• Tidak ada hasil yang ditemukan

KATEGORIA ZA RARA KATIKA AWAMU NNE ZA MAENDELEO

8. Wimbo Nkulila Umwana

Yeli: Nkulila umwna wane x2,

wee njoha

Kiitikio: Nkulila umwana

wee njoha

Yeli: Nkulila umwna wane x2

, wee njoha

Kiitikio: Nkulila umwana

wee njoha

Yeli: Wandila umwana,

Uhalya nu tata, Wandila umayi,

Yeli: Nkulila umwna wane x2,

wee njoha

Kiitikio: Nkulila umwana

wee njoha

Yeli: Namlilia mtoto wangu x2 wee nyoka

Kiitikio: Namlilia mwanangu wee nyoka

Yeli: Namlilia mtoto wangu x2 wee nyoka

Kiitikio: Namlilia mwanangu wee nyoka

Yeli: umemla mwanangu, Umemla baba yangu, Umemla mama yangu, Yeli: Namlilia mtoto wangu x2 wee nyoka

Kiitikio: Namlilia mwanangu wee nyoka

Katika wimbo huu maudhui yake yanaegemea katika kifo ambacho kinaaminika kusababishwa na uchawi na ushirikina. Aidha, watu wengine wanatajwa katika mfululizo huu kama baba na mama ambao nao wanahusishwa na aina ya kifo kilichomkuta mtoto huyu. Imani ya uchawi na ushirikina katika jamii ambazo hazina huduma za jamii kama vile afya na elimu ni mambo ya kawaida na haya ni matokeo ya maendeleo duni katika jamii.

Mikakati ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha 1967, ilitokana na jitihada zilizokuwa zimefikiwa tangu kipindi cha baada ya uhuru. Msukumo mkubwa wa serikali ulikuwa kusogeza maendeleo kwa wananchi. Jambo hili lilikutana na vikwazo na changamoto zilizokuwepo wakati huo kama uchumi tegemezi na wasomi wachache ambao ndio waliotegemewa kushika nyadhifa mbalimbali za serikali, ikilinganishwa na ukubwa wa nchi kijiografia na idadi ya watu waliokuwa hawajapata elimu ya Kizungu (Coliman, 1977; na Shivji, 1987). Changamoto hizi ziliwafanya watawala kuamini kuwa kundi kubwa la wakulima, hususani wa vijijini ndio waliokwamisha kusonga mbele kwa uchumi. Haya yalidhaniwa kutokana na kwamba, wakulima wengi hawakuwa na uwezo wa kulipa kodi. Na zaidi ndio waliohitaji kwa kiasi kikubwa huduma za jamii kama shule, hospitali, maji safi, barabara na wakati mwingine chakula.

Sera ya kuundwa kwa vijiji vya Ujamaa ilianza utekelezaji wake mara moja kama njia ya serikali ya kutatua changamoto zilizoainishwa. Lengo kubwa lilikuwa kuwapatia wakulima na wafanyakazi huduma muhimu kama za shule, hospitali, barabara, na utawala. Aidha, ilikuwa ni njia mojawapo ya kuwafanya wananchi kuzalisha ziada. Hili lilionekana kama suluhisho la wananchi kupata kipato cha mtu

mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Pamoja na yote hayo, ilibainika kwamba utamaduni wa mtanzania ungeweza kujengwa na wanajamii waliokaa pamoja. Nyerere, (1977) anasema; “ ..tumepiga hatua ya maana katika kuwapatia wananchi huduma za afya, elimu, na usafirishaji wa umma. Mafunzo ya watumishi yameongezwa sana, na kutokana na ushirikiano wa wananchi chini ya chama, pamoja na serikali, tumeweza kujenga zahanati nyingi mpya, shule, majumba ya maendeleo, mifereji ya maji na mengine… wananchi sasa wanaishi katika vjiji vya ujamaa ambako wanaweza kufanya kazi pamoja, kutumia pamoja na kufanya shughuli za utamaduni pamoja katika kuinua hali zao za uchumi”. Mambo haya yanajitokeza pia katika nyimbo na mashairi ya wakati huo. Mfano mzuri ni Ngonjera za Ukuta Mnyampala, (1971);

Wito wetu Kujitegemea, Ujamaa ndilo lengo kuu Usawa kujiletea, tangu wa chini hadi wa juu Mafanikio tujiletea, hebu nasi tusogeze guu

Tangu sasa dara mwendo huu, acha ubaguzi kuufanya Baba yatazameni mavazi, vijana wetu wamelemaa Mabinti nao wao mashangazi, zile taiti wanazovaa Utacheka utoe machozi, zimebana na kung’ang’anaa Tangu leo bora kukataa, hizo nguo fupi kuzifanya Kikundi chema kingaliundwa, kikauhami utamaduni Utamaduni ungalilindwa, kila mwanachi kuuthamini Ulinawiri na kupendwa, na walo ng’ambo wakatamani Tangu sasa vijana lindeni, jitihada njema mkifanya

Dhamira ya serikali ilikuwa kuwapelekea wananchi madaraka na shughuli za kiutawala wananchi wenyewe. Hii ilionekana kama njia rahisi ya kutatua changamoto za maisha, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Hata hivyo, ilikuwa kusuruhisha manung’uniko kwamba wakulima walikuwa ni mzigo kwa wafanyakazi hasa wasomi waliokuwa wameshika nyadhifa za serikali. Aidha, malengo haya

hayakufikiwa kama asemavyo Nyerere, (1977) baada ya miaka kumi ya Azimio la Arusha; sasa ni miaka kumi tokea Azimio la Arusha kutangazwa, na Tanzania bado haijawa nchi ya kijamaa, wala haijajitegemea. Namna ya unyonyaji imebadilika; lakini unyonyaji wenyewe haujafutika. Bado kuna tofauti kubwa za maisha baina ya raia. Demokrasia yetu bado ina walakini. Maisha ya umasikini bado ni ya kawaida.

Watu wengi mno bado wanasumbuliwa na ujinga na maradhi yanayoweza kuzuilika. Wazee na vilema hawajaweza kuishi maisha mazuri na ya salama, ingawa Azimio la Arusha limeeleza wazi. Nyerere anakili kwamba Azimio la Arusha lilishindwa kufikia malengo yake. Badala ya kuwawezesha na kuwapelekea madaraka hayo wakulima, walipelekwa watawala kama asemavyo Hyden (1980) “Jamii ya wakulima iliachwa bila uwezeshwaji kama lengo la serikali lilivyokuwa mpaka miaka ya 1970. Matokeo yake ni vyama vya ushirika ambavyo vilianzishwa na serikali kwa kushirikiana na watu binafsi waliokuwa na uchumi wa kati kupoteza uwezo na hatimaye kufa mwaka 1976”.

Hali hii ilisababisha hali ngumu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na makundi ya watu kwa ujumla wake yaliyokuwa yameundwa kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi. Njaa, umasikini uliokithiri, uhaba wa matibabu, na huduma za msingi zilikosa kwa kiasi kikubwa. Matokeo yake iliongezeka misiba inayotokana na ukosefu wa huduma hizo. Aidha, kutokana na wanajamii kutokuelewa hasa chanzo cha misiba hii uchawi na ushirikina ndio uliosingiziwa kama katika wimbo huu ulioimbwa na ‘Kalungwanje’ kutoka kijiji cha Nambala Wilaya ya Mbozi Katonzi kwa maana ya ‘Ndege’;

9. Wimbo Katonzi