• Tidak ada hasil yang ditemukan

Maudhui ya Rara Katika Kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea 1967 Hadi 1988 Hadi 1988

MAUDHUI NA FANI YA RARA ILIVYOBADILIKA KATIKA KILA AWAMU YA MAENDELEO

7. Rara Umwoyo

5.1.4 Maudhui ya Rara Katika Kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea 1967 Hadi 1988 Hadi 1988

Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa fasihi simulizi ni sanaa ya kuwaunganisha wanajamii, chombo cha uzalishaji mali, kuhifadhi utamaduni, na kuchambua na

kuhakiki maisha ya wanajamii (Finnegan, 1970; Sengo, 1987; Okpewho, 1992; Mulokozi, 1996). Kutokana na dhima hizi fasihi simulizi hueleza jamii kiutamaduni, kiuchumi, na kisiasa. Aidha, huzungumzia juu ya yale mambo ambayo huzunguka jamii na mambo haya huenda sambamba na mabadiliko ya jamii husika.

Baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha mwaka 1967 utekelezaji wake ulianza mara moja. Sera ya kutaifisha mabenki ya watu binafsi, na kuhamisha wananchi kutoka mashambani na kuwapeleka katika vijiji vya ujamaa ilianza kufanya kazi. Madhumuni ilikuwa kuleta maisha yenye nafuu kwa wananchi. Badala yake, hali hii iliongeza matatizo kwa wananchi ambao hata kabla ya kuhamishwa walikuwa na matatizo ya kiuchumi. Katika hili Nyerere, (1977) anasema; “Matatizo ya kila siku lazima yawepo. Kukosekana kwa vitu vya anasa katika maduka yetu ni tatizo kwa watu wachache tu. Lakini kukosekana mara kwa mara kwa mahitaji ya kawaida, na ya lazima, ni tatizo linaloendelea kwa wananchi, hasa wale wanaoishi vijijini”.

Nyerere anakiri kuwepo kwa matatizo ya kukosekana kwa huduma muhimu kwa wananchi wake waliohamia katika vijiji vya ujamaa. Ingawa kuanzishwa kwa ujamaa na kujitegemea ilikuwa ni utekelezaji wa kuishi kijamaa kwa kuwafanya wananchi wote kuwa sawa kiuchumi, kisiasa na kijamii; maelezo ya mwalimu Nyerere yanaonesha kutokuwepo usawa huo. Kuna kundi la watu wachache ambalo linaishi maisha ya anasa huku kundi kubwa likiwa halina hata mahitaji ya msingi.

Rara ilikuwa ni sehemu ya faraja katika matatizo haya na mahubiri juu ya matatizo ya kijamii iliwasilishwa kupitia rara. Hata hivyo, nyimbo zilizokuwa zikiwahamasisha wananchi kwenda katika vijiji vya ujamaa na siasa ya kujitegemea

ziliimbwa. Mifano ya nyimbo hizi ni Ngonjera za Ukuta za Mnyampala (1971). Ngonjera hizi zilighanwa na vijana wa TANU YOUTH LEGUE katika mikutano ya kisiasa na mara nyingi ziliambatana na ala za muziki kama ngoma; ‘Mnyonge Hapigani kwa Fedha’;

Mnyonge hapigani kwa fedha, yeye hupigana kwa maguvu Tusiuondoe kwa karadha, miili tukatia uvivu

Usikie haya mawaidha, mwili wako siwe mlegevu Siasa yetu zaidi tuzidi nguvu, ihusuyo kujitegemea Viongozi wote sikieni, TANU, UWT na Bunge Na wale wengine washirikani, wa ushirika wasijitenge Na wewe TAPA hubagukani, kwa siasa hii ujiunge Siasa yetu hii tuchunge, ya kutaka kujitegemea Fedha toka nje ya Tanzania, na hiyo ina mambo yake Na tusije tukaililia, jua ina mikataba yake

Pengine heri hutujilia, nap engine baa tujitwike Siasa yetu hii tushike, ya mambo ya kujitegeme

Katika wimbo huu kinachosisitizwa ni siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Msanii anahimiza wananchi kuwa wavumilivu juu ya umasikini wao kutokana na serikali ya TANU na vyombo vingine vya serikali kuwa katika hali ngumu ya kiuchumi. Aidha, anawaonya viongozi kuepuka matumizi ya mikopo ya fedha kutoka kwa mataifa ya nje. Hali hii anaitazama kama sehemu ya kurudisha utawala wa kikoloni. Mbinu hii inatumika kama hali ya kuwatuliza wananchi wanaoteseka na maisha duni. Aidha inatumiwa ili kupanda mbegu ya woga kwa serikali kutegemea fedha za misaada hata kama taifa halikuwa na fedha za kutosha kuendesha mambo yake. Kwa hakika, wakati huu watunzi mashuhuri wa mashairi hasa Mnyampala na wengine, walihimizwa kutunga nyimbo zilizoeneza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi na mafunzo haya yalipelekwa mpaka mashuleni kuwafundisha na kuwafanya waijue na kuitetea sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Mkakati huu pia ulitumia katika rara zilizoimbwa na wanavijiji huko mashambani.

Matatizo ya wananchi yaliongezeka miaka ya katikati mwa 1974 na 1978. Wananchi waliokuwa wametolewa katika makazi yao ya awali kupelekwa vijiji vya Ujamaa, walipoteza baadhi ya mali zao. Mategemeo na ahadi ya kupata maisha bora katika vijiji vya ujamaa yalikwisha baada ya muda kupita bila hata dalili hiyo. Wananchi walizikumbuka mali zao walizopoteza wakati wanahamishwa, hasa baada ya kutokupatiwa hata zile huduma zilizokuwa zimeahidiwa kama shule, hospitali, maji, barabara na huduma nyingine za jamii.

Kwa upande wa muziki, katika miaka ya 1970 kulikuwa na majaribio yaliyofanywa na baadhi ya vijana, kama vile Union Jazz Band, Dar es Salaam Jazz Band, Kilwa Jazz Band, Morogoro Jazz Band, Kiko Kids, Unyanyembe Jazz Band, NUTA Jazz Band, Western Jazz Band, Cuban Marimba, Atomic Jazz Band, Jamuhuri Jazz Band, na kadhalika. Bendi hizi mara nyingi ziliimba muziki wa Kilingala kwa Kiswahili bila hata kubadilisha mahadhi, au ziliiga tu upigaji wa mitindo ya Kongo. Mifano ya nyimbo hizi ni kama;

Lau Nafasi (Kilwa Jazz) Napenda nipate lau nafasi, nipate kusema nawe kidogo, Aaaah! Mama aaah!

Moyoni naumiaa ………….

Mayowe (Dar Jazz)

Mpenzi sema unachotaka oooh! Nikupe upate kufurahi oooh! Wataka muziki aina gani oooh! Ili upate rejea tena oooh

Pamoja na kupiga muziki wa kiasili uliochanganya kidogo na midundo ya Kikongo kwa kutumia ala za kisasa, lakini maudhui yalibakia kuwa siasa ya ujamaa na kujitegemea ingawa haikutamkwa moja kwa moja. Haya yalidhihirika katika vionjo vya maudhui hasa kuhusiana na kudumisha utamaduni, hali za maisha, na mshikamano ambao ulitiliwa mkazo wakati huo. Majaribio haya yalipopata umaarufu kiasi, yalitekwa nyara na serikali ambayo iligeuza mashindano ya muziki wa dansi kuwa fursa ya upigaji wa muziki wa “asili” wa nyimbo ambazo ziliishia katika kusifu Chama, Serikali na viongozi wao. Mwaka 1975, serikali chini ya sheria ya Bunge ilianzisha Baraza la muziki la Taifa (BAMUTA), ambalo lililenga katika kukuza muziki wa kiasili kwa kuzingatia sera za nchi.

Hata hivyo, kulikuwa na vijana ambao mwanzoni mwa miaka ya 1970 walioibuka na aina ya muziki ambao ulichanganya midundo ya asili na midundo kutoka mataifa ya nje, ikiwa ni pamoja na Charanga, nao wakaghani hata ngano na ushairi katika nyimbo zao, ikiwa ni pamoja na kuuchambua uhusiano wa kijamii. Hawa ni kama Safari Treppers na Kimulimuli ambao umaarufu wao ulifanana na uliokuwa ukijitokeza miongoni mwa vijana wengi wa mjini wa tabaka la juu—ule wa disko pamoja na filamu za Kutoka Ulaya. Katika madisko hayo vijana walicheza Kungfu fight na Bumping’. Wakajitambulisha na akina Bruce Lee, Jim Kelly, Nora Miao na wengine ambao walipigana dhidi ya waonevu na mafisadi. Huu ulikuwa ni uasi, miongoni mwa vijana, dhidi ya mfumo wa kitamaduni uliochukulia kwamba jukumu la vijana ni kuendeleza “utamaduni wa taifa”, na siyo kuendeleza maisha yao. Dhima ya asasi za kitamaduni kwa ujumla ilikuwa imelenga katika kuwaamsha na kuwahimiza wananchi kwa ujumla kushiriki katika maendeleo, kujenga Ujamaa na

kupigania ukombozi wa Afrika. Mfano ni wimbo uliokusanywa kutoka TBC ‘Ukombozi wa Afrika’;

Sisi Watanzania, hatutabadili ahadi yetu ya Afrika, Tutaitetea Afrika yote mpaka iwe huru,

Tumesimama imara

Hatutakubali kuchezewa na yeyote

Tupo tayari kufa Watanzania kuliko kuonewa x3 Maghani: Eeeeh heeee

Ooooh! Ooooh! Wazumi: Afrika tutayari kufa Afrika kuliko kuonewa Yeli: Na Tanzania iko tayari kufa Mpaka ione Afrika nzima iko huru Wazumi: Afrika tutayari kufa

Afrika kuliko kuonewa Yeli: Hii Zambia iko tayari kufa Mpaka ione Afrika yetu iko huru Wazumi: Afrika tutayari kufa

Afrika kuliko kuonewa

Yeli: Guine na Mali, Ghana tayari kufa Mpaka ione Afrika yote iko huru Wazumi: Afrika tutayari kufa

Afrika kuliko kuonewa

Yeli: Kongo Kishansa na Braza tayari kufa Mpaka ione Afrika nzima iko huru Wazumi: Afrika tutayari kufa

Afrika kuliko kuonewa

Yeli: Kenya Burundi Rwanda tayari kufa Mpaka ione afrika yetu iko huru Wazumi: Afrika tutayari kufa

Afrika kuliko kuonewa

Yeli: Ethiopia, Sudani, Somali tayari kufa Mpaka ione afrika yetu iko huru

Wazumi: Afrika tutayari kufa Afrika kuliko kuonewa

Wimbo huu unahimiza Waafrika wote kuungana katika kuhakikisha nchi zote za Kiafrika zinakombolewa kutoka katika utawala wa kikoloni. Hii ilikuwa ndiyo sera ya chama ya wakati huo, na haikuishia katika matamshi, bali katika vitendo. Aidha, suala la kujenga maadili, utamaduni na kuimarisha ujamaa na kujitegemea lilikuwa katika ngazi zote za maamuzi kuanzia serikali mpaka kwa wananchi wa kawaida.

Kutokana na mkabala huu, Redio Tanzania Dar es Salaam, ambayo ndiyo ilikuwa redio pekee, ilikuwa ikirekodi na kutangaza muziki ambao ulidhaniwa ni wa Kitanzania na “unaokubalika” kimaadili—ikiwa ni pamoja na Taarab (ambao asili yake ni Mashariki ya Kati) na ngoma za asili (ambazo nyingi zake zilitokana na Beni Ngoma, Mganda, Babatoni, Wigashe na nyingine). Kwa ujumla, kulikuwa na udhibiti wa vyombo vya utamaduni, ambao ulisababisha kuzuia au kupiga marufuku kila kile kilichoonekana kwamba kinaenda kinyume na maadili ya Kiafrika ama yale ya ujamaa na kujitegemea.

Zaidi ya ngonjera za Mnyampala ambazo zilihubiri mipango dhabiti ya Ujamaa na Kujitegemea, hakukuwa na nyimbo zilizolitaja Azimio la Arusha moja kwa moja. Aidha, maudhui ya maisha duni ya wakulima na wafugaji yanajitokeza wakati huu. Hii ni kusema kwamba, mfumo huu pamoja na kuhubiriwa katika sera za kisiasa wananchi hawakuona manufaa yake zaidi ya kuongezewa matatizo juu ya matatizo ya kiuchumi waliyokuwa nayo kabla. Masuala ya uchawi na ushirikina na pamoja na matatizo ya kiuhusiano yanaonekana kwa kiasi kikubwa. Maudhui ya namna hii

yalionesha ni kwa kiasi gani jamii ilikuwa imekata tamaa juu ya maisha bora yaliyokuwa yameahidiwa na viongozi wa chama na selikari.

Kwa mfano wimbo wa Katonzi uk. 116 wa tasnifu hii, ni wimbo ambao ni mfululizo wa maombolezo ya msiba baada ya mhusika kufiwa na mama na mtoto wake. Aidha, mfiwa anamwomba mganga ampigie lamri ili kujua chanzo cha vifo hivyo. Hali hii inaonesha kwamba kuna uwezekano chanzo cha vifo hivyo ni uchawi na ushirikina. Jambo hili lilikuwa ni la kawaida katika jamii ambayo iliongozwa na mitazamo ya imani pekee. Maudhui ya uchawi na ushirikina katika kipindi hicho yalikuwa ni sehemu ya maisha na nyimbo nyingi ziliyasawiri moja kwa moja kama wimbo unaoimbwa na Petro A. Sabini (Awilo Kidume cha Mbeya) ‘Avalozi’ yaani ‘Wachawi’ unavyobainisha;

8. Wimbo Avalozi kwa Maana ya Wachawi