitabu vya historia. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba vitabu visipotunzwa huweza kupoteza historia ya jamii husika kwa
kupoteza ubora wa maandishi, kuchanika au kupotea. Lakini kama majina yataendelea
kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine ni dhahiri jamii zitaendeleza kutunza
historia ya jamii husika kwa kupokea kutoka vizazi tangulizi. Hii inatudokeza
kwamba majina yasiyo ya jamii husika hayawezi kueleza historia ya jamii hiyo kwani
majina hayo ni urithi wa jamii nyingine ambayo kwayo hutambulishwa.