• Tidak ada hasil yang ditemukan

Wimbo Bazungu Bhashetani Bazungu Shetani

KATEGORIA ZA RARA KATIKA AWAMU NNE ZA MAENDELEO

7. Wimbo Bazungu Bhashetani Bazungu Shetani

Bazungu shetani Na Bahindi shetani Na Balabu shetani ntale Batubulagaga

Batukomaga misumali Ku magulu

Ulu twalilababyuduta ndezu Bubina mbina

Bubeja shigukulu

Gubi bwanhana twitawalile Ng’na mbagule

Wazungu ni mashetani Wazungu ni mashetani Wahindi ni mashetani

Ana Waarabu ni mashetani wakubwa Walizoea kutuua

Walitudunga misumali Miguuni

Tulipolia kwa uchungu walivuta ndevu zao Kwa furaha kubwa

Na kufanya sherehe Na iwe dhahiri Kuwa tumejitawala Mwana wa Mbagule Chanzo: Mulokozi, (1996)

Wimbo huu unabainisha hasira za waafrika dhidi ya mkoloni kwa matumizi ya lugha kali. Hata hivyo, nyimbo nyingi ziliweka mkazo katika imani waliyokuwa nayo wanajamii kwa watawala wao wa kiafrika. Haya yanajibainisha katika mashairi na Ngonjera za Ukuta za Mathias Mnyampala na baadhi ya nyimbo za wakati huo.

Katika kipindi hiki, wanajamii walikuwa na matumaini ya kuwa na maisha bora ya kujitawala wenyewe na kuacha kutawaliwa na wageni. Mambo yaligeuka na kuwa kinyume na yale wali- yotarajia. Viongozi wengi walioingia madarakani, waliiga yale yote waliyokuwa wakiyafanya Wakoloni. Matokeo yake yakawa kinyume kabisa na matarajio ya wanajamii hawa. Kukatokea kuwa na uongozi mbovu, uliokuwa na uroho wa kutafuta mali kwa manufaa yao wenyewe. Katika uongozi pakaibuka ubadhirifu, wizi na ufujaji wa mali ya umma. Rushwa, unyang’anyi, unyanyasaji, ubeberu, ufisadi vilikithiri kwa baadhi ya viongozi.

Fasihi ya Kiswahili kwa ujumla na rara kwa upekee haikulifumbia jicho suala hili. Ziliandikwa kazi nyingi zilizokuwa zikiwasema, zikiwakosoa na zikiwakejeli

vibaraka na wasaliti hawa. Kwa mfano, katika riwaya za Ruhumbika, (1995) Miradi Bubu ya Wazalendo na Liwenga, (1981) Nyota ya Huzuni ambao wamewakosoa viongozi katika kuonesha hali halisi ya maisha katika kipindi hicho ingawa zimekuja kuchapishwa miaka ya hivi karibuni. Wameweka suala la rushwa na usaliti uliofanywa na viongozi waliojilimbikizia mali kipindi hiki. Aidha, wanatuonesha matabaka, uchu wa madaraka, usaliti na uhujumu wa uchumi uliokithiri katika jamii. Hata hivyo, hii ni mifano kutoka katika fasihi andishi ambayo si rara kuonesha kwamba kama fasihi ni kielelezo cha maisha ya jamii katika mazingira na wakati husika, basi haina shaka kuwa rara zilizokemea masuala haya ziliimbwa.

Ni katika kipindi hikihiki, ndipo wanajamii walipotambua kuwa maisha yao si bora kama walivyokuwa wametarajia. Waligundua kwamba, viongozi wengi walioingia madarakani, walikuwa wakifanya zaidi ya yale waliyokuwa wakifanya Wakoloni. Kazi andishi za Miradi Bubu ya Wazalendo na Nyota ya Huzuni ambazo zimechapishwa miaka ya hivi karibuni zinakimulika kipindi hicho cha miaka ya 1961 hadi 1967.

Aidha, kazi hizi ni vielelezo vya yale yaliyofanywa na watawala wa wakati huo. Katika kazi hizo, tunaoneshwa jinsi viongozi walivyokuwa wakiwanyanyasa wanajamii waliokuwa wamewachagua kwa kura zao. Kwa mtazamo wa nje tu, jina la riwaya Miradi Bubu ya Wazalendo linamkejeli mzalendo na jamii nzima ya kuwa hawana jipya la kuweza kufanya kwa kuwa yote wanayoyawaza hayatekelezeki. Mwandishi anawataka wanajamii kujitokeza kuibua mawazo na kuhimiza mapambano ili kuutetea ukombozi utakaowaletea uhuru wa kujenga jamii mpya.

Kwa kuwa dhima ya sanaa ni kuyasema mabaya na mazuri yanayojitokeza katika jamii, rara iliyojitokeza kipindi cha baada ya uhuru ilitekeleza wajibu huo. Na kutokana na kwamba msanii ni zao la jamii na jamii husawiriwa katika sanaa, watunzi na watambaji wa rara wa kipindi hiki waliyasema maozo ya wakati huu kupitia nyimbo kama asemayo Plekanovu, (1957);

Ili fasihi simulizi iwe na manufaa katika jamii, ni lazima iwe chombo kinachoaminika cha jamii husika. Ni lazima iwe na jukumu la kuieleza jamii, kuichambua, kuikosoa, na kuiongoza katika lengo lake la kuupindua unyonge na uchafu uliosakini katika jamii. Pia fasihi hutoa pongezi kwa watu waliotoa mchango wa kuiendeleza jamii. Vivyo hivyo, hushutumu wanajamii ambao nia yao ni kuipotosha jamii.

Hali kama hii inajidhihirisha katika kazi nyingi za sanaa ya rara na aina nyingine kama inavyojadiliwa katika sura ya tano. Kwa upande wa utamaduni ambao ulikuwa katika hatua za mwanzo kutoka katika misingi iliyojengwa na utamaduni wa kikoloni, nao ulikuwa na matatizo yake. Wasomi wachache waliokuwa katika utawala wa kikoloni hawakusaidia kuuenzi utamaduni wa Mtanzania. Pamoja na kwamba lugha ya Kiswahili ilitangazwa kuwa kielelezo cha utamaduni wa Mtanzania, lakini baadhi ya wasomi wachache hawakutilia mkazo lugha hiyo na waliendelea kuithamini lugha ya Kiingereza.

Aidha, mavazi na matendo yote ya kila siku yaliyokuwa sehemu ya utamaduni wa mkoloni hayakubadilishwa kama taratibu za kula, kunywa, kuoa na mengine. Mambo kama hayo yaliachwa kwa wakazi wa vijijini na wakati mwingine waliyaona kuwa ni ya kishamba. Hali kama hiyo, yawezekana ikawa ni sababu kubwa ya Watanzania na nchi ya Tanzania kwa ujumla wake kukosa utamaduni

unaolitambulisha taifa lao. Lugha ya Kiswahili kutokana na msisitizo uliowekwa na mwalimu Nyerere ikibaki kama kielelezo pekee cha utamaduni wa Mtanzania. Aidha, Fanon, (1990), aliwahi kutamka kwamba, utamaduni wa taifa si hadithi, nyimbo, ngano au desturi na habari za watu wa kale au udhahania pendwa (abstract populism) ambao unaamini kwamba unaweza kugundua asili halisi ya watu.

Utamaduni wa taifa hautokani na kudumisha mabaki ya matendo yaliyotendwa, yale ambayo kila kuchapo hayana uhusiano na hali halisi ya watu ya wakati unaohusika. Utamaduni wa taifa ni ujumla wote wa juhudi zifanyikazo na watu katika fikra zao kuelezea, kutetea/kuthibitisha na kusifu matendo ambayo yanawawezesha kujenga, kulinda na kuyadumisha maisha yao. Daima, utamaduni wa taifa hufungamana na upiganiaji wa uhuru, heshima na haki ya mwanadamu. Fanon akiendelea na mjadala huu, anawadhihaki watetezi wa Utu Weusi (Negroism), alimaka:

Kuamini kwamba kuna uwezekano wa kuunda utamaduni wa mtu mweusi ni kusahau kwamba watu weusi wanatokomea, kama wale ambao waliosababisha kuwepo kwao wanavyoshuhudia kuvunjika kwa mfumo wao wa kiuchumi na upeo wa utamaduni wao. Haitawezekana kuwepo kitu kama utamaduni wa mtu mweusi kwa sababu hakuna hata mwanasiasa mmoja ambaye anajisikia mwenye wito wa kujenga jamuhuri za watu weusi.

Akamalizia kwamba, la muhimu kutafakari ni suala la mwelekeo wa wanasiasa na mahala wanapotarajia kuwapeleka watu, aina ya mahusiano wanayokusudia kuyajenga na aina ya fikra za ujenzi wa jamii na maisha ya baadaye ya binadamu wanazozinadi. Hayo ndiyo muhimu: mengine yote si lolote. Kwa wasomi wengi waliokuwa katika utawala wa kikoloni, hata baada ya kukabidhiwa nchi zao hawakuwa na mitazamo chanya juu ya jamii zao kama anavyopendekeza Fanon hapo

juu. Aidha, hawakuwa na imani kwamba walikuwa katika nafasi ya kulinda na kutetea heshima, utu, na maisha ya jamii zao. Ama hawakuamini kuwa wangeweza kufanya sawa na walivyofanya wazungu, na hata baadhi ya waliokuwa na uwezo zaidi ya wazungu walipoteza ari na moyo wa kujiamini katika kazi zao. Matendo na kila walichokifanya kilielekea kuwaiga Wazungu kuanzia matamshi ya lugha zao, miondoko yao na huduma walizotakiwa kuwapa Waafrika wenzao waliowapatia nafasi za kuwaongoza.

Hali kama hii si kuwa ilirudisha nyuma maendeleo ya utamaduni wa Mwafrika tu, bali iliendelea kupandikiza kasumba ya Kizungu miongoni mwa watawala wa Kiafrika. Rara na aina nyingine za sanaa ya Waafrika ziliendelea kudharauliwa kama ilivyokuwa awali. Fasihi simulizi na rara iliyofuata mila na taratibu za Kiafrika kama vile Kingwengwi, Mganda, Lelemama na nyingine zikaendelea kuishi vijijini ambako hakuna uzungu, bali Uafrika na Utanzania kwa upekee.

4.4 Rara Katika Mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea 1967 hadi 1988

Kabla ya mfumo wa Ujamaa na kujitegemea nchini Tanzania kulikuwa na hatua mbalimbali zilizokuwa zimechukuliwa kama harakati za kudumisha utamaduni, uchumi na siasa ya Watanzania wenyewe. Hatua hizi ni pamoja na kuunganisha nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar kuunda Tanzania mwaka 1964, na kutangazwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa la Tanzania na kutangazwa kwa siasa ya Ujamaa na kujitegemea mwaka 1967. Aidha Mnyampala, (1971) katika Ngonjera za Ukuta anasema;

Lengo la ngonjera za Ukuta ni kuwafundisha vijana wetu chipukizi mambo matatu maalum. Kwanza ni

kuwazoeza kutamka maneno fasaha ya Kiswahili na kuwajenga wawe makhatibu bora kwa siku za mbele wasimamapo jukwaani kuieleza siasa ya nchi yao. Pili, wanapotumia maneno hayo ya kishairi kwa ghibu bila kutazamia, wanajifunza siasa ya nchi yao kuhusu Azimio la Arusha, siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, faida ya Vijiji vya Ujamaa, Elimu ya Kujitegemea na kuwatukuza viongozi wa nchi yao. Tatu, watajali utamaduni wa taifa lao na kuutukuza na kuachilia mbali desturi na utamaduni wa kigeni (Ukuta 1, uk. 1).

Kinachosemwa na Mnyampala ni sera halisi na malengo makuu ya mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea. Masuala yanayohusu kujitegemea, utamaduni wa Mtanzania, matumizi ya Kiswahili na kuepuka aina zote za utamaduni wa kigeni ambao ulikuwa umepandikizwa miongoni mwa watawaliwa. Hata hivyo, kidokezo hiki ni ufunguzi mzuri katika mjadala wetu katika sehemu hii.

Aidha, Mlama, (2002) anasema kuwa jamii ina mtazamo juu ya mfumo wa maendeleo kwa kuelekea ustawi wa jamii husika. Mtazamo huu umejikita katika mabadiliko yanayotokea kila siku, zaidi juu ya kukidhi mahitaji ya lazima kama mavazi, chakula, makazi na usalama wao. Haya hayatimii nje ya mila na desturi zinazoiongoza jamii husika kama namna ya kufikiri, imani, thamani ya utu na mienendo ya jamii. Mlama tunachukua mtazamo wake kutokana na kuwa katika kipindi cha 1968 kinajulikana kama kipindi chenye historia kubwa katika nchi ya Tanzania. Mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea ulitangazwa kama dira ya maendeleo ya jamii ya Watanzania. Mfumo huu ulitoa si sera tu kama unavyojulikana kuwa mfumo wa kisera, bali mwelekeo wa Mtanzania alivyotakiwa kuishi katika mazingira yake na jamii iliyokuwa ikimzunguka. Kufanikiwa kwa mfumo au kushindwa kufikia malengo kwa mfumo kulikuwa na matokeo makubwa kwa

mwananchi wa kawaida. Sanaa iliyojitokeza katika kipindi hiki iliusawiri mfumo mzima, nyimbo na sanaa andishi za kipindi hiki hazikuacha kubeba majukumu ya mfumo huu. Kwa mfano, kazi andishi kama; Njozi Iliyopotea, Nyota ya huzuni, Kichwa Maji, Lina Ubani kwa kuzitaja chache. Uwingi wa kazi andishi zilizoshangilia kwa namna moja na kuukejeli mfumo huu wa ujamaa na kujitegemea ni dhihirisho tosha kuwa kazi simulizi kama rara zisingeweza kuacha kuingia katika kujadili mfumo huu. Nyimbo nyingi zinazojitokeza wakati huu katika jamii zinazozungumzia masuala ya kijamii kama vile misiba na ushirikina ambao kwa kawaida haukwepeki katika jamii yenye mwelekeo wa kukata tamaa juu ya maisha magumu. Aidha, uchawi na ushirikina katika kipindi hiki unaonekana kushamiri kama matokeo ya jamii yenye uwezo mdogo wa kiuchumi unaotokana na ukosefu wa huduma za jamii kama elimu, afya, maji, na nyingine. Kwa mfano wimbo ‘Nkulila Umwana’ unaoimbwa na Kalugwanje msanii wa rara katika msiba kijiji cha Nambala Mbozi: